13/08/2025
SOMO: UKOMBOZI WA FIKRA
KNGZ : MCH GEORGE MWANYIKA
Ukombozi ni mchakato ambao mtu lazima apitie ili kurudi kwenye asili yake na kuwa mkamilifu.
Ukombozi ni hatua ya mtu kukamilishwa, kuna aina tatu kuu za ukombozi.
(1)Ukombozi wa nafsi
(2)Ukombozi wa mwili
(3)Ukombozi wa roho
UKOMBOZI WA NAFSI
Nafsi ni kiunganishi kati ya mwili na roho, hivyo kwenye nafsi ndipo palipo na asili yetu
( mwanzo 2:7)
Uwezo na asili ya mtu imebebwa kwenye nafsi, hii ndio maana falme zikitaka kukufanya usiwe chochote chini ya jua wanak**ata nafsi yako
HIVYO NAFSI NDIO INAYOKOMBOLEWA NA SIO ROHO WALA MWILI
(Isaya 42:22 )
Kwenye nafsi ndio mtu anafungwa minyororo, Kamba, nira na katika mwili unaona huyu mtu hakuna mahali anakwenda
Kwenye nafsi ndio kuna; fikra, maamuzi, uwezo, akili.
UKOMBOZI WA MWILI
Hapa ndio kuna kuponywa magonjwa, maradhi
Hapa ndipo unaona yote yanayoendelea katika nafsi na roho
Ndio maana yesu alitoa mwili wake kuwa sadaka takatifu kwaajili yetu, hivyo na wewe unapaswa kutoa mwili wako kuwa dhabihu kwa Bwana,
(WARUMI 12: 1-2)
Hivyo namna ulimwengu unavyoenenda ambavyo mwisho wake ni uharibifu,Paulo anatushauri tutoe miili yetu kuwa dhabihu kwa Bwana
(WARUMI 8:13)
Hivyo njia salama ya kuponya mwili wako na uharibifu ni kuufanya kuwa dhabihu,
Paulo kaanisha matendo ya mwili
(WAGALATIA 5:19-21)
UKOMBOZI WA MWILI UNAHUSISHWA NA MAAMUZI YAKO MWENYEWE
UKOMBOZI WA ROHO
Hapa ndipo mtu anazaliwa kwa mara ya pili
Hapa ndipo asili yetu ilipo (YOHANA 3:3-6)
SASA BAADA YA HAYA YOTE KUFANYIKA HAIMAANISHA SASA UPO SALAMA, LIPO JAMBO LA MSINGI SANA LA KUZINGATIA , ILI UFIKE KWENYE UKAMILIFU
(MATHAYO 12: 43-45)