Upendo wa Yesu

Upendo wa Yesu Hakuna Upendo pasipo Mungu maana Mungu ni Upendo wenyewe. Twajifunza kwa Kristo Upendo na Uvumilivu.

KUTOKA MASHAKA NA KUTOKUAMINI HADI KUFIKIA IMANI YA KWELI KATIKA KRISTOHuu ni ushuhuda huu wenye nguvu sana, ambapo Joan...
11/06/2026

KUTOKA MASHAKA NA KUTOKUAMINI HADI KUFIKIA IMANI YA KWELI KATIKA KRISTO

Huu ni ushuhuda huu wenye nguvu sana, ambapo Joan anasimulia safari yake kutoka kwenye mashaka na kutokuamini hadi kufikia imani ya kweli kwa Kristo, akieleza jinsi alivyokutana na Mungu katikati ya ugonjwa mkali na maswali mengi moyoni mwake.

Licha ya kujaribu kuupinga ukweli na kuuthibitisha Ukristo kuwa si wa kweli, Joan anapitia mabadiliko makubwa ya ndani baada ya kutambua ukweli kuhusu Yehoshua (Yesu) kuwa ndiye Masihi wa Ulimwengu na Wayahudi wote.

Akiwa anakabiliana na magonjwa zaidi ya 75 yaliyokuwa yakimdhoofisha, pamoja na saratani ya endometria, Joan hatimaye anapata uponyaji kupitia maombi na toba ya kweli. Leo hii, ana shauku kubwa ya kuwafundisha wengine kuhusu Israeli na imani yake, huku akiendelea kushikilia urithi wake wa Kiyahudi kwa kina na wakati huo huo akimkubali Yeshua k**a Masihi wake.

Ushuhuda wa Joan ni ushuhuda uliobeba nguvu ya uponyaji ya Mungu na namna kukutana na ukweli wake kunavyoweza kubadilisha maisha kabisa.

Alikuwa amekonda sana kiasi kwamba hata kuinua kichwa chake kitandani ilikuwa shida. Mwili wake ulikuwa umechoka sana. Nguvu zote zilikuwa zimeisha. Na sasa madaktari walikuwa wanamwambia:

“Una saratani mbaya sana. Utahitaji miezi sita ya chemotherapy yenye nguvu sana, na wiki sita za mionzi kila siku.”

Aliposikia hayo, kitu pekee kilichokuwa kichwani mwake ni:

“Hii tiba itanua.”

Lakini kabla ya kufika kwenye kitanda hicho cha hospitali, kulikuwa na safari ndefu sana iliyomfikisha hapo.

Joan alizaliwa na kukulia Southern California katika Familia ya Kiyahudi katika mila na tamaduni zao. Kumbuka Wayahudi wako strict sana kwenye mila na taratibu zao. Kila wiki walikwenda katika sinagogi zao kwa masomo ya dini, na wakishiriki sikukuu zote muhimu za Kiyahudi.

Akiwa na miaka 12, familia yao ilisafiri kwenda Israel huo ni mwaka 1966. miezi mitano kabla ya vita vya mwaka 1967.

Anakumbuka siku moja akiwa sehemu ya juu akiangalia mbali, mwongoza watalii akiwaambia:

“Huo ndio mji wa kale… lakini haturuhusiwi kwenda huko.”

Akasimama akitazama kwa mbali na kujiuliza

“Ingekuwaje k**a tungeruhusiwa kuingia huko?”

Mama yake alikuwa ameishi Israel tangu akiwa na miaka 12 mpaka 24. Alikuwa sehemu ya harakati za siri za Israeli, akafanya kazi k**a jasusi kwa Waingereza.

Kwa hiyo, hata akiwa anaishi California, Israel ilikuwa katika damu yake. Kadri alivyokuwa anakua, alitamani kuielewa zaidi dini yake ya Kiyahudi. Walifundishwa hadithi za Nuhu, Musa na Kutoka Misri, lakini hakuwahi kuona picha nzima ya mpango wa Mungu kwa taifa la Israeli kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Kuna kitu hakikuwa kinaungana pamoja moyoni mwake.

Shuleni kwao alikuwa Myahudi pekee. Walipoimba nyimbo za Krismasi na jina “Yesu” lilipotajwa, kwa namna fulani alijisemaea,

“Hilo jina halipaswi kutoka kinywani mwangu.”
Kwa hiyo kila walipolitaja, alikuwa anafunga mdomo wake.

Mpaka alipofika chuo kikuu. Huko alipata roommate Mkristo mwaka wa kwanza. Kwa macho yake, Wakristo walikuwa watu dhaifu tu waliotafuta kitu cha kuwafariji kihisia. Aliamini hawakuwa na msingi wa kweli wa kile walichokiamini.

Lakini boyfriend wa roommate wake alikuwa kijana mtulivu aitwaye Gary. Mara nyingi alikuwa anazungumza naye kuhusu Mungu.
Siku moja akamwambia:

“Gary, nitathibitisha kwamba kile mnachoamini hakina msingi wowote.”

Gary akamjibu kwa utulivu: “Sawa. Lakini kabla hujaanza safari yako, naomba usome kitabu kimoja.” Akakubali.

Kitabu kile kilikuwa kinaitwa Late Great Planet Earth. Na hicho ndicho kilibadilisha kila kitu. Kwa mara ya kwanza maishani mwake, alianza kuona picha kubwa ya historia ya Wayahudi kuanzia Mwanzo hadi mwisho wa mpango wa Mungu.Kilichomshtua zaidi kilikuwa unabii. Hakuwahi kufundishwa unabii kwenye sinagogi.

Lakini sasa alikuwa anaona jinsi Mungu alivyotoa utabiri maalum mamia na maelfu ya miaka kabla na mambo hayo yakatokea sawasawa kabisa. Na unabii huo wote ulikuwa unaelekeza kwa mtu mmoja Yehoshua (Yesu).

Jambo hilo lilimkasirisha sana.Kwa sababu kitu cha mwisho kabisa alichotaka maishani mwake… kilikuwa kuwa Mkristo.

Akaenda kwa rabbi wake na kumuuliza:
“Naomba unielezee Isaya 53. Kwa sababu hii inaonekana kabisa k**a Masihi wa Agano Jipya.”

Rabbi aliiangalia ile sura.
Halafu akasema kwa uaminifu:
“Samahani… siwezi kukuelezea. Sijui.”

Kadri alivyoendelea kusoma, kila kitu kilikuwa kinaonyesha upande mmoja tu. Kwamba Yeshua ndiye Masihi wa Wayahudi.Na jambo hilo lilimvuruga sana kwa sababu lengo lake tangu mwanzo lilikuwa kupinga hilo.Usiku mmoja akiwa amelala kitandani, akiwa amechanganyikiwa kabisa, alimlilia Mungu.

“Mungu… sitaki kuwa Mkristo.”

Halafu akaongeza:
“Lakini k**a kweli unataka kuniokoa… basi fanya utakavyo.”

Ndani yake alifikiri:
“Sawa. Hakuna kitakachotokea.”

Lakini ghafla…akaanza kuhisi kitu kinatembea kuanzia kichwani mwake. Kana kwamba uwepo fulani ulikuwa ukimwambia kuwa Mungu alikuwa anamsafisha dhambi zake.Hali ile ikatembea kutoka kichwani taratibu… ikashuka mwilini mpaka miguuni.

Usiku huo alilala vizuri.Na alipoamka asubuhi…alikuwa mtu tofauti kabisa. Nia yake ilibadilika. Sababu za kuishi zikabadilika.
Yule msichana aliyekuwa anaogopa hata kutamka jina la Yesu sasa alikuwa anasimama kwenye stage (mimbari) chuoni mbele ya mamia ya watu akishuhudia:

“Mungu ni halisi. Na Yesu ndiye Masihi wa Wayahudi.”

Miaka ikapita. Akaolewa. Baadaye ndoa yake ikaishia kwenye talaka baada ya miaka mingi.Kisha maisha yakaanza kubadilika tena na safari hii kwa maumivu makali.

Alipata fibromyalgia. Chronic fatigue syndrome. Mwili wake ulikuwa unateseka kila siku kwa miaka karibu nane.Hali ilizidi kuwa mbaya.Halafu madaktari wakampa habari nyingine mbaya zaidi kuwa ana Saratani ya kizazi. Stage 3C.

Walimwambia:
“Una nafasi nzuri ya kupona ikiwa utapitia chemotherapy kali kwa miezi sita, halafu tiba mionzi kila siku kwa wiki sita.”
Alishtuka sana.

Kwa sababu tayari alikuwa dhaifu sana.
Alikuwa amekonda kupita kiasi. Hata kutembea hadi kwenye mailbox ya nyumba yake ilikuwa kazi kubwa.
Ndani yake alifikiri:

“Tiba hii itanua.”

Lakini badala ya kukata tamaa, alianza safari nyingine.Safari ya toba.Usiku mmoja wa Mkesha wa Mwaka Mpya, alimwaga moyo wake mbele za Mungu huku analia.

“Bwana… unisamehe. Sikujua hata jinsi moyo wangu ulivyokuwa wenye dhambi.”

Akamwambia Mungu:
“Nitakesha mpaka unionyeshe kuwa uko pamoja nami.” Aliendelea kukesha mpaka saa tisa za usiku. Hakuhisi chochote. Lakini hakukata tamaa.

Kila siku aliendelea kudumu katika kuomba. Kuendelea kutubu. Kuendelea kumtafuta Mungu.Na polepole kila kitu kilianza kubadilika ndani yake.Alianza kusoma Biblia kwa namna ambayo hajawahi kufanya kabla.Alikesha mpaka saa nane au saa tisa usiku akisoma.

Anasema:
“Kila neno lilionekana k**a pumzi halisi ya Mungu.” Wakati huo huo alianza kula vitu ambavyo zamani vilikuwa vinamfanya awe mgonjwa k**a ice cream, dairy, gluten, chips lakini safari hii mwili wake haukupata shida k**a zamani.

Siku moja akasema:
“Lazima nijaribu kutembea hadi kwenye mailbox.”
Na akafanikiwa.Bila maumivu makali. Polepole, ndani ya miezi nane mpaka mwaka mmoja… Mungu alimponya.Si saratani tu.
Lakini pia karibu magonjwa 75 aliyokuwa nayo.

Na kitu kikubwa zaidi ambacho alikuwa amepambana nacho tangu akiwa mtoto mdogo ni Hofu kali na wasiwasi.

Anasema:
“Nilikuwa na nguvu. Sikuhofia tena. Kwa sababu nilijua Mungu wa ulimwengu wote alikuwa upande wangu.”

Halafu akaeleza jambo ambalo lilikuwa muhimu sana kwake;

“Hapana, sikugeuka kutoka kuwa Myahudi kwenda dini nyingine.”

Wayahudi wamekuwa wakimsubiri Masihi kwa maelfu ya miaka.Na yeye aliamini kuwa amempata.Yeshua.Masihi wa Wayahudi.

Mwaka 2012 aliporudi Israel, alipouona Mji wa Kale kwa macho yake mwenyewe, aliona k**a amerudi nyumbani.

Baadaye akaandika travel guide kuhusu Israel kwa ajili ya waamini, akaanza kupeleka vikundi Israel, na akaanzisha taisisi ya kusaidia kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa Israel na kusaidia manusura wa Holocaust.

Na kila alipofikiria maisha yake…...alijawa na shukrani. Kwa sababu Mungu alimtoa kutoka mahali pa maumivu, hofu, ugonjwa, na kukata tamaa… na kumpa maisha mapya.

Hapa kuna la Kujifunza;

Yesu bado anaokoa watu wake. Hakuna wokovu mkuu namna hii. Tafuta taaluma zote na unajimu wa maarifa ya kila kitu bado Yesu atabaki kuwa Mungu katika nia ileile kuwaokoa waliopotea na kuwarejesha.

Wakati mwingine Mungu hukuruhusu ufikie mwisho wa nguvu zako ili ujue kwamba tumaini la kweli halipo kwenye uwezo wako, afya yako, au mipango yako, mwenza wako bali kwake pekee.

Pia, si kila mtu anayemtafuta Mungu anaanza akiwa tayari kuamini. Wengine wanaanza safari yao wakitaka kupinga ukweli. Lakini ukweli unapokuwa wa kweli, una nguvu ya kugusa moyo hata wa mtu aliyepinga zaidi.

Na jambo kubwa zaidi: Usikate tamaa hata hali yako inaonekana imefika mwisho. Ukiwa bado unapumua, bado kuna tumaini. Mungu anaweza kubadilisha moyo, kuponya maisha, na kuleta nuru hata katikati ya giza kubwa kabisa.

Natamani Mtu mmoja aokoke leo. Ikiwa uko tayari komenti hapa chini
Upendo wa Yesu

10/06/2026
Mama yake Johnny akaokoka.Kutoka kuwa Mbuddha wa maisha yake yote, sasa alikuwa shemasi kanisani. Johnny aliona k**a mam...
04/06/2026

Mama yake Johnny akaokoka.Kutoka kuwa Mbuddha wa maisha yake yote, sasa alikuwa shemasi kanisani. Johnny aliona k**a mama yake amechanganyikiwa.Siku moja gari la mama yake liliharibika. Akamwomba Johnny ampeleke kanisani.Hakutaka aingie.

Amshushe tu kanisani arudi zake.

Johnny alipofika pale, alinusa harufu fulani.
Jajangmyeon.Tambi za maharage meusi ambazo alikuwa akizitamani tangu akiwa gerezani.Mchungaji alikuwa anazipika kwa ajili ya fellowship.

Mchungaji akatoka nje, akamshukuru Johnny kwa kumleta mama yake, kisha akasema:
“Ngoja nikufungie chakula uende nacho.”
Lakini Johnny alikuwa amelelewa kwenye culture ya heshima za mtaani.Hakuweza kuchukua chakula aondoke bila kuingia.

Akasema:
“Nitakaa dakika chache.”
Dakika chache zikageuka saa moja na nusu.
Akiwa amekaa mezani na bakuli la tambi mbele yake, Johnny alimwambia mchungaji wazi:
“Mimi ni Mbuddha. Siamini Mungu.”
Mchungaji hakubishana naye.
Alimuuliza swali moja:
“Unafikiri dhambi ni nini? Na wewe ni mwenye dhambi?”

Johnny akasema:
“Dhambi ni kufanya mabaya k**a kuiba, kuua, kusema uongo. Ndio, mimi ni mwenye dhambi.”

Mchungaji akatabasamu.
“Sio hivyo.”

Maneno hayo yakamshangaza Johnny akitafakari kwa udadisi "Umesemaje?"
Mchungaji akafungua Yohana 16:9:
"Dhambi ni kutomwamini Yesu."

Akamuambia:
Dhambi haianzi kwenye matendo mabaya.
Dhambi inaanza pale mwanadamu anapoamua kujiamini kuliko Mungu.Pale Mungu anasema nenda kulia, lakini wewe unaenda kushoto.
Hapo ndipo kila dhambi nyingine huzaliwa.

Kisha akampeleka Mwanzo 6:5:
"Kila kusudi la mawazo ya moyo wa mwanadamu lilikuwa baya siku zote." Johnny akapinga:“Lakini nawapenda marafiki zangu. Niko tayari kufa kwa ajili yao.”

Mchungaji akamwuliza:
“Unachokiona wewe na anachokiona Mungu ni kitu kimoja?”

Halafu akampeleka Warumi 7:15: "Mambo ninayotaka kufanya siyafanyi, na ninayoyachukia ndiyo nayafanya."

Mchungaji akamuuliza kwa upole:
“Ulipenda kuwa depressed? Ulipenda kuishia gerezani?” Johnny akasema hapana. Mchungaji akasema: “Basi kwanini uliishia hapo?” Johnny hakuwa na jibu.

Ndipo mchungaji akasema maneno yaliyobadilisha maisha yake:“Sio wewe tatizo kuu. Kuna dhambi ndani yako inayokuendesha. Wewe sio ugonjwa, bali wewe ni mwenye kubeba ugonjwa.”

Kisha akaongeza:
“Utupu unaouhisi ni kawaida kwa mwanadamu anayejaribu kuwa mkamilifu bila Mungu.”

Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Johnny alihisi kueleweka.
Sio yule little monster aliyeitwa na mama yake.
Sio yule mtu aliyeharibika beyond repair.
Bali mwanadamu aliyekuwa anapigana vita ambavyo hakuvielewa.

Unataka kujua zaidi ....soma sehemu inayofuata.

Johnny akiwa pale bado. Mchungaji akaendelea. Akafungua Yohana 1:29:
"Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu."

Akamwambia:
“Dhambi zako ziko wapi? Mbinguni? Kuzimu?”
Johnny akasema:
“Duniani.” Mchungaji akasema:
“K**a Yesu alibeba dhambi za ulimwengu - basi alibeba zako pia.”

Zote.
Za zamani.
Za sasa.
Na hata zijazo.
Warumi 6:23:
"Mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele."
Karama. Ndio karama. Na karama hailipiwi.

Waebrania 10:14:
"Kwa sadaka moja amewakamilisha milele wale wanaotakaswa."

Kisha Waebrania 10:17:
"Dhambi zao sitazikumbuka tena."

Mchungaji akauliza:
“Mungu anaweza kusema uongo?”
Johnny akasema hapana.
“Basi k**a amesema hazikumbuki tena atazileta tena?”
Kimya.

Ndani ya Johnny kuna kitu kilianza kuyeyuka.
Sio miujiza ya ghafla. Bali tumaini la kweli.
Lakini hata tumaini lilipoanza kuingia, sauti nyingine ilianza kusema:
“Johnny, unajua mambo uliyofanya. Unafikiri wewe ni mwenye haki?” Sauti hiyo haikuwa kubwa bali sauti ya kawaida.

Lakini Johnny akaamua kuuliza badala ya kupinga.“Vipi nikitenda dhambi makusudi?” Mchungaji akamjibu kwa upendo:
“Mtu aliyeokoka haishi kwa sheria tu anaishi kwa uhusiano” Akatoa mfano wa ndoa.

Mume hamtii mke wake kwa sababu ya sheria tu.Anatii kwa sababu ya upendo.Johnny akaanza kuelewa kuwa Mungu hakuwa anajaribu kumhukumu. Alikuwa anataka kumponya.

Baada ya siku hiyo, mchungaji alimpa assignment moja tu: “Nenda kaongee na baba yako. Muombe msamaha.”
Johnny alikasirika sana.Yeye ndiye alikuwa muhanga.Lakini mchungaji akasema:“Unafikiri kuwa sahihi kutakupa amani? Maisha yako yanaonyesha nini?”

Siku moja Johnny alikutana na baba yake kwenye mgahawa wa Kivietnam. Bakuli la pho lilikuwa mezani.Kisha Johnny akasema:
“Baba… nisamehe. Nisamehe kwa kuwa mtoto mbaya. Nisamehe kwa aibu niliyowaletea.”

Baba yake akamwangalia.Halafu mwanaume ambaye hakuwahi kusema "Nakupenda Mwanangu" wala "samahani" akaanza kulia.
Kwa nguvu.

Akisema: “Hapana mwanangu… mimi ndiye mwenye makosa. Nilijaribu kuacha pombe lakini nilishindwa.”

Miaka 20 ya hasira ikayeyuka mezani kwenye bakuli la supu.
Tangu mwaka 2015, Johnny Chang ameenda kwenye magereza yenye ulinzi mkali na kuhubiri kwa wauaji, wafungwa wa maisha, na watu waliokata tamaa. Hawaambii kwanza waache dawa za kulevya.Hawaambii kwanza wajirekebishe.

Anawaambia:
“Wewe sio ugonjwa. Kuna ugonjwa ndani yako. Na Yesu ndiye tiba.”

Na Mungu amemtumia kuleta amani hata kati ya maadui waliotaka kumuua zamani.
Mama yake aliyekuwa anamwita "little monster "ameona Mungu akimgeuza mwanawe kuwa mhubiri.

Johnny, mtoto wa Section 8 aliyeingia magenge ya wahuni akiwa na miaka 12 na kutumia miaka 12 gerezani…Leo hii anamhubiri Yesu.Sio kwa sababu alijisafisha kwanza. Bali kwa sababu aliamini kabla hajawa tayari.

Huenda wakati unasoma udhuhuda huu kuna kitu kinaguswa ndani yako. Sio majuto wala
Sio pressure.

Ni ule utupu wa ndani ambao hakuna pesa, starehe, au mafanikio yaliowahi kuujaza kabisa.Habari njema ni hii; Yesu hakuja kwa ajili ya watu wakamilifu. Alikuja kwa waliovunjika moyo.

Kwa waliopotea.
Kwa waliochoka.
Kwa watu k**a Johnny.
Na kwa watu k**a wewe.
Kwa sababu injili sio orodha ya sheria.
Ni habari njema kwamba Mungu bado anakupenda hata baada ya kila kitu.
Na bado anakuita urudi kwake.

Johnny Chang alikulia mazingira ambayo ndoto nyingi hufa kabla hata hazijaanza.Sio lile jiji la kifahari la Los Angeles ...
04/06/2026

Johnny Chang alikulia mazingira ambayo ndoto nyingi hufa kabla hata hazijaanza.

Sio lile jiji la kifahari la Los Angeles linaloonekana kwenye filamu, mji wenye mitende barabarani, mastaa, na maisha ya kifahari. Johnny alikulia bustani za Ramona, upande wa mashariki wa Los Angeles, kwenye nyumba za miradi ya serikali kwa watu maskini. Mahali ambapo serikali ilisaidia kodi kwa sababu matumaini yenyewe yalikuwa yamepungua.

Wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka China. Walikuja Marekani wakiwa hawana kitu, wakiamini maisha yangekuwa bora. Lakini kati ya ndoto na uhalisia, kila kitu kiliharibika.Baba yake mzazi alikuwa mlevi kupindukia.Na kila alipokunywa, aligeuka mtu wa hasira na vurugu.

Johnny na kaka yake walijifunza mapema sana maumivu ya kupigwa, kuishi kwa hofu, na ukimya wa baada ya vurugu kana kwamba hakuna kilichotokea.

Mama yake alikuwa Mbuddha kwelikweli. Alikuwa mwanamke mpole, mnyenyekevu, aliyefundishwa kuvumilia. Alimpenda mume wake, aliwapenda watoto wake, lakini hakuwa na nguvu ya kuwakinga kikamilifu.Familia yao iliishi kwa koponi za chakula. Walikuwa wanaishi tu ili kuishi. Kuishi kwa kujiokoa.

Na Johnny alipokuwa anakua, aliona kitu kimoja kuwa, wahalifu wa magenge ndio waliokuwa wanaonekana “wamefanikiwa.”
Walikuwa na magari. Fedha. Wanawake. Nguo nzuri.Lakini zaidi ya yote hayo walikuwa na heshima.Na kwa mtoto aliyekulia akiwa hana kitu, heshima ilionekana kuwa kila kitu.

Johnny Chang aliingia magenge ya wahuni akiwa na miaka 12 tu. Ndio! Miaka 12.
Umri ambao watoto wengi wanawaza homework au michezo ya shule kwa Johnny, uchaguzi huu wa kuwa muhuni ulikuwa rahisi:

Arudi nyumbani apigwe na baba yake?
Abaki nje na kunyanyaswa na vijana wakubwa?
Au ajiunge na genge ili awe na “familia” ya kumlinda? Alichagua genge la wahuni.Na alijitoa kabisa ndani yake kwa moyo wake wote.

Hasira zote alizobeba tangu utotoni na maumivu ya kupigwa, umaskini, aibu, kukosa upendo wa baba, zote zilianza kumtoka kwa kasi. Johnny akaanza kuwa mtu wa kuogopwa.
Alipigana. Aliiba. Alichoma watu visu. Alifyatua risasi.Sio kwa sababu alizaliwa mwovu.Bali kwa sababu maumivu yalikuwa yamemfundisha lugha moja tu,lugha ya wahuni.

Johnny alipokuwa mtu mzima, alikuwa tayari ameingia na kutoka kwenye mfumo wa magereza tangu akiwa mtoto. Kwanza California Youth Authority.Baadaye gereza kubwa la serikali.Kwa jumla alitumikia miaka 12 gerezani.Na ndani ya miaka hiyo, aligundua jambo la kushangaza sana.

Utupu wa ndani haukuishia gerezani.
Kila asubuhi aliamka akiwa na uzito mkubwa moyoni. K**a kuna kitu kilikuwa kimekaa juu ya kifua chake.Hakutaka kuishi. Sio kwa kuigiza.Bali uchovu wa ndani.Alikuwa yupoyupo tu anaishi kwa kuwepo tu.

Siku moja, mfungwa mwenzake Mkorea ambaye ni mtoto wa mchungaji aliyepotea njia alimshauri wasome Biblia pamoja.
Wakaisoma kutoka mwanzo mpaka mwisho mara mbili.

Lakini Johnny alikuwa na maswali ambayo hakuna aliyemjibu:“Nikifa bila kutubu dhambi fulani je? Nitaenda motoni?”

Makasisi waliokuja gerezani walimwambia kitu kilekile:“Tubuni la sivyo mtaenda jehanamu.”Hofu nyingi. Tumaini kidogo.

Akaifunga tena alaachana na Ukristo.
Baadaye akaisoma Qur’an mara tatu.
Bado hakupata majibu.Akaamua kuachana kabisa na mambo ya dini.

Johnny alipotoka gerezani, alidhani huzuni ilikuwa ya gerezani tu.Lakini alikosea.
Akaanza kutengeneza pesa nyingi kupitia biashara ya dawa za kulevya hadi dola elfu 30 au 40 kwa mwezi.

Alienda Las Vegas. Akanunua vitu.
Akaishi maisha ambayo kila kijana wa mtaani anaota kuwa nayo.Lakini ndani yake alikuwa mfu anayeishi.Alijaribu kujiua mara tatu.
Kwa sababu kuna aina ya mateso ambayo hutokea pale unapopata kila kitu lakini bado unabaki mtupu.Aliogopa kufa.Lakini pia hakuweza kuishi.

Ndani ya siku k**a kumi, matukio matatu yakatokea:Rafiki yake akapigwa risasi na kufa mbele yake. Barua kutoka kwa rafiki aliyekuwa gerezani ikafika na ujumbe wa kuaga maisha. Siku tatu baadaye, rafiki huyo akajiua.Kisha kijana asiye na hatia, aliyekuwa akifanya kazi Taco Bell kulipia shule, akapigwa risasi kichwani na kufa.
Vifo vitatu kwa mpigo.Ndani ya siku kumi.

Na Johnny akaanza kuhisi: “Mimi ndiye ninafuata.”

Unataka kujua nini kilifuata ....soma post inayofuata.

Leo naomba kushare ushuhuda wa Johnny Chang. Wengine waweza kuwa wanamfahamu lakini nataka tufahamu zaidi kuhusu maisha ...
04/06/2026

Leo naomba kushare ushuhuda wa Johnny Chang. Wengine waweza kuwa wanamfahamu lakini nataka tufahamu zaidi kuhusu maisha yake na namna ambavyo Kristo Yesu alimuokoa na kumpa maisha mapya.

Alijiunga na genge akiwa na miaka 12, akaishi maisha ya vurugu, pesa, mpaka kufungwa gerezani lakini kitu kilichomvunja kabisa hakikuwa risasi wala jela… ilikuwa utupu wa ndani moyoni.

Johnny Chang alikuwa na kila kitu ambacho vijana wa mtaani wana ndoto ya kuwa nacho, lakini kila usiku alilala akijiuliza kwanini bado aliona kufa ndani yake.

Baada ya kufungwa miaka 12 gerezani, majaribio matatu ya kujiua, na kuona vifo vitatu ndani ya siku kumi… maisha yake yalibadilishwa si kwa muujiza mkubwa, bali kwa bakuli la tambi kanisani.

Mchungaji mmoja alimwambia maneno mawili ambayo hakuna mtu alikuwa amewahi kumwambia Johnny: “Sio hivyo.” Na hapohapo safari yake kutoka gizani kwenda kwa Yesu ilianza.

Alikuwa mtu ambaye watu walimwogopa mitaani, lakini siku aliyokaa mbele ya baba yake na kusema “nisamehe,” miaka 20 ya maumivu ilianza kuyeyuka kwa machozi.

Hii sio hadithi ya mtu aliyebadilika kwa sababu alikuwa mzuri bali ni hadithi ya mtu aliyekuwa amevunjika kabisa, lakini akagundua kwamba Mungu bado alikuwa anamtafuta.

Nazichukua hizi shuhuda sehemu mbalimbali k**a youtube, naziandaa mwenyewe na kuziweka humu ili kuwafikia watu ambao kwa namna moja au nyingine waweza kuponywa na kuchagua njia ya kumfuata Yesu.

Leo naomba kushare ushuhuda wa Johnny Yang. Wengine waweza kuwa wanamfahamu lakini nataka tufahamu zaidi kuhusu maisha yake na namna ambavyo Kristo Yesu alimuokoa na kumpa maisha mapya.

Unataka kujua zaidi...Soma Post Inayofuata.

03/06/2026

Ni Kwa Nini Unamhitaji Yesu

1. Kila mtu amezaliwa na asili ya dhambi ambayo inamtenga mbali na Mungu. Mungu ni Mtakatifu (Warumi 3:23)

2. Dhambi inaleta mauti ya milele na hakuna namna ya kibinadamu inayoweza kuokoa roho yake (Warumi 6:23).

3. Yesu alikuja duniani akiwa Mungu katika mwili wa binadamu, akiwa mkamilifu na bila dhambi, ili kuwa jibu la tatizo hilo (Yohana 1:14)

4. Alitoa maisha yake msalabani kwa hiari yake mwenyewe. Alifanyika kuwa dhabihu halali ya kulipa deni lako la dhambi mbele ya Mungu (Warumi 5:8)

5. Bila yeye, unaishi ukiwa na mzigo wa hatia, hofu ya kifo, na kutembea bila mwelekeo wa kweli.

6. Anapokusamehe, si maneno matupu bali ni uhakika kamili kwamba dhambi zako zimefutwa milele. Hii ndiyo Injili (Habari Njema) (Wakolosai 1:14).

7. Anapoingia moyoni mwako, anakupa Roho Mtakatifu. Yeye ndiye anakupa nguvu ya ndani ya kushinda dhambi na kuishi kwa utakatifu (Yohana 14:16-17)

8. Katika maumivu ya maisha, Yesu peke yake ndiye anayeweza kusema kwa kweli: "Najua unachopitia, kwa sababu mimi mwenyewe nilipitia" (1 Petro 2:24).

9. Ufufuko wake umethibitisha kwamba kifo hakina nguvu ya mwisho na milele ya kweli inatungoja (Yohana 11:25)

10. Kumhitaji Yesu ni kukubali upendo mkubwa zaidi uliowahi kutolewa ulimwenguni kwamba Mungu hakutuacha tufe dhambini, bali alikuja Mwenyewe kukuokoa (Yohana 3:16)

Wewe si mali ya Mtu. Wewe ni Wangu.Ushuhuda wa LeilaJina langu ni Leila. Nina miaka 31. Kwa muda mrefu sana, niliamini k...
02/06/2026

Wewe si mali ya Mtu. Wewe ni Wangu.

Ushuhuda wa Leila

Jina langu ni Leila. Nina miaka 31. Kwa muda mrefu sana, niliamini kwamba thamani yangu ilitegemea macho ya mwanaume aliyenitawala kuliko wote. Si mwingine baba yangu mzazi.

Nilizaliwa katika familia ya Kiislamu yenye msimamo mkali ndani ya mji mdogo uliozungukwa na jangwa. Kila mtu alijua jina letu. Baba yangu hakuwa tu mtu mwenye mamlaka. Alikuwa Sheikh maarufu sana na kiongozi wa kiroho aliyekuwa akiheshimiwa k**a mungu mtu mtakatifu.

Alipoingia msikitini, watu walinyamaza kimya.Walimsikiliza kana kwamba kila neno lake limetoka moja kwa moja kwa Mungu.

Nyumbani kwetu, sauti yake haikuwa maoni. Ilikuwa sheria. Na sheria hiyo haikuruhusu kuuliza maswali.

Tuliishi katika nyumba kubwa yenye ukuta wa juu k**a ngome. Baba alikuwa na wake wawili, watoto wengi, na nguvu kiasi kwamba hata polisi waliogopa kumpinga.

Kwa nje tulionekana k**a familia iliyobarikiwa.Lakini kwa ndani… tuliishi k**a watumwa na wafungwa wa dini iliyopotoka.

Nilikuwa mmoja wa mabinti waliopendwa zaidi kwa sababu nilikuwa mtiifu.Sikuangalia wanaume machoni. Nilijua dua zote. Nilifuata sheria zote za dini.Nilijifunza kunyamaza haraka.Lakini ndani yangu kulikuwa na kitu kisichotulia.

Wakati mwingine usiku nilikuwa napanda juu ya paa la nyumba yetu nikiwa na miaka 13, nikitazama nyota. Na kwa sauti ya chini nilikuwa nikiuliza:

“Mungu… unaniona kweli?
Au unahesabu tu makosa yangu?”

Hakukuwa na jibu, kimya.
Ilikuwa ni ukimya wa baridi wa anga la usiku.

Nilipofikisha miaka ya 20, nilikuwa tayari nimebeba majukumu mengi ya nyumbani. Nilipika, nilipanga wageni, nilihudumia familia nzima ya baba yangu. Katika tamaduni yetu, binti alikuwa anaandaliwa kuolewa.Lakini baba yangu hakuwahi kutafuta mchumba kwa ajili yangu. Nilidhani ni kwa sababu alinipenda sana.Sikujua ukweli.

Usiku mmoja baada ya swala ya Isha, niliitwa ofisini kwake. Nilisimama mbele yake nikitazama chini k**a nilivyofundishwa maisha yangu yote. Kisha akasema kwa sauti tulivu akasema “Leila… nimekuchagua uwe mke wangu.” Mwili wangu ulipata ganzi.
Nilidhani nimesikia vibaya.

Nikauliza tena “Mke wako?” Akatabasamu.

Kisha akaanza kunukuu aya, hadithi, na maneno kuhusu utiifu na heshima.

Alisema: “Hii ni halali mbele ya Allah.”
Ndani yangu kila kitu kilinyamaza.
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nilihisi kwamba mtu aliyepaswa kuwa mlinzi wangu alikuwa amegeuka kuwa mtesi wangu.Na mbaya zaidi… alikuwa anatumia jina la Mungu kuhalalisha uovu wake.

Nilijaribu kumwangalia mama yangu kwa msaada.Lakini macho yake yalikuwa tayari yamejaa hofu ya miaka mingi.
Hakukuwa na mtu wa kunitetea.Kwa ndugu zangu wa kiume, kumpinga sheikh ilikuwa sawa na kumpinga Mungu.
Baada ya siku 14, baba yangu aliniita chumbani kwake usiku. Harufu ya ubani ilikuwa nzito hewani. Kitanda kilikuwa kimeandaliwa. Vikombe viwili vya chai vilikuwa mezani.Na hapo ndipo nilijua…

Hakukuwa tena na njia ya kurudi nyuma.

Nilimwambia kwa sauti iliyovunjika:
“Baba… tafadhali…”Lakini alinitazama kwa ukali na kusema: “Usiniite baba tena.Kuanzia leo mimi ni mume wako.” Sentensi hiyo ilinipasua roho yangu. Alitumia aya, hadithi, na vitisho vya kidini kuniambia kwamba nikikataa, nitakuwa nimemkataa Mungu mwenyewe. Na hapo nilielewa jambo moja la kutisha sana. Hii haikuwa tu dhambi ya mwanaume.Ilikuwa ni dini iliyopindishwa kuwa silaha ya mateso.

Baada ya hapo maisha yangu yaligeuka kuwa gereza.Nilifichwa.Nilidhibitiwa.Nilinyimwa uhuru.Watu waliniona k**a mwanamke mwenye heshima kubwa.Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa mfungwa.Usiku nilikesha nikilia.Nilisali zaidi kuliko kawaida. Nilifunga sana. Nilijaribu kuwa mtakatifu zaidi nikidhani labda Mungu angeniona.Lakini ukimya pekee ndio uliorudi. Polepole nilianza kujiuliza: “Ikiwa haya ndio mapenzi ya Mungu… basi Mungu ni mwema kweli?”
Swali hilo lilinitisha kuliko kila kitu.

Siku moja nilikuwa nasafisha ofisi ya baba yangu nikafungua Qur’an yake kubwa ya zamani. Macho yangu yakatua katika Surah Al-Ahzab 33:50. Nilisoma maneno yaliyokuwa yakitumiwa kuhalalisha kile alichokuwa ananifanyia.Mikono yangu ilianza kutetemeka. Kwa miaka yote nilikuwa nimeamini kwamba tatizo ni wanaume wabaya si dini.Lakini sasa niliona maandishi yale mbele yangu. Na hapo nilijiuliza kwa mara ya kwanza: “Je… nimefundishwa uongo maisha yangu yote?” Nilikaa sakafuni nikalia sana.

Na kwa mara ya kwanza sikumuomba Allah.
Nilisema tu: “Yeyote uliopo… k**a unaniona… tafadhali nisaidie.”

Siku moja usiku nikiwa na maumivu makali kabisa moyoni. Nimevunjika vunjika ndani sina chenye afadhali. Nilivua bangili ya dhahabu ambayo baba yangu alinipa k**a “zawadi ya utiifu.” Kwangu ilikuwa k**a pingu. Nikalia na kusema: “K**a upo… k**a wewe ni wa kweli… njoo.”

Sijui hata nililalaje ila usingizi ulinichukua.
Lakini ghafla nilijikuta ndani ya jangwa kubwa la ajabu.Nilikuwa peke yangu. Kisha nikamwona. Mwanaume aliyekuwa amevaa mavazi meupe yanayong’aa k**a nuru yenyewe.Alikuwa anatembea kuelekea kwangu. Na nilipomwangalia… sikuhisi hofu.
Nilijiona salama.Aliponifikia, alinitazama machoni.Na katika macho yake nilipata kitu ambacho sikuwahi kuona maishani mwangu:
Kuonekana. Aliniona kabisa. Alijua maumivu yangu. Alijua machozi yangu. Alijua kilio changu cha siri.Kisha akaniambia; “Wewe si mali ya mtu. Wewe ni wangu.”

Nilipiga magoti nikilia.

Nikamuuliza: “Wewe ni nani?” Akatabasamu kwa upendo ambao sikuwa nimewahi kuuona kwa mwanaume yeyote duniani. Kisha akaniambia: “Mimi ndiye ambaye siku zote nimekuwa nikikuona.” Nilipoamka, macho yangu yalikuwa yamejaa machozi.
Lakini moyo wangu ulikuwa tofauti.
Kwa mara ya kwanza kulikuwa na tumaini.

Kesho yake niliiba simu ya zamani ya mama wa kambo wangu na kuandika mtandaoni “Mwanamke wa Kiislamu anaota mwanaume wa mavazi meupe.” Nilichokiona kilinishtua.
Mamia ya shuhuda kutoka Iran, Syria, Somalia, Yemen, Indonesia…Wote walizungumza kuhusu mtu yuleyule.
Na wote walitaja jina moja "Yesu"

Nilijua ni Isa bin Mariam wa Qur’an. Lakini hawa watu walizungumza kuhusu Yesu kwa njia tofauti kabisa. Walizungumza kuhusu upendo,msamaha,uhuru na amani. Usiku huo nilitamka jina hilo kwa mara ya kwanza maishani mwangu: “Yesu…”Na ndani yangu… lilisikika k**a jina ambalo moyo wangu ulikuwa ukilisubiri maisha yote.

Siku moja mdogo wangu alinifumania nikitazama ushuhuda wa mwanamke aliyemfuata Yesu. Alikimbia kumuita baba yangu.Dakika chache baadaye chumba changu kilijaa hasira. Nilipigwa sana. Nikafungiwa. Imam aliitwa kuniombea kana kwamba nina pepo.Walisema nimepotoshwa na majini.Lakini ndani yangu nilijua ukweli.
Haikuwa pepo. Alikuwa YESU.

Usiku wa tatu nikiwa nimefungiwa ndani, nilipiga magoti nikasema: “Yesu… najua kidogo sana kuhusu wewe.Lakini nina hakika uliniona.Tafadhali usiniache.” Na kwa mara ya kwanza maishani mwangu… nilipata amani.

Siku ya nne nilisikia sauti mlangoni.
“Leila… ni mimi, Isa.” Alikuwa jirani yetu.
Mwanamke mwenye macho ya huruma.
Akaninong’oneza: “Mimi ni Mkristo. Na nitakusaidia kutoka hapa.”

Usiku huo alinipitishia waya mdogo wa kufungulia kufuli.Mikono yangu ilikuwa inatetemeka nilipofungua mlango.Nilipotoka nje ya nyumba ile kwa mara ya mwisho, sikuwa nimebeba chochote.

Hakuna nguo.
Hakuna kumbukumbu.
Hakuna mali.
Nilitoka na hofu tu… na uamuzi wa kutorudi nyuma.

Isa alinifikisha nyumbani kwake.Akanipa maji, mkate, na blanketi. Kisha akanikalia mbele yangu na kuniuliza: “Leila… unataka kweli kumfuata Yesu? Si tu kutoroka kwa baba yako…bali kumpa Yesu maisha yako?”

Nikalia sana.Nikakumbuka mtu wa mavazi meupe. Nikakumbuka maneno yake.“Wewe ni wangu.” Nikamjibu: “Ndiyo.Hata k**a itanigharimu kila kitu.” Usiku huo huo nilimpa Yesu maisha yangu. Na kwa mara ya kwanza maishani mwangu nilijiona niko nyumbani.

Wiki moja baada ya kutoroka, Isa alinionesha ujumbe kutoka kwa baba yangu. Aliandika: “Binti yangu Leila amekufa kwetu.” Nilisoma ujumbe ule mara mbili. Nilikuwa nimefutwa kabisa.Lakini ndani ya maumivu hayo, nilisikia tena sauti ile ya upendo: “Wewe ni wangu.”
Na hapo nilielewa kuwa Dunia yangu imenikataa. Lakini Yesu amenipokea.

Baadaye nilifika katika kanisa la siri. Halikuwa jengo kubwa. Ilikuwa ni sebule ndogo yenye watu wachache waliokuwa na upendo ambao sikuwahi kuuona maisha yangu yote.Waliponiona hawakunihukumu. Walinikumbatia.Mwanamke mmoja alinong’ona sikioni mwangu: “Karibu nyumbani, binti wa Mungu.” Siku chache baadaye nilibatizwa ndani ya beseni ndogo la maji baridi.

Mchungaji akaniuliza: “Unataka jina jipya kwa maisha yako mapya?” Nikajibu: “Miriam.”Nilipozama ndani ya maji yale, nilihisi k**a aibu, minyororo, na utumwa wangu wote unazama pamoja nami. Nilipotoka nje ya maji, nilihisi uhuru.Kwa mara ya kwanza kweli niliamini maneno haya ya Biblia;

“Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” — Yohana 8:36

Leo hii maumivu hayajatoweka kabisa.
Bado wakati mwingine naamka usiku nikitetemeka. Bado ninakumbuka sauti ya baba yangu. Lakini sasa kuna sauti nyingine yenye nguvu zaidi. Sauti ya Yesu. Sauti inayoniambia: “Wewe ni binti yangu.”Sasa najua tofauti kati ya umiliki na upendo.

Baba yangu alisema “wewe ni wangu” ili kunimiliki Lakini Yesu alisema “wewe ni wangu” ili kuniweka huru. Na hiyo ndiyo tofauti iliyobadilisha maisha yangu milele.

K**a umefika mwisho wa ushuhuda huu nataka ujue jambo moja: Huenda kuna mwanamke mahali sasa hivi analia gizani k**a nilivyokuwa mimi. Huenda kuna mtu anayeteswa kwa jina la dini.Huenda kuna mtu anayehisi haonekani.Huenda kuna mtu anayehitaji tumaini moja tu ili asianguke kabisa. Usiipite ushuhuda huu kimya kimya. SHARE na Wengine

Shiriki.
Toa maoni.
Tuma kwa mtu mwingine.
Kwa sababu hujui nani anasubiri kusikia kwamba bado kuna Mungu anayesema:“Nimekuona.Na wewe ni wangu.”

Na maneno haya ndiyo yakawa wimbo wa maisha yangu mapya:
Bible“Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” Yohana 8:36

Address

Kimara
Dar Es Salaam
00000

Telephone

+255768004412

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Upendo wa Yesu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Upendo wa Yesu:

Shortcuts

Share