Nguvu ya msalaba

Nguvu ya msalaba Huduma ya MAOMBI & MAOMBEZI

08/06/2022

RHAPSODI YA UHAKIKA (PATA NAKALA YAKO YA MACHI HAPA=> http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1)

Jumatano, Machi 24

KUPOKEA MSAMAHA NI KITENDO CHA IMANI

Mchungaji Chris

Bali tukienenda nuruni, k**a yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote (1 Yohana 1:7).

Je! Ulijua kuwa katika Agano Jipya, Mungu hakutuambia tumuombe msamaha? Kumuomba msamaha ni k**a vile kumuomba Akuokoe. Fikiri kuhusu hili: K**a ukimuomba msamaha, ni lini utajua kuwa amekujibu?

Vile vile, k**a unamuomba aiokoe nafsi yako, utajuaje kuwa amekuokoa? Kamwe hutojua, kwasababu hakuna kitu chochote kuhusu kukuokoa ambacho Yeye bado hajakifanya. Ni vivyo hivyo na msamaha; unapokea msamaha; hauombi, kwasababu damu ya Yesu Kristo ilimwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Baadhi ya Wakristo kila siku humuomba Mungu msamaha, na kwasababu wanaomba kitu walichopewa tayari, hawatumii imani. Unapaswa kupokea msamaha k**a tendo la imani yako. Baada ya hapo, ishi juu ya hali hiyo kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu na Neno.

Tayari umeoshwa na kusafishwa dhambi zako. Wakolosai 1:21-22 inasema, “Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama.” Hili lilitokea kabla hata hujafanya chochote sahihi au kisicho sahihi. Kwa hiyo, kataa kuwa na ufahamu wa dhambi. Wewe ni haki ya Mungu katika Kristo Yesu; fikiri na uiishi haki.

Andiko letu la ufunguzi linasema k**a tukienenda nuruni (katika Neno) k**a Yeye alivyo nuruni, damu ya Yesu yenyewe yatusafisha [moja kwa moja] kutoka katika dhambi yote. Kwa kuwa hili ni kweli, huna haja ya kuwa unaungama dhambi zako wakati wote. K**a ukifanya kosa, wewe sema tu, “Bwana, samahani kwa nilichofanya; ninapokea msamaha katika Jina la Yesu”; hivyo tu. Unaweza kuuliza, “Ndio rahisi namna hiyo?” Ndiyo, ni hivyo. Ndani ya Kristo, tuna kusafishwa dhambi moja kwa moja [bila kuomba wala kufanya chochote]; hilo ni sehemu ya kazi ya ukombozi ya damu Yake kwa niaba yetu.

UKIRI

Nimeooshwa na kutakaswa. Nimehesabiwa haki kwa neema ya Yesu Kristo, ninatembea katika haki Yake, nikiwa huru dhidi ya mash*taka ya yule muovu, na nipo huru kumtumikia Bwana, Kristo! Haleluya!

Kumbuka kujisajili kwa ajili ya Siku ya Maombi Ulimwenguni na Mchungaji Chris itakayofanyika Ijumaa, Machi 26 hadi Jumamosi, Machi 27. Jisajili hapa prayer.rhapsodyofrealities.org/swahili

MAFUNZO ZAIDI:

1 Wakorintho 6:11
Warumi 8:1

TUOMBE

👉🏾 http://prayer.rhapsodyofrealities.org/swahili

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Luka 5:17-39 & Kumbukumbu la Torati 28

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
Mathayo 25:14-30 & Kutoka 33

Mpatie mtu mwengine nafasi ya kupokea Neno la Mungu litakalobadilisha maisha yake. Shiriki leo katika usambazaji wa Rhapsodi ya Uhakika kwa kuchangia walau kiasi cha kopi moja. Tafadhali fuata tovuti hii kushiriki: https://bit.ly/2F2t0mY

Mungu akubariki.

Kutoka 15:26
22/05/2022

Kutoka 15:26

Mwanzo 3:21Neno la mungu ni pumzi ya uhai
22/05/2022

Mwanzo 3:21
Neno la mungu ni pumzi ya uhai

Power of Cross Ministry
10/04/2022

Power of Cross Ministry

Wakati wa mungu ni wakati sahihi
10/04/2022

Wakati wa mungu ni wakati sahihi

Mhubiri 5:1Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapu...
10/04/2022

Mhubiri 5:1

Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.

10/04/2022

Karibuni Ibada jumapili ijayo

10/04/2022

Karibu Tusifu na kuabudu kwa pamoja

10/04/2022

Kwaya ya kanisa

Power of Cross Ministry Mburahati

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nguvu ya msalaba posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Nguvu ya msalaba:

Share

Category