01/09/2026
MAJIRA YA KUKUTANA NA MUNGU
Shalom shalom tunaamini Mungu anakutunza na unaendelea kulitumikia kusudi la Mungu kwenye maisha yako.
Naomba kuchukua nafasi hii kukuribisha Ijumaa hii ya tarehe nne September tunaanza Kambi yetu ya mfungo wa Tatu kavu,
Hii ni Kambi yetu ya Tisa tangu mwaka 2026 uanze.Karibu sana tumlingane Bwana kwaajili ya majira mapya ya Mwezi wa tisa.Kambi yetu itaanza ijumaa saa tisa jioni na kuisha Jumapili saa kumi na mbili jioni.
Mambo ya kutarajia katika Kambi hii
1:Kupata muda wa kutosha wa kusoma Neno la Mungu pamoja,kumbuka kwa kadri unavyojaza Neno la Mungu ndani yako ndivyo unavyozidi kuyajua mapenzi yake kwako.
Na Kambi hii tutasoma vitabu vifuatavyo kwa pamoja
1:Nehemia
3:Yakobo
3:Waefeso
4:Wafilipi
5:Nahumu
6:Malaki
7:Ruth
8:Esta
2:Lakini pia utapata muda wa kujitenga Ili kuweza kuomba kwa muda mrefu,
Tunapokuwa nyumbani mara nyingi ni vigumu kupata muda wa utulivu wa kukaa na kupata muda wa utulivu wa kuomba.Hata Yesu mara nyingi alikuwa akijitenga Ili kupata muda wa utulivu Ili kuomba,hapa utapata muda wa utulivu kwaajili ya kuomba.
3;Na utapata muda wa utulivu wa peke yako wa kumsikiliza Mungu walau masaa matatu,lisaa limoja kwa kila siku ukiwa peke yako.
4:Utapata kusikia shuhuda zitakazokujenga kutoka kwa watu wengine.Hizi zitakujenga na kukupa nguvu ya kuendelea.
KUMBUKA HILI SIKU ZOTE, MUDA UNAOUTUMIA KWA MUNGU HAUUPOTEZI BALI UNAUWEKEZA,KARIBU TUWEKEZE TENA MUDA KWAAJILI YETU NA VIZAZI VYETU.
KANISA LIPO NJIA YA GOBA KUTOKEA MAKUMBUSHO, MBEZI MWISHO,AU KAWE.
Utaomba msaada kushuka kwa pembe
Ukishuka utaona bango limeandikwa Empower Life Ministries
Jisajiri kwa kutuma Jina lako kamili ,na Neno Kambi ya maombi kwa namba 0769141105.
Hakika hii siyo ya kukosa
Pastor Winnie Kilemo
Empower Life Ministries
0769141105
Umebarikiwa