07/03/2026
Video ya kwanza imeonekana ikionyesha Marekani ikirusha kwa mara ya kwanza kombora lake jipya la Precision Strike Missile.
Video hiyo inaonyesha mfumo wa roketi wa M142 HIMARS uliopo nchini Bahrain ukirusha kombora la PrSM kuelekea maeneo yaliyopo Iran, kuvuka Persian Gulf.
Mfumo huu wa silaha ni kombora la kisasa la kizazi kipya la ardhini-kwa-ardhini (surface-to-surface ballistic missile) lililoundwa kuchukua nafasi ya mfumo wa zamani wa ATACMS.
Kombora hili lina uwezo wa kufika umbali wa zaidi ya kilomita 500 (ikilinganishwa na takribani kilomita 300 za mfumo wa zamani wa ATACMS zinazotumiwa na HIMARS), huku matoleo yajayo yakipangwa kufikia hadi kilomita 1000.
Kichwa cha kombora (payload) kina takribani uzito wa kilo 91 za vilipuzi vinavyogawanyika vipande vipande (high-explosive fragmentation unitary warhead).