06/05/2014
Papaa On Tuesday.....Pakacha Pakachuka.....Kuvuja kwa Pakacha Ni Nafuu ya Mchukuzi.....Wapo baadhi ya watu wamewabeba watu ndani ya mioyo yao, wapo watu wamewabeba wapenzi wao wa zamani, wapo watu wamebeba ma boss zao waliosababisha wao kufukuzwa kazi, wapo waliowabeba wazazi wao, wapo waliobeba watu waliowakosesha fursa za kwenda kusoma, wapo waliobeba Kero za tabia mbaya za Waume zao wama wake zao, wapo ambao mioyo yao imebeba uchungu wenye maumivu wa yale yaliyowahi tokea kwao. Swali la kujiuliza utabeba mpaka lini?ama umevibeba hivyo vyote mpaka lini, ukiyaruhusu haya mambo yakaondoka kwako utashangaa afya yako inarejea, unashangaa ule ung’aavu wa sura yako unarudi, utashangaa tabasamu lako linarejea natambua kuwa maumivu ni makali lakini umewahi jaribu njia nyingine mbadala wa hiyo unayotumia sasa. K**a umelia muda mrefu embu jaribu kunyamaza pengine katika kunyamaza unaweza pata suluhu ya lile ulilo nalo.
Huzuni haijawahi msaidia mtu kwenye maisha. Huzuni inasababishwa sana na majuto, na waswahili wanasema Majuto ni Mjukuu na k**a ni Mjukuu lazima ana babu yake ama bibi yake anayeitwa Matendo na Mzazi anayeitwa Maamuzi. Unapoamua jambo na Ukafanya lile jambo majuto huwa yanakuja baada ya Matokeo yale uliyotarajia kutokuwepo. K**a mtu alitarajia akifanya ngono zembe atapata mimba hawezi juta, ila majuto yanakuja iwapo kile ulichotarajia sicho kilichokuja, badala mtu kujifunza unakuta mtu anaanza kujilaumu ana juta kwa kile kilichotokea, ukishaanza kujuta kuna mtoto anazaliwa anaitwa huzuni, huzini na majuto vinakufanya wewe ujione useless, vinakufanya wewe ujione hufai, vinakufanya wewe ujione ni mjinga wa wajinga, ukishaanza kujiona mjinga wa wajinga unakosa furaha unakosa ujasiri, unapoteza uwezo wako wa kufanya mambo mengi sana badala ya kunyanyuka baada ya kuanguka unaanza kulalamika aliyeweka jiwe chini wewe ukajikwaa, unaanza kulaumu aliyesababisha wewe uanguke. Mwisho wa siku unajikuta umebeba watu ndani ya maisha yako hasa wale walisababisha wewe kuingia kwenye majuto uliyonayo. Ok ni sahihi kubeba k**a mwanadamu wa kawaida je utabeba mpaka lini?na unabeba ili iweje?.....gonga hapa kusoma zaidi...http://samsasali.blogspot.com/2014/05/papaa-on-tuesdaypakacha-pakachukakuvuja.html