Ufalme Wa Mungu Hutekwa Na Wenye Nguvu

Ufalme Wa Mungu Hutekwa Na Wenye Nguvu Tunatakiwa kuutafuta ufalme wa MUNGU kwa nguvu na kwa akili nakwa mali zetu nzote

09/06/2017
24/05/2017

Bwana Mungu Ndie Kiongozi Wa Maisha Yetu Kwa Kua Hutuongoza Kwa Kila Jambo Hutulinda Na Kila Matatizo Na Shida Na Majanga Na Kila Adha Na Huweza Kila Jambo Kwani Jambo Gani Asilo Liweza, Amen!

22/05/2017

Mpende Jirani Yako K**a Nafsi Yako Inamaana Gani? Inamaana mtendee binadam mwenzako k**a wewe unavyotaka utendewe Tunaposema jirani haimanishi ni yule unaeishi nae jirani tu hapana ila ni kila binadam mwenzio unaekutana nae iwe njiani ama popote anapohitaji msaada wako msaidie usimpite na huo ndio upendo Amen! Na Mungu Akubari Msomaji Wangu

Watu wa MUNGU shida siyo kuamini  na kujua kuwa MUNGU  yupo la ila shida ni kumwamini, Yeye mwenyewe na kazi zake anazot...
26/01/2017

Watu wa MUNGU shida siyo kuamini na kujua kuwa MUNGU yupo la ila shida ni kumwamini, Yeye mwenyewe na kazi zake anazotenda kwetu na hapa wengi huwa tunajua kuwa ni utani ama ni ushilikina ama ni usanii tu wa watumishi wa MUNGU na waumini
Lakini mi nakwambia hivi ingia mwenyewe uone ukubwa na uzuri wake na jinsi anavyotenda kazi ili uhakiki mwenyewe
angalizo usije kujaribu tia nia yaani amini tu maana MUNGU huwa hajaribiwi hata kidogo maana Yeye huangalia moyo nasio mwili

22/01/2017

Ukowapi ule upendo wa kwanza kanisa lilikuwa linapendana na kushilikiana kwa mambo yote ikiwemo kuhakikisha INJILI inasonga mbele kwa kualikana kwenye mikutano pamoja na kutembeleana kwa makanisa?
K**a kanisa linatawaliwa naubinafsi tunadhani tunalipeleka wapi kwa kuwafundisha waumini kuamini vitu ambavyo hata havina mashiko kwao
Tunatakiwa kuhubili upendo na kulifanya kanisa liwe na upendo k**a MUNGU mwenyewe alivyo pendo kwa watu wote
Tusibaguwane na kuonekana kuwa kanisa lako ndo linalompenda MUNGU kuliko kanisa la mtu mwingine turudi kwenye upendo k**a walivyofanya waasisi wetu walioanzisha kanisa kwa ushiliano yani MUNGU BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kwa kifupi BWANA YESU KRISTO
AMINA ukisoma ujumbe huu msilikishe mwenzako nae ausome

21/01/2017

Inasikitisha sana pale tunapoona mahubili ama mafundisho ya sasa haiendi sawasawa na na imani husika tumekua tukiamini vitu kuliko MUNGU jamani9 tunaenda wapi na kwanini? Tulijenge kanisa katika kumjua MUNGU nasio kuzijua baraka zake tu kwani imeandikwa "mtafuteni kwanza ufalme wa MUNGU na hayo mengine mtazidishiwa";
Lakini sasa ni tofauti tunatafuta baraka alafu ndo tumate MUNGU, siyo hivyo soma biblia utajua inataka nini ufanye na ili kumuona MUNGU na baraka zake usikubari kunyonywa Roho na mafundisho manyonge
By mwl Hezekia Sanawa

21/12/2016

like ukurasa huu kupata masomo haya na kushea baada ya kusoma

21/12/2016

ili kupata masomo haya like page hii na kushea barikiwa

20/12/2016

NGUGU MPENDWA WETU TUNAENDELEA NA SOMO LETU LEO TUKIWA TUNAITAZAMIA IMANI

Tuliona kuwa imani ndicho kiunganisho cha mawazo yetu na nguvu kuu yani MUNGU napenda kukupa mfano wa mtu mmoja anaeitwa Ibrahim ambaye ndiye Baba wa imani
Ibrahim anakuwaje Baba wa imani , ni kwasababu alionesha kuamini kuwa MUNGU peke yake ndiye anayeweza kuaminika katika maisha yake na siyo mwanadam
Lakini tunaona kwa kumwamini MUNGU IBRAHIM alifanikiwa na akawa na mali nyingik**a mavumbiya nchi (mwanzo 13;18)


Kwa imani hiyo hiyo tunaona vitu vikizaliwa katika akili zetu na kuzaa matunda na pia hua halisi baada ya kufikiri na kuamini chukua hatua ya kuamini nawe utaona vitu vikizaliwa maishani mwako maana kila mtu ni nabii wa maisha yake

Tunawezaje kutunza imani zetu

1 kutokubali mtu akukatishe tamaa, hapa wengi huwa hatukifikii kile tunachokiami kwa sababu ya kukubali katishwa tamaa na watu ambao eidha hawataki kuona tunafanikiwa ama watu ambao hawaamini katika kuamini

2 kuwa mwaminifu mbele za MUNGU yule anayekupa kulingana na imani yako, Nilazima kuwa mwaminifu kwa yote akutendeayo MUNGU na watu pia wanaokuzunguka

3 kutokuketi watu wenye mizaha wanaopenda utaniutani kwa imani yako na kukushusha kwenye imani yako

4 Lakini pia tengeneza mahusiano mazuri na MUNGU Kkwa kuhudhulia katika ibaada n akusoma vitabu vitakatifu itakufanya kuongeza kiwago chako cha IMANI

5 Usiwe mtu wa kufuata mkumbo simama kwa kitu unachokiamini, Maana hapa watu wengu huwa wanatafuta mafanikio kwa kufuata mkumbo inatufanya tusifanikiwe maana siyo stahiki yetu fuata moyo wako unavyo kushudia


AHSANTENI SANA NA MUNGU AWABALIKI SANA

15/12/2016

SHALOM NDUGU MSOMAJI WANGU
Leo tunaendelea na somo letu la IMANI ambalo tulilianza wiki iliyopita, hata hivyo naomba radhi kwa kwa kuchelewesha mwendelezo wake

KAZI YA IMANI AMA JINSI YA KUTENDA KAZI KWA IMANI

1 Imani ni suluhisho la peponi ambalo hutoa uhai, nguvu na vitendo kwa msukumo wa fikra

2 2 Imani pia ndiyo mwanzo wa malimbikizo yote mafanikio ya mtu na kila kitu anachokitaka ama alicho nacho maana kila kitu huanza kwa imani alafu kinakuwa katika uhalisia

3 Lakini pia imani ndio msingi wa miujiza na maajabu yote ambayo hayawezi kuchanganuliwa kwa kanuni za kisayansi
(mathayo 8;5-13)

4 Pia imani ni kiasili ama kemikali ambayo ikichanganywa na maombi humpa mtu mawasiliano ya moja kwa moja na nguvu kuu ya asili (MUNGU) (1 WAFALME18 ; 1-46)

5 Vile vile imani ni kiungo kinachobadilisha mtetemo wa kawaida wa fikra za mtu, unaotengenezwa na akili ya kawaida ya mtu kwaenda katika hali ya kiroho iliyokuwa na ukubwa sawasawa na imani yake aliyonayo,.

6 Imani ndiye wakala pekee ambaye kupitia kwake nguvu kuu zisizo za kawaida na zisizokuwa na mwisho (MUNGU) zinaweza kuvunwa na kutumiwa.

IMANI INAHITAJI VITU VIFUATAVYO KULETA MATUNDA

1 Kwa shauku uliyo nayo akilini mwako, hii hukufanya kuona kua imani uliyonayo kuwa inaishi na ipo siku kila kitu kitakua sawa

2 Uvumilivu ulionao katika hali unayo kutana nayo, Hapa wengi huwa tunaiacha imani tuliyonayo kwa kuona tumechelewa na kufuata ama kutafuta upande wa pili ambao ni lahisi kwetu na mwisho wake kupoteza kila kitu
Ukikutana na hali ngumu usikimbie imani uliyo nayo baali pigania imani yko hakika utaona matunda yeke

3 Lakini pia kuwa mbunifu kwa ili kuijega imani yako kwa kutafuta maarifa mapya kwa kuipanua zaidi na zaidi soma vitabu vitakatifu vinavyojenga imani

AMINA MPENDWA KWA LEO TUFIKIE HAPA KESHO TUTAENDLEA NA SOMO LETU BADO LINAENDELEA

KUWA NA IMANI   Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo/ Kuwa na uhakika na mambo yele yasiyoonekana kwa macho ya ...
08/12/2016

KUWA NA IMANI

Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo/ Kuwa na uhakika na mambo yele yasiyoonekana kwa macho ya nyama ama mwili na kuamini kuwa yamekwisha kua hai
Na imani ndiye mkemia mkuu wa akili yako na mawazo yako maana kila kitu huanza na kuamini.
Imani ikichnganywa na msisimko ama mtetemo wa fikra ama akili ya ndani huwa inachukua msisimko na kutafsiri na kua katika kipimo cha imani na kusafirisha kwenda kwenye nguvu kuu isiyo ya kawaida (MUNGU)

Lakini pia imani ndio nguvu ama mfumo wa pekee wenye uwezo uwezo wa kuwasiliana na nguvu kuu yaani MUNGU

(MATHAYO 17;20)YESU akawambia, kwa sababu ya upungufu wa imani yenu, Kwa maana, nawaambia mkiwa na imani kiasi cha punje ya haladali mtauambia mlima huu, ondoka hapa uende kule nao utaondoka; wala halitakuwepo neno lisilowezekana kwenu 21 (lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga)

JINSI YA KUJENGA IMANI
1 Tunaweza kujenga imani kwa kusali na kufunga
Hii inaonesha kuwa ukotayari kujitoa mwili wako kwa kile unacho kitafuta katika akili yako ya ndani

2 Tunajenga imani kwa kanuni ya kujishauri binafsi
Hii inatokana na kujiuliza maswali kwa kuyarudiarudia mara kwa mara

3 Kwa kurudiarudia jambo unarolihitaji
Hii pia husaidia katika kuuijenga imani katika akili yako ya ndani namaanisha yule mtu wa ndani anakuwa anajenga uhalisia wa kile kitu anachokihitaji kukiona kwa macho ya uhalisia

4 Kutafakari ama kufikilia kwa undani
Hii humfanya mtu kuchukua mda kwa kuliwazia analolikusudia na kulijengea picha na muonekano wake halisi

AMINA
HII SILABASI YA IMANI NI PANA SANA BADO TUNAENDELEA KESHO KUZIJUA KAZI ZA IMANI NA UTENDAJIKAZI WAKE
USIACHE KUFUNGUA UKURASA HUNA NA KU-SHARE NA RAFIKI YAKO NAE APATE HAYA MAARIFA

" AHSANTENI NA TUONANE KESHO"

Address

Pugu Kigogo Fresh
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufalme Wa Mungu Hutekwa Na Wenye Nguvu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ufalme Wa Mungu Hutekwa Na Wenye Nguvu:

Share