06/01/2025
KARAMA YA MUDA, HEKIMA, NA FEDHA NDANI YA UFALME WA MUNGU. 09
MHUBIRI 3:1-11.
“Kila jambo kuna majira yake na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu…”
Shalom Mwana wa Mungu Baba katika Kristo Yesu. Ninamtukuza Mungu Baba kwa ajili yako wewe ambaye umepata neema hii ya kujifunza na kufundishika juu ya Karama hii ya Muda, Hekima na Fedha ndani ya Ufalme wa Mungu hapa duniani.
TAMKO
Natamka kwa jina la Yesu Kristo, kwamba macho ya moyo wako yametiwa nuru, nawe umeuona na kuujua upendo wa Mungu Baba uliowekwa wazi kwako ktika Kristo Yesu, na ufahamu wa Kristo na maarifa ya kiungu yapitayo ya dunia hii. Umethibitika katika Hekima ya Kiungu na Unatembea katika utukufu wa ufahamu wa Mungu wewe na uzao wako katika Kristo Yesu hapa duniani. AMEN
Karibu tuendelee na Darasa letu na Roho Mtakatifu Mwalimu wetu na kiongozi wetu katika somo letu hili la Karama ya Muda, Hekima na Fedha ndani ya Ufalme wa Mungu Baba hapa duniani
Kuwa na ufahamu sahihi wa ufalme wa Mungu ni kufunuliwa karama ya Muda, Hekima, na Fedha ndani ya ufalme wa Mungu. Kwani ufahamu wa Mungu ndani ya Ufalme ndio ufunguo na kanuni ya kwanza katika kufanya jambo lolote lile kwa Mwana wa Mungu.
Gods understanding it is the insight to understand about God and His Kingdom and His Time, wisdom and Money na kuishi hapo.(Ufahamu wa Kiungu ni muono wa ndani tunaofunuliwa na Roho Mtakatifu kumuelewa Mungu Baba, Ufalme wake, muda, hekima na fedha na kuuishi katika damu na nyama hapa duniani.) Hauwezi kutawala hapa duniani k**a hauna ufahamu sahihi wa ufalme wa Mungu.
NB, Kuwa na ufahamu sahihi ni kuishi sahihi.
Mungu Baba kumwambia Adamu wa kwanza kuwa aende akazae, akaongezeke, akatiishe, na kutawala juu ya nchi alimtaka kwanza atambue neema ambayo Mungu ameiachilia kwake kwamba siyo kwa nguvu zake katika hayo yote, Bali inamuhitaji ajifunze na kuthibitika katika ufahamu wa Mungu ndipo ataweza kufanikiwa katika hayo yote. Na ndiyo maana alimuweka Edeni.
K**a ilivyo kwa mkulima ndivyo ilivyo kwa Mwana wa Mungu kwamba kuna kipindi cha kuandaa shamba na mbegu, kuna kipindi cha kupanda, na kuna kipindi cha mavuno(kula matunda) ndivyo ilivyo kwa Mwana wa Mungu ndani ya ufalme wa Mungu. Hauwezi ukayaishi Maisha ya Mungu pasipo kuwa na ufahamu sahihi ambao Mungu ameufunua kwako ukauthamini na ukaamua kuushi.
Katika vipindi hivi vyote Mungu Baba amevifungamanisha katika Karama ya Muda, Hekima na Fedha, hivyo hututaka sisi kuendelea kujifunza na kupata ufahamu zaidi wa ufalme wa Mungu na kuthibitika katika huo. Ni kipindi cha kukubaliana na ufahamu wa Mungu, wazo la Mungu na kulithamini na kuliishi. Yaani kuishi k**a Mungu, kuona k**a Mungu, kusema k**a Mungu na kufanya k**a Mungu.
SOMA ZAIDI
Mwanzo 1:28, 2 :15, Rumi 12:1-2, Efeso 5:15-17
Itaendelea…
Na nabii Tumikiael Nassary
# Roho wa Neema na Madhabahu