01/10/2024
NYWELE ZAKO ZIKUFUNDISHE, SAUTI YA MUNGU.
Kwanini Mungu akuumbe hivyo ulivyo?
usipoweza kuelewa utendaji kazi wa mwili wako jinsi viungo vinavyoshirikiana huwezi kuelewa jinsi kanisa la Kristo linavyopaswa kufanya kazi likutanikapo, kwasababu sisi tunaitwa viungo mbalimbali ndani ya mwili wa Kristo.
Umeona?
Bwana akasema kiungo kimoja kikiumia, vyote vimeumia.
Hivyo tumeumbwa, kimalengo sio kimwonekano bora au kiuzuri,.
Ni sawa na mtu aulizwe kati ya jiko, na maua kipi kina umuhimu zaidi kuwepo ndani mwako.
Ni wazi kuwa atasema jiko,kwasababu litamsaidia kupika.
Hakulichagua kwasababu lina mwonekano bora, lakini kwasababu lina matumizi muhimu zaidi ya vingine.
Vivyo hivyo na wewe ujitazamapo mwili wako, usijitazame kiuzuri kuliko viumbe vingine, au wanadamu wenzako, bali fikiria tu katika picha ya matumizi ya kila kiungo ulichopewa, kinakufundisha nini kuhusu muumba wako au kinatimiza kusudi gani kwa Mungu wako.
Hilo ndio lengo hasaa la wewe kubuniwa hivyo ulivyo.
Leo tutaanza na NYWELE,
_Utazamapo nywele zako Bwana anataka ujue yafuatayo;_
1️⃣ *Mambo yako yote, yapo katika hesabu za Mungu.*
Mathayo 10:30-31
30 lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
31 Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi
Ni kawaida kudhani kuwa Mungu hathamini, au hajui kila kitu, au anasahau sahau. Lakini sivyo, ukimfuata Mungu, vitu vyako vyote vinavyotoka na kuingia vipo kimahesabu, hakuna kitu kinachotokea kwa ghafla tu, bila yeye kujua au kuruhusu, Hivyo mashaka yakija, kumbuka nywele zako zilivyo nyingi lakini zimehesabiwa, vivyo hivyo mambo yako yote yamehesabiwa.
2️⃣ *Huwezi epukana na maadui.*
Zaburi 69:4
4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.
Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua
Jinsi nywele zako zilivyo nyingi, maadui nao vivyo hivyo.
Na maadui zetu sio wanadamu bali ni mapepo ambayo mara nyingine huweza pia yavaa wanadamu, kutudhuru. Hivyo usiwe mtu wa kunung’unika au kulamimika, ujue kila mwanadamu yupo vitani.
K**a Bwana wetu Yesu Kristo hakuwa na dhambi hata mmoja lakini alikuwa na jopo la maadui kwanini wewe usiwe nao.
Hivyo kuwashinda ni kuwa mwombaji daima, na kutembea katika njia za Bwana sikuzote.
Ukikumbuka kuwa maadui ni jambo la kawaida, k**a tu nywele zako zilipo hapo kichwani.
3️⃣ *Si kila kitu unaweza kufanya. hivyo kuwa na kiasi.*
Mathayo 5:36
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
Wakati mwingine, tunajiaminisha na kujihakikishia mambo na kuweka na viapo juu yake kana kwamba mambo yote yapo ndani ya uwezo wetu.
Kauli k**a, “leo nife,k**a sitakupa hiyo fedha” au “Mungu anipige hapa hapa k**a ninalokuambia ni uongo” Kauli k**a hizi, za kuongezea hakikisho lingine juu, hazitokani na Mungu, maneno yetu tumeambiwa yawe ndio ndio, au sio sio, zaidi ya hapo yanatokana na Yule mwovu.
Kwahiyo popote unapojiona unakaribia kuzidi mipaka kumbuka hizo nywele zilizo juu yako hujawahi kuzifanya ziwe hivyo ulivyo, Bwana ndiye azibadilishaye, hivyo jiwekee mipaka.
4️⃣ *Zithamini nguvu zako za rohoni.*
Nywele zako hufunua nguvu zako za rohoni. Wanadhiri wote wa Mungu hawakuruhusiwa kukatwa nywele, Samsoni alipewa nguvu, kwa agano la kutokatwa nywele, kufunua kuwa watakatifu wote nywele zao za rohoni ndio nguvu zao.
Lakini unapoacha mpango wa Mungu adui anazikata, k**a ilivyokuwa kwa Samsoni.
Lakini baadaye alipojua amefanya makosa ziliota tena lakini katika gharama za ‘kutoona’ tena.
Waamuzi 16:22
22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
Tunza nguvu zako, usiruhusu kiwembe chochote cha mwovu kikupitie.
Kwasababu hata zikirejea tena, hutakuwa k**a hapo mwanzo.
5️⃣ *Uwe na nyakati za maombolezo.*
Yeremia 7: 29
29 Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana Bwana amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.
Zamani, kukatwa nywele zote kuisha kabisa ilikuwa ni ishara ya kuingia kwenye maombolezo, kwasababu utukufu wako umeuvua.
Maombolezo, kwa agano jipya sio kulia k**a msiba, hapana bali kuingia kwenye maombi ya ndani kabisa, ya kuutafuta uso wa Mungu, ambayo huambatana na mifungo. Na leo, ni kila mara tunakwenda saluni kukata nywele zetu.
Tujue Bwana anatutaka k**a vile tukatavyo nywele zetu mara kwa mara ndivyo tukumbuke maombi ya kujimimina sana mbele zake.
6️⃣ *Jisitiri*
1 Wakorintho 11:15
15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.
Nywele ni vazi lililobuniwa na Mungu la kujisitiri hususani kwa mwanamke.
Uzitazamapo nywele zako, tambua, ni ujumbe wa kujisitiri mwili wako. Vaa vizuri.
Ubarikiwe saana
From Baba Paroko