23/02/2026
Injili ya Tomaso /Gospel Of Thomas sio kitabu cha masimulizi k**a zilivyo Injili zingine za kikanuni katika Biblia, bali ni mkusanyiko wa kauli zinazo husishwa na Yesu...ni misemo mifupi inayo mualika mtafutaji wa nuru kutazama ndani yake mwenyewe. Tofauti na mafundisho yaliyo ratibiwa na kupangiliwa na kanisa la Mwanzo, Injili ya Tomaso inamuwasilisha Yesu k**a mwalimu wa maarifa ya moja kwa moja ya kiroho yaani Gnosis, ikielezea kwa kina kwamba "Ufalme wa mbinguni" sio eneo la nje bali ni utambuzi unao tokea ndani ya Nafsi.
Moja ya kauli zake zenye uzito mkubwa ipo kwenye kauli ya :3
"Ufalme upo ndani yenu, na upo nje yenu; mtakapo jitambua ndipo mtajulikana, nanyi mtatambua ya kuwa ninyi ndiyo watoto wa Baba aliye hai. Lakini msipojitambua, mnakaa katika umasikini, na ninyi wenyewe ndio huo umasikini".
Hapa yesu anamaanisha kwamba; "Wokovu" haupatikani kupitia mafundisho rasmi ya kidini ama desturi zilizo pangiliwa za kidini, bali wokovu hupatikana kwa Kuamka kiroho, kwamba kujitambua ndiyo Ufunguo wa kutambua Uhalisia wa Kimungu.
Mtazamo huo pia unapatikana katika kanuni za "The Kybalion" na katika falsafa za Kihemetiki pale walipo sema "k**a ilivyo ndani, ndivyo ilivyo nje".
Ufalme wa Mungu haupatikani kwa kusubiri tukio la nje, haupatikani kwa kumsubiri fulani aliyepanda farasi mweupe akitokea mawinguni, Bali Ufalme unapatikana kwa kujitambua na kugundua cheche ya kimungu ambayo tayari ipo ndani ya mwanadamu ... Ufalme wa mbinguni upo ndani yenu.
Kwahiyo, Injili ya Tomaso si kwaajili ya wafuasi wa imani na desturi wanao fuata tu bila kuhoji, bali ni maandiko ya watafutaji...wale walio tayari kuvuka pazia la mazoea na dhana za juu juu, ili kutafuta ukweli ndani yao wenyewe.