26/07/2026
IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 26/07/2026 KANISA LA EFATHA MKOA Wa USHINDI, DAR ES SALAAM TANZANIA
Tenzi No 24
1.Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.
2.Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu, Mwanawe Mungu.
3.Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
kwa kuwa ninaye Yesu.
Zaburi 51:1-4 "Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu."
Tenzi No 157
1.Kijito cha utakaso
ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo
kunipa wokovu
Kijito cha utakaso,
Nizame kuoshwa humo
Namsifu Bwana kwa hiyo
Nimepata utakaso
2.Viumbe vipya naona;
damu ina nguvu,
imeharibu uovu
ulionidhulumu
Zaburi 24:1-10 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu."
©️ MTUME MAGRETH ILOMO - KANISA LA EFATHA MKOA WA USHINDI.