Maranatha Reconciliation Church Kigamboni

Maranatha Reconciliation Church Kigamboni Maranatha Reconciliation Church is a pentecostal church that believes in the salvation through Jesus Christ the Son of God.

We believe that men can never become Christians unless they are born again through the Holy Spirit, by being washed in the Blood of kanisa la Maranatha Reconciliation ni kanisa linalofuata mfumo wa kipentekoste. Neno Maran atha kwa kiswahili la maanisha BWANA WETU ANAKUJA(1wakorinto16:22) na RECONCILIATION likimaanisha upatanisho. Kupitia maneno haya, ni wazi huduma ya MRC ipo ili mabadiliko chanya ya kiroho na kimwili katika jamii, na kuwapatanisha wanadamu na Mungu..

Kongamano lilifanyika tarehe 9 - 15 September 2019
15/09/2019

Kongamano lilifanyika tarehe 9 - 15 September 2019

NGUZO ZA UPENTEKOSTE
01/09/2019

NGUZO ZA UPENTEKOSTE

23/03/2019
19/02/2019
Mungu azidi kukufanikisha katika masomo yako, Ushindi na ufaulu Wa juu ni fungu lako, Joshua Mkoma
26/03/2018

Mungu azidi kukufanikisha katika masomo yako, Ushindi na ufaulu Wa juu ni fungu lako, Joshua Mkoma

05/03/2018

MARANATHA RECONCILIATION CHURCH
Maombi 4 – 11 Machi, 2018

Ungana na maelfu ya waamini kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake kwa kukulinda, kukulisha kiroho na kimwili, na kukutana na mahitaji yako, katika kipindi cha mwezi Februari.
Maana za tarakimu katika utamaduni wa Kiebrania, 18 ni tarakimu za hukumu na mwanzo mpya. Tumwombe Mungu ili hukumu yake iangukie mifumo yote inayolenga kuharibu jamii kiroho na kimwili, pia tuombe ili kianze kipindi kipya cha mafanikio, kwa watoto wa Mungu.
Unabii wa Chuck Pierce unaonyesha kuwa huu ni mwaka wa malango, milango, vita na malaika. Tuombe ili malango yanayozuia baraka za watoto wa Mungu yaachie mwaka huu, malaika wawafungulie watu wa Mungu milango ya kutenda mambo makuu na uwe mwisho wa vita zilizokuwa zikiwasumbua waamini kwa muda mrefu.
Neno linasema tukimpenda Mungu tutatii amri zake. Kutokana na maneno haya, ni wazi kutokutii maagizo yanayotolewa na wachungaji, ni ishara ya kuporomoka kwa kiwango cha upendo wa waamini, kwa wachungaji wao. Inua kizazi kipya, cha waamini wenye kiu ya kuwapenda na kuwaheshimu wachungaji wao.
Ombea ustawi wa kiroho na kimwili, kwa Waafrika wanaoishi nje ya bara hili, wanaotegemeza kazi ya Mungu barani Afrika.
Msalaba unatutenga na dhambi, ubatizo wa Roho Mtakatifu unatutenga na dini zilizokufa, na udhihirisho wa karama za rohoni unatuwezesha kuzifanya kazi zilizofanywa na Yesu Kristo. Tufungulie kiu ndani ya kanisa, ya kuona udhihirisho wa karama za rohoni.
Omba kuwe na mabadiliko ya kisiasa yatakayoruhusu uhuru wa kuabudu, katika mataifa kumi yanayoongoza kwa kutesa Wakristo. Mataifa haya ni Korea kaskazini, Afghanistan, Somalia, Sudan, Pakistan, Eritrea, Libya, Iraqi, Yemen na Iran.
Kulingana na takwimu za kiuchumi, nchi 9 kati ya 10 maskini kuliko zote duniani, ziko barani Afrika. Nchi hizi ni Afrika ya kati, DRC, Burundi, Liberia, Niger, Malawi, Msumbiji, Eritrea na Madagasca. Tuwaombee waamini wa mataifa haya, ustawi na mafanikio ya kiuchumi.
Wakati Wakristo wakilaumu magaidi kwa kufunza watoto wao kuua, nao wamekuwa wakifanya hivyo bila kujua, kwa kuwanunulia watoto wao ‘video games’ za vita, mauaji na uchawi. Tuwaombee waamini watambue hili kuzuia uchafu huu kwa watoto wao.
TuombeE kuachiliwa kwa waamini waliofungwa katika nchi zisizokubali Ukristo. Ni pamoja na Shafgat Emanuel na mkewe Shagfuta Kausar, waliokamatwa tarehe 20/7/ 2013 na kuhukumiwa kuuawa kwa madai ya kumkufuru mtume Muhammad.
Ingawa bado wako watumishi wa k**e wanaowika duniani, bado hawajapatikana wanawake wa kuvaa viatu vya Catheren Khulman na Maria Woodworth-Etter. Tumwombe Mungu ili ainue jeshi la wanawake wenye kiu ya kutumiwa na Mungu, kwa kiwango cha kustaajabisha.
Tufungulie kiu ya kutafuta uso wa Mungu, kwa waamini wote waliookoka katika juma la tarehe 25/2 – 4/3.
K**a unafurahishwa na huduma yetu ya kufikisha Injili vijijini, waweza kutoa sadaka yako katika akaunti ya: Maranatha Reconciliation church, CRDB Holland House Branch, no 1022645600

Address

Dar Es Salaam, Kigamboni
Dar Es Salaam
S.L.P7812

Telephone

+255785788196

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maranatha Reconciliation Church Kigamboni posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Maranatha Reconciliation Church Kigamboni:

Share