30/12/2017
KISHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI (Siku ya Sabato)
Tarehe 30- Disemba - 2017
SOMO :MAMBO ya KWANZA KUWA ya KWANZA
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mathayo 6:33.
Ahadi hii haitashindwa kamwe. Hatuwezi kufurahia fadhila za Mungu k**a hatutakubaliana na masharti ambayo kwa hayo fadhila zake zimetolewa. Kwa kufanya hivyo, itatujia amani, ridhaa na hekima ambayo dunia haiwezi kutoa wala kuiondoa….Akili nyenyekevu na moyo wenye shukrani vitatuinua juu ya majaribu madogo madogo na changamoto hakika. Kadiri tunavyopungua katika ari, nguvu na kuwa macho katika utumishi wa Bwana, ndivyo akili itakavyozidi kudumu katika nafsi, ikikuza vichuguu na kuvifanya milima ya matatizo…
Mzigo wa kazi ya Mungu, ambao uliwekwa mabegani mwa Musa, ulimfanya yeye awe mtu wa nguvu. Kwa miaka mingi, alipokuwa akitunza mifugo ya Yethro, alipata uzoefu uliomfundisha unyenyekevu wa kweli… Agizo la kwenda kuikomboa Israeli lilionekana kuwa kubwa sana; lakini, kutokana na kumcha Mungu, Musa alikubali amana. Tambua matokeo: Hakuishusha kazi hadi kwenye udhaifu wake; bali kwa nguvu ya Mungu aliweka jitihada ya dhati kujiadilisha na kujitakasa kwa ajili ya utume wake mtakatifu.
Kamwe Musa asingeandaliwa kwa ajili ya nafasi hii ya kuaminiwa k**a angemngojea Mungu kuifanya kazi kwa ajili yake. Nuru kutoka mbinguni itawajia wale wanaojisikia kuihitaji na ambao wanaitafuta k**a kutafuta hazina iliyofichwa. Lakini ikiwa tutazama hadi kwenye hali ya kutoshughulika, tukiruhusu udhibiti wa nguvu ya Shetani, Mungu hatatuletea uvuvio wake. Tusipotumia nguvu zetu zote ambazo ametupatia, daima tutabaki kuwa dhaifu na wazembe. Maombi mengi na zoezi kali la akili ni muhimu k**a tunataka kuandaliwa kufanya kazi ambayo Mungu ametuaminia. Wengi hawafikii kamwe nafasi ambazo wangeweza kuzishika, kwa sababu wanamngoja Mungu awatendee kile ambacho amewapa uwezo wajifanyie wenyewe. Wale wote ambao wameandaliwa kutumika, katika maisha haya ni lazima waandaliwe kwa kunidhamishwa vikali kiakili na kimaadili na kisha Mungu atawasaidia kwa kuunganisha nguvu ya kimbingu na jitihada ya kibinadamu…
Mazoea mabaya hayashindwi kwa juhudi ya namna moja. Nafsi inaweza tu kutawaliwa kwa kupitia kwenye pambano refu na kali.