Efatha Church Makabe

Efatha Church Makabe Christian Church
Efatha Makabe is located at Mbezi Mwisho,Makabe Road near Makabe Police Station

KUNDI LA WANAWAKE LILILOONGOZANA KATIKA KABURI KWENDA KUMPAKA BWANA YESU MAFUTA:Ni wakina nani hao? Luka 24:9-10 “Wakaon...
09/08/2026

KUNDI LA WANAWAKE LILILOONGOZANA KATIKA KABURI KWENDA KUMPAKA BWANA YESU MAFUTA:

Ni wakina nani hao? Luka 24:9-10 “Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote. Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao;”

Pale wanaume walipokuwa wamejawa hofu lakini hawa wanawake waliamka asubuhi na mapema wakaenda kumpaka Yesu mafuta, hawakuuliza wanaume wako wapi, bali waliamka na kwenda moja kwa moja kwa Bwana wao.

MWANAMKE WA EFATHA:
Wewe mwanamke wa Efatha onesha upendo wako kwa Kristo Mwokozi wako;
Luka 23:28 “Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.” Nakuita wewe mwanamke wa Efatha, k**a Biblia isemavyo kuwa wanawake ni jeshi kubwa, onesheni hivyo.

Wagalatia 6:7-8 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.”

Kile utakachoenda kufanya mbele za Baba yako wa mbinguni usifanye katika mwili bali katika roho maana katika mwili utavuna uharibifu lakini katika roho utavuna uzima wa milele kwako na wa kizazi chako.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

WANAWAKE WALIYOONESHA NGUVU WALIZONAZO KATIKA BIBLIA:ABIGAIL – MAANA YA JINA HILI NI (FURAHA YA BABA)Abigail alikuwa ni ...
09/08/2026

WANAWAKE WALIYOONESHA NGUVU WALIZONAZO KATIKA BIBLIA:
ABIGAIL – MAANA YA JINA HILI NI (FURAHA YA BABA)

Abigail alikuwa ni mke wa Nabali, alipotambua kuwa mumewe amefanya mambo yasiyofaa na akajua kuwa Daudi anakuja ili kumwangamiza mumewe aliamua kuchukua chakula na kumfuata Daudi.

Abigail alikutana na Daudi katika nyika, akampa Daudi chakula na akamshawishi Daudi asilipe kisasi kwa kumwangamiza mumewe na Daudi akaridhia. Wanawake wanazo nguvu; wanaweza kwenda mahali na kuzuia hasira ya mtu, wanazo hizo nguvu na huo ujasiri.

1 Samweli 25:25 “Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana k**a lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.”

MWANAMKE MSAMARIA.

Yohana 4:4-42 “ Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe…''

Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya Neno lake. Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.”

Mwanamke Msamaria alihubiri Injili na akavuta watu wengi sana kwa Yesu, mwinjilisti wa kwanza aliyefanya uinjilisti mkubwa ni huyu Mwanamke Msamaria, unaweza kuona namna wanawake walivyo, wanaweza kutoka katika uovu na akawa mtumishi ambaye ana ushawishi mkubwa sana, wanawake hawasubiri uthibitisho bali wanajishawishi wenyewe kwamba wanazo nguvu na kwamba wamekusudiwa kufanya hilo jambo, lakini wanaume wanakuwa na maswali mengi sana kabla ya kufanya jambo.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

SOMO: MWANAMKE WA EFATHAZaburi 68:11 “BWANA analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;” Biblia inase...
09/08/2026

SOMO: MWANAMKE WA EFATHA

Zaburi 68:11 “BWANA analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;”

Biblia inasema wanawake ni jeshi kubwa, maana yake ni kuwa; kuna nguvu kubwa inayowasukuma wanawake. Wamama wanapokuwa wanajifungua wanatumia nguvu sana ili kusukuma mtoto atoke, k**a wanawake wanaweza kusukuma mtoto mpaka atoke basi elewa kuwa wana nguvu kubwa na Mungu anatambua hilo na ndiyo maana akasema “Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa”

Kutoka 1:9 “Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si k**a wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.”

Hivyo wanawake wanazo nguvu za kujihudumia; wanawake wana nguvu ndani yao ya kujisaidia wenyewe, maana yake wao si k**a wanaume, wanaume wana nguvu za mwili; wanawake hawana misuli ya nguvu lakini wana nguvu ndani yao, ndiyo maana huweza kusukuma jambo lolote na likatokea, hivyo wakiwa mahali popote wanasababisha mambo yaende. Wanawake ninyi ni jeshi kubwa na mnazo nguvu, kwa maana Mungu mwenyewe ametangaza kuwa wanawake ni jeshi kubwa.

Wamisri waliwatambua wanawake wa Kiebrania ya kwamba wanazo nguvu, katika Kutoka anasema “wazalisha wakamwambia Farao, ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si k**a wanawake wa kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.”

Nakutangazia leo wewe mwanamke wa Efatha kuwa wewe siyo k**a mwenye dhambi, unazo nguvu katika roho, unazo nguvu ndani ya moyo wako, unaweza kuomba pasipo kukoma, una uwezo wa kushuhudia pasipo kuogopa chochote. Simama na chukua nafasi yako, wewe una nguvu.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

SIKU YA PARAPANDA. Siku ile itakuwa ni siku makini sana, dunia yote itanyamaza kimya, wakati wana wa Mungu wanainuliwa, ...
09/08/2026

SIKU YA PARAPANDA.

Siku ile itakuwa ni siku makini sana, dunia yote itanyamaza kimya, wakati wana wa Mungu wanainuliwa, siku ile ni siku ya kitisho, tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu hakujawahi kutokea tetemeko la aina hiyo, tetemeko la ajabu litaitikisa dunia wakati wana wa Mungu wanaondoka.

Kwa nini dunia itatikisika? Ni ili kuruhusu makaburi kufunguka na watu watoke huko, kuruhusu bahari kutoa watu walioko huko.
Huu siyo wakati wa kuwaandaa watu wanene kwa lugha mpya au waponywe magonjwa yao, la! Bali ni ili kuwaandaa watu kwa ajili ya Unyakuo.

Usifikiri Kanisani ni mahali pa mzaha mwana wa Mungu, bali ni mahali makini sana, una heri wewe unayesikia kile ambacho anaongea mtumishi wa Mungu na kutenda sawa sawa, yale unayoshindwa sawa lakini yale unayoweza kuyafanya na ukakataa kufanya hiyo ni mbaya sana. Una heri wewe ambaye utaiona siku ile na kuingia. Wewe uliyepata Neema ya kuokoka ndani ya Efatha usije ukadharau au kusahau kile ulichokipata Efatha.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

09/08/2026

Unapotaka kumsifu Mungu hakikisha moyo wako ni msafi; kwa maana sifa zinazotoka kwenye moyo safi na halisi ndizo zinazom...
09/08/2026

Unapotaka kumsifu Mungu hakikisha moyo wako ni msafi; kwa maana sifa zinazotoka kwenye moyo safi na halisi ndizo zinazomfanya Mungu akufurahie, k**a unajua moyo wako si safi na una vitu ndani yako, kabla haujaanza kumsifu Mungu tubu kwanza na uusafishe moyo wako ndipo umsifu Mungu. Mungu anapendezwa na sifa zinazotoka katika moyo safi.

Omba na useme:
Baba sasa naelewa, ninatubu, nisamehe, Roho Mtakatifu nitakase, Bwana Yesu acha damu yako inioshe maana nataka kumsifu Baba, Bwana Yesu niruhusu.

Yawezekana unaomba sana kuhusu chakula, mavazi na vitu vya duniani lakini haujawahi kumwambia Mungu chochote kuhusu Ufalme wake, mwambie leo; dunia itapita na mambo yake lakini Neno la Mungu halitapita, amesema atakuja kuwachukua watu wake, je! Wakati huo akija wewe utakuwa ni mmoja wao?

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.

Zaburi 20:1-9 “BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na...
09/08/2026

Zaburi 20:1-9 “BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa Jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake; Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja Jina la BWANA, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. BWANA, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.”

Mwana wa Mungu unapaswa kutambua kuwa unapotoa sadaka zako mbele za Bwana Yesu si bure, bali huwa inazungumza mbele za Bwana. Unapotoa matoleo yako kwa usahihi mbele za Bwana Yesu, Yeye atakukumbuka, atakumbuka sadaka zako na atakufanyia usaidizi pindi pale utakapokuwa una uhitaji.

© MTUME ELIAKUNDA MWINGIRA

Zaburi 150:1-3 "Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo y...
09/08/2026

Zaburi 150:1-3 "Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;"

IBADA YA PAMOJA YA SIKU YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE TAREHE 09.08.2026Leo ni ibada ambayo unaenda kumwona Mungu k...
09/08/2026

IBADA YA PAMOJA YA SIKU YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE TAREHE 09.08.2026

Leo ni ibada ambayo unaenda kumwona Mungu kwa namna ya tofauti, hutatoka k**a ulivyokuja maana unaenda kukutana na Bwana Yesu hivyo kaa tayari kupokea yale ambayo Mungu amekuandalia kwa ajili ya utukufu wake.

© MCHUNGAJI CLAUDIA CHALLO

IBADA YA NENOMCH:PATRICK MHINA SOMO:MISINGI YA VIZAZI MAMBO 5 YANAYO HALIBU MISINGI YA VIZAZI 1.Miungu ya wafu.2.Roho za...
19/07/2026

IBADA YA NENO
MCH:PATRICK MHINA
SOMO:MISINGI YA VIZAZI

MAMBO 5 YANAYO HALIBU MISINGI YA VIZAZI
1.Miungu ya wafu.
2.Roho za wafu.
3.Sadaka za wafu.
4.Agano la mauti.
5.Madhabahu za wafu.

Katika sehemu hizi Tano ndipo ufalme wa giza na mamlaka zake wanapata Nguvu

1.Roho za wafu
Roho za wafu ni wale ambao wamekufa wakiwa hawajaokoka ,Roho za wafu ndizo hujenga misingi kwenye ukoo na kwenye familia
Zaburi 11:3
K**a misingi ikiharibika,
Mwenye haki atafanya nini?

*Wazazi wetu waliingia mikataba na shetani kwasababu hawakuwa wanamjua kristo ,kwanzia Hapo ndo matatizo yalipo anzia Kwasababu kuzimu inauhalali na mtu.

*Roho hizi ndizo zinazo pingana na kushindana na mafanikio yako,
Kwenye Roho za wafu ndipo zinapo jengeka tabia za familia(mfano k**a baba zako walikuwa walevi nawewe inakuwa mlevi k**a wao ,unakuwa mlevi kwasababu tabia inatembea katika familia .

-kwa kupitia wazazi wetu familia nyingi zinakuwa mateka, nafsi za watu zinak**atwa kuzimu hii ni kwasababu ya asili za baba zetu.
Hagai 1:7
Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.

2.DHABIHU
Dhabihu ni zaidi ya sadaka,dhabihu ni kile kitu ambacho kinauma mfano kile kitu Cha thamani unachokipenda ,mtu ,mali

Taswira ya zile dhabihu katika ulimwengu wa Roho zinaishi.
-misingi ya Roho za wafu ndizo zilizo fungulia Roho za uharibifu kwako

*Roho za wafu zinafanya kazi kupitia DNA yako .ili uweze kujitoa lazima utumie damu ya Yesu kwasababu Haina chembe chembe za uharibifu wowote lakini haliwezi kufanya kaz mpaka uamue.

3.BARAKA
Hesabu 6:22-27
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia;Bwana akubarikie, na kukulinda;Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani.Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.

-Baraka ya Mungu inakaa juu ya ufahamu wa mtu kwasababu baraka sio mafanikio bali baraka ni ni nguvu ya Mungu inayokaa juu ya ufahamu wa mwanadamu.

*Kila familia ambayo Mungu ameiweka chini ya dunia inabaraka zake , ile baraka ikiwa ndani yako inakufanya ufanikiwe .

Mungu akikufanikisha Kwa baraka zake anakuwa mlinzi wa baraka zako

*Mungu anam’bariki mtu ambaye ni mnyenyekevu na ni jinsi gani anavyo muheshimu yeye.

Address

Mbezi Makabe
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
23:00 - 05:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 07:30 - 17:00

Telephone

+255713402322

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Makabe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share