FPCT Guluka Kwalala

FPCT Guluka Kwalala Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from FPCT Guluka Kwalala, Religious organisation, Dar es Salaam.

RATIBA ZETU:
Jumatano: Mafundisho (Saa 10:00-11:30 Jioni)
Ijumaa: Maombi & Maombezi
Saa 4:00 Asubuhi - 9:00 Alasiri
Jumapili: Saa 3:30 Asubuhi - 6:30 Mchana

05/09/2026
Leo katika ibada tulitembelewa na uongozi wa HUIMA kutoka kanisa la FPCT Manzese. Pichani ni ndugu Shimrod Jiste (mwenye...
30/08/2026

Leo katika ibada tulitembelewa na uongozi wa HUIMA kutoka kanisa la FPCT Manzese. Pichani ni ndugu Shimrod Jiste (mwenye suti ya Navy blue) - Katibu na ndugu Paul Fanuel - mjumbe wa k**ati tendaji.

Ujio wao ilikuwa ni kuhamasisha vijana juu ya mkesha wa vijana utakaofanyika siku za usoni.

Hakika tulifurahi kuabudu pamoja nao.

PICHANI: MAHUBIRI YA NENO LA MUNGU Waumini wakifuatilia kwa makini na kwa karibu, mahubiri ya Neno la Mungu katika ibada...
30/08/2026

PICHANI: MAHUBIRI YA NENO LA MUNGU

Waumini wakifuatilia kwa makini na kwa karibu, mahubiri ya Neno la Mungu katika ibada ya jumapili ya leo.

Mungu akubariki wewe uliyehudhuria ibada ya leo. Ni imani yetu kwamba hukuondoka k**a ulivyokuja.

Mahubiri ya Neno la Mungu kupitia Mchungaji kiongozi Philipo Mdaraga. Ujumbe usemao "KUGUSA VAZI LA YESU ILI KUPATA UZIM...
30/08/2026

Mahubiri ya Neno la Mungu kupitia Mchungaji kiongozi Philipo Mdaraga. Ujumbe usemao "KUGUSA VAZI LA YESU ILI KUPATA UZIMA". Kutazama mahubiri yote tafadhali tafuta (search) katika ukurasa huu huu au nenda YouTube kwenye channel yetu ya FPCT Guluka Kwalala.

Tunaomba radhi kwa usikivu usio mzuri katika video zetu, ni nje ya uwezo wetu na tunaendelea kufanya maboresho.

Mungu akubariki sana!

30/08/2026

Karibu kutazama na kufuatilia mahubiri ya Neno la Mungu pamoja na maombi na maombezi katika ibada ya Jumapili ya leo mbashara kutoka hapa FPCT Guluka Kwalala.

Leo ni Jumapili ya mwisho wa mwezi na Mungu anao ujumbe kwa ajili yako. Ubarikiwe usikilizapo na kutazama.

Usiache kutupa maoni yako unatufuatilia kutoka wapi. Mungu akubariki sana!

UTAABUDU WAPI JUMAPILI YA KESHO?Karibu sehemu sahihi, anapoabudiwa Mungu wa mbinguni katika viwango vikubwa na Neno lake...
29/08/2026

UTAABUDU WAPI JUMAPILI YA KESHO?

Karibu sehemu sahihi, anapoabudiwa Mungu wa mbinguni katika viwango vikubwa na Neno lake likihubiriwa bila kughoshiwa.

Mungu akuongoze ufike tuabudu pamoja, ni Jumapili ya mwisho wa mwezi Agosti, tukamtake BWANA na nguvu zake.

Mungu akubariki sana.

Kanisa linapatikana Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, kata ya Gongo la Mboto kitongoji cha Mwisho wa lami karibu na shule ya Highmount.

28/08/2026

Karibu kusikiliza na kutazama mahubiri ya Neno la Mungu pamoja na Maombi na Maombezi ya ibada ya Jumapili ya Agosti 23, 2026. Mhubiri alikuwa mwinjilisti Shukrani Lugomoka Shukrani Lugomoka na ujumbe uliosema "KATIKATI NA MOTO MKALI MUNGU ANASIMAMA KUKUTETEA".

Tuachie maoni unabarikiwa kutoka wapi.

Asante sana

HABARI-PICHAIlivyokuwa ibada ya leo Jumapili Agosti 23, 2026. Tumemuona Mungu akitenda matendo makuu katikati ya watu wa...
23/08/2026

HABARI-PICHA

Ilivyokuwa ibada ya leo Jumapili Agosti 23, 2026. Tumemuona Mungu akitenda matendo makuu katikati ya watu wake.

Karibu tena katika ibada zetu zinazoendelea katikati mwa wiki:
1. Jumatano - Mafundisho - Saa 10 Jioni hadi 11:30
2. Ijumaa - Maombi na Maombezi - Saa 4:00 Asubuhi hadi saa 9 Alasiri

Siku ya Jumapili ibada ni moja tu na inaanza saa 3:30 Asubuhi hadi saa sita na nusu mchana.

Kanisa letu linapatikana Mwisho wa lami (ya Gongo la Mboto) - Jijini Dar es Salaam, jirani na shule ya Highmount.

Mungu akubariki sana.

📸 Festus MP Media Unit

MAHUBIRI YA NENO LA MUNGU Siku ya leo tumehudumiwa Neno la Mungu na mwinjilisti Shukrani Lugomoka Shukrani Lugomoka  Na ...
23/08/2026

MAHUBIRI YA NENO LA MUNGU

Siku ya leo tumehudumiwa Neno la Mungu na mwinjilisti Shukrani Lugomoka Shukrani Lugomoka Na ujumbe iliokuwa ukisema "KATIKATI YA MOTO MKALI, MUNGU ANASIMAMA KUKUTETEA".

Hakika ilikuwa ni ibada ya moto 🔥 mkuu na mioyo yetu imejengwa kwa ujumbe huu wa kuponya na kuhuisha.

Mungu akubariki uliyehudhuria ibada ya leo.

Kwa wewe uliyepitwa, kaa karibu na ukurasa huu utapata kutazama na kusikiliza mahubiri hayo.

Mungu akubariki sana!

📸 Media unit

Karibu siku ya kesho mpendwa, Jumapili ya Agosti 23, 2026 katika ibada yetu tujumuike pamoja kumuabudu na kumsifu Mungu....
22/08/2026

Karibu siku ya kesho mpendwa, Jumapili ya Agosti 23, 2026 katika ibada yetu tujumuike pamoja kumuabudu na kumsifu Mungu. Njoo ukutane na Yesu ambaye kwake hakuna linaloshindikana.

Unateseka na dhambi? Huwezi kuacha mwenyewe bila nguvu ya Yesu!
Unateseka na magonjwa? Yupo Yesu aponyaye magonjwa YOTE.

Kanisa letu linapatikana Mwisho wa lami Gongo la Mboto jirani na shule ya Highmount.

Karibu sana na Mungu akubariki!

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255757867350

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FPCT Guluka Kwalala posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to FPCT Guluka Kwalala:

Shortcuts

Share