01/02/2024
ISRAEL NA HEZBOLLAH ZAFYATULIANA MAKOMBORA MPAKANI
Jeshi la Israel limetangaza kuwa limefanya mashambulizi ya anga kwenye miundombinu na majengo ya kijeshi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Siku ya Alhamisi asubuhi, Hezbollah ya Lebanon ilirusha makombora mawili kutoka kwa vifaru vyake kuelekea eneo la jeshi la Israel katika Mlima Hermon kaskazini mwa Israel, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel.
Hakuna habari iliyoripotiwa kuhusu majeraha yoyote.
Jana usiku, Hezbollah ilitangaza kuuawa kwa mmoja wa wanachama wake, na kufanya idadi ya vifo kufikia 177 tangu Oktoba 8.