An Abdulrazzaq

An Abdulrazzaq FannaniGPT

📝 MTUNZI:
✏️ Mashairi.
✏️Tenzi.
✏️ Hadithi Fupi.
🕋BASED ON ISLAMIC LAWS. THE GUARDIAN TEACHER

MIMI NAANZA:Allah atujaalie Mabachela sote tupate ndoa... Allahumma amyn 🤲
15/08/2026

MIMI NAANZA:

Allah atujaalie Mabachela sote tupate ndoa... Allahumma amyn 🤲

14/08/2026
MAJIBU KWA Najma Rashid - TATIZO LAKO NI PUPA -1.Haya hudhuria hapa, na mimi nikupe neno. Umenivunja mifupa, umefika mba...
09/08/2026

MAJIBU KWA Najma Rashid

- TATIZO LAKO NI PUPA -

1.
Haya hudhuria hapa, na mimi nikupe neno.
Umenivunja mifupa, umefika mbali mbali.
Na tabu zote wajipa, vipi kumaliza wino.
Tatizo lako ni pupa, tulia ule vinono.

2.
Wewe sio jikeshupa, waonavyo si maono.
Hupaswi japo kuchupa, hakika wewe ni nino.
Punguza kutapatapa, mwisho ukang'oka meno.
Tatizo lako ni pupa, tulia ule vinono.

3.
Na mimi moyo nakupa, fanya hapa tulizano.
Ni kwako ninajitupa, sitaki hata mfano.
Namba moja iko hapa, sina mbili wala tano.
Tatizo lako ni pupa, tulia ule vinono.

4.
Mbele za watu naapa, kuwa nawe inteno.
Raha zako ziko hapa, dozi kutwa mara tano.
Tule papa na lupapa, nyama ziko nyingi mno.
Tatizo lako ni pupa, tulia ule vinono.

5.
Na wala aikukuwepa, ama kuvunja agano.
Nikuweke kwa kichupa, moyo kuupa kibano.
Na mwisho nitakulipa, kwa kila lako sonono.
Tatizo lako ni pupa, tulia ule vinono.

An Abdulrazzaq
Replies
👇

SUBIRI NDOA
09/08/2026

SUBIRI NDOA

- MFANO WANGU - 1.Niwambie sitokwisha, kwa kunipunguza kwenu. Ni bure mutajichosha, na kutupa muda wenu. Hamtoninyamazis...
05/08/2026

- MFANO WANGU -

1.
Niwambie sitokwisha, kwa kunipunguza kwenu.
Ni bure mutajichosha, na kutupa muda wenu.
Hamtoninyamazisha, kwa hizo kelele zenu.
Ardhi ni yenu maisha, ndo mfano wangu kwenu.

2.
Japo mwajiaminisha, mimi si muhimu kwenu.
Kawa mwajihangaisha, kunikwepa kila mbinu.
La hamtofanikisha, mimi ni msingi wenu.
Ardhi ni yenu maisha, ndo mfano wangu kwenu.

3.
Nasema namaanisha, mufungue mbongo zenu.
Sipate tabu kukesha, mtaumwa macho yenu.
Mola amempandisha, juu ya mawazo yenu.
Ardhi ni yenu maisha, ndo mfano wangu kwenu.

4.
Leo nazisawaziaha, potovu fikira zenu.
Mulizozihalalisha, kunidharau mwenzenu.
Wacha kujitakatisha, kwa kuchafua wenzenu.
Ardhi ni yenu maisha, ndo mfano wangu kwenu.

5.
Kuitwa kwenu Aisha, Abdallah ama Wanu.
Hikuwa kigezo tosha, cha utakatifu wenu.
Kitaka kujisafisha, safisheni nyoyo zenu.
Ardhi ni yenu maisha, ndo mfano wangu kwenu.



04/08/2026

UJUMBE KUHUSU SHETANI 😈

゚viralシfypシ゚

03/08/2026

Big shout out to my newest top fans! Salim Salim Sharif, Mwanamisi Bwata, Raina Raina, Facet Mood, Hussein Alsibtwiy, Patchess Lite

02/08/2026

MIMI NA WEWE SIO MAADUI 💬💬💬

゚viralシ

01/08/2026

LEO TUPO NA KAKA KIONGOZI


゚viralシ

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
11101

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when An Abdulrazzaq posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to An Abdulrazzaq:

Shortcuts

Share