Dagi Church Tanzania

Dagi Church Tanzania •DELIVERANCE ASSEMBLIES OF GOD INTERNATIONAL (D.A.G.I)
•NEW LIFE MIRACLE CENTRE•
•KIMARA-MWISHO DAR ES SALAAM
[email protected]
•P.O.BOX 31275

Deliverance Assemblies of God International Church inawatakia Heri ya Krismasi ✨🎄Tunawaalika waumini na jamii kwa ujumla...
24/12/2025

Deliverance Assemblies of God International Church inawatakia Heri ya Krismasi ✨🎄
Tunawaalika waumini na jamii kwa ujumla kuungana nasi katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyezaliwa kuleta wokovu, amani na upendo kwa wanadamu wote.
Maandiko yasemavyo:
“Kwa maana amezaliwa kwenu leo, katika mji wa Daudi, Mwokozi, ambaye ni Kristo Bwana.”
— Luka 2:11
🙏 Karibuni katika ibada za Krismasi na tuabudu pamoja kwa shukrani na sifa kwa Mungu.Deliverance Assemblies of God International Church inawatakia Heri ya Krismasi ✨🎄
. 🎄

Hongera sana Rev. Dr. Josephine Lyengi kwa kuteuliwa kuwa Makamu  Askofu Mkuu wa Deliverance Assemblies of God Internati...
12/10/2025

Hongera sana Rev. Dr. Josephine Lyengi kwa kuteuliwa kuwa Makamu Askofu Mkuu wa Deliverance Assemblies of God International! 🙌🏽
Mungu aendelee kukuongoza katika huduma hii ya heshima na neema. ✨
“Bwana atakutengenezea njia ya ushindi.” — Isaya 45:2

Hongera  kwa Mch. Edith Wambura kwa kuchaguliwa kuwa Mhasibu Mkuu! 🎉 Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii muhimu katika safa...
12/10/2025

Hongera kwa Mch. Edith Wambura kwa kuchaguliwa kuwa Mhasibu Mkuu! 🎉 Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii muhimu katika safari yako ya kiroho na kitaaluma. Neema ya Mungu iendelee kukuongoza katika majukumu mapya na kukupa hekima ya juu zaidi.

> “Bwana atakubariki na kukuimarisha; atakunyooshea uso wake akupe amani.”
— Hesabu 6:24-26

Tunakuombea mafanikio, amani, na baraka tele katika kila hatua ya safari hii mpya. 🙏🏽✨

Hongera Mch. Philipo Dabali kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Deliverance Assemblies of God International.Uteuzi huu n...
12/10/2025

Hongera Mch. Philipo Dabali kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Deliverance Assemblies of God International.

Uteuzi huu ni ushuhuda wa uaminifu, bidii na moyo wa utumishi aliouonesha katika kazi ya Mungu.
Tunaamini Mungu ataendelea kukuinua, kukutia nguvu na hekima zaidi katika majukumu haya mapya.

Tunakuombea neema, upendo na uongozi wa Roho Mtakatifu katika kila hatua ya safari hii mpya ya huduma.
Hongera sana mtumishi wa Mungu! 🙏🔥

HONGERA ASKOFU MKUU DR. GERMANUS B. P. LYENGI Tunamshukuru Mungu wa mbinguni kwa neema yake kuu aliyomimina juu ya mtumi...
12/10/2025

HONGERA ASKOFU MKUU DR. GERMANUS B. P. LYENGI

Tunamshukuru Mungu wa mbinguni kwa neema yake kuu aliyomimina juu ya mtumishi wake, Askofu Dr. Germanus B. P. Lyengi, kwa kuchaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Deliverance Assemblies of God International (DAGI).

Hii ni hatua kubwa ya kiroho na ushuhuda wa uaminifu, unyenyekevu, na utumishi wa kweli kwa Bwana kwa miaka mingi. Mungu ameendelea kuthibitisha kazi yake kupitia mtumishi huyu kwa ishara, maajabu na matendo makuu ya imani.

K**a Maandiko yasemavyo katika Marko 16:15–20,

> “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe… na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio…”

Tunatambua kwamba wito huu ni wa mbinguni, na tunaamini Mungu ataendelea kumpa hekima, nguvu, upendo na maono mapya ya kukuza ufalme wa Mungu ndani na nje ya mipaka ya taifa. 🔥

Tunampongeza yeye pamoja na familia yake kwa utii na kujitoa kwa kazi ya Mungu. Mungu aendelee kumtumia kwa nguvu mpya na wingi wa neema! 💫










MAOMBI YA SIKU 30 YA KUFUNGA NA KUOMBAKuanzia Jumatatu  tarehe 6 Januari hadi Jumanne ya tarehe 4Februari 2025Kutakua na...
03/01/2025

MAOMBI YA SIKU 30 YA KUFUNGA NA KUOMBA

Kuanzia Jumatatu tarehe 6 Januari hadi Jumanne ya tarehe 4Februari 2025

Kutakua na Maombi ya kufunga na kuomba kwa kanisa na washirika wake wote wa DAGI nchi nzima
Maombi ya kuombea;
-Uamsho
-Ulinzi
- Ukuaji wa makanisa ya DAGI
-Familia zetu
-Nchi ya Tanzania
-Kuukabidhi mwaka 2025
-Mahitaji ya kanisa la mahali pamoja

Mstari wa kusimamia:
Zaburi 37:5-7
5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.

6 Ataitokeza haki yako k**a nuru, Na hukumu yako k**a adhuhuri.

7 Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.

Kuanzia saa 10:30 had saa12:00 jioni kila siku!!
Karibu sana!





#30 days

CROSS OVER NIGHT-COME CROSS WITH YOUR BLESSINGS!!Karibuni sana katika Mkesha wa Kuvuka na Baraka zako Ndani ya kanisa la...
31/12/2024

CROSS OVER NIGHT-COME CROSS WITH YOUR BLESSINGS!!

Karibuni sana katika Mkesha wa Kuvuka na Baraka zako
Ndani ya kanisa la Deliverance Assemblies of God International lililopo Kimara Mwisho Vyumba Vinane Mtaa wa kwa Mama Nunuu
Kuanzia saa 3 kamili usiku had saa 7 usiku .
NYOTE MNAKARIBISHWA!



Tunawatakieni Heri ya Krismaass na Mwaka Mpya 2025 wenye baraka tele!Isaya 9:6-76 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, ...
26/12/2024

Tunawatakieni Heri ya Krismaass na Mwaka Mpya 2025 wenye baraka tele!

Isaya 9:6-7
6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.



#2025

WOTE MNAKARIBISHWA KUABUDU NASI!!!Jumanne 24/12/2024 Mkesha wa Krismass (Christmass Eve)Jumatano 25/12/2024 Ibada ya Kri...
24/12/2024

WOTE MNAKARIBISHWA KUABUDU NASI!!!

Jumanne 24/12/2024 Mkesha wa Krismass (Christmass Eve)
Jumatano 25/12/2024 Ibada ya Krismass (Christmas's Day)
Jumapili 29/12/2024 Ibaada ya Jumapili ya mwisho wa mwaka (Last year's Sunday Service )
Jumanne 31/12/2024 Mkesha wa Kuvuka Mwaka (New Year's Eve)
Jumatano 1/1/2025 Ibada ya shukrani (Thanks giving day)

Mahali ni Kimara Mwisho Vyumba Vinane




Mwimbaji Paul Mwazembe atakuwepo kuhudumu katika kongamano kubwa la KUWALETA WATU KWA YESU!!Hakika   la Yesu ni moto!!!E...
12/12/2024

Mwimbaji Paul Mwazembe atakuwepo kuhudumu katika kongamano kubwa la KUWALETA WATU KWA YESU!!
Hakika la Yesu ni moto!!!
Ewe ndgu karibu uwekwe huru kwa jina la Yesu, maana jina la Yesu ni moto ulao!!!

Mwinjilisti  Batilda Mahundi na Mwenyekiti k**ati ya maandalizi atakuwepo !!! Walete Wagonjwa na wenye shida mbalimbali ...
12/12/2024

Mwinjilisti Batilda Mahundi na Mwenyekiti k**ati ya maandalizi atakuwepo !!!
Walete Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa
sana mtu wa Mungu

Upendo Sanga Mwimbaji atakuwepo kuhudumu
12/12/2024

Upendo Sanga Mwimbaji atakuwepo kuhudumu

Address

Kimara-mwisho
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dagi Church Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Dagi Church Tanzania:

Share