Mlima wa Baraka Gospel Assembly Mission Church

Mlima wa Baraka Gospel Assembly Mission Church Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mlima wa Baraka Gospel Assembly Mission Church, Religious organisation, Mlima wa Baraka Street, Dar es Salaam.

29/04/2024

YESU KRISTO YU HAI NA MUNGU YUKO KAZINI

13/01/2022

MLIMA WA BARAKA PENTECOSTAL MISSION CHURCH.

25/02/2020
01/11/2018

Tarehe 1/12/2018 tutakuwa na semina ya vijana. Kichwa cha somo ni "AKILI SABA ZA MWANADAMU" CHAKULA CHA ASUBUHI NA MCHANA KITATOLEWA BURE.

01/11/2018

Nakutakia Baraka za mwezi wa 11.

31/10/2017

HAKUNAGA MAOMBI YA KUACHA DHAMBI, ILA KUNA UAMUZI WA KUACHA DHAMBI. TAFAKARI CHUKUWA HATUWA

12/10/2017

Tuendelee kidogo katika somo letu. Mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu ya ke mda mrefu alikutana na kikwazo cha sheri za dini, hakujali akasema:" nitakwenda hivyo hivyo, nami nitafanya neno moja tu, nitaligusa pindo la va\i lake, nami naamini nitapona." hiyo ilikuwa imani yake. Mara nyingi sheria za dini zetu zinakuwa kikwazo katika kukutana na Mungu na kufunguliwa. Dini haiwezi kuku saidia kabisa. Huyu mwanamke alitumia ile sheria kuwa kinga yake itakayomsaidia kumfikia yesu kwa haraka na wepesi sana. maana alijuwa " kila atakaye mwona atampisha ili asigusane naye asije akawa najisi pia, Hivyo wote walimpisha. Leo acha kila kilichokuinukia kinacho kuzuia usiingie katika muujiza wako kikupishe. Milango ya uponyaji na Baraka ikufungukie kwa jina la Yesu

10/10/2017

Katika mwendelezo wa somo letu la jana ni kwamba mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu kwa mda wote ule, aliposikia kuwa ni Yesu anapita aliadhimia moyoni mwake kwamba mimi nitakwenda kwa yesu, ila nitafanya kitu kimoja tu. " nitagusa tu pindo la vazi lake, nami naamini nitapona" hiyo ilikuwa imani yake. " kugusa tu pindo la vazi la Yesu. wewe je, imani yako inakuambia ufanye kitu gani kwa yesu?
KATIKA KUMWENDEA YESU, yule mwana mke alikutana na vikwazo:
1. alikutana na sheria ya wayahudi iliyosema " mwanamke k**a akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au k**a anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake atakuwa k**a alivyokuwa katikasiku za kutengwa kwae..........................na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni. Nkila kitu atakachokigusa kitakuwa najisi............." Mambo ya walawi 15: 25-27

SOMO LA LEO: Mara nyingi sheria za dini zinatuchelewesha kukutana na Yesu na kupokea miujiza yetu, hapo mtu anaendelea kuteseka na shida szisizokwisha. leo navunja kila sheria iliyosimama mbele yako inayokuzuia kumwendea yesu. kila vikwazo vikuachie tangu sasa kwa jina la yesu. huu ni wakati wako wa kuinuka na kusonga mbele. Barikiwa.
itaendelea kesho

09/10/2017

Luka 8:40-56 Hapo unakuna na ujumbe wa ajabu kwa ajili ya maisha yako. 1. Mkuu wea sinagogi kumpigia yesu magoti na kumwomba aje kumponya mwanaye ambaye alikuwa katika hali ya kufa. Ilikuwa si kawaida au desturi kwa wayahudi kumpigia mwanaume mwenzio magoti. ila kwa Yesu kila goti linakunjwa. Katika shida yako, mwendee Mungu kwa unyenyekevu. Mungu halaumiwi.
2. Walipokuwa katika safari ya kwenda, njiani walikuna na mwanamke aliyekuwa akitoka damu kwa muda wa miaka18 huyu aliadhimia kumwendea ili ilimradi aguse tu pindo la vazi lake. Aliamini kuwa akigusa tu pindo la vazi la yesu atapona. leo mwendee yesu utpona.
UJEMBE WA LEO: " HAKUNA ALIYEKUTANA NA MUNGU AKABAKI K**A ALIVYO"

04/10/2017

Kila jambo lina Sababu
Na
Askofu
Munga Ibrahim

Kila tatizo nyuma yake kuna roho (fungamano)
Hata nyuma ya wokovu wetu kuna Roho Mtakatifu.
Yohana 5:14

Ukiona ugonjwa hausikii dawa, ujue nyuma yake kuna roho.
Kila dhambi unayo tenda, ina gharama yake(itakugarimu)
Dhambi ndio iliyo mshikilia ili asipate uponyaji yule mgonjwa kwenye kisima, watu walikua wanakuja wanapokea uponyaji na yeye yuko pale pale.
Kila jambo lina sababu yake.
Furaha ina sababu yake na huzuni pia ina sababu yake.
Je, wewe furaha yako inatokana na nini
Je, huzuni yako inatokana na nini?
Mungu anaweza mambo yote.
Huwezi kufurahi bila sababu wala kuhuzunika bila sababu. Kila furaha ina matokeo yake.

Uvumilivu wako utakufikisha kwenye muujiza

Neno: "siwezi" ni ugonjwa
Maana Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.
Wafilipi 4:13

Unajua kwanini hujapona?
Ni kwa sababu akili yako imekaa kufikiria vile ulivyo shindwa jana.
Ishara ya uponyaji ni Mabadiliko yanayo tokea ndani yako.
Yohana 5:8

USIKOSE KU SHARE NENO HILI

MUNGU AWABARIKI

By
Bishop
Munga Ibrahim

Word of the dayBy Bishop Munga Ibrahim Waefeso 3:2020 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote ...
26/09/2017

Word of the day
By Bishop Munga Ibrahim

Waefeso 3:20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Waefeso 3 :20

MUNGU hufanya mambo makubwa mno kuliko mawazo yetu na kuliko maombi yetu. Maana njia zake ziko juu sana kuliko sisi, naye hutuwazia mema daima.
Wakati mwingine tunaweza kuhitaji vitu vilivyo dhaifu kumbe yeye hutuwazia mambo ya kudumu, anataka atupatie vitu vinavyo dumu.

MAJIBU YA MUNGU YANA TEGEMEANA NA NGUVU IPI ITENDAYO KAZI NDANI YAKO.

Je, ndani yako ipo nguvu ipi inayo tenda kazi?

Address

Mlima Wa Baraka Street
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 15:15

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mlima wa Baraka Gospel Assembly Mission Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share