18/08/2024
SOMO; Maamuzi
Hauwezi kufika mahali popote bila ya kuwa na maamuzi, sababu ni Muhimu sana katika maisha ya mwamini..Maamuzi ya mtu yapo katika AKILI na MOYO hivyo tunazungumzia NAFSI na ndani yake ndipo kulipo kuzingatia
Mwamini akili Yako unatakiwa kuilisha Neno la Mungu na si vinginevyo ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi
Nini umeweka Moyoni mwako hicho ndicho kinachokufanya uamue nini,Vile unavyosikia ndivyo inakufikisha katika ukuu wako.
Mda mwengine ukiona mambo Yako hayaendi Rudi iulize akili yako na ipeleke taarifa kwenye moyo wako ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi juu ya jambo fulani
Ili uwe na maamuzi sahihi lazima uwe na uponyaji wa NAFSI, Hatufiki hapa tunapotakiwa kufika kwa urahisi kuna changamoto nyingi.
Wafilipi 4;8 "Hatimaye,ndugu zangu,mambo yo yote yaliyo ya kweli,yo yote yaliyo ya staha,yo yote yaliyo ya haki,yo yote yaliyo safi,yo yote yenye kupendeza yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote,ikiwapo sifa nzuri yo yote,yayafakarini hayo."
Maamuzi yamebeba kushinda au kushindwa (mabadiriko) kwa mtu.
Mwanzo 11;6 " BWANA akasema ,Tazama, watu Hawa ni taifa Moja, na lugha Yao ni Moja na haya ndio wanayoanza kuyafanya ,Wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya"
K**a tukifika sehemu ya kuamua chochote hakuna kitu kitakachokuzuilia, kuokoka MUNGU Alikuamulia ili kutembea katika wokovu ni wewe mwenyewe
Ayubu 22;28 "Nawe utakusudia Neno,nalo litathibitika kwako, Na mwanga utazitimiliza nadhiri zako"
Mwanzo 4;7 "K**a ukitenda vyema ,hautapata kibali.? Usipotenda vyema dhambi Iko,inakuotea mlangoni,nayo inakutamani wewe,lakini yapasa uishinde"
1 Wafalme 11;38 " Tena utakuwa,ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenenda katika njia zangu ,na kutenda yaliyo mema machoni pangu,ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu k**a Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara ,k**a nilivyomjengea Daudi ,nami nitakupa wewe Israel"
©Mtumishi; EINHARD NDOMBA
IBADA YA JUMAPILI 18/08/2024 KANISA LA EFATHA YERUSALEM-MAJOHE