Neno Ministry

Neno Ministry Ukrasa huu ni kwa ajili ya kujifunza na kuelimishana juu ya imani ya kikristo

05/05/2026
05/05/2026

Ñjia iendayo uzimani imejaa jasho na damu. Yatupasa kuubeba msalaba wa Yesu kwa uaminifu

04/05/2026

Celebrating 8th year of neno Ministry-Tz on Facebook. Thank you for your continuing support. I could never have made it without you. 🙏🤗🎉

04/05/2026

Dhambi ina athiri mfumo wa maisha ya mtu

‎‎HESHIMU WATU – Tafakari ya leo ‎‎Ndugu zangu wapendwa, leo napenda tuchukue muda tufikirie maneno hili: KUWAHESHIMU WA...
30/01/2026


‎HESHIMU WATU – Tafakari ya leo

‎Ndugu zangu wapendwa, leo napenda tuchukue muda tufikirie maneno hili: KUWAHESHIMU WATU, nasema kuwaheshimu wafu na zinasema mtu.Hapa maanisha wakiwemo hata wale walio dhaifu.

‎Kwa nini?

‎Kwanza, lazima tujue kuwa kila kiumbe aliye duniani, iwe binadamu au mnyama, pengine hata mimea Mungu amemuumba kwa ajili ya kusudi lake na moja wapo ya kimakusudi hayo ili mwanadamu aishi duniani kwa furaha. Fkiria kuhusu dunia bila uwepo wa mimea itakuwaje?.

‎ Kwa hiyo Hata viumbe au watu wale ambao kwa mtazamo wa dunia hawawezi kuonekana kuwa na thamani mfano vichaa, Mungu amewaweka kwa kusudi maalum.

‎Amewaweka ili wafanyiwe msaada kwako wakati wa uhitaji wakiwa, wakati wewe mwenyewe huwezi kutatua changamoto yako, hivyo hatupaswi tukisha kwa upendo na kuheshimu uimbaji wa Mungu.

‎Mfano: Mungu aliwatumia nzige na simba kuwadhibu wale waliokiuka maagizo yake. (2Wafalme17:25-26)

‎Mfano mwingine: Rahabu, kahaba, alitumika kuokoa Waisraeli, na pia akahifadhi familia yake. (Yoshua 2:1-21), japo ukweli alikuwa kahaba, na pengine family yake haakumdhamini kwa tabia yake ya ukahaba lakini ndiye ayealiwaokoa

‎Hivyo basi, si jambo jema kuwabeza wengine kwa sababu ya hali yao ya sasa. Kwa macho ya dunia wanaweza kuonekana dhaifu, watu wenye dhambi au wasio na thamani, lakini jua kuwa Mungu anaweza kuwatumia katika baraka au msaada ambao haukutarajiwa.

‎Ngoja niseme hili. N kweli Mungu anachukia dhambi, dhambi hututenga mbali na Mungu, dhambi inaharibu mpango wa Mungu katika maisha yetu. Lakini nataka ufahamu kuwa Mungu akiamua kumsogelea mwenye dhambi, dhambi basi itakimbia yenyewe wala haiwezi kamwe kumchafua Yesu.

‎Ngoja niseme kwa mifano.

‎Tunasoma habari za
‎Mama aliyeugua ugonjwa wa kutoka damu kwa muda mrefu alipomsogelea Yesu, alihisi huruma na kuponywa bila kumdharau na tunaona kwa dhambi za yule mama hakumdhuru Yesu. (Marko 5:25-34)

‎Unaona hapa. Kwa muijibu k**ani au sheria za Musa mtu akitokwa na damu alikuwa anatengwa na wengine kwa sababu yu najisi na chochote atakachogusa kitakuwa najisi. Lakini unaona huyu mama alipomgusa Yesu, Yesu hakuwa najisi

‎Binti aliyepasua kibweta cha mafuta kumgusa Yesu, ingawa alikuwa mwenye dhambi, ile dhambi yake haikumdhuru Yesu bali iliondoka kwa yule mama maana Yesu alisema umesamehewa dhambi zako.(Mathayo 26:6-13)

‎Hivi ndicho inavyokuwa pale Mungu huamua kutupa zawadi ya wokovu, hatusomgelei sisi kwanza ingali tuna dhambi zetu, si kwamba tunaanza sisi kinaongelewa Mungu la hasha bali Mungu ndiye kuanzisha mchakato wa wokovu ndani yetu.

‎Ni vema tuelewe kuwa hata sisi kabla ya kumjua Mungu tulikuwa tumechafuka na dhambi, neema ya kristo kupitia Damu yake imetusafisha. K**a vile tulivyo pata neema hiyo jua kubwa hata hao Mungu aweza kuwapa neema hiyo.


‎Mara nyingi Mungu huwaleta watu katika maisha yetu kwa sababu maalum

‎Kila mtoto, kila mtumishi, kila mtu aliye karibu nawe ana sababu maalumu kwako, anaweza kuwa chombo cha baraka.

‎Mfano: Yosefu, aliyekuwa houseboy, ndani ya nyumba ya Potufa alileta amani na baraka ndani ya nyumba ya Potifa. (Mwanzo 39:2-6)

‎Potifa alipotazama baraka hizi zote ajua hakika zimekuja kwa sababu ya huyu kijana Josefu, akaamua kumheshimu kwa kumfanya awe mkuu wa nyumba yake.

‎Ninani aliyetarajia kuwa Josefu atakuja kuwa msaada kwa taifa lote la Misiri?.vipi wale mak**anda kule gerezani walio mtumikisha Josefu walijisikiaje Joseph alipoinuliwa juu ya taifa zima.


‎Mfano mwingine: binti wa nyumba ya mkuu wa majeshi, alileta uponyaji wa ukoma. (2 Wafalme 5:1-14)

‎Binti huyu mtumwa katika nyumba ya majeshi huyu alileta furaha ya kudumu kwa majeshi huyu mashuhuri

‎Kwa hivyo, usiwanyanyase wale walio chini yako au dhaifu kwako, labda ni binti wa kazi au ni mfanyakazi wako n.k, waombee, wapende na uwalee kwa upando Wanaweza kuwa msaada wa Mungu, hata k**a leo hawaonekani sasa kubwa na thamani.

‎Ukweli wa upendo

‎Heshimu watu,hata wale walio dhaifu. Hii inatufundisha kuwa kila mtu anstahili upendo na heshima, kwa sababu hatuwezi kujua mpango wa Mungu katika maisha yao.

‎Angalia, Yesu alikuwa wanafunzi wake wa karibu sana, sasa angalia alipo kufa wanafunzi wake wote wakakimbia, huoni wakijadili namna ya kumzika Bwana wao kaburini hawapo kabisa. Lakini Mungu alimwinua mtu asiyejulikana, wala hakuwa na ukaribu au urafiki na Yesu, Yosefu ndiye uweka mwili wa Yesu kaburini kwa gharama zake mwenyewe. (Mathayo 27:57-60).

‎Usiwe na kiburi kwa sababu umezungukwa na watu muhimu, huwezi jua je ni yapi atakaye kutwa misaada kwako.Heshimu watu.

‎Kumbuka tabia mhimu ya Mungu tunaye mwabudu ni kubwa yeye ni pendo na anata wote wamwabuduo wawe na tabia ileile aliyo nayo.

‎"K**a mtu anasema: ‘Ninaupendo kwa Mungu,’ lakini hana upendo kwa ndugu yake, ndiye mdanganyifu." (1 Yohana 4:20)

‎Hitimisho

‎Heshimu kila mtu unayemkutana naye, iwe maskini, mdhambi, mzee au mtoto.

‎Upendo na heshima kwa wengine huonyesha uwepo wa Mungu katika maisha yetu.

‎Usiwe na dharau kwa wale ambao bado hawajapata wokovu; Mungu anaweza kuwatumia baraka zisizotarajiwa katika siku zijazo.

‎Tafakari leo: je, unawaona wote walio karibu nawe kwa macho ya upendo na heshima, au unaona tu kile wanacho au hawana?

Neno Ministry -Tz
Mwl.Samuel A.Mwakatajila
© January 2026



🌱 TENDO LIGUSALO HISI ZA MTU 🌱Kulikuwa na watu wawili ambao japo walikuwa juu ya uso wa nchi lakini walishi dunia mbili ...
16/01/2026

🌱 TENDO LIGUSALO HISI ZA MTU 🌱
Kulikuwa na watu wawili ambao japo walikuwa juu ya uso wa nchi lakini walishi dunia mbili tofauti kabisa.

Mmoja aliitwa Mwalinyasyo – tajiri, mwenye mali nyingi, lakini moyo wake haukuwa na nafasi ya kumsikiliza Mungu. K**a ilivyoandikwa katika Mithali 18:11 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni k**a ukuta mrefu katika mawazo yake. Mwingine aliitwa Kisoti – kijana maskini sana, asiye na kitu cha kujivunia isipokuwa upendo wake kwa Mungu na kwa watu.

Kisoti alikuwa mgeni wa kudumu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu. Hakwenda huko kwa sababu ya kamera, wala kwa sifa. Alienda kwa sababu ya moyo. Aliwaombea watoto, aliimba nao nyimbo za kumsifu Mungu, na aliwafundisha kuwa thamani yao haipungui kwa sababu ya hali yao.
“Bwana yu karibu na waliovunjika moyo.” (Zaburi 34:18)

Siku moja, akiwa katikati ya watoto hao, wazo zito likamgonga moyo wake:
“Laiti watoto hawa wangekuwa na baiskeli za walemavu, wangetabasamu zaidi, wangetembea kwa uhuru zaidi.”
Lakini mara moja akakumbuka ukweli mchungu — umasikini wake. Alikuwa na nia, lakini hakuwa na uwezo.
Usiku ule hakutaka akitafakari na kuomba Mungu ameonyeshwa njia.Akitafakari kwa muda mrefu, na mwisho akapata wazo kumwendea rafiki yake tajiri,

Alipofika kwa Mwalinyasyo.
Kwa unyenyekevu akasema:
“Rafiki yangu, moyo wangu unatamani jambo moja tu… je, waweza kunisaidia?”
Mwalinyasyo akajibu kwa mzaha:
“Usiniambie tena habari za Mungu, nilishakuambia sitaki kusikia.”
Kisoti akatabasamu kwa utulivu:
“Sio habari za Mungu leo. Naomba msaada wa viti na baiskeli za walemavu 100.”
Tajiri akacheka kwa sauti:
“Basi sawa, nitakusaidia. Lakini acha hayo mambo ya Mungu, nianzishe biashara kwanza.”
Kisoti hakubishana. Alishukuru.
Kwa sababu upendo haubishani, upendo hutenda na kuvumilia.
“Upendo huvumilia yote.” (1 Wakorintho 13:7)

Tajiri Mwalinyasyo akafanya haraka kuagiza Mzigo, mzigo ukafika bandarini DSM, Mwalunyasyo akambidhi Kisoti. Kisoti alimshutumu Mwalunyasyo na kusema naomba pia unisindikeze kwa watoto hawa, wewe ndiye atakaye kabidhi zawadi hizi kwa watoto hawa.
Siku ya kukabidhi zawadi ikafika.
Mwalinyasyo, kwa mara ya kwanza, akaingia katika kituo cha watoto walemavu.
Walipoingia tu. Watoto walipomuona Kisoti walimkubalia na kumkumbatia wengine wakimbuzi kisoti mikono yake huku wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu kwa furaha kuu.

Mwalunyasyo alisimama pale… akashangaa.
Watoto walikuwa wanacheka, wanaimba nyimbo za kumsifu Mungu, wakimkumbatia Kisoti kana kwamba ni ndugu yao wa damu. Hakukuwa na unafiki, hakukuwa na maigizo — palikuwa na furaha ya kweli.
Kisoti akawatuliza watoto na kusema:
“Leo, kila mmoja wenu atapokea zawadi ya baiskeli.”
Furaha ikalipuka tena. Nderemo, vifijo, machozi ya shukranivilitawala eneo lote la kituo.
Kisha Kisoti akaongeza kwa sauti ya upole lakini yenye uzito:
“Sio mimi nimenunua hizi zawadi. Mimi sina uwezo. Ashukuriwe Mungu, aliyempa mtumishi wake huyu mali, si kwa kujisitiri, bali kwa kuleta furaha kwa wengine.”
“Kwa maana kila mmoja amepewa kwa faida ya wote.” (1 Wakorintho 12:7)
Leo mtu huyu ametusaidia sisi pale mkono wetu hauwezi kuguswa , nasi kesho utamsaidia yeye pale mkono wake hauwezi kuguswa kwa njia hoi furaha yetu sote htumilika kwa maana Mungu aliumba ili tupate kuhitajikana. Amini nawaambieni hakuna hata mmoja wetu anaye kutosheleza kwa kila kitu.
Watoto walilia — si kwa huzuni, bali kwa kuguswa moyo na maneno ya Kisoti.

Mtoto mmoja akasimama na kusema:
“Nilidhani matajiri wanajali pesa zao tu. Leo nimeona upendo. Mtazamo wangu umebadilikakuhsu matajiri.”
Mwalinyasyo hakujua k**a anaota au yuko macho.
Alipoitwa kugawa zawadi, machozi yakamtoka. Akasema:
“Hakika Mungu anawapenda ninyi. Tunasikia wito wa kusaidia, lakini mioyo yetu huwa migumu. Sisi tuliojariwa uwezo lakini hata hatujui kwa nini tumeshakuwa uwezo, kwa sababu hoi tumejikita tunatumia kile tumejaliwa kwa vitu visivyo na maana.”
Watoto wakaimba kwa sauti:
“Mungu awasamehe nyote maana Mungu wetu humsamehe uovu.”
Walipokuwa wakiondoka, mtoto mmoja alimshika mguu Mwalinyasyo na kusema:
“Naomba uniambie jina lako. Nikifika mbinguni, nitakutafuta. Nataka uwe rafiki yangu milele.”
Njiani, Mwalinyasyo akamwambia Kisoti kwa sauti ya kunyenyekea:
“Nibatize. Nataka kuijua furaha hii. Nataka moyo wangu ubadilike.”
Tangu siku hiyo, Mwalinyasyo akawa mfadhili wa kituo kile.
Sio kwa kulazimishwa.
Bali kwa injili iliyohubiriwa kwa vitendo.
“Kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula.” (Mathayo 25:35)

📌 FUNZO LA MAISHA
Ziko njia nyingi za kuhubiri injili.
Wakati mwingine mikono husema zaidi kuliko midomo.
Usimzuie mtu kutoa, hata k**a haamini k**a wewe.
Mwelekeze mahali sahihi pa kutoa— Mungu atafanya yaliyobaki.Nami nataka kukuambia kuna madhabahu iliyo hai katika kutoa sadaka zinazo visa maisha ya mtu binafsi hawa wahitaji wa kweli, Yesu ametufundisha hili kuptia
Mfano wa Msamaria Mwema (Luka 10:33–37)
❤️ Injili inayogusa maisha ndiyo injili inayoacha alama.

Na Mwl. Samuel A.Mwakatajila.

Neno Ministry
© January 16 2026

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026Kutoka kwa:Mwl. Mr & Mrs. Samuel A. MwakatajilaKwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakat...
01/01/2026

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026

Kutoka kwa:
Mwl. Mr & Mrs. Samuel A. Mwakatajila

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
Tunawasalimu wapendwa wote katika upendo wa Kristo Yesu.
Heri ya Mwaka Mpya! Tunamshukuru Mungu kwa ulinzi wake katika mwaka uliopita na kwa neema ya kutuvusha kuingia katika mwaka mpya wa matumaini, urejesho na mwanzo mpya.

“Hata hivyo fadhili za Bwana hazikomi, rehema zake hazina mwisho; ni mpya kila asubuhi.”
— Maombolezo 3:22–23

Mpendwa wetu tunapukaribisha mwaka 2026 tunapenda kukuhirikisha haya machache ambayo Roho wa Bwana amesema nasi katika safari ya kuelekea mwaka 2026. ametushirikisha juu ya HiTORIA

Ni jambo la kweli na la msingi kwamba hakuna mwanadamu asiye na historia. Hatuiombi historia ije, bali tunajikuta tumeibeba. Historia ni sehemu ya maisha, iwe ni ya furaha au ya huzuni, ushindi au maumivu.

Pengine unajiuliza: Historia ni nini?
Kwa ufafanuzi rahisi, historia ni mkusanyiko wa matukio ya maisha yaliyopita—maamuzi, makosa, majeraha, baraka, na mazingira yaliyotujenga au kutuumiza.

“Kumbuka siku za zamani, zitafakari miaka ya vizazi vingi.”
— Kumbukumbu la Torati 32:7

Cha kushangaza zaidi, hata jina la mtu linaweza kubeba historia, na mara nyingi historia huwa na tabia ya kujirudia kutoka kizazi hadi kizazi (Kutoka 20:5). Huzuni huwa nzito zaidi pale historia ya mtu au familia imejaa maumivu, kwa sababu maumivu huanza kuonekana k**a sehemu ya kawaida ya maisha.

Kwa maneno mengine, historia inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika maisha ya kila siku—kiroho na kimwili. Hebu tulitazame jambo hili kwa mwanga wa Biblia.

HISTORIA KATIKA NURU YA BIBLIA

1. Historia ya familia: Kisa cha Yakobo

Tunaposoma habari za Yakobo, tunaona wazi namna historia ya familia ilivyokuwa kikwazo katika safari yake ya kupata mke aliyempenda (Mwanzo 29:25–26). Badala ya Raheli, alipewa Lea, kwa sababu ya desturi na historia ya familia:

“Haitendeki hivyo kwetu, kumpa mdogo kabla ya mkubwa.”
— Mwanzo 29:26

Hapa tunaona wazi kuwa historia ya familia ilimkwamisha Yakobo, hata katika jambo la msingi k**a ndoa.

👉 Hili si simulizi la kale tu. Hata leo:

Kuna familia zenye historia ya uchawi au migogoro

Kuna makabila yenye historia zinazowatisha wengine

Kuna mabinti na vijana waliokosa kuoa au kuolewa si kwa sababu hawakupendwa, bali kwa sababu ya historia ya familia

2. Historia inayohama kupitia jina

Biblia inatupa taswira ya kushangaza kuhusu majina. Jina linaweza kubeba kumbukumbu na tabia.

Kwa mfano jina Yuda:

Yuda mwana wa Yakobo alihusishwa na tamaa ya mali (Mwanzo 37:26–27)

Yuda Iskariote alimsaliti Yesu kwa fedha (Mathayo 26:14–15)

Hii haimaanishi kila aitwaye Yuda ni msaliti, bali inatufundisha kwamba historia inaweza kujificha hata katika majina, na bila Mungu kuingilia kati, historia inaweza kujirudia.

“Jina jema lapasa kuchaguliwa kuliko mali nyingi.”
— Mithali 22:1

3. Historia ya eneo: Kisa cha Nazareth

Nazareth ni mji aliokulia na kuzaliwa Yesu Kristo. Hata hivyo, jamii ilishangaa:

“Je, jambo jema laweza kutoka Bethlehemu?”
— Yohana 1:46

Hii inaonyesha kuwa mji huu ulikuwa na historia isiyotegemewa. Lakini Mungu akachagua eneo hilo hilo kuleta Mwokozi wa ulimwengu.

👉 Hili linatufundisha kuwa:

Eneo linaweza kuwa na historia mbaya, na k**a unafuatilia kwa ukaribu masomo yahusuyo ardhi na vitu vilivyo bebwa na a arithi ya mji huo utaelewa kuwa uko uhusiano kati ya mji na wakaazi wa mji huo.

Hata katika maisha haya hatushangai kuona kiongozi wa nchi ametoka eneo fulani, lakini kuna maeneo likitajwa tunajua hakuna kitu huko.

Lakini Mungu anaweza kubadilisha taswira ya eneo hilo

4. Historia ya mtu binafsi: Gideoni na Sauli

Gideoni

Gideoni alijiona mdogo kwa sababu ya historia ya familia yake:

“Kabila langu ni maskini zaidi… nami ndimi mdogo kuliko wote.”
— Waamuzi 6:15

Lakini Mungu alimwita:

“Bwana yu pamoja nawe, wewe shujaa hodari.”
— Waamuzi 6:12

K**a Mungu asingeingilia kati, Gideoni angepoteza fursa ya maisha yake.

Sauli (Paulo)

Baada ya kuokoka, kanisa lilimkimbia Sauli kwa sababu ya historia yake ya mateso:

“Wote wakamwogopa, wasiamini ya kwamba ni mwanafunzi.”
— Matendo 9:26

Ni mpaka Mungu aliingilia kati kupitia kwa mtumishi wake Barnaba ndipo huduma ya Paulo ilipata nafasi (Matendo 9:27).

👉 Hapa tunaona ukweli mmoja:
Historia inaweza kuwa kikwazo hata baada ya toba, k**a Mungu hakuingilia kati itakusumbua.

HISTORIA NA MAISHA YA SASA

Mpendwa, mifano ni mingi, lakini somo ni moja:
👉 Moja ya maadui wakubwa wa mafanikio ya kiroho na kimwili ni matukio ya historia ya maisha yako.

Mara nyingi, unapokaribia kuinuliwa, adui huitumia historian yako kukukwamisha

Biblia inamwita shetani:

“Msh*taki wa ndugu zetu.”
— Ufunuo 12:10

👉 Shetani hamsh*taki mtu asiye na hatima.
👉 Historia yako ndiyo ushahidi anaoutumia kukuzuia usiinuliwe.

Mfano wa Biblia – Kuhani Yoshua:

“Kuhani Yoshua alikuwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili amsh*taki.”
— Zekaria 3:1

Yoshua alikuwa:

Tayari kwa nafasi mpya

Tayari kwa huduma mpya
Lakini historia yake (mavazi machafu) ilitumika kumzuia.

Mungu hakubishana na Shetani kwa hoja juu ya HiTORIA hiyo, bali alimletea:

“Ondoleeni mavazi machafu.”
— Zekaria 3:4

👉 Hii inatufundisha kuwa:

Historia lazima iondolewe kabla ya kuinuliwa na si jambo mepesi kujitetea mwenyewe juu ya kikwazo vya histori maana ni ushahidi halali wa matendo yako, unamwitaji Yesu akusaidie

Mungu mwenyewe ndiye anayeondoa historia, si juhudi za mtu.

Wakati Mungu anakuinua, si shetani pekee anayekumbuka historia yako, bali hata wanadamu.

Mfano – Yesu Kristo:

“Je, huyu si mwana wa seremala? Tunamjua baba yake na mama yake.”
— Mathayo 13:55–57

Walimkataa Yesu si kwa sababu hakuwa na mafuta, bali kwa sababu:
👉 Walijua historia yake ya kimwili

Hata Biblia inasema:

“Hawakupata kuamwai.”
— Mathayo 13:58

👉 Kuna watu leo:

Hawawezi kukukubali k**a mchungaji kwa sababu wanajua jana yako

Hawawezi kukuona k**a kiongozi kwa sababu wanakumbuka makosa yako

Hawawezi kukuamini kwa sababu wanajua ulipotoka.

Ni historian ya nabii ndio humfanya nabii alitambulika e katika mji wake mwenyewe

Watu wengi leo hawajazuiliwa na watu, bali wamefungwa na sauti ya historia ndani yao.
Unajiona mdogo, dhaifu, hustahili—si kwa sababu ni kweli, bali kwa sababu historia imekufundisha hivyo.

“K**a mtu ajifikiriavyo moyoni mwake, ndivyo alivyo.”
— Mithali 23:7
HABARI NJEMA: MUNGU ANAWEZA KUBADILI HISTORIA YAKO.

Hatufahamu historia yako:

Ya ujana, Ya ndoa ,ya a jina lako, ya familia au eneo lako

Lakini tunamfahamu jambo moja kubwa kuwa Mungu hubadili histori za watu wake:

Isaya 43:19
“Angalia, nafanya jambo jipya; sasa linachipuka, je, hamlitambui? Nitaweka njia katika nyika, na mito jangwani.”

Alibadilisha:

Historia ya Gideoni aliye kutoka kabila masikini akawa mtu mkuu

Historia ya Bethlehemu, mji ulio dharauliwa ukawa ndio mkiwaalikozaliwa nasihi.

Historia ya Yabesi aliyelia kwa Mungu

“Ee Bwana, unibariki kweli, uipanue mipaka yangu.”
— 1 Mambo ya Nyakati 4:9–10

Mwaka huu mpya ni mwaka wa tumaini.
Ni mwaka wa kufutwa kwa historia mbaya.
Ni mwaka wa kuumbwa kwa jambo jipya.

“Angalia, nafanya jambo jipya.”
— Isaya 43:19
Mungu hana kuja kusahau, unapaswa jambo moja tu kumligna Mungu wako k**a alivyofanya Yabesi

Jambo moja muhimu saanà ni uwà mwagalifu sana vile unaishi leo kwa sababu leo ndio inajenga histori yako ya kesho

Tunataka kuomba pamoja nawe sasa k**a uko tayari, tuombe:

Ee Baba wa mbinguni,
Kwa jina la Yesu Kristo, tunakushukuru kwa maisha ya kila msomaji wa ujumbe huu.
Katika mwaka huu mpya, tunakuomba uingilie kati.

Bwana:

Futa historia ya maumivu

Vunja minyororo ya yaliyopita

Badilisha kumbukumbu za machozi kuwa ushuhuda

Uandike historia mpya ya baraka, neema na ushindi

“Nitawarejeshea miaka iliyoliwa na nzige.”
— Yoeli 2:25

Tunatangaza kwamba:
Historia mbaya haitatawala tena.
Neema yako itatawala.

Tunaomba haya kwa imani,
Kwa jina la Baba, la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Amina.

Na Mwl.Mr&Mrs Samuel A Mwakatajila
Neno Ministry
Januari 1 2026

Address

Mabibo Garage, , P. O. Box 7583
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Neno Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share