PST KATO_ Prophet

PST KATO_ Prophet we bring the world to Jesus

16/01/2024
07/01/2024
31/12/2023

Heri ya siku ya kumbukizi ya Kuzaliwa Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Tunamshukuru Mungu kwa ajili Yako. Tunathamini uwepo wa Mungu katika maisha yako na uaminifu na haki yako. Katika siku yako maalum ya kumbukizi ya kuzaliwa, hakuna kitu bora zaidi kuliko kumshukuru Mungu kwa rehema zake juu ya maisha yako.

Umeakisi maisha ya watu wengi kwa njia chanya kupitia maneno yako ya hekima. Wema na rehema za Mungu ziendelee kuwa na wewe leo na daima. Tunakuombea upako mpya, nguvu mpya, hekima mpya na maisha marefu kwa jina la Yesu.

Asante Baba kwa kusema ndiyo kwa mwito huu mkuu wa Mungu, sisi kwa mamlaka ya mbinguni tunakupenda na tunathamini mchango wako katika kuujenga mwili wa Kristo. Furaha, Kicheko na Baraka za Mungu zisipungue kwako. Mungu Akubariki uingiapo na utokapo siku zote za maisha yako. Amen

31/12/2023

HERI YA MWAKA MPYA 2024

HAPPY NEW YEAR 2024


31/12/2023
31/12/2023

NAFASI
ILI UREJESHO UTOKEE LAZIMA UZINGATIE MAMBO YAFUATAYO.

1:Lazima utambue majira yako katika uweza wa Mungu na sio katika uweza wa kibinadamu,MDO 1:6; Daniel 9:1-2 mungu alitoa majira ya mwanzo wa utumwa na mwisho wa utumwa, kwa kukisoma kitabu cha Mungu lazima utatambua majira na nyakati. Daniel kupitia kusoma vitabu aliweza kutambua majira mbalimali, hivyo alikuwa na chachu ya kutafuta maarifa ya Mungu, ni muhimu sana kufahamu majira maana usipofahamu huwezi kuamishwa katika nafasi, Usipotambua majira ya uamisho wako utaendelea kuwa palepale.
Na sio kila majira utafunuliwa na mungu, majira mengine yatafunuliwa na Mungu kupitia watumishi wake, hivyo ni muhimu kukusanyika katika ibada na kuwapenda watumishi Mungu alikupa.

2: Maombi
Mtu akijua majira yake lazima aongeze bidii katika kuomba Daniel9:3-4, israel walikaa misiri miaka 430 kwa sababu walitambua mjira na nyakati ya Mungu kuwatoa katika nchi ya utumwa na mda ulipofika walimuomba Mungu naye mungu akasikia kilio chao.

3:ukishaomba lazima matamko ya kinabii yatokee kwa huyo aliyepewa mamlaka au majira( omba na toa unabii). isaya38:5; kuna wanaongezewa muda wa kuishi,UKIRI :hamna atakaye kufa kabla ya wakati wake kutimia, AMEN. ...
SNP: VICTOR MALAMLA

31/12/2023

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255627805291

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PST KATO_ Prophet posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to PST KATO_ Prophet:

Share

Category