08/12/2020
roho ya yezebel ( JEZEBEL SPIRIT/ THE FREEMASONRY SPIRIT
- Mwezi huu mzima nitakuwa na muda wa kuielezea hii roho na ntakuongoza vyema katika kushinda hii roho
- hii roho ilikuwa inatawala dunia, Iliingia na kutawala makanisa,
- lengo ilikuwa ni kuisambaza hii roho kwenye mifumo yote ya kidunia kwa mfano kwenye siasa, elimu, mziki, dini, nk
Ndio maana unapokuwa mahali fulani jua roho inayotawala mahali pale
- hii roho ndio ilikuwa inawafanya manabii watabiri uongo ili kuwajaza watu tamaa ya vitu kuliko kiu ya MUNGU ambaye ndio mwenye kutoa Kila kitu
MBINU AMBAZO SHETANI ALIKUWA ANATUMIA KUSAMBAZA HII rOHO
1. Kupitia injili, ila injili ya uongo, mafundisho ya uongo, utabiri wa uongo, nk
- hii roho ilikuwa imejificha kwenye mambo ya Imani ( dini ), ili kuharibu Imani za watu
2. Lakini pia hii roho ilikuwa inasambazwa kupitia mziki, uimbaji
3. Hatua ya mwisho kubwa kabisa iliyokuwa inatumika kusambaza hii roho ni kupitia kurekodi filamu za ngono kwa mtu ambaye anaonekana Ni maarufu/ kuwa anaushawishi mkubwa kwa watu ili kuiingiza hiyo roho
- ukiangalia tu hizo video, hiyo roho inakuingia
- Naomba nieleweke hivi, roho ya yezebel ilikuwa inawatawala wote wanawake na wanaume
Mfano mfalme Ahabu alikuwa na roho ya yezebel. ( 1 WAFALME 21)
MFAHAMU YEZEBEL NI NANI?
- Yezebel ni shetani mwanamke ( shetani wa k**e)
- Jina jingine anaitwa malkia wa mbingu
- Yeye anamsaidia Baali, ( mfalme wa Anga / mkuu wa Anga )
- malaika Michael ndio kiboko ya yezebel atampasua pasua yezebel
- yezebel anajiita kahaba mkuu, atakaemshughulikia yezebel anaitwa malaika mkuu
- yezebel anaitwa mama wa makahaba, yaani makahaba wote unaoona wanajiuza , yaani Yeye ndio mama yao
UFUNUO 17:5
Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa kwa siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI
UFUNUO 19: 2
Kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake na kuipatiliza damu ya watumwa wake mikononi mwake
- Yezebel Ni mwuaji, ( roho ya uuaji)
UFUNUO 17:6
nikamwona Yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu,
1 WAFALME 18:4
Kwa kuwa ikawa Yezebel alipowaua manabii wa Bwana
1 WAFALME 18:15
Je BWANA wangu hauambiwa nilivyofanya hapo yezebel alipowaua manabii wa BWANA
- Anawafunga midomo manabii wa kweli wa MUNGU wasiseme ( roho ya kuwafumba watu midomo wasiseme ukweli )
1 WAFALME 19
Basi Ahabu akamwambia Yezebel habari ya mambo yote aliyoyafanya Elia, na jinsi alivyowaua manabii wote wa uongo kwa upanga, ndipo yezebel akampelekea Eliya mjumbe kusema , miungu wanifanyie hivyo na kuzidi nisipokufanya roho yako kesho panapo wakati huu, k**a roho ya mmojawapo wa hao
- Anaitwa kahaba mkuu
UFUNUO 17
" Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami akisema , njoo huku nitakuonesha hukumu ya Yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake
- Yezebel anapenda urembo kujipamba pamba
2 WAFALME 9:30
Hata yehu alipofika yezreel , yezebel amapata habari, akatia uwanja machoni pake, akapamba kichwa chake akachungulia dirishani
LAKINI YEHU ALIPOTUMWA KWENDA KUMUUA, HAKUANGALIA UREMBO WAKE WALA WANJA WAKE, ALIMUUA K**A ALIVYOAGIZWA NA MUNGU
2 WAFALME 9:31
Hata yehu alipoingia lango la mji, alisema je ni Amani? Ewe zimri mwenye kumuua Bwana wako? Yehu akainua uso wake kuelekea dirishani, akasema aliye upande wangu ni Nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia, wakasema mtupeni chini, na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta
- yezebel anachochea maovu ( roho ya kuchochea maovu )
1 WAFALME 21:25
Lakini hapakuwa na mtu k**a Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA ambaye yezebel mkewe alimchochea
- yezebel Ni mzinzi na ni mchawi ( roho ya uchawi )
2 WAFALME 2:9
" Yehu akajibu, Amani gani maadam uzinzi wa mama yako yezebel na uchawi wake Ni mwingi?
- yezebel Ni mwanamke aliyelaaniwa ( roho ya laana )
2 WAFALME 9:34
" Alipoingia akala na kunywa Kisha akasema mwangalieni mwanamke huyu aliyelaaniwa, mkamzike, kwa maana Ni binti mfalme
- Yezebel Ana kiburi ( roho ya kiburi )
- roho ya kujiona Mimi ndio Mimi, hakuna wa kuniweza, hakuna wa kunishusha, bila kujua kuwa MUNGU ndiye ndiye aliyewaumba wanadamu wote
UFUNUO 18:3
Kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanyabiashara wa nchi wamepata Mali kwa nguvu za kiburi chake
- yezebel Ni mpotoshaji ( roho ya kushauri watu uovu)
1 WAFALME 21:5
Lakini yezebel mkewe akamwendea, akamwambia kwa nini roho yako Ina huzuni hata usile chakula?
Akasema kwa sababu nimesema na Nabothi myezreel nikamwambia unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha au ukipenda nitakupa shamba la mizabibu jingine badala yake. Akajibu sitakupa shamba langu la mizabibu
- yezebel ni muongo ( anashauri watu uongo )
1 WAFALME 21: 7
Yezebel mkewe akamwambia je sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israel? Ondoka ule chakula moyo wako ufurahi , Mimi nitakupa shamba la nabothi