29/09/2020
Tyk
Tunamshukuru Mungu kwa makuu aliyotutendea Parokia ya Mwananyamala kwa tukio la jana, la kutabaruku Kanisa, asante Mungu tumeuona mkono wako
Pili tunaishukuru k**ati nzima ya Kutabaruku Kanisa ikiongozwa na mwenyekiti ngugu Caesar na Katibu Bi Blandina, k**ati imefanya kazi yake kwa mafanikio na weledi makubwa. Hongereni sana
Kwa namna ya pekee nizipongeze k**ati zote kwa kazi nzuri, pongezi za pekee kabisa kutoka rohoni ziende kwa k**ati ya chakula ikiongozwa na Mama Nyambo imefanya vizuri sana, kwenye chakula ndio eneo lililokuwa na wasiwasi kwani watu wasiporidhika inafuta mema yote. Hongereni sana
Tunawapongeza wana Halimashauri wote, viwawa, wawata, Uwaka, utoto Mtakatifu kwa kila mmoja kuona sherehe hii inatuhusu wote.
Baba Kanali Tarimo hakika umekuja na wazo jipya ambalo hata sisi k**a Kamati Tendaji hatukulitegemea, hongera sana baba.
Hata nasi Kamati Tendaji team work ilikuwa juu kufikia kilichofanyika tunamshukuru Mungu
Ni vigumu kumtaja kila mtu kwa alichokifanya ila kweli tunatambua jitihada zilizofanyika eg mapambo, picha, video, nk
Tunawashukuru Makleri wetu kwa kutuongoza hatua kwa hatua kuelekea mafanikio haya
Team work iliyooneshwa hapa iendelee kuwa chachu ya maendeleo kwa Parokia yetu
Mt Martin de Porres Utuombee
Mchomvu
Mwenyekiti H/W Parokia