Wanyenyekevu wa Mama Maria

Wanyenyekevu wa Mama Maria Karibuni katika tafakari na sala kwa heshima ya Mama yetu Bikira Maria, Mama Maria ni Mama wa Matumaini, Mama Maria ni Mama wa Shauri Jema..

SOMO: MAANA YA AMECEA, MIKUTANO YAKE, MADA ZAKE NA MAKAO MAKUU YAKENa Mkatoliki MgayaUtanguliziKanisa Katoliki barani Af...
25/07/2026

SOMO: MAANA YA AMECEA, MIKUTANO YAKE, MADA ZAKE NA MAKAO MAKUU YAKE

Na Mkatoliki Mgaya

Utangulizi

Kanisa Katoliki barani Afrika lina vyombo mbalimbali vinavyoratibu shughuli za kichungaji na uinjilishaji. Mojawapo ya vyombo muhimu zaidi ni AMECEA, ambacho huunganisha Mabaraza ya Maaskofu wa nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati ili kushirikiana katika kutangaza Injili na kujibu changamoto za wakati.

Maana ya AMECEA

AMECEA ni kifupi cha:

Association of Member Episcopal Conferences in Eastern Africa

Kwa Kiswahili:

Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Wanachama wa Afrika Mashariki na Kati.

Lilianzishwa mwaka 1961 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Mabaraza ya Maaskofu katika uinjilishaji, malezi ya waamini, maendeleo ya jamii na kukuza amani na haki.

Makao Makuu ya AMECEA

Makao makuu ya AMECEA yako Nairobi, Kenya.

Kutoka hapo huratibiwa shughuli mbalimbali za kichungaji, mafunzo, mikutano na ushirikiano wa Kanisa katika nchi wanachama.

Nchi Wanachama wa AMECEA

AMECEA linajumuisha Mabaraza ya Maaskofu kutoka nchi zifuatazo:

- Tanzania
- Kenya
- Uganda
- Zambia
- Malawi
- Ethiopia
- Eritrea
- Sudan Kusini
- Sudan
- Djibouti

Malengo ya AMECEA

- Kuimarisha uinjilishaji.
- Kukuza ushirikiano kati ya Mabaraza ya Maaskofu.
- Kuendeleza haki, amani na maridhiano.
- Kukuza malezi ya mapadre, watawa na walei.
- Kukuza Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo.
- Kujibu changamoto za kijamii kwa mwanga wa Injili.

Mikutano ya AMECEA

AMECEA hufanya mikutano ya kawaida ya viongozi wa Kanisa, hasa Maaskofu, ili:

- Kutathmini hali ya Kanisa katika nchi wanachama.
- Kujadili changamoto za kichungaji.
- Kupanga mikakati ya uinjilishaji.
- Kutoa mwelekeo wa pamoja kuhusu masuala yanayoikabili Afrika Mashariki na Kati.

Mikutano hii hufanyika kwa nyakati tofauti na mara nyingi huandaliwa na nchi mwanachama kwa zamu.

Baadhi ya Mada Zinazojadiliwa na AMECEA

- Uinjilishaji mpya.
- Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo.
- Familia na ndoa.
- Vijana katika Kanisa.
- Malezi ya makatekista.
- Elimu ya Kikatoliki.
- Haki, amani na maridhiano.
- Utunzaji wa mazingira.
- Uongozi wa kichungaji.
- Matumizi ya vyombo vya habari na teknolojia katika uinjilishaji.

Umuhimu wa AMECEA

AMECEA limechangia kwa kiasi kikubwa:

- Kuimarisha umoja wa Kanisa katika Afrika Mashariki na Kati.
- Kuendeleza huduma ya makatekista na walei.
- Kukuza Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo.
- Kukuza mshik**ano kati ya Makanisa ya nchi wanachama.
- Kuhamasisha Kanisa kushughulikia changamoto za kijamii kwa mwanga wa Injili.

Hitimisho

AMECEA ni chombo muhimu kinachoratibu ushirikiano wa Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki na Kati. Kupitia mikutano, mafunzo na mipango yake, limeendelea kuimarisha uinjilishaji, haki, amani na maendeleo ya Kanisa katika ukanda huu.

Rejea za Biblia

- Mathayo 28:19–20 – "Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi."
- Matendo 2:42–47 – Ushirikiano wa Kanisa la kwanza.
- Waefeso 4:1–6 – Wito wa kudumisha umoja katika Kristo.

SIKU YA SITA YA MKUTANO MKUU WA 21  AMECEA - 2026- Leo Julai 24, 2026 Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB)  limeongo...
24/07/2026

SIKU YA SITA YA MKUTANO MKUU WA 21 AMECEA - 2026
- Leo Julai 24, 2026 Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB) limeongoza shughuli za kiliturujia katika Adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa 21 AMECEA unaoendelea nchini Kenya.

- Misa Takatifu imeadhimishwa na Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Mombasa, Mhashamu Dominic Kimengich, huku Waamini na wajumbe kutoka nchi mbalimbali wanachama wa AMECEA wakishiriki kwa umoja katika sala na ibada k**a sehemu ya safari ya pamoja ya Sinodi.

MKUTANO MKUU WA 21 WA AMECEA UMEFUNGULIWA RASMIMkutano Mkuu wa 21 wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (AME...
20/07/2026

MKUTANO MKUU WA 21 WA AMECEA UMEFUNGULIWA RASMI
Mkutano Mkuu wa 21 wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (AMECEA) umefunguliwa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki (CUEA), Jimbo Kuu Katoliki Nairobi, nchini Kenya.

Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Wakenya Wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora), Mheshimiwa Wycliffe Musalia Mudavadi, ambaye aliongoza hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaowakutanisha viongozi wa Kanisa Katoliki kutoka nchi wanachama wa AMECEA kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utume wa Kanisa na maendeleo ya jamii.

Hongera sana kwake baba Askofu Joseph R. Mlola ALCP/OSS kwa kutimiza miaka 29 ya utumishi katika daraja takatifu ya upad...
12/07/2026

Hongera sana kwake baba Askofu Joseph R. Mlola ALCP/OSS kwa kutimiza miaka 29 ya utumishi katika daraja takatifu ya upadre. Twamwomba Mungu aendelee kumbariki na kumfanya baraka kwa watu wake.

11/07/2026

Baba Mtakatifu LEO wa Kumi na Nne amemteua Padri VINCENT LAURENT MPWAJI, kuwa Askofu Msaidizi Mpya wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.

Taarifa ya Uteuzi huo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Mhashamu JUDE THADDAEUS RUWA'ICHI, katika Ukumbi wa Kardinali PENGO, Kanisa Kuu la Mt. Yosefu.

Ask. Mkuu RUWA'ICHI amesema amepokea Taarifa hiyo kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini kwamba Baba Mtakatifu ameridhia Ombi la Jimbo Hilo kupata Askofu Msaidizi mwingine na Tangazo rasmi limetolewa Saa 6:00 mchana huko Roma sawa na Saa 7:00 mchana Afrika Mashariki.

Ameeleza kuwa hadi Sasa Askofu Msaidizi Mteule VINCENT LAURENT MPWAJI ni Chansela wa Jimbo Kuu hilo.

Askofu Msaidizi Mteule MPWAJI atakapowekwa Wakfu atafanya Idadi ya Maaskofu waliopo wenye asili ya Dar Es Salaam kufikia watatu.

Wengine ni Mhashamu EUSEBIUS NZIGILWA, Askofu wa Jimbo la Mpanda na Makamu wa RAIS TEC na Mhashamu HENRY MCHAMUNGU, Askofu Msaidizi wa DSM.

Baba Mtakatifu LEO wa Kumi na Nne amemteua Padri VINCENT LAURENT MPWAJI, kuwa Askofu Msaidizi Mpya wa Jimbo Kuu la Dar E...
11/07/2026

Baba Mtakatifu LEO wa Kumi na Nne amemteua Padri VINCENT LAURENT MPWAJI, kuwa Askofu Msaidizi Mpya wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.

Taarifa ya Uteuzi huo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Mhashamu JUDE THADDAEUS RUWA'ICHI, katika Ukumbi wa Kardinali PENGO, Kanisa Kuu la Mt. Yosefu.

Ask. Mkuu RUWA'ICHI amesema amepokea Taarifa hiyo kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini kwamba Baba Mtakatifu ameridhia Ombi la Jimbo Hilo kupata Askofu Msaidizi mwingine na Tangazo rasmi limetolewa Saa 6:00 mchana huko Roma sawa na Saa 7:00 mchana Afrika Mashariki.

Ameeleza kuwa hadi Sasa Askofu Msaidizi Mteule VINCENT LAURENT MPWAJI ni Chansela wa Jimbo Kuu hilo.

Askofu Msaidizi Mteule MPWAJI atakapowekwa Wakfu atafanya Idadi ya Maaskofu waliopo wenye asili ya Dar Es Salaam kufikia watatu.

Wengine ni Mhashamu EUSEBIUS NZIGILWA, Askofu wa Jimbo la Mpanda na Makamu wa RAIS TEC na Mhashamu HENRY MCHAMUNGU, Askofu Msaidizi wa DSM.

04/07/2026

Baraka ya kwanza kutoka kwa Mapadre wapya Jimbo kuu Katoliki Dar es Salaam, wakiwabariki Askofu Mkuu Mhashamu Judathadei Ruwaichi na Askofu Msaidizi Henry Mchamungu...

MISA TAKATIFU YA UPADRISHO KWA WALIOKUWA MASHEMASI 18 - JIMBO KUU LA DAR ES SALAAMPicha mbalimbali ni wakati wa Adhimish...
04/07/2026

MISA TAKATIFU YA UPADRISHO KWA WALIOKUWA MASHEMASI 18 - JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
Picha mbalimbali ni wakati wa Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu kutolewa kwa Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre kwa waliokuwa Mashemasi 18.

Misa Takatifu imeadhimishwa na Mhashamu Henry Mchamungu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Viwanja vya Msimbazi Centre - Jimboni humo.
www.radiomaria.co.tz

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255654684864

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wanyenyekevu wa Mama Maria posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Wanyenyekevu wa Mama Maria:

Shortcuts

Share