03/11/2017
*JIFUNZE KUONGEZA KIWANGO CHAKO CHA IMANI NA NGUVU ZA KIROHO KWA KUSOMA NENO LA MUNGU NA *
Waebrania:11.6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Waebrania:11.11
Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
Waebrania:11.12
Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa k**a mfu, watu wengi k**a nyota za mbinguni wingi wao, na k**a mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
Bwana Yesu asifiwe.
Ukisoma Waebrania 11:1-2 tunapata tafsiri ya maana ya imani.
Neno linasema hivi
" Waebrania:11.1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Waebrania:11.2
Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa."
Kulingana na tafsiri ya imani tuseme ivi
*"Ongeza kiwango chako cha nguvu au uwezo wako wa kiroho kwa kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia na kuwa na uhakika wa bayana ya mambo yasiyoonekana bado kwako kwa neno la Mungu*.
Ukisoma ile Warumi 10:17 inasema ivi
" Warumi:10.17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."
Kulingana na tafsiri ya maana ya imani na chanzo cha imani tunapata jambo hili hapa
Ukitaka kuongeza kiwango chako cha nguvu au uwezo kiroho hakikisha unakuwa na uhakika wa mambo ambayo unayoyatarajia na bayana ya mambo yasiyoonekana kwa kuwa makini kwenye kulisikia neno ambalo Mungu amekupa kwenye maisha yako k**a mbegu ya mambo ambayo umetumainishwa kwa neno la Mungu kuwa utayapata.
Kwa hiyo kusikia kwako neno la Mungu ni mtaji mkuu wa kupata nguvu za kiroho kwa imani ndani ya hayo maneno.
Kwa hiyo kumbe ukitaka upokee uwezo au nguvu zaidi kaa macho na kiwango chako cha imani ulichokijenga moyoni mwako baada ya kusikiliza neno la Mungu wako.
Hapo ndipo penye siri ya utendaji kazi wa nguvu za Mungu ndani ya mtu.
Unasikia nini toka kwa Mungu na unaamini kwa kiwango kipi mpaka ile nguvu au uwezo wa Mungu unajifunua kwako kwa wazi.
Waebrania 11:6 inatueleza kuwa *pasipo imani* haiwezekani kumpendeza Mungu na biblia inatueleza kuwa Mungu uwa afanyi jambo tu ivi ivi bali ufanya yote kwa *shauri la mapenzi yake* na ukisoma hapa chini
Waamuzi:18.5
Nao wakamwambia, Tafadhali tutakie shauri la Mungu, ili tupate kujua kwamba njia yetu tuiendeayo itafanikiwa.
Utaona kuwa *shauri la Mungu* ukiwa nalo moyoni mwako litakupa kujua juu ya mambo yaliyokusudiwa katika njia ya maisha yako, litakupa kuona vitu au mambo ambayo wengine hawaoni ,utasema na kutenda mambo au vitu ambavyo wengine hawawezi kutenda kwa nguvu au uwezo wa kiimani toka ndani ya shauri la Mungu Ooh haleluya na ndio maana mtume Paulo alikuwa hodari na kutenda makuu ya kumpendeza Mungu kwa sababu ya kulisikia shauri la Mungu na kulielewa na kuliamini na kulifuata kwa bidii zote k**a Wagalatia 1:10-24 , mtume Paulo alipewa uwezo , nguvu na mamlaka ya kuwa Mtume wa kimataifa kwa *kulisikia shauri la Mungu tu pekee*
Hakufanya shauri na Petro au Yakobo bali yeye binafsi aliposikia aliamini na kuamua kuliishi shauri la Mungu na akafanikiwa sana kwa mambo ya kiroho.
Waebrania 11:2 inatueleza kuwa imani ni nguvu au uwezo ambao ukikaa ndani ya mtu umshuhudia moyoni mwake juu ya mambo ya maisha yake ambayo kwa jinsi ya kawaida uwezi kutarajia na kuona k**a yanawezekana lakini nguvu au uwezo huu wa kiimani ukikaa ndani ya mtu ufunua uwezekano wa kufanya jambo juu ya hali zake zote ziwe ngumu au la kwa uwezo au nguvu za Mungu.
Sara alipokuwa mwili wake umekufa juu ya mambo ya uzazi imani ilimpa kupokea uwezo wa kuwa na mimba na ingawa mazingira ya mwili yalisema haiwezekani mwili umeshakufa lakini alimhesabu Mungu alichokishauri kwao na mume wake kuwa kimesemwa na Mwaminifu wa kweli hakika kitakuwa tu na akapata mtoto.
Na kwa imani hiyo wakazaliwa watu wengi mno k**a mchanga ingawa alikuwa k**a mfu wakati analisikia shauri la Mungu wake.
Pengine umelisikia shauri la Mungu juu yako napenda kukutia moyo kuwa liamini tu hata k**a mazingira yanakataa we amini tu na itakuwa sawa sawa na neno la Bwana Mungu.
Amen