27/12/2025
CHRISTMAS IMEISHA LAKINI JE IMEACHA ALAMA GANI KATIKA MAISHA YAKO KIROHO NA KIMWILI โ
โโโโโโโโโโโโโโโโ
KWA HABARI YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO KUNA MAPOKEO YA AINA MBILI:
1. MATOKEO KWA UPANDE MMOJA, NA
2. MATOKEO KWA UPANDE MWINGINE,
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Isaya 53:1
[1]Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?
Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
NI MUHIMU SANA KUWA NA HAKIKA YA CHANZO CHA HABARI UNAZOPEWA KWA SABABU NI MATOKEO YA JINSI ULIVYO LEO,
ISSUE SIYO TU KUAMINI HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO MAANA HATA SHETANI NAYE ANAAMINI,
MAANA HATA KIJAKAZI MWENYE PEPO WA UAGUZI ALIWATAMBUA NA KUWATAJA AKINA NA KUWA NI WATUMISHI WA KWELI WA MUNGU,
(MATENDO 16:16-18),
LAKINI KIUHALISIA K**A MGANGA WA KIENYEJI ALIKUWA NA LENGO LAKE MAANA ALIKUWA AMEWAPOTOSHA WENGI WAKIACHA NJIA YA BWANA NA KUIABUDU MIUNGU MINGINE,
ISSUE NI NANI HASA ANAYEKULETEA HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO NA KUSUDI HALISI LA KUZALIWA KWAKE โ
:
HABARI SAHIHI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO ZIKITOLEWA NA MTU SAHIHI NDIPO ZINALETA MATOKEO YA KILE KILICHOMLETA YESU HAPA DUNIANI,
LAKINI PIA HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO ZILITOLEWA NA MTU ASIYE SAHIHI KWA NAMNA YA HILA (UPOTOSHAJI) NDIPO ZINALETA MATOKEO MBALI NA KILE KILICHOMLETA YESU HAPA DUNIANI,
1. : (HABARI CHANYA)
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Luka 2:8-20
[8]Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
[9]Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawangโaria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
[10]Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
[11]maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
[12]Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ngโombe.
[13]Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,
[14]Atukuzwe Mungu juu mbinguni,
Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
[15]Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
[16]Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.
[17]Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.
[18]Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.
[19]Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.
[20]Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, k**a walivyoambiwa.
HABARI NJEMA ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO NA KUSUDI LA KUZALIWA KWAKE HAPA DUNIANI ZILITOLEWA KWA USAHIHI NA AKIWAPA WACHUNGAJI WALIOKUWA WAKILINDA MAKUNDI YAO KWA ZAMU USIKU (WATU WA IMANI WANAELEWA MAANA YA MCHUNGAJI KULINDA MAKUNDI LAKE USIKU "MAANA YAKE WALIKUWA WAOMBAJI") NA
HABARI WALIYOILEZA MALAIKA NI HII:
๐
MSIOGOPE KWA KUWA MIMI NINAWALETEA HABARI NJEMA YA FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE MAANA LEO KATIKA MJI WA DAUDI AMEZALIWA KWA AJILI YENU MWOKOZI NDIYE KRISTO BWANA,
KUKAWA NA FURAHA KUU NA NA WAKAMSIFU MUNGU KWA PAMOJA WAKISEMA:
๐
ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA,
HABARI HIZI NJEMA ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO ZILIZOLETWA NA MOJA KWA MOJA KUTOKA MBINGUNI WAKIWAPASHA NA KWA HABARI YA ZILE HUDUMA TANO K**A ZILIVYONENWA KATIKA (WAEFESO 4:11) HUWENDA PIA , , NA , AU
KUMJILISHA KILA AAMINIYE K**A APENDAVYO ROHO WA MUNGU WALIPEWA HABARI NJEMA,
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA ULE MSTARI WA 15A AKIISHA KULETA HABARI NJEMA ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO WALIONDOKA HUKU WAKIACHA FURAHA KUU NA SHANGWE KWA WACHUNGAJI NA MAKUNDI YAO,
HALLELUJAH ๐๐๐
2. : (HABARI HASI)
LAKINI KWA UPANDE WA PILI HALI ILIKUWA TOFAUTI KABISA NENO LA MUNGU LINASEMA HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO ZILIZOLETWA NA ZILIMFANYA MFALME HERODE AFADHAIKE NA YERUSALEMU PAMOJA NAYE โ๐ณ
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Mathayo 2:1-18
[1]Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
[2]Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
[3]Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
[4]Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
[5]Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
[6]Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;
Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
[7]Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
[8]Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
[9]Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
[10]Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.
[11]Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
[12]Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
[13]Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
[14]Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;
[15]akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
[16]Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.
[17]Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
[18]Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio, na maombolezo mengi,
Raheli akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
KWA UJUMLA TUNA MENGI YA KUJIFUNZA KATIKA HILI LAKINI KWA UFUPI SANA UKICHUNGUZA HABARI ZILIZOLETWA NA NA ZILE ZILIZOLETWA NA NI VITU VIWILI TOFAUTI NA MATOKEO TOFAUTI โ๐ณ
:
1. MALAIKA WALILETA HABARI NJEMA ZA FURAHA KUU YA KUZALIWA MWOKOZI,
(LUKA 2:10-11) NA
HABARI HIZI ZIKAACHA MATOKEO ,
2. LAKINI MAMAJUSI WAO WAKALETA HABARI ZA KUZALIWA HABARI AMBAZO ZILIZUA TAHARUKI KWA UFALME ULIOKUWEPO KATIKA TAWALA ZA WANADAMU NA KWA SABABU MFALME HAKUWA NA UFAHAMU JUU YA NENO LA MUNGU MATOKEO YAKE YALIKUWA YAKISABABISHA MAUAJI MAKUBWA KWA WATOTO KATIKA TAIFA ZIMA,
(MATHAYO 2:2-3).
NENO LA MUNGU LINASEMA "MBONA MATAIFA NA MAKABILA NA WAFALME WANATAFAKARI UBATILI NA KUFANYA SHAURI PAMOJA JUU YA BWANA NA MASIHI WAKE, "ANAENDELEA KUSEMA KINACHOWEZA KUWASAIDIA WAFALME NA WAAMUZI WA DUNIA NIKUFANYA AKILI KWA KUMTUMIKIA BWANA KWA KICHO HUKU WAKIMSHANGILIA NA KUTETEMEKA WAKISHIKA YALIYOMEMA ILI MUNGU ASIJE AKAWAUA,
(ZABURI 2:1-12 ),
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
MATHAYO 2:3-5
[3]Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
[4]Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
[5]Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
๐
NENO LA MUNGU LINATUONYESHA JINSI AMBAVYO MFALME HERODE HAKUWA NA UFAHAMU JUU YA KILICHOANDIKWA NA MANABII KWA HABARI YA UJIO WA YESU KRISTO NA KUSUDI LAKE HAHA DUNIANI NA
SIYO YEYE TU LAKINI PIA PAMOJA NA KUNDI LAKE (YERUSALEMU) WALIOFADHAIKA PAMOJA NAYE WAKIAMINI HABARI KUTOKA KWA (MAMAJUSI) KWAMBA KUNA MFALME MWINGINE WA WAYAHIDI AMEZALIWA HIVYO UFALME WA HERODE ULIKUWA MASHAKANI KUPINDULIWA โ๐ณ
HILI LIKAZAA MAUAJI YA MAELFU YA WATOTO, NA
HATA WALE WALIOMUUNGA MKONO MFALME WAKIHUZUNIKA PAMOJA NAYE PIA MKONO WA UOVU HAUKUWAPITA โ๐ญ
HATA KATIKA KANISA LA LEO KUNA WENGI WAMEPOKEA HABARI TOFAUTI JUU YA YESU KRISTO (KI-BIBLIA ZINAITWA HABARI ZILIZOOGOSHIWA),
WENGINE WALIAMINISHWA KWAMBA YESU KRISTO NI WA DINI FLANI TU,
LAKINI UKWELI NI KWAMBA YESU KRISTO HAKULETA DINI WALA DHEHEBU DUNIANI AMBAVYO WENGI WAMESHIK**ANA NAVYO KULIKO KUSHIK**ANA NA YEYE MWENYEWE ALIYETULETEA MAISHA YA MUNGU YAANI UZIMA WA MILELE KWA KILA AAMINIYE NA BADALA YAKE WAKASHIK**ANA NA MATENDO YA MWILINI NAYO YAKAZAA CHUKI NA MAFARAKANO,
โช๏ธSIJUI WEWE KATIKA CHRISTMAS HII UMEPATA WAPI HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO โ
1. JE NI KUTOKA KWA KUPITIA NAZO ZIMEKUACHIA AMANI NA FURAHA NA TUMAINI JIPYA KATIKA UZIMA WA MILELE, AU
2. JE NI KUTOKA KWA WASOMA NYOTAโ (MAMAJUSI/WAGANGA WA KIENYEJI) NAZO ZIMEACHA MAUMIVU, UCHUNGU, CHUKI, VISASI NA MENGINEYO YANAYOFANANA NA HAYO โ
MATOKEO ULIYONAYO KWA HABARI YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO YANATOKANA NA HABARI ULIYOIPOKEA KATIKA NAMNA CHANYA AU HASI,
NAPENDA LEO UFAHAMU KWAMBA YESU KRISTO SIYO MILKI YA MTU FLANI AU DINI AU DHEHEBU FLANI TU HAPANA,
YESU KRISTO ALIKUJA KWA AJILI YETU SOTE ILI KILA ATAKAYE MWAMINI ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE,
(YOHANA 3:16),
BAADA YA DHAMBI YA ADAMU WOTE TULISTAHILI KIFO LAKINI NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Maombolezo 3:22
[22]Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
It is of the LORD'S mercies that we are not consumed, because his compassions fail not.
ACHA KUJITABISHA YESU KRISTO HANA HAJA YA CHEO CHAKO, AMA UTUME WAKO, AMA UNABII WAKO, AMA UCHUNGAJI WAKO, AMA UASKOFU WAKO, AMA UPADRI WAKO, AMA USHEMASI WAKO, AMA UWAZIRI WAKO, AMA UBUNGE WAKO, AMA URAIS WAKO ISIPOKUWA ROHO YAKO ILI APATE KUIPONYA ISIPOTEE,โ๐ณ
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Yakobo 4:1
[1]Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu ?
LAITI K**A MFALME HERODE ANGEPATA HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO TOKA KATIKA CHANZO SAHIHI BILA SHAKA ANGETAMBUA KWAMBA YESU KRISTO HAKUWA NA HAJA YA UFALME WAKE HIVYO ASINGEJITANISHA KWA KUFADHAIKA NA KUUA WATOTO AKILINDA NAFASI YAKE AMBAYO MWISHO ALIIPOTEZA,
BAADA YA CHRISTMAS NI WAKATI WA KUTAFAKARI UZURI WA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO HATA AKAMTOA YESU KRISTO KWA AJILI YAKO HILO LITAKUOKOA,
ULIMWENGU HAUPENDI UJUE KWELI,
ULIMWENGU UNATAKA UWE K**A HERODE BADALA YA KUMFURAHIA YESU KRISTO UISHIE KUFADHAIKA,
โช๏ธCHRISTMAS MAANA YAKE NI KUSANYIKO LA KRISTO,
โช๏ธLAKINI ULIMWENGU UNAPINGA HILO KWA NAMNA YA UJANJA-UJANJA,
MFANO:
โช๏ธULIMWENGU UNAMUONDOA CHRISTO KWA ALAMA YA "X" NA KUACHA "MAS" TAFSIRI YAKE IKIWA NI KRISTO HAKUZALIWA NA WALA HANA KUSANYIKO (X-MAS) BE VERY CAREFUL โ๐ณ
๐HUU NI MFANO HALISI KATIKA KIPINDI HIKI CHA CHRISTMAS JINSI AMBAVYO MTU ANAWEZA KUPOKEA HABARI ZA KUZALIWA KWA YESU KRISTO ISIVYO SAHIHI NA KWA SABABU HIYO AKAISHIA KATIKA NAMNA YA MATESO MBALI NA FURAHA ALIYOKUWA AMEKUSUDIWA,
BAABA YA CHRISTMAS TAFUTA KUMJUA SANA YESU KRISTO KWA MAPANA NA MALEFU, KIMO NA KINA NA KWA KUIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAKUWEKA HURU,
NENO LA MUNGU LINASEMA KATIKA:
๐
Ayubu 22:21
[21]Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
BAADA YA CHRISTMAS NAKUTAKIA SAFARI NJEMA YA MAISHA YA IMANI KWA JINA LA YESU KRISTO WANA ZARETI MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
MERRY CHRISTMAS ๐ ๐ ๐ AND
HAPPY NEW YEAR 2026.