Kibo spiritual centre

Kibo spiritual centre Sisi ni kanisa la KIpentekoste chini ya Dhehebu la Tanzania Assemblies OF God (T A G) Tunaoamini kuwa Kwa msaada wa Mungu Tutatenda makuu Zaburi 60:12

26/04/2026
12/04/2026

Ibada ya Jumapili April 12, 2026

10/04/2026

IBADA YA PASAKA 2026

USIKOSEEE
18/02/2026

USIKOSEEE

29/07/2025

Tunakukaribisha katika ibada zetu zinazoendelea kila siku ya wiki.

wasiliana nasi kwa namba 0738784161 ili kupata msaada wa kiroho ushauri na maombezi bure kabisa.

29/07/2025

JE UNAJUA KUWA MUMGU ANAKUPENDA?
Biblia katika Injili ya Yohana inasema " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milile"
+ Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu huu ambamo wewe unakaa na kufanya shughuli za maisha yako.
+ Kusudi la Mungu la kukupatia zawadi hii yaani ulimwengu ni ili awe na ushirika na wewe, awe Mungu na Baba kwako nawe uwe mwana wake wa kiume au wa k**e.
Biblia katika Waraka kwa Warumi 5:12 inasema " Kwa hiyo k**a kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.
+ Mtu wa kwanza kuishi hapa ulimwenguni( Adamu) alimkosea Mungu kwa kuasi amri yake. Akavunja ushirika na Mungu.
+ Binadamu wote wamezaliwa kutokana na Adamu aliyemwasi Mungu kwa kutenda dhambi na kwa sababu hiyo wako dhambini, hawana ushirika na Mungu. Hata wewe uko dhambini.
+ Mungu ni Mtakatifu sana na mwenye haki anachukia dhambi, na hivyo atamhukumu mwanadamu mwenye dhambi kwa kumtupa katika ziwa la moto wa milele yaani Jehanamu.
+ Lakini Mumgu pia ni mwenye upendo na ni mwenye huruma. Kwa kumpenda na kumhurumia Mwanadamu alimtuma Yesu Kristo ili aje azichukue dhambi za Mwanadamu ili kurudisha ushirika na Mungu kwa kujitoa kufa msalabani badala ya mwanadamu.
Biblia katika waraka kwa Warumi 10:9 inasema " Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka
+ Kwa kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako( kuwa dhabihu ya dhambi zako); Utasamehewa dhambi zako zote, utasafishwa na udhalimu wako wote na kufanywa Mwana wa Mungu. Ushirika wako na Mungu muumba wako utarudishwa tena.Utaokoka na madhara ya dhambi.
K**a unapemda kuitikia upendo huu wa ajabu wa Mungu, omba ombi hili kwa kumaanisha: Baba Mungu nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi. Napokea upendo wako. Namkiri Yesu kuwa Bwana wangu na Mwokozi wangu. Unisamehe dhambi zangu zote. Kwa Jina la Yesu unifanye kuwa mtoto wako, Amina.
Kwa msaada zaidi wasiliana nami kwa simu namba 0754290177 au Fika Kanisa la TAG Kibo Spiritual Centre.

Address

Unnamed Road
Dar Es Salaam
KSC2002

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kibo spiritual centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kibo spiritual centre:

Share