UTANGULIZI KUHUSU TAYO MSEWE
Tanzania Anglican Youth Organisation-Msewe yaani Umoja wa Vijana wa Anglikana Tanzania ipo ndani ya kanisa la Mtakatifu Stephano-Msewe chini ya usimamizi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam. Huu ni umoja unaowaunganisha vijana wa Kianglikana Msewe na Tanzania kwa ujumla. MSINGI WA TAYO MSEWE:
Kuimarisha upendo, utumishi katika kanisa na mshik**ano wa vijana
ndani ya kanisa la Anglikana Msewe pamoja na madhehebu mengine kiujumla. MADHUMUNI:
• Kusimamia huduma zote za vijana katika nyanja zote ikiwemo uinjilisti kwa njia ya uimbaji, michezo mbalimbali nk.
• Kuwalea vijana kiroho zaidi na katika mwenendo mzima wa Kikristo.
• Kukuza moyo wa ushirikiano baina ya vijana, waumini na watu wote katika kuleta umoja ndani ya kanisa.
• Kuhakikisha shughuli zote za kikanisa zinazohusu vijana zinasimamiwa ipasavyo na kutekelezwa na umoja huu.
• Kutumia vikao zaidi kuweza kupata mawazo ya vijana ili kuleta na kuharakisha maendeleo ya umoja na kanisa kiujumla.
• Kushirikiana na asasi mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha vijana juu ya mambo mbalimbali ya kijamii.
• Kuwaunganisha vijana walio ndani na nje ya kanisa na kuzidisha ushirikiano na makanisa/madhehebu mbalimbali.
• Kumjua, kumpenda na kumtumikia Yesu Kristo k**a Bwana na Mwokozi wetu. MALENGO YA TAYO MSEWE:
• Kuleta na kudumisha mshik**ano.
• Kujiimarisha kiuchumi na kukusanya wanachama wapya katika umoja.
• Kueneza neno la Mungu kwa kufanya uinjilisti.
• Kuandaa warsha/semina kwa vijana ili wapate muda wa kujifunza neno la Mungu.
• Kusimamia maisha ya vijana kiroho, kiafya, kielimu na ndoa.
• Kutoa msaada kwa wahitaji. MOTTO:
Motto wa umoja huu ni “Vijana Nguzo ya Kanisa”. Mwisho tunawakaribisha kwa maoni, ushauri nk. tuweze kupiga hatua ili tutoke hapa tulipo na hatimae twende mbele zaidi.