Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote

Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote "Nyumba Ya Sala Kwamataifa Yote" Inasaidia Watu kujifunza Neno la Mungu Nakupelekea Watu Kukua Kiroho na Kuweza Kuwa Walimu Wazuri wa Neno la Mungu

05/07/2024
12/06/2024

"MSINGI WA BWANA YESU"

“Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

— 1 Wakorintho 3:11 (Biblia Takatifu)

Bwana Yesu atukuzwe mtu wa Mungu

Upo msingi mmoja uliowekwa maishan mwetu nao ni wa wa Bwana Yesu, kuna misingi mingi imewekwa maishan mwetu ili itutoe kwenye njia ya Mungu, kwenye njia ya Baraka za Mungu, njia ya kumtumikia Mungu na njia mbalimbali zakumtafuta Mungu

Na katika hiyo misingi iliyowekwa imepelekea hata kukubali kuwa sisi ni wahivyo hivyo kwamba hatuwezi kutoka wala kushinda na imepelekea kuchoka na kurudi nyuma na kukata tamaa kabisa, Neno moja ulifahamu misingi yote iliyowekwa kwako ni batili

Msingi ni mmoja tu nao ndio halisi, msingi usio yumbishwa ni Bwana Yesu, kufa kwa Yesu nakufufuka ilikua ni kusimamisha msingi wake ambao katika huo sisi tunashinda zaid ya kushinda, Warumi 8:37

Kuna wakati macho yako yanafungwa yasione ukuu wa Mungu na ile nguvu iliyo ndani ya Yesu, 2Korinto 4:4, nikwambie shtuka na fungua macho na fahamu zako zitiwe nuru kwa jina la Yesu ili uione nuru na nguvu uliyonayo katika Kristo Yesu,

Mtu wa Mungu amka katika usingizi wa wafu, usingizi uliofunikiwa ili usijielewe, jitie nguvu katika Bwana na isimamishe akili yako kwa iman, Ushindi wetu na furaha yetu, aman yetu ipo kwa iman, anza kufurahia hayo katika Kristo Yesu ili uweze kuvuka hapo ulipo

Mkumbushe Mungu kwa maombi mazito, jitamkie kuinua msingi wa Kristo iliuweze kukushindia, sikia wakati mwingine umemuacha Mungu na kufuata njia zako kuliko pelekea Mungu kukuacha, sasa rudi kwa toba kisha rejesha nguvu ya msingi wa Mungu maishan mwako, kwenye hatua zako

Kumbuka Musa alipotupa fimbo mbele ya farao waganga nao wakatupa fimbo zao na kugeuka nyoka lakini fimbo ya Musa ilimeza vinyoka vyote vya waganga, vile vinyoka vya waganga ndio k**a vimsingi uchwala vilivyoweka na adui kwako lakini wewe unafimbo ya Musa ambayo ni Bwana Yesu hiyo ni msingi halisi usioyumbishwa hata, hivyo simama imara fungua akili yako kuona ukuu wa Mungu ulio ndani yako

Adui amechezea akili yako kuona kuwa wewe si kitu si chochote leo amka ona ukuu wa Mungu uliondani yako, mkumbushe Mungu na katika hilo usichoke, sema na Mungu kwa bidii usiku na mchana, sema na Mungu kila wakati, ujue anga, ardhi vimesemeshwa sana habari zako, sasa nawewe weka bidii kubatilisha vilivyosemeshwa humo kisha vitamkie ushindi, baraka na mpenyo, usikae kimya, usiishi kizembe utakufa kizembe wakati wewe ni shujaa wa Mungu, tumia ushujaa ulio ndani yako, kumbu kumbu 32:1

Hakuna msingi unaoweza kukuyumbisha kwakua Mungu wako nimkuu sana, acha kujichukulia poa, kukichukulia wakawaida, na kujichukulia dhaifu kwani umejengwa kwenye msingi imara na wa wapekee wa Yesu Kristo, Waefeso 2:20

Ninakuombea katika jina la Yesu ule msingi wa Kristo uliyojengwa kwako ukadhihilike na ukafumue kila msingi batili uliojengwa kwenye maisha yako ili ili usifanye yaliyo ya Mungu na usishinde vita zinazokukabili, wewe ni mbarikiwa, na nguvu ya baraka, nguvu ya ushindi ikakufunike na kukupigania katika jina la Yesu

Hatuendi kwa kuona tunakwenda kwa imani amini Mungu anakupigania na kukushindia, semesha moyon, semesha mazingira kuwa wewe ni mkuu, wewe ni mshindi, unafanikiwa tena kwakua Bwana Yesu yupo nawewe, warumi 8:31

Uinuliwe Kiroho na Bwana Yesu

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwa whatsup namba 0657 048393, kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
0657 048393
Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote

07/06/2024

TAMANI KUTUMIWA KWA VIWANGO

Luka 2:25-26
25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu

Natamani urudie kusoma hiyo mistari hapo juu uuone upekee, heshima na neema aliyopewa mtumishi wa Mungu Simeoni, mpaka kutolewa mfano, na kuwa sehemu ya kutufundisha katika kizazi na vizazi sio kawaida kunakitu kikubwa alichokua amefanya kipindi chote cha maisha yake

Maandiko yanatuambia Simeon alikua mtu mwenye haki, mcha Mungu, hakua mcha-Mungu wakubabaisha bali alidhamilia kwa dhati kuwa mchaji, aliacha vyote na kumfuata Mungu, aliachana na dunia alifuata kutenda ya Mungu kiasi cha kushuhudiwa na Roho mtakatifu kuwa hata kufa kabla hajamuona mwokozi wa ulimwengu Kristo Yesu

Simeoni anatufundisha tujitoe asilimia 100 kwa Mungu, jua liwake na mvua inyeshe tusimuache Bwana, ikimaanisha tupitapo katika hali zote za raha na maumivu tusimuache Mungu tumtegemee yeye tumuamini yeye tufanye yaliyo yake tu

Mtunga zaburi ya 37:5 anatuambia ‘Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.’, na anasema pia ‘Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.’, maana yake anataka tuzame kwake, tuzame ndani ya Roho mtakatifu ambae yeye ni kiongozi wetu, na yeye ndio nguvu yetu

Nikwambie Roho mtakatifu alimshuhudia Simeoni kuwa maono ya kumuona Kristo Yesu yatatimia, na ilimpasa Simeoni afanye bidii yakutunza yale maono, mtu wa Mungu haikua rahisi k**a unavyodhani, bali alijikana nakufuata maelekezo ya Roho mtakatifu, alikua ni msomi wa maandiko tunapata wapi kujua hayo, maandiko yanatuambia alikua mchaji, na mtu wa haki alijifunza kuishi katika haki na jinsi yakua mcha Mungu halisi

Injili ya Yohana mtakatifu mlango 4:23 unasema ‘Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu’ Ili uwe mcha Mungu halisi, mwabudu halisi inatakiwa uwe mtu wakujifunza sana Neno la Mungu na kutenda, kuyaishi yale unayo jifunza, unapofanya kila siku ndipo unapokuja kuwa jabali la rohon katika uchaji na kupitia hayo utatamani kuwatendea watu mema, kutenda katika haki kwenye jamii unayoishi

Kwenye jamii yako, familia yako, na nchi yako tafuta kuwa watofauti, tafuta kuwa mtu wa Baraka kwa Wengine, tafuta watu wajifunze ucha Mungu wako na mazuri unayo yafanya ili hata utakapo ondoka kwenye ulimwengu huu yawepo mengi mema yanayoishi na kuwabariki watu badala yako na hapo tutasema huyu mtu amelala mauti lakini kazi zake zinaishi

Ili uweze kuacha alama isiyofutika kwenye ulimwengu huu lazima ujikane, lazima ujitoe jumla kwa Bwana, maandiko yanatuambia katika Warumi 12:1-2 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Tunaonyeshwa mambo kadhaa kwenye hayo maandiko kuitoe miili yetu dhabihu kwa Bwana, kuishi kitakatifu, utakatifu unaozungumziwa hapo ni kujitenga na dhambi na mambo yasiyo faa mbele za Mungu, katika hayo ndipo kuna sehemu hautaweza kwenda ili kutunza uchaji ulio ndani yako, kuna mavazi hauta vaa kuendana na fasion ili kutunza uchaji wa rohoni, kwaujumla mtume Paulo anatuambia tusifuatishe namna ya dunia hii bali tugeuzwe kwa upya nia zetu katika Kristo,

Nia yamwili ni kutenda yasiyo faa mbele za Mungu lakini tunapaswa kuomba Nia zetu zigeuzwe zimtii Kristo na zitende yaki-Mungu{Ombea sana Nia yako} kwakua nia ndio inapelekea kuamua uishije na umfuate Mungu au laa

Mtu wa Mungu simeoni alimtafuta Mungu sana, nandie aliewekwa kuomba ili Bwana Yesu azaliwe, aliomba kuondoa vikwazo vitakavyozuia Kristo asizaliwe alikua yeye na Nabii mke Anna Binti Fanueli

Nikusihi na wewe mtu wa Mungu tamani kwa dhati kutumiwa na Mungu, na katika tamaa hizo tafuta kwabidii kuishi maisha matakatifu yanayo mpendeza Mungu, hata k**a akili na mwili havitaki lazimisha kumpenda Mungu na kufanya ya Ki-Mungu na kadiri unavyofanya ndivyo mabadiliko yanavyotokea katika maisha yako ambapo uchaji na haki vinadhihilika ndani yako

Ninakuombea badiliko kubwa na kuwa mtu wa viwango vyakuubadilisha ulimwengu katika jina la Yesu.

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwenye whatsup nambari ya +255 657 048393, Kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
+255 657 048393
Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote

06/06/2024

SIRI YA IMANI YENYE MATOKEO KWETU

“Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu."
— Yohana 3:18 (Biblia Takatifu)

“Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. ”
— 1 Yohana 4:9 (Biblia Takatifu)

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu

Imani yangu umejifunza sana maana ya iman, somo la leo limekuja kwako ili kukuonyesha thaman ya iman kuiweka katika matendo ili upate matokeo makubwa.

Maandiko yanaanza kutuambia amwaminiye yeye hahukumiwi, maana yake usipoamini hukumu yako unakua umesha ipokea, na hiyo hukumu haisubiri mpaka siku ya mwisho kule mbinguni hapana, utaanza kuiona hapa hapa dunian

Nikukumbushe tena wewe nibarozi wa Mungu hapa dunian maana yake unatakiwa ufanye yale yote uliyo agizwa na Mungu, usipofanya ndipo unapoanza kuona ugumu katika yale uyafanyayo

Imani haipo mwilin bali ipo rohon, na ili uweze kuishi kwa iman au ili uweze kuamini inatakiwa ubadilishe mfumo wako wa maisha, ubadilishe mtazamo wako, namaanisha ubadilishe jinsi yakutazama mambo, usiyaangalie mambo kwajinsi ya kawaida au k**a watu wengine wamataifa wanavyo yatazama bali inakupasa uyatazame mambo ki-mbingu,

Kutazama mambo ki-mbingu inamaanisha kuwa wengine watasema hapa haiwezekan wewe mtazamo wako utatazama kuwezekana, hapo kwenye kutazama akili yako, moyo wako, na fahamu zako zitaweka kwa Mungu kuwa inawezekana

Na kanuni ya Mungu ni kutaka kumtegemea yeye katika yale ambayo watu wanajua na wanadhani hayawezekeni katika hayo Mungu anataka kujifunua kupitia wewe kuwaonyesha watu yanawezekana, itajulikana kwakua wanaweza kuja kukuuliza na utawajibu kuwa ni Mungu alietenda ama watu wenyewe wataona automatically kuwa Mungu wako ni mkubwa, ila wengi wetu tumeshindwa kuwashuhudia watu kuwa tumepiganiwa na Mungu badala yake tumejipambanua kuwa akili zetu ndizo zilizo tuvusha, ikiwa nawewe upo kwenye kundi hilo la kusifia akili zako acha mara moja kwakua utamzua Mungu kufanya makubwa kwako, mara zote wewe Mtukuze Mungu.

Ninamfano mmoja niliowahi kuupata mahali, mwanajeshi mmoja alipewa funguo za gari bovu kambini kwao aliendeshe na lile gari lilikua limechakaa sana na kwakua walimlazimisha sana wakubwa zake ilibidi aende kuliendesha walimkebehi sana yule ndugu lakini alijitia ujasiri nakwenda kuliwasha, kwamuujiza wa Mungu na iman ya yule ndugu kwa Mungu alivyoweka funguo kwenye lile gari na kuliwasha gari ikawaka na kutembea wale waliomfanyia kebehi walinyamaza na kubaki wanashangaa

Sikia mtu wa Mungu kinachohitajika ni iman yako tu kwa Mungu, mengine yote muachie Mungu, anasema kila muombalo aminini mmesha pokea, acha kusikiliza sauti za kichwan kuwa haiwezekani wewe focus kuona inawezekana kule kuona inawezekana ndiko kunakuja kuzaa kuwezekana

Usiruhusu kutokuamini kutokuwezekana kutawale ndani yako na kutokuamini huwa kuna kuja na hofu ndani yako, kataa hofu weka ujasiri, weka kuwezekanika hata katika yale ambayo damu na nyama yanaonekana hayawezekaniki, na ukiweza kutune mtazamo wako kuona yote yanawezekana amini utakua umemshinda adui pakubwa kwakua yeye anachilia hofu na kutoamini ili usipokee baraka zako na kuuona uzuri wa Mungu

Weka iman yako kwa Bwana Yesu kwa jina lake na damu yake, unapolitamka na kuiachilia mahali fahamu kuwa vinakwenda kufanya kazi kwa ukubwa sana, kwakua Bwana Yesu aliachiliwa ulimwenguni kwaajili yetu na kwa faida yetu ili tuweze kumshinda adui na kurudisha nguvu ya utawala wetu katika ulimwengu huu

Sasa Mungu anapoona hatuoni ile thaman ya kumleta Bwana Yesu ndipo anaachilia hukumu juu yetu na kwenye mambo yetu tunayoyafanya, na anatuacha tuelekee kwenye njia tunazotaka sisi ambazo hazina usalama ndani yake, maandiko yako wako yanasema "“Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; Kumbukumbu la Torati 28:1" maana yake tusipoisikia na tusipofanya hukumu ii upande wetu, na kufanikiwa kuu mbali kwetu hivyo nakusihi mwamini Yesu Kristo na amini ile kazi aliyoifanya pale msalaban ni kubwa na inathaman na inanguvu kubwa ya kuleta matokeo mwilini ndipo utakapo uona uzuri na utamu wa Yesu.

Nakuombea kuumbika kwa iman thabiti ndani yako katika jina la Yesu

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwenye whatsup namba 0657 048393, Kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
0657 048393
Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote

05/06/2024

KUNA SABABU NYINGI ZA KUMSHUKURU MUNGU

Zaburi 92:1
Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.

Mtu wa Mungu

Bwana ni mwenye fadhili nimwingi wa rehema, anaetupigania kila iitwapo leo,hatuna budi kumshukuru yeye kwa matendo makuu na yaajabu,

Nikwambie mtu wa Mungu, tungetazama vile Mungu anavyotupigania, vile anavyotuongoza usiku na mchana tungetetemeka na tusingeacha kuimba sifa zake kila wakati,

Yeye anatufadhili kila leo, yeye anatubariki kila leo, unaweza ukaona giza katika hatua zako lakini unashangaa unalala na unaamka salama asubuhi ukiwa na afya sikia unawajibu wa kumshukuru Mungu mpendwa, Unawajibu wa kumtukuza na kumuinua Mungu katika kila hatua katika kila hali kila hatua,

Mtunga zaburi anatuambia ni neno jema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, shukuran zinamleta Mungu karibu, shukuran zinatuonyesha kwa Mungu kuwa tunajua uthaman wake, tunakumbuka kuwa ni yeye ndie kiongozi wetu hapa dunian

Nikukumbushe mtu wa Mungu sisi tu mabarozi wa Mungu katika dunia hii, tumeletwa na Mungu mwenyewe kufanya kusudi lake, na nikwambie tena hapo ulipo kuna kusudi kubwa unatakiwa ufanye, sasa huo uzima, hiyo afya nikwaneema za Mungu ili uweze kutimiza kusudi lake USIJISAHAU ukaishia kuponda raha na kufanya mambo yako yasio na utukufu wala faida mbele za Mungu na yasiyojenga ufalme wa Mungu



Katika shukuran utapokea maelekezo mapya kutoka kwa Mungu, katika shukuran utapokea nguvu mpya, nikuhakikishie katika shukuran utapata furaha na aman tele kwakua Mungu wetu anatutazama kipekee na anaona katika watu walio sahau ukuu wake na uweza wake wewe unaona na unathamini, uwepo wake lazima afanye kitu cha pekee kwako

Katika Zaburi 9:1 anatuambia “Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote, Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu, nimengi ambayo Mungu amekufanyia, na mengine unashindwa hata jinsi ya kuelezea, katika hayo Mungu anahitaji kupewa shukuran zako kila wakati na kila saa kwakua amekutetea na kukupigania ili yeye atukuzwe kwa watu kupitia wewe.

USIJISAHAU wala usichukulie kawaida upendo mkuu wa Mungu kwako, ona sababu ya kila wakati kumshukuru Mungu wetu kwa makuu anayokutendea na kukupigania.

Roho mtakatifu akakuguse na kuweka kiu ya shukuran ndani yako kila wakati

Neema ya Bwana Yesu isikupungukie katika jina la Yesu

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwenye whatsup namba 0657 048393, Kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
0657 048393
Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote

27/05/2024

SIRI YA KUMKIMBILIA BWANA

Zaburi 118:8-9
8 Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.

Zaburi 100:3
3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu

Kuna wakati inabidi tuzilazimishe fikra, fahamu, miili yetu kumtafuta Bwana, kuwekeza kusimama katika Mungu na kulazimisha kumpenda Mungu na kufanya yaliyo yake.

Ipo nguvu inayosukuma kukataa kumpenda Mungu na kukataa kujisogeza kwa Mungu, ikionyesha hakuna maana kukaa kumtafuta Mungu na kufanya yaliyo ya Mungu, nyakati hizi ni zauovu tusipokaa vizuri nakulazimisha kumtafuta Bwana na nguvu zake zitusaidie tutalia k**a yatima wakati sisi sio yatima tunae Mungu Baba atuwezeshae

Mtu wa Mungu ipo faida kubwa katika kumkimbilia Bwana kwakua yeye ndie ametuumba nayeye ndie mfadhili wetu katika ulimwengu huu Zaburi 117:2, Nikwambie mtu wa Mungu hakuna mtu atakae kuelewa katika ulimwengu huu, nikwambie hakuna k**a usipo amua kumtafuta Mungu kwa bidii, hakuna atakae kuonea huruma kwa lolote na chochote ni Mungu pekee ndie atakae kusaidia kufanikisha malengo yako kwakua ni yeye ndie alie yaweka ndani yako na niyeye ndie atakae yatimiliza kwa Nguvu zake, Kumbu 8:18a Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, Nimetaka kukuonyesha Mungu ndie anaekupa nguvu pasipo nguvu ya Mungu hufanikiwi, hivyo zitafute nguvu za Mungu upate kufanikiwa

Roho mtakatifu amekuletea ujumbe leo kukwambia Ni heri umkimbilie Bwana ili akufanikishe katika malengo yako na mipango yako, akushindie katika kila vita iliyo mbele yako, akushindie katika kila ugumu ulio mbele yako, Unaweza ukatabiriwa sana lakini pasipo msukumo wako binafsi toka ndani wakumtafuta Mungu, kufanya yaliyo ya Mungu hauta fanikiwa, wekeza kwenye kumtafuta Mungu, wekeza kwenye kuisikia sauti ya Roho mtakatifu inayokuelekeza ufanye nini na wakati gani

Nikwambie mtu wa Mungu Neema yakukufanikisha ipo, kazi yako ni kuamua kufanya, kazi yako ni kuzitafuta nguvu za Mungu na kutafuta sana kusikiliza Mungu anasema nini na anataka ufanye nini

Shida yetu waKristo tunataka twende vile tunavyotaka sisi si k**a Mungu anavyotaka, na sababu hatujawekeza kwenye kumtafuta Mungu na kuyafanyia kazi maelekezo yake, kwenye maombi hatuna utulivu tunawaza tuombe kisha tuondoke kwenda kulala, lazima upate muda wa kutafakari na kusikiliza ndani yako kuna sema nini na hicho utakachokisikia ndani maana yake ni Roho anae sema na utajuaje k**a ni Roho litakuja Neno la Mungu ndani yake kugonga muhuri kile ulicho semeshwa

Jambo kubwa wekeza kumtafuta Mungu na hilo ndio kimbilio lako pekee lakukufanikisha kutimiza makusudi yako na makusudi yaliyowekwa na Mungu katika Maisha yako uyafanye katika ulimwengu huu

Ni heri kumkimbilia Mungu kuliko kuwatumainia wanadamu, wanadamu hawatakupa msaada kwakua wanadamu wenyewe wanauhitaji wanataka kusaidiwa, AMUA kumtafuta Mungu kwa dhati ya moyo wako.

Zaburi 28:7-8
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
8 Bwana ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake

Nasikia furaha ya kimbingu ndani yangu kukwambia nguvu za Mungu ni halisi, na tuna ulinzi mkubwa sana ni ile kwamba mwana wa Mungu hujajua kuwa nguvu iliyo ndani yako ni kubwa, matatizo changamoto zimezuia kuuona ukuu wa Mungu katika maisha yako

Mpendwa mtegemee Mungu pekee, mtumaini yeye, weka Imani kwa Mungu kuwa atafanya njia, na ukiweka Imani kwake endelea kufanya kile unachosukumwa kufanya ukiamini mpenyo utatokezea mbele, katika kuishi kwa iman unaweza kuonekana chizi kwa wanadamu kwakua wao wanaona haiwezekani ila iman yako inasema inawezekana na katika kuamini kwako ndipo Mungu anapo jitukuza kwako kwa kufanya ili awaonyeshe wanaokucheka na kukudharau kuwa MUNGU WAKO ANA NGUVU.

Nikuombe badala ya kusubiria wanadamu wakusaidie wewe kimbilia chumba chasiri kumwomba Mungu, mwambie akupe njia za kuvuka, akupe njia za kufanya, akutokezee msaada kutoka patakatifu pake ili uweze kufanikisha malengo yako, uweze kuvuka katika yale unayoyaona nimagumu, Zaburi 20:2

Usiruhusu mawazo ya kushindwa yakutawale, usiruhusu kukata tamaa kukutawale ndani yako, bali mshangilie Mungu, mwabudu Mungu, kwani katika kujitia moyo katika Bwana kiwango chako cha iman kinakua na ile zile nguvu za Mungu zinachukua nafasi ndani yako kukutetea katika vita zako na kukufanisha katika mambo yako, Yesu ni Mzuri mtu wa Mungu, hebu onja thamani iliyo ndani yake kwa kumwamini yeye na kumtafuta yeye.

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwenye whatsup namba 0657 048393, Kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
0657 048393

NGUVU YA UTHUBUTU“Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. ”  — Ayubu 22:28 (Bi...
23/05/2024

NGUVU YA UTHUBUTU

“Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. ”
— Ayubu 22:28 (Biblia Takatifu)

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu
Kwaneema za Mungu tumepata kibali cha kutafakari Neno lake na umebarikiwa wewe uliepata nafasi ya kusoma ujumbe huu

Kitabu cha Mithali 18:21 kinasema, “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. ”

Ndani yako kuna mambo mengi yanayo zungumzwa, kuna makubwa na madogo, kuna ya muda mrefu na muda mfupi, yote hayo nikwambie tu ni halisi na ni kweli, yanasubiri kuyawekea imani na msukumo wa kufanya

Kila kitu katika huu ulimwengu kinaanzia ndani maana yake katika ulimwengu wa roho, na ulimwengu wa roho unatengenezwa na maombi ili kuvifanya vya rohon vidhihilike mwilini, ndio maana katika mstari wa Ayubu 22:27a unasema "Utamwomba yeye naye atakusikia"

Ili uweze kuvidhihilisha vya rohon kuja mwilin lazima kuomba, na sio tu kuomba bali kuomba kwa bidii ili kuachilia msukumo mkubwa wakuweza kuvidhihilisha, ule msukumo utakua na nguvu ya Mungu itakayofanya adui asiguse lile kusudia lako hata limefanikiwa

Kumbuka "Nawe utakusudia neno" kusudio lako la ndani ni lipi, nazungumza na wewe ambae ndani yako unamsukumo mkubwa wa kufanya kitu fulan, ambacho hicho kitu kimepiga kelele sana ndani yako lakini hujachukua hatua, nikwambie ipo Nguvu ndani ya hilo kusudio lako na ndio iliyosababisha kuachilia hilo kusudi linalopiga kelele ndani yako ili lidhihilike

Yamkini umeshaanza kufanya jambo ambalo ulisukumwa kufanya ndani yako lakini unaona matokeo madogo au vita ni kubwa, nikwambie hilo jambo tayali limethibitika tayari litamkie mwangaza/Nuru ya Kristo kuangazia hilo jambo nanjia zake zote

Kukusudia ni jambo lingine na kuthibitika ni jambo lingine nikwambie kuwa na maono nikitu kingine na kuyatimiza maono nikitu kingine kwakua vyote vinakuhitaji wewe muhusika kufanya, nanikwambie wewe ndio dereva, kiongozi inakupasa uwe na uthubutu wa kufanya, nikwambie anza kufanya hata kwa kukosea Mungu anaiona nia yako atainyoisha nakufanikisha, wengi hawana uthubutu, isiwe hivyo kwako katika jina la Yesu.

Nikwambie hata k**a unakesi kubwa unaona utashindwa lakini haki unayo yakukufanya ushinde, wewe focus mawazo yako na nia yako kwenye ushindi usifikilie kwenye kushindwa au kufeli,wewe kusudia kushinda kazi yako ni kutamka ushindi, kuwapangua wanaozuia ushindi wako, achilia uthibitisho wa ki-Mungu katika jina la Yesu, achilia nuru ya Kristo kung'aza jarada lako, waombee wote wanaoshughulika na kesi yako Mungu awaguse ili uweze kushinda

K**a upo kazini au kwenye biashara na unaona mambo hayaendi vizuri na ndani yako unasikia sauti ya mabadiliko na ushindi wewe kazia uthibitisho wa ki-Mungu na kukupa nafasi ya upendeleo wa kupokea baraka zako kwa ukubwa

Nikwambie mtu wa Mungu vyote vitathibitika, usijiangalie ukoje fahamu huu niwakati wako wa kufanya na kupokea kwakua Mwangaza wa Kristo Yesu utaangazia njia zako zote

Haijalishi ulianguka nyuma na matumaini yanakuja na kupotea nikwambie shikilia sauti ya kunyanyuka kisha songa mbele kwakua nguvu ya kusudi ipo ndani yako inakusubiri uitumie ili ifanye kazi

Makuhani wakati wa Joshua waliambiwa waanze kukanyaga maji ya mto yordan ili njia ipatikane wana wa Israel waweze kuvuka, nawewe ili njia ipatikane lazima uanze kukanyaga maji yaliyo mbele yako, hatua za kukanyaga maji ni kuanza kufanya jambo ili Mungu aweze kujidhihilisha kwenye kile unacho kifanya, Yoshua 3:13-27

Ondoa mashaka weka iman mbele, usijiangalie udhaifu wako wewe amini Bwana alie kuweka katika ulimwengu huu anaweza kukufanikisha katika yote na anaweza kukufanya kuwa shujaa katikati ya mashujaa.

Jiwekee tabia ya kutamkia ushindi, kufanikiwa mambo yako, makusudi yako yanayopiga kelele ndani yako, na usikae nayo sana moyon hiyo mipango kwakua nguvu ya mashaka itakomaa na kushindwa kutatawala, ukisikia kulifanya chukua hatua haraka kufanya kwakua hiyo ni sauti ya Roho inayozungumza, watu wa giza wanabidii sana ya kusemesha mabaya yatupate na sisi wakristo tuamke tuongeze bidii ya kubatilisha na kutamka kufanikiwa, uthubutu kila wakati ili tuweze kushinda zaid ya kushinda kwakua tunae Mungu

Tumia nguvu ya kinywa kujitamkia mazuri, tumia nguvu ya kinywa kupangua kila ubaya uliokusudia kwako, wewe ni mtu shujaa na mkuu katika ulimwengu huu Usijidharau, tamkini adui zako wamekutamkia kuwa hutashinda wala kufanikiwa wewe pangua vyote kwa jina Yesu kisha jivike ushujaa na omba uthibitisho wa ki-Mungu usimame juu yako.

Nakuombea Roho mtakatifu akusaidie kuelewa na kila ugumu ndani yako wa kuthubutu ukaondoke na vyote vikatimilike katika jina la Yesu, na ukalete ushuhuda mkuu wa yale Mungu atakayokufanyia.

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwa whatsup namba 0657 048393, kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
0657 048393

25/04/2024

WEKEZA UPENDO WAKO KWA MUNGU

Zaburi 91:14-16
¹⁴ Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
¹⁵ Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
¹⁶ Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu

Imempendeza Mungu leo kutafakari Neno lake la uzima

Hakuna kitu kizuri k**a kung'ang'ania kufanya kitu kitachokuletea faida au kinachokuletea faida, endapo utajua thaman na maana yake utakifanya kwa bidii pasipo kuziangalia changamoto unazozipitia au utakazozipitia.

Ipo faida kubwa katika kukaza kumpenda Mungu, kung'ang'ania kumpenda, kumsikia na kufanya yanayopempendeza Mungu, vile unavyoweka bidii na nguvu Mungu mwenyewe anaona, na yamkini unaweza usione kwa macho ya damu na nyama ila katika ulimwengu wa roho ukuu wa Mungu unadhihilika sana kwako

Anasema "kwakua amekaza kunipenda nitamwokoa" usione unapoteza muda katika yale mazuri unayoyafanya tambua Mungu anaona, usivunjike moyo kuona unafanya kazi isiyo na faida bali fahamu kabla haujazimia moyo utalipwa, usiruhusu kurudi nyuma kumwomba Mungu usiruhusu kurudi nyuma kumtumia Mungu kuona hakuna faida bali weka akilini ipo faida kubwa na Mungu anayaona yote ufanyayo na katika hayo ndio ijenge akili yako kuweka bidii zaid ya kufanya yampendezayo Mungu na kumtumia Mungu

Mungu Ameahidi katika Neno lake kuwa ukikaza kumpenda yeye atakuinua na atakuweka juu, katika hilo nikwambie kuwa yamkini unaweza usione k**a unainuliwa ila fahamu unainuliwa mno kwakua vingine hatuoni kwa jinsi ya mwilin bali ni kwa jinsi ya rohon, na vile unavyoendelea kufanya yaliyo ya Mungu kwa upendo ndivyo mwilini utakavyoona matokeo makubwa

Jambo kubwa usichoke kutenda mema, usichoke kufanya kazi ya Mungu, hata k**a utahisi kuchoka wewe jitie nguvu katika Bwana Yesu, na nikwambie pale unavyosikia kuchoka fahamu rohon kuna matokeo makubwa ambayo yapo na kuna faida unakaribia kupata sasa adui anaachilia kuchoka juu yako ili upishane na baraka za Mungu juu yako, hivyo ujisikiapo kukata tamaa tazama faida iliyombele yako utakayo ipokea hivyo katika hiyo ikutie nguvu ya kusonga mbele kwa kufanya yaki-Mungu

Katika yote utakapozidi kumpenda Mungu kwakufanya yale anayokuelekeza utajiwekea ukaribu mkubwa wa kusikiwa na Mungu, kutiwa moyo na Mungu katika nyakati ngumu utakazopitia au unazopitia, jambo lingine kubwa weka usikivu wa rohon kumsikia Roho anavyokwambia na kukufunulia yakupasayo kufanya katika wakati ufaao, wekeza sana katika kuomba kumsikia Mungu akusemeshapo na omba sana kumwambia Mungu akusaidie kuyafanya yale anayokwambia, usiwe mkaidi ukiambiwa wewe fanya hapo ndipo baraka zako utapopokea kwa ukubwa

Kumbuka jambo hili na likutie moyo, amesema katika Neno lake, Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona" bidii yako sio bure inafaida kubwa mbele za Mungu hivyo kazana kuyaishi na kufanya yanayopendeza Mungu, USIKATE TAMAA, WALA KURUDI NYUMA, kwani baraka zako zimefichwa wakati unasikia ndani yako kukata tamaa, hivyo muda huo puuzia hiyo sauti na kuweka bidii ya kumtafuta Mungu tu hapo utshibishwa siku nyingi za kuishi na utauona wokovu wa Mungu ili uwe shuhuda kwa kizazi na vizazi.

Uinuliwe Kiroho na Bwana Yesu

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa rafiki zako facebook na Whatsup. Pia like page yetu ya "Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote" kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu tuma majina yako mawili kwa whatsup namba 0657 048393, kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini.

Merito Tagalile
~0657 048393
~0748048366

21/01/2024

WENYE HAKI WATASTAWI
Isaya 3:10-11
¹⁰ Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
¹¹ Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu
Tuna mtukuza Mungu kwa neema yake aliyotupa hata leo amependa tulitafakari Neno lake, nijambo jema mbele za Mungu kutafakari Neno lake kila wakati, jambo kubwa zaidi kulifanyia kazi / kuliweka Neno la Mungu kwenye matendo ili tuweze kufaidi matunda ya Neno la Mungu kupitia ahadi zilizomo humo.

Tunapoanza mwaka lazima tuweke mipango na malengo yakwenda nayo mwaka mzima, na katika hayo malengo na mipango lazima tufahamu ili tufanikiwe k**a Wakristo lazima tusimame sana kwa Mungu wetu, yaani tuwe wacha Mungu,tuwe watakatifu kwani anasema katika Ebrania 12:14b pasipo utakatifu hatuwezi kumuona Bwana Yesu,

Maana yake mwaka huu ili ufanikiwe ili ufike viwango Mungu anataka lazima matendo yako yampendeze Mungu, mwenendo wako uwe safi, epuka ujanja ujanja, epuka kudhurumu watu, epuka kuvunja watu moyo, ndio yako iwe kweli sio yako iwe sio kweli, usifanye kwa kuwatazama wanadamu wewe fanya ukimtazama Mungu,

Mungu kupitia kinywa cha Nabii Isaya anasema "Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, maana ya heri iliyotumika hapo ni kuwa na furaha, kwahiyo wewe utakae kwenda katika njia za Mungu na kutenda haki utafurahi na utakula matunda ya matendo yako

Kuna angalizo katika hilo Neno" WATAKULA MATUNDA YA MATENDO YAO" ikiwa utafanya matendo yasiyo haki ufahamu HAUTAFANIKIWA kwasababu Mungu wetu ni mtakatifu na mwenye haki, Nikusihi mtu wa Mungu tafuta sana, jitahidi sana kuishi maisha matakatifu tenda matendo ya haki ndipo utakapofanikiwa katika mipango na malengo yako uliyojiwekea. Isaya 3:11, Isaya 57:20,

Nikusaidie kitu kingine anaposema "WENYE HAKI...….WATAKULA MATUNDA YA MATENDO YAO" inamaanisha unatakiwa uwe mtu wa matendo, kuna mambo umepanga kufanya inatakiwa uanze kuyafanya, katika kuyafanya na kule kuenenda katika haki ndipo Mungu atakufanikisha na utakula matunda ya yale unayoyafanya, hautadhurumiwa wala kupata hasara

Jambo moja ulifahamu watu wengi wamelia kutofanikisha mambo, na hata wewe umesikia na wamekuogopesha kufanya baadhi ya mambo, moja ya sababu watu kutofanikiwa nikutokwenda katika haki na UTAKATIFU, tumeona katika Ebrania 12:14b PASIPO UTAKATIFU HATUWEZI KUMUONA BWANA, -Hatutaweza kumuona Bwana Yesu akifanya kwenye mambo yetutukiwa sio waaminifu, ila tukifanya yaliyo mema mbingu zitakua upande wetu katika kufanikisha mambo na mabaya yatakayokuja juu yako yatabatilika kwakua Mungu yuu upande wako kukupigania, 2Nyakati 6:23, Eze 24:14

Napia ukiwa mtu wahaki ukiona jirani yako anadhurumiwa/anaonewa yakupasa umsaidie kusema kweli, kupitia hiyo utakua umetangaza injili ya aman na haki katika jamii na kila utakapo kuwepo- usikae kimya paza sauti kwa mambo yaliyo ya haki

Neno katika kumbukumbu 5:33 linasema "Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki." Ipo njia tuliyo agizwa na Bwana tuenende nayo tunatakiwa tuifuate hiyo ili mambo yetu yasife yawe hai- yastawi, na miaka yetu iongezeke lakini katika yote hayo kubwa Kumbu 28:1, 2-14,

Ukisimama katika haki Bwana atakutetea atakupigania, atakushindia katika yote utakayofanya Zaburi 37:17, Yeremia 22:15, Mwanzo 15:1,Zab 128:1

Mwaka huu tafuta kwa bidii kutenda haki na kuishi katika utakatifu ili umuone Mungu kitofauti katika mambo yako

Tuombe
Baba katika jina la Yesu, asante kwaneema yako kuu kwetu, asante kwakua unatuwazia mawazo yaliyo mema, asante kwakutupa mwaka huu wenye baraka, neema tele, tunakusihi utusaidie tukaenende katika haki na utakatifu, matendo yetu yakakupendeze, na k**a ulivyosema katika Neno lako wenye haki watakua heri na watakula matunda ya matendo yao, tupe kula matendo ya baraka, tupe kufanikiwa katika kila tulifanyalo, zile baraka zarohoni ulizotubariki nakusihi tukazipokee kimwili sawasawa na ahadi zako, asante kwakua utakwenda kufanya yote k**a tulivyoomba sawa sawa Neno lako, katika jina la Yesu tumeomba na kupokea amen.

NB: 2024 Taman Sana Kuwa Shujaa Wa Maombi-Omba Sana

Nakutakia baraka za Mungu katika jina la Yesu

K**a umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like page yetu ya Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote kwa masomo mengi zaidi.

Merito Tagalile
0657 048393

Address

Posta Mpya
Dar Es Salaam

Telephone

+255657048393

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Nyumba Ya Sala Kwa Mataifa Yote:

Share