Faithisprayer

Faithisprayer Behold, My servant shall deal wisely and shall prosper; he shall be exalted and shall stand very high. Isaya52:13 Na anauwezo wa Kufanya zaidi ya Uombavyo..

Ni Muhimu sana katika maisha yetu kuwa na maombi ya Muda mrefu, lakini watu wengi tuna pata shida katika maombi haijalishi ni ya muda mrefu au ni ya muda mfupi au ni ya dharura, KILA BAADA YA KUOMBA KUNA SAUTI INAANZA KUKWAMBIA NDANI "mmh Mungu atajibu kweli" na wengine wengine wanaenda mbali zaidi wanasahau k**a waliomba muda mfupi uliopita wanaanza kujiuliza mmh " HATA HILI MUNGU ATAJIBU" unaanz

a kuona tatizo lako ni kubwa kuliko Mungu. IMANI ni neno lenye herufi 5 tu, lakini linamaana kubwa sana, neno hili ndo linafanya wewe na mimi tukamjua Mungu, Neno hili ndilo linalokufanya ujue kuna siku hii dunia itafika mwisho wake, neno hili ndilo linalokufanya kila siku ujitahidi kuwa na maisha safi ili hata ukifa Leo tuweze kumuona Mungu. Sasa k**a kwa imani uliyonayo unaamini MUNGU yupo na unajitahidi kutenda mema ili ukamuone siku ya Mwisho ina maana ndani yako Una uhakika MUNGU yupo lakini hujawahi kuiona sura yake, ila unasikia tu. 2kor 5:7, Gal3:14b

Ni kwa imani hii hii maandiko matakatifu yanatuambia "tusipokuwa nayo hatuwezi kumpendeza Mungu (Ebrania 11: 6)

Na imani hii ndiyo itakayo uwezesha Kupokea vile vitu unavyovihitaji kutoka kwa Mungu, Kwa kutumia imani unafanya vile vitu ambavyo mwanzo vilikuwa haviwezekani vionekane kuwa vinawezekana na vipo na unaweza kuwa navyo. k**a jinsi ilivyo kwa kuona mbingu mpya siku ya Mwisho ambapo kila mtu anaamini hilo na habari ya siku ya Hukumu ambayo pa Kila mtu anajua ipo, si kwamba kuna Mtu aliiona kwa macho, NOP, ila tunaamini na tunajiandaa kila siku kuipokea. Ndiyo imani hihi hihi itakusaidia kukuonyesha kuwa Mungu ni mkuu sana kuliko hitaji lako Lolote. Efeso 3:20

Kwa hiyo ndani ya moyo wako bila kujalisha ni mahali gani unapitia kitendo cha kusema moyoni mwako "MUNGU NAKUAMINI WEWE KATIKA HILI " hii ni imani, na ni maombi pia na imani hii italeta kile kilichokuwa hakiwezekani kwako kiwezekane, kipatikane, kutokee or kifanyike. Mathayo 21: 22, inasema " na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea"

hayo hapo juu ni maneno ya yesu Mwenyewe, aliwaambia Mitume wake, na leo hii ananiambia mimi na wewe, kuwa "LOLOTE" NITAKALOOMBA NIKIAMINI BASI NITALIPOKEA . Basi anza leo kujifunza hatua kwa hatua Kila jambo ambalo Mungu analifanya ndani yako Ni Maombi yangu leo liwe Msingi imara wa kukuwezesha kuamini kuwa hata yale unayodhani wewe kuwa ni makubwa sana yeye Mungu anayaweza yote. Amini na Moyoni mwako wakati wote sema "I TRUST YOU GOD"

Address

Dar Es Salaam
6141

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Faithisprayer posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share