Walk in the Holy Spirit Ministry.

Walk in the Holy Spirit Ministry. Ukurasa huu ni kwa ajili ya kujifunza kuishi ,kutembea na Roho Mtakatifu ili kuweza kushinda dhambi n

15/08/2020
27/07/2020

TO BE AN OVERCOMER BY THE POWER OF GOD.

Did you know that no matter how you feel right now, someone wants to be where you are, someone wants to have what you have and someone want to be like you? you were created to be a vessel for God to use but God can not use a discouraged servant.

Worry interferes with God's Spirit in our lives. Despite the temptation to feel discouraged, we must overcome this as Christians. By saying about ourselves what Bible says about us, we are made overcomers. What does the Bible say about you?

*Are you sick? The Bible says in Isaiah 53:5 that by His wounds you are healed.
*Are you weak? The Bible says in Psalm 27:1 that your God is the strength of your life.
*Are you experiencing failure? The Bible says in Romans 8:37 that you are more than a conqueror through Jesus Christ.
*Are you trapped? The Bible says in John 8:36 that the son has set you free.
*Are you facing lack? The bible says in Philipians 4:19 that your God shall supply all your needs.

Words of confession of God's Word indeed work wonders! When the Word of God prevails in your life, people will see it in your dominion, in the way you talk, in the way you walk . Are you ready to win today? Say to yourself, "I AM AN OVERCOMER!" .

KUSHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA KWA NGUVU ZA MUNGU ALIYE HAI.

Mpendwa katika Bwana wetu Yesu Kristo unajua haijalishi upo katika hali gani au unapitia wakati mgumu kiasi gani hivi sasa , kuna mtu anataka kuwa hapo ulipo, kuna mtu anatamani kuwa nacho ulichonacho na kuna mtu anatamani kuwa k**a wewe? Mungu alikuumba k**a chombo chake akitumie hapa duniani lakini Mungu huwa hamtumii mtu aliyekata tamaa au mtu ambaye haoni thamani yake.

Roho Mtakatifu hakai kwa mtu mwenye hofu ya mambo yanayokuja mbele yake, anakaa ndani ya watu majasiri. Ndiyo majaribu yapo duniani kwa macho ya damu na nyama yanakatisha tamaa, lakini k**a Wakristo tunashinda na zaidi ya kushinda kwa Imani katika yeye aliyetupenda. Tunajitamkia maneno sisi wenyewe kile ambacho Biblia imesema kuhusu sisi, Mungu alituumba kuwa washindi, Je Biblia inasema nini kuhusu wewe?

*Je ni mgonjwa? Biblia inasema ISAYA 53:5 na kwa kupigwa kwake sisi tumepona .
*Je ni mdhaifu? Biblia inasema ZABURI 27:1 Bwana ni ngome ya uzima wangu.
*Je unafeli katika kila unalolifanya? Biblia inasema WARUMI 8:37 Lakini katika mambo yote tunashinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda(Yesu Kristo).
*Je ni mtumwa wa dhambi au vifungo vya nguvu za giza? Biblia inasema YOHANA 8:36 Basi mwana(Yesu Kristo) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
*Je una uhitaji au kupungukiwa? WAFILIPI 4:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake..

Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, na ni Roho tena ni uzima. Neno la Mungu litakapokuletea ushindi katika maisha yako watu wataona katika jamii yako, jinsi unavyoongea, jinsi unavyotembea. Je uko tayari kuwa mshindi leo? Isemeshe nafsi yako "mimi ni mshindi!".
Written by Eng B. NYAMEGA

25/07/2020

MUNGU HADHIHAKIWI.
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi,kwa kuwa chochote apandacho mtu,ndicho atakachovuna.Maana yeye apandaye kwa mwili wake,katika mwili wake atavuna uharibifu, Bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele." Imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila Neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu, either unajua Neno la Mungu au haujui lakini Neno la Mungu halibadiliki linafanya kazi au kutimiza kusudi alilolikusudia hapa duniani ,ndugu zangu tuangalie na tujichunguze maisha yetu kwa Neno la Mungu Je tunapanda wapi katika mwili au katika Roho? Apandaye katika mwili awe na uhakika wa kuvuna uhatibifu maana mwili ni mbegu iharibikayo ,mwili ulitwaliwa katika mavumbi na katika mavumbi utarudi,Lakini Roho ni mbegu isiyoharibika sawasawa na Mhubiri 21:7" Nayo mavumbi kuirudia nchi k**a yalivyokuwa,nayo Roho kumrudia Mungu aliyeitoa" sasa tujiulize mwili tutauacha hapa duniani lakini Roho itarudi kwa aliyeitoa Je umejiandaaje au unajiaandaa vipi kurudi kwa aliyekuumba? Chagua pando lako tunapanda wapi kwenye mwili wenye kuharibika au kwenye Roho ili kupata uzima wa milele ule ulio ndani ya Yesu Kristo. Mpokee Yesu Kristo ujazwe Roho Mtakatifu ili uweze kuenenda katika Roho.

18/07/2020

Nakusalimu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth kila mwenye Roho, nafsi na mwili.
SOMO: KUTEMBEA NA ROHO MTAKATIFU

Unaweza kujiuliza nataka kutembea na Roho Mtakatifu ,nitafanyeje ili niweze kutembea na Roho Mtakatifu, hii ni misingi michache ya kutembea na Roho Mtakatifu.

(I) Ukweli na uhalisia kuhusu Roho Mtakatifu.
(ii) Kuelekeza na kuwekeza akili kwenye mambo ya Rohoni na si ya mwilini.
(iii)Kuusulubisha mwili.

Utofauti wa agano la kale na agano jipya ni kwamba kwenye agano la kale hawakupewa karama au zawadi ya Roho Mtakatifu ambayo inamsaidia mwamini kushinda dhambi.Roho Mtakatifu ni ahadi na zawadi ya Bwana Yesu Kristo mwenyewe kwamba imempasa yeye aende kwa Baba ili aje msaidizi hapa duniani.

(i) Ukweli na uhalisia kuhusu Roho Mtakatifu.
-Roho Mtakatifu ndiye anatufanya kuwa familia moja na Mungu, tunakuwa watoto wa Mungu Warumi 8:14 "kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu" na ukisoma Wagalatia 4:4-7" Hata ulipowadia utimilifu wa wakati Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke ,amezaliwa chini ya sheria kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu aliaye aba yabi Baba" Katika andiko hili amtumwa Yesu Kristo na baada ya Yesu kuondoka akatumwa Roho Mtakatifu duniani ili amdhihirishe Yesu Kristo duniani.
-Kazi ya Roho Mtakatifu ni msaidizi ambaye anatembea na mwamini muda wote na anatuweka katika uhusiano wa moja kwa moja na Yesu kwa sababu ni Roho wa Mungu mwana na anatupa uhusiano na Mungu Baba kwa sababu ni Roho wa Mungu.
-Roho Mtakatifu anatufanya kuwa sehemu ya mwili wa Kristo kwa sababu ni Roho wa Roho wa mwana wa Mungu(Yesu).1Wakorintho 6:17" Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni Roho moja naye"

-Roho Mtakatifu anatupa nguvu ya kushinda dhambi.Hatuko chini ya sheria ila tuko chini ya neema Wagalatia 5:16" Basi nasema enendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kwamwe tamaa za mwili" ili uweze kushinda maisha ya dhambi unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu akuongoze katika mambo yote.
Wakristo wengi wa sasa tunaishi katika kiwango ambacho Mtume Paulo alisema katika kitabu cha Warumi 7:19 "Kwa maana lile jema nilipendalo,silitendi,Bali like baya nisilolipenda ndilo nilitendalo"
Mtume Paulo alikuwa anaelezea maisha bila Roho Mtakatifu yanavyokuwa yani Roho inashindana na mwili ata usijue ufanye nini lakini Roho Mtakatifu akiongoza hatuki chini ya sheria na unakuwa huru mbali na dhambi" 2Wakorintho3:17" Basi Bwana ndiye Roho walakini alipo Roho wa Bwana hapo ndipo penye Uhuru".

(ii) Kuelekeza na kuwekeza akili kwenye mambo ya Rohoni na sio ya mwilini.
-Kwanza inatakiwa mwamini ajazwe Roho Mtakatifu.Kusifu na kuabudu ni muhimu kuwa kuwa katika uwepo wa Roho Mtakatifu.
-Kuomba msaada na kushirikiana na watu waliokuwa kiroho kuliko wewe.Anza Siku
na maombi

(iii) Kuusulubisha mwili. Wagalatia 5:24" Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake" mwili wa mwamini umesulubiwa lakini bado haujafa.
Roho nia yake ni uzima na dhambi zote ni za mwili bila mwili mwanadamu hawezi kufanya dhambi kwa sababu ili afanye dhambi hap duniani anahitaji kitambulisho cha kuonekana kwa macho ya damu na nyama ambacho ndiyo mwili ,Wagalatia 5:19" Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati,uchafu,ufisadi,ibada ya sanamu,uchawi,uadui,ugomvi,wivu,hasira,fitina,husuda,uzushi,faraka,ulevi,ulafi na mambo yanayofananana hayo" andiko jingine linatupa athari za kuongozwa na Mwili ni Warumi 8:13" Kwa maana k**a tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili mwataka kufa Bali k**a mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho mtaishi".

Ashukuriwe Mungu atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Eng B.G Nyamega,
+255653664479,
Dar es salaam.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Walk in the Holy Spirit Ministry. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share