Tanzania Episcopal Conference

Tanzania Episcopal Conference This is an official page for the Tanzania Episcopal Conference with its headquarters in Kurasini Dar es salaam Tanzania.We bring evangelism to you

~JOIN US ONLINE ON SATURDAY 11th APRIL~10 AM (SAST), 11 AM (EAT), 1.30 PM (IST)PROACTIVE FAITH LEADERSHIP IN TIMES OF CR...
10/04/2020

~JOIN US ONLINE ON SATURDAY 11th APRIL~
10 AM (SAST), 11 AM (EAT), 1.30 PM (IST)
PROACTIVE FAITH LEADERSHIP IN TIMES OF CRISIS

Online Webinar on the Important Role of Faith Leaders in Africa and India in Responding to Covid-19
Hosted by the Global Interfaith WASH Alliance, in partnership with UNICEF TANZANIA

Taking part in the high-level and unique panel:

- Pujya Swami Chidanand Saraswatiji - Muniji: President, Parmarth Niketan; Co-Founder/Chair, Global Interfaith WASH Alliance (GIWA)�
- Archbishop Thabo Makgoba: South African Anglican Archbishop of Cape Town, Trustee of GIWA
- Archbishop Dr. Maimbo Mndolwa: Primate of Tanzania; Bishop of Tanga�
- Archbishop Dr. Frederick Shoo: Presiding Bishop,� Evangelical Lutheran Church in Tanzania
- Sadhvi Bhagawati Saraswatiji: Secretary-General, Global Interfaith WASH Alliance; President, Divine Shakti Foundation
- Rev. Canon Moses Matonya: Secretary General, Christian Council of Tanzania (CCT)
- Rev. Dr. Charles Kitima - Secretary General, �Tanzania Episcopal Conference
- James Elder - Chief of Communications, Eastern and Southern Africa, UNICEF

TUNE IN here on the GIWA page or the Parmarth Niketan YouTube Channel to be part of this historic LIVE event this Easter weekend!

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1071413353221160&id=648150258880807
20/03/2020

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1071413353221160&id=648150258880807

JANGA LA KORONA: TEC YATOA TAMKO

Machi 19/2020

Wapendwa,

Maaskofu, Mapadri, Watawa na Waamini wote,

Tumsifu Yesu Karisto

YAH: KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KUSAMBAA KWA VIRUSI VYA CORONA NCHINI.

Wapendwa Taifa la Mungu,

Sisi maaskofu wenu kwa kuzingatia taarifa ambayo ilitolewa na serikali kuhusu kugundulika kwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya Corona hapa nchini na maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa tarehe 17/3/2020 ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivi nchi nzima, tunatoa maelekezo yafuatayo kwa waamini wote kuhusiana na huduma zetu za Kichungaji Katoliki;

A. SALA.

Tunawaomba waamini wote kusali sala maalumu ili kumwomba Mungu atukinge dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona. Tumwombe Mungu aendelee kutulinda kwa mkono wake na kuwaponya wale wote ambao wamepata maambukizi haya. Na wataalamu wetu wapate ufumbuzi wa kisayansi kuzuia kuenea kwa virusi hivi.

Sala hii ni jukumu la kila mtu mmoja na jukumu la pamoja k**a Kanisa kitaifa. Na Kutakuwa na sala maalumu itakayotolewa na maaskofu lakini kila mmoja wetu anaweza kusali sala inayomfaa kadri inavyoelekezwa na Askofu Jimbo.

Ni wakati sasa wa kusali na kufanya toba k**a taifa ili kujiunganisha na Muumba wetu.

B. KWENYE IBADA MBALIMBALI ZA LITURUJIA.

Tunaagizwa kuzingatia taratibu za kujikinga na virusi vya Corona kadri serikali ilivyoagiza.

Hakikisha kutumia maji safi kwa kuosha mikono kwa sabuni mara kwa mara unapokuwa nyumbani kwako na unapokwenda kujumuika na wengine katika shughuli za kiibada.

Maji ya baraka ya kuchovya kwenye milango yatasitishwa kwa muda na tutatakiwa kutumia maji ya baraka kadri tutakavyoelekezwa kijimbo.

Wakati wa kutakiana amani tusipeane mikono na waamini wafumbe mikono na kuinamiana kwa heshima.

Waamini watakomunika kwenye mikono tu, mapadri wazingatie hili wanapowakomunisha watu.

Mapadri wanapoadhimisha Misa pamoja , watakomunika maumbo yote mawili kwa kuchovya Hostia Takatifu.

Waamini wote wanaombwa kutoshiriki ibada na jumuiya ndogondogo k**a unajisikia kuumwa. Badala yake washiriki ibada na huduma kwa njia ya redio na njia nyingine zitakazoelekezwa.

Kila muumini ajitahidi kutumia vitabu vya ibada vya kwake.

Wale wote wanaohesabu fedha za matoleo watumie sanitizers kwa ajili ya kusafisha mikono.

C. HUDUMA ZA MASAKRAMENTI.

Wagonjwa watapakwa mafuta kwa kutumia pamba na padri aambatane na mhudumu wa afya anapokwenda kwa wagonjwa.

Wakati wa kupokea Sakramenti ya Kitubio, Padri anayeungamisha na muumini wasiangaliane uso kwa uso, na kiti cha kitubio kisitumike bali maungamo yafanyike katika sehemu ya wazi kwa kuzingatia sharia za maungamo.

D. MAADHIMISHO YA JUMA KUU.

Ibada ya kuabudu msalaba ishara ya wokovu wetu, itafanyika kwa kuinamia msalaba bila kuugusa.

Sisi Maaskofu wenu tutaendelea kutoa maelekezo kadri serikali yetu itakavyoendelea kutoa miongozo na maelekezo ya jinsi ya kudhibiti maambukizi katika nchi yetu.

E. MIKUTANO NA MAKONGAMANO.

Mikutano yote ya vikundi vya sala na vyama vya kitume itasitishwa kwa muda.

Neema na Amani ya Kristo iwe nanyi nyote,

Ni sisi Maaskofu wenu,

Mha. Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1069421036753725&id=648150258880807
17/03/2020

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1069421036753725&id=648150258880807

TAARIFA MAHUSUSI TOKA JIMBO KUU KATOLIKI DSM

Wah. Mapadri, Mashemasi, Watawa na Waamini wote, Kristo. Napenda kuwafahamisha maagizo yaliyotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM, Mhashamu Yuda Thadei Ruwa'ichi, Leo tarehe 17 Machi 2020 Maagizo hayo yanalenga kujihadhari na ugonjwa wa CORONA. Nayo ni:

1. Kutopeana Amani kwa mikono wakati wa Misa.

2. Kupokea Ekaristi Takatifu kwa mikono tu na siyo kwa midomo. Ila umakini uhimizwe ili Yesu anayebaki mikononi katika vipande vidogo vidogo, ASITUPWE CHINI

3. Kutotumia Maji ya Baraka ya Kuchovya. Sehemu zote yalimowekwa (Milangoni MAKANISANI) YAKAUSHWE. Katika Adhimisho, Kiongozi wa ibada anaweza kuwanyunyizia Waamini maji ya Baraka.

4. Tunaombwa kuchukua kila tahadhari ili kujiepusha na ugonjwa huu.

5. Kufuata kwa makini maelekezo yaliyotolewa na Serikali katika kuudhibiti ugonjwa huu.

N.B: maelekezo mengine yatatolewa taratibu

Pd. Frank Mtavangu
Katibu-Jimbo

USIKOSE kipindi hiki maalum Jumapili hii Star TV..
28/02/2020

USIKOSE kipindi hiki maalum Jumapili hii Star TV..

21/02/2020
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=831686097193888&id=648150258880807
12/05/2019

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=831686097193888&id=648150258880807

TEC INA MATUMAINI MAKUBWA NA UTUME WA ASKOFU MKUU NKWANDE

Rais wa TEC Baba Gervas Nyaisonga amwombea ushirikiano kwa waamini.

Kanisa Katoliki linajivunia hospitali ya rufaa ya Bugando na chuo cha Mtakatifu Augustino SAUT.

Kanisa Katoliki linajivunia utoaji bora wa huduma za kijamii nchini.

Mshik**ano baina ya serikali na Kanisa Katoliki unahitajika kufanikisha ufanisi katika utoaji huduma hasa kwa watoto na vijana.

Kapongeza nia njema ya serikali kushirikiana na Kanisa Katoliki.

Askofu Mkuu Renatus Nkwande ni mchapakazi.

Apewe ushirikiano ili mafanikio yaliyopo yaendelezwe.

Waamini wampe ushirikiano Askofu Mkuu Renatus Nkwande alitumikie vyema Jimbo Kuu Katoliki Mwanza na Jimbo Katoliki Bunda.

Bernard James-Milele Amina!

https://www.facebook.com/648150258880807/posts/831659653863199/
12/05/2019

https://www.facebook.com/648150258880807/posts/831659653863199/

ASKOFU MKUU RENATUS NKWANDE AANDIKA HISTORIA MWANZA

ATOA KAULI 9 ZA MATUMAINI KWA WANANCHI

Namshukuru Rais John Magufuli kwa yote anayoyatenda kwa sababu yana nia njema kwa nchi yetu

Watanzania wanapendana licha ya changamoto kadhaa zilizopo

Kanisa lazima liwe mwalimu na liendelee kufundisha na kuielimisha jamii.

Imani potofu za uchawi ni ushamba wa elimu na kushindwa kumwamini Mungu.

Nia ya Kanisa kujenga na kuboresha huduma za kijamii k**a elimu, afya, maji n.k zina lengo jema kabisa la kuikomboa jamii

Nachukia sana Ushoga na kutoa mimba, jamii isiige mambo haya ya kishenzi.

Taasisi zinazotetea ushoga na kutoa mimba zinamuunga mkono shetani.

Serikali isilegee kutokana na ahadi na misaada toka nje bali ikemee vikali ushoga na utoaji mimba

Amewaomba waamini wote na serikali wampe ushirikiano katika utume wake

NB: Aliteuliwa na Baba Mtakatifu Fransisko tarehe 11 Februari 2019

Ni Askofu Mkuu wa 3 na Askofu wa 5 kwa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.

Baba Mtakatifu amteua kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Bunda.

Bernard James-Milele Amina!

Address

Dar Es Salaam
2133

Telephone

+255713412407

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Episcopal Conference posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Tanzania Episcopal Conference:

Share