Living Water Church Tanzania

Living Water Church Tanzania Living Water Center is an Interdenominational God's word based church
gather together and committ to have a close Relationship with God based on the Bible.

WASAA WA PASTOR MONYO — IMEFANA! Jumatano ilikuwa siku ya maswali, majibu, kujifunza na kujengwa katika Neno la Mungu. 🙏...
02/09/2026

WASAA WA PASTOR MONYO — IMEFANA!

Jumatano ilikuwa siku ya maswali, majibu, kujifunza na kujengwa katika Neno la Mungu. 🙏🔥

Maswali mbalimbali yaliibuliwa kuhusu maisha, mahusiano, ndoa, wokovu, kazi na mambo yanayowakabili vijana na jamii, na kwa neema ya Mungu tukapata nafasi ya kujifunza pamoja. ❤️‍🔥

🙏 Tunamshukuru Mungu kwa uwepo wa Roho Mtakatifu na kwa kila aliyeshiriki.

Hii haikuwa tu TALK SHOW — ilikuwa ni nafasi ya kupata ufahamu, mwelekeo na kujengwa kiroho. 🔥

📸 Hizi ni baadhi ya picha za kilichojiri.

👉 Endelea kufuatilia WASAA WA PASTOR MONYO kwa vipindi vingine vyenye maswali, majibu na mafundisho yenye kujenga maisha.

🔥 LIVING WATER CHURCH, KAWE 🔥

01/09/2026

EWE NI NANI?
Jitambue kwanza, ndipo utaanza kuishi maisha ya ushindi. .Somo UTAMBULISHO

01/09/2026

Utambulisho wako unakupa kushinda vita ya ndani na kua na Matokeo nje . Mithali 23:7

29/08/2026
27/08/2026

MUNGU USIMJUE KWA AJILI YA MTU MWINGINE — MJUE KWA AJILI YAKO MWENYEWE!

Kumjua Mungu si kusikia tu ushuhuda wa watu wengine kuhusu Yeye. Si kumjua Mungu kwa sababu ya mchungaji wako, mzazi wako, rafiki yako au mtu unayemheshimu.

Lazima ufikie mahali ambapo Mungu anakuwa ufunuo wako binafsi.
Ujue sauti yake. Ujue tabia yake. Ujue Neno lake. Ujue njia zake. Ujue anachotaka kufanya ndani na kupitia maisha yako.

Kwa sababu kuna wakati utabaki peke yako—na hapo ndipo ufahamu wako binafsi wa Mungu utakavyokutengenezea usalama.

Usiishi kwa “Mungu wa fulani alisema…”
Fika mahali pa kusema: “MIMI NAMJUA MUNGU WANGU.”

«“Lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.” — Danieli 11:32»

🔥 Kumjua Mungu ni usalama wako.
🔥 Kumjua Mungu ni msingi wa imani yako.
🔥 Kumjua Mungu ni nguvu yako katika nyakati ngumu.
🔥 Na mwisho wa yote, maisha yako yanapomdhihirisha Mungu, jina lake hutukuzwa.

Usiridhike na kumjua Mungu kupitia wengine.
Mtafute. Mjue. Muelewe. Tembea naye.

MUNGU ANATAKA UWE NA UFUNUO WAKO BINAFSI JUU YA YEYE. 🙏🏽🔥

18/08/2026

Neno la Mungu = msingi wa kuaminika.

17/08/2026

HEKIMA KATIKA KAZI Apostlelilianndegi

Leo Jumapili tumekuwa na ibada njema na yenye baraka kubwa ndani ya uwepo wa Mungu. 🙏❤️Dr. Apostle Lilian Ndegi ametufun...
16/08/2026

Leo Jumapili tumekuwa na ibada njema na yenye baraka kubwa ndani ya uwepo wa Mungu. 🙏❤️

Dr. Apostle Lilian Ndegi ametufundisha somo lenye nguvu la “HEKIMA YA KAZI.” 🔥

Tumejifunza kwamba kazi si adhabu, bali ni sehemu ya kusudi la Mungu katika maisha yetu. Mungu ametupa uwezo, vipawa na nafasi ili tufanye kazi kwa hekima, bidii na uaminifu. Tunapokuwa na hekima katika kazi, tunajua namna ya kutumia kile Mungu ametuweka nacho ili kuleta matokeo na kuwa baraka kwa wengine.

Usifanye kazi kwa mazoea; fanya kwa hekima. Usifanye kwa kulazimishwa; fanya kwa moyo. Na katika kila unachofanya, mtukuze Mungu. 🙌🔥

Hakika ilikuwa Jumapili ya kujifunza, kujengwa na kufanywa upya.
Utukufu wote ni wa Mungu! ❤️🙏

16/08/2026

Usiwe mzigo kwa watu. Jifunze kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika. Kazi hujenga heshima, huleta thamani na hufungua milango ya mafanikio. Lilian ndegi, kuna ujumbe kafundisha wa kukubadilisha na kuachilia vibali katika kazi 🔥

Address

Kawe
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Living Water Church Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Living Water Church Tanzania:

Shortcuts

Share