Kila Mwenye Pumzi Na Amsifu Bwana

Kila Mwenye Pumzi Na Amsifu Bwana Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumili

Roho Wa Bwana Yu Juu Yangu, Kwa Maana Amenitia Mafuta Kuwahubiria Maskini Habari Njema. Amenituma Kuwatangazia Wafungwa Kufunguliwa Kwao, Na Vipofu Kuona Tena, Kuwaacha Huru Walisetwa, Na Kutangaza Mwaka Wa Bwana Uliokubarika. - Luka 4: 18-19

MWAMININI MUNGU - Hii ni siraha kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku, hatua ya kwanza ya uponyaji wako, wa kuvuka ...
21/03/2026

MWAMININI MUNGU - Hii ni siraha kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku, hatua ya kwanza ya uponyaji wako, wa kuvuka kwenye vikwazo, kuona Mungu akikuvusha na kukupigania kwenye kila jambo na hali yoyote ni kumwamini yani kujenga imani ndani yako kwamba hakuna jambo lisilowezekana kwa huyu Mungu tunaemubudu katika Kristo Yesu.
_
Mahali popote ulipo anza kumuamini Mungu kwanza kabla ya mtu yoyote, amini kwamba Mungu anaweza kukuvusha hapo, anaweza kukuponya na magonjwa yote, na anaweza kukunyenyua tena mahali ulipoanguka.
_
Kwa namna gani utamwamini Mungu ni kwa kusoma Neno lake, kwa kusikiliza watumishi wa Mungu na shuhuda mbalimbali wanazozitoa watu ambao ameisha wavusha katika majaribu yao.
_
Sijui unapitia nini, ila nachoweza kusema mwamini Mungu, amini hilo tatizo lako linaenda kuisha maadamu umeomba na umemwamini Mungu aliye hai katika Kristo Yesu.

2026 Ukawe Mwaka wenye mafanikio katika shughuli zenu zote, Mungu akasikie maombi yenu na kuwajibu na kuwapatia haja za ...
01/01/2026

2026 Ukawe Mwaka wenye mafanikio katika shughuli zenu zote, Mungu akasikie maombi yenu na kuwajibu na kuwapatia haja za mioyo yenu sawasawa na mapenzi yake, na kila mwenye pumzi na aseme, Amen.

Baba Mungu Mfalme wa Mbingu na Nchi k**a vile Neno lako linenavyo, tunaomba uzuri wako uwe juu yetu, tukatamalaki, na ka...
15/08/2025

Baba Mungu Mfalme wa Mbingu na Nchi k**a vile Neno lako linenavyo, tunaomba uzuri wako uwe juu yetu, tukatamalaki, na kazi za mikono yetu utufanyie udhabiti na uzithibitishe katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amen.

Unapomtumikia Mungu aliye hai katika Kristo Yesu,  unafungua milango ya kukibariki chakula chako, maji yako na kila kitu...
14/08/2025

Unapomtumikia Mungu aliye hai katika Kristo Yesu, unafungua milango ya kukibariki chakula chako, maji yako na kila kitu unachomiliki na anasema atakuondolea magonjwa kwenye familia yako.
_
Hii ni siri kubwa sana Mungu anataka tuifahamu, kitendo cha kumtumikia tu unakuwa mahali salama wewe pamoja na familia yako, mali zako, ukoo wako pamoja na rafiki zako.
_
Baba Mungu tusaidie wanao tupate kulielewa na kulitii Neno katika jina la Yesu, Amen.

Moja ya jambo ambalo Mungu hapendezwi nalo na mtu kuwa na maneno mengi ukiwa na maneno mengi inakupelekea kwenye kulalam...
06/07/2025

Moja ya jambo ambalo Mungu hapendezwi nalo na mtu kuwa na maneno mengi ukiwa na maneno mengi inakupelekea kwenye kulalamika.
_
Mungu anajua mahitaji yetu, kabla hajakuumba anakujua na anajua mapito yako yote, usijisumbue kuongea maneno mengi, bali jikite katika kusali, kuomba, kushukuru na kupeleka hoja zako mbele za Mungu.
_
Ukifanya hivyo utamuona Mungu katika viwango vya hali ya juu sana kwenye maisha yako.

Chochote unachokisikia na ukendelea kukisikia kila mara kinaenda kukaa kwenye moyo wako na kwenye akili zako na mwisho w...
22/04/2025

Chochote unachokisikia na ukendelea kukisikia kila mara kinaenda kukaa kwenye moyo wako na kwenye akili zako na mwisho wa siku utaanza kukiamini hata k**a ni kibaya.
_
Ndio maana ukikata kumuamini Yesu lazima uwe na Neno la Mungu kwa wingi ndani yako, maana isipite siku haujajifunza, haujasoma Neno hata k**a mstari mmoja unatosha sana kubadilisha mtazamo wako na imani yako.
_
Ukipata nafasi unawasikiliza watumishi wa Mungu wanaohubiri habari za Kristo, wanaofundisha habari za Yesu, moyoni mwako usijaze mambo ya duniani hayatakusaidia, kabla ya kujaza hayo, anza na Neno la Mungu kwanza likae kwa wingi ndani ya moyo wako.
_
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. - Ayubu 22:21
_
Kumbe ukimjua Mungu kwa kusoma Neno lake pia unapata amani na mema yatakavyokujia, ukiisha mjua Mungu hakuna jambo hapa duniani litakuogopesha sababu unajua nguvu na uwezo ambao Mungu wetu aliye hai anao.

Unapoimaliza wiki na kuianza wiki nyingine, usihangaike na maneno ya kujilaumu au kujutia wala usiwe na maneno mengi bal...
09/02/2025

Unapoimaliza wiki na kuianza wiki nyingine, usihangaike na maneno ya kujilaumu au kujutia wala usiwe na maneno mengi bali jikite sana katika kusali, kuomba na kushukuru, na haja zako zote zijiulikane na Mungu.
_
Maana yake mipango yako yote uliyopanga kuifanya Mungu aijue yani uichukue uende mbele za Bwana na kumkabidhi ili mapenzi yake yatimizwe juu ya haja zako.
_
Ukifanya hivyo hakika utafanikiwa.

Unapokutana na Neno lolote litokalo kwenye Biblia basi ni Roho Mtakatifu anazungumza wewe, sijui unapitia kitu gani sasa...
21/01/2025

Unapokutana na Neno lolote litokalo kwenye Biblia basi ni Roho Mtakatifu anazungumza wewe, sijui unapitia kitu gani sasa hivi lakini naamini Roho wa Mungu anajua ndio maana anazungumza na wewe.
_
Kwamba tuwe wepesi wa kusikia na wala tusiwe wepesi wa kuzungumza na kukasirika, kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu, maana yake ukikasirika hautatenda haki ya Mungu.
_
Mungu hapendi watu ambao wanazungumza sana, bali anapenda wasikivu na wale ambao sio watu wa kukasirika hovyo hata wakisikia wanasemwa vibaya au wamezungumziwa vibaya, watu ambao wana roho ya utulivu.
_
Jitahid basi uwe msikilizaji na mwenye roho ya utulivu, baraka za Mungu zitakuwa juu yako.

Nayakati hizi ni za kwenda nazo kwa umakini sana, usipokee wala usiamini kila neno ambalo halijatoka kwenye Biblia, wala...
14/01/2025

Nayakati hizi ni za kwenda nazo kwa umakini sana, usipokee wala usiamini kila neno ambalo halijatoka kwenye Biblia, wala usimpokee kila mtumishi kisa anaijua Biblia, maana hata makristo wa uongo wanao uwezo wa kufanya ishara na maajabu.
_
Moyoni mwako muweke Yesu, uwe na tabia ya kuzungumza na Mungu kabla ya kumuamini mtumishi yoyote na usome sana Biblia (Neno la Mungu) ili iwe rahisi Roho Mtakatifu azungumze na wewe kwa urahisi.
_
Usiwe mwepesi kuamini kila neno unaloambiwa, kabla ya kufanya maamuzi yoyoye tafakari kwanza kuhusu hayo maneno uliyoambiwa. uwe na busara utazame sana jinsi uendavyo.

Neno linatuhimiza tufanye kazi kwa bidii ila tusipende fedha kwasababu inaweza kukingia kwenye mtego wa dhambi, unatakiw...
14/01/2025

Neno linatuhimiza tufanye kazi kwa bidii ila tusipende fedha kwasababu inaweza kukingia kwenye mtego wa dhambi, unatakiwa uwe na moyo wa kuridhika ukimtumainia Mungu na ukifanya kazi kwa bidii fedha yako ipate kuongezeka bila kupitia njia za mkato.
_
Kupenda fedha ni kubaya sana sababu unaweza kuingia mtego wa kupokea rushwa ili upindishe haki, sikia usiwe na haraka ya kufanikiwa kwasababu Mungu hata kuacha wala usiwe na hofu ya maisha kabisa, mahali popote ulipo tenda haki, Mungu atakuinua na atakufanikisha.

Chanzo cha kwanza cha mafanikio na cha kutokufanikiwa ni wewe namna unavyojitazama nafsini mwako, k**a unajiona mshindi,...
12/01/2025

Chanzo cha kwanza cha mafanikio na cha kutokufanikiwa ni wewe namna unavyojitazama nafsini mwako, k**a unajiona mshindi, unajiona hakuna jambo gumu kwako, unajiona tajiri hata k**a sio tajiri, basi unaenda kufanikiwa ndio namna Mungu anataka watu wenye kujiamini na kumuamini Yeye hata k**a anapitia hali ngumu, moyo wako ni kielelezo tosha mbele za Mungu.
_
K**a unajiona ni mwenye mikosi, unaona kushindwa kila jambo, unajiona kukataliwa, unaona huna unaloweza, unajiona maskini, sikia hayo unayoyaona ndani ya nafsi yako yanaena kukutokea hata ubandikwe mikono vipi huwezi fanikiwa mpaka hapo utakapojiona watotauti ndani ya nafsi yako.
_
Uliumbwa kwa mfano wa Mungu ndani yako kuna nguvu aliyoiweka ili kukusaidia wewe binafsi kabla hata ya kuombewa au kubandikwa mikono namna utakavyowaza na kujiona na kujitamkia hayo ndio yataenda kutokea kwa ile nguvu ambayo Mungu ameiweka ndani yako.
_
Badilisha namna unavyojiona nafsini mwako ili upate kufanikiwa.

Address

Mbezi
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kila Mwenye Pumzi Na Amsifu Bwana posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kila Mwenye Pumzi Na Amsifu Bwana:

Share