Injili Na Utakatifu

Injili Na Utakatifu Ukitaka kwenda Mbinguni, ni lazima umwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, Uokoke.

16/06/2025

KRISTO AYATAWALE MAISHA YETU.

20/05/2025

Bwana ni mwingi wa rehema

26/11/2024

Kumwamini Yesu ndiyo suluhisho la maisha yetu

17/06/2024

Yesu anatupenda sana Wanadamu. Alikufa kwa ajili ya kutuokoa toka kwa shetani.

IJUE SIRI YA KULA MEMA YA NCHI.Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu, ni siku nyingine tena Mungu ametupatia kibali na neema y...
15/04/2024

IJUE SIRI YA KULA MEMA YA NCHI.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu, ni siku nyingine tena Mungu ametupatia kibali na neema ya kukutana pamoja tukizidi kujifunza habari za uzima.

Somo letu la leo linaenda kukupa mwanga na kukusogeza hatua nyingine kwenye safari yako ya Ukristo.

Ni hitaji la kila mwandamu aliyepo Duniani kuyapata na kuyafurahia Mema ya nchi yaani hakuna anayependezewa au kuhitaji apate mabaya ya nchi. Juhudi na Bidii ya kila mwanadamu ni kuyapata mema ya nchi lakini bahati mbaya ni kwamba wengi wanayahitaji mema ya nchi ila hawajui siri na msingi wa kwanza wa kupata mema ya nchi hivyo leo unaenda kujifunza msingi wa kwanza wa kuyapata Mema ya nchi.

MEMA YA NCHI NI NINI?

Haya ni mambo mazuri ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya mwanadamu ayapate pindi tu anapozaliwa na kipindi chake chote cha maisha juu ya Uso wa nchi. Mambo haya mengi ni mahitaji ya msingi na mambo ya muhimu kwa mwanadamu.

Mfano wa Mema ya nchi ni Afya njema, kuishi miaka mingi, hali nzuri ya maisha, mafanikio ya kimwili yaani utajiri na Mali, Ndoa, familia Bora, furaha, amani na mengine Mengi.

YANAPATIKANA VIPI?

Kila mmoja amekuwa na namna yake na msingi wake wa kuyatafuta Mema ya nchi wapo ambao wameamini kuwa bidii ndio msingi wa kuyapata mema ya nchi lakini hawajafanikiwa kuyapata na hata walipolipata moja halikudumu.

Wapo wengine wanahama makanisa kila siku wakitafuta muujiza na siri ya kuyapata mema ya nchi. Kila upepo unaopita umewachukua lakini bado hawajayapata.

Wengine wapo kwenye Maombi miaka Nenda Rudi lakini bado hawajafanikiwa kuyapata waneshangaa pale wanapoona wengine wakiyapata.

Wengine wapo kwa waganga huko, walilipata moja nalo likazaa uchungu na kugeuka kuwa ubaya.

Wengine wapo kwa mitume, wachungaji na manabii wakitafuta upako wakiamini ni michezo ya watu au laana zinawafuata au wamerogwa lakini bado wamejilisha upepo na hakuna matokeo kwao.

NENO LA MUNGU LINASEMA.

Msingi wa kuyapata mema ya nchi upo mmoja pekee na ndio mema yote yanazaliwa hapo hakuna mema ya nchi nje ya msingi huo ambao nabii Isaya ameutaja hapa.

Isaya 1:19-20
[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
[20]bali k**a mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.

anasema
MKIKUBALI KUTII MTAKULA MEMA YA NCHI.

Kumbe UTIIFU ndio msingi wa kwanza wa kula mema ya nchi na huo utiifu ni kumtii MUNGU kwa kulishika na kulitenda NENO LAKE, hii ndio tiketi ya kwanza ya kula mema ya nchi.

Hakuna mema ya nchi yanayopatikana pasipo kumtii na kuyatenda mapenzi ya Mungu kwano hata yakipatikana huleta uharibifu na kuzaa uchungu.

Msingi wa kwanza wa mafanikio yako mwanadamu ni kumtii Mungu na baada ya hapo unaweza kuyapata Mema yote ya nchi uliyoandaliwa na Mungu.

Msingi wa kuwa na ndoa Bora, familia bora, maisha bora, furaha, amani, utajiri na mengine unaanzia kwenye kulishika na kulitenda Neno la Mungu kwanza.

Pasipo kumtii Mungu utafanya bidii na mwisho utafika ukiwa umefanya kazi ya kuchosha usiku kucha pasipo matokeo.

TUNAPATAJE KUMTII MUNGU?

Njia pekee ya kumtii na Kulishika Neno la Mungu ni kwa kumwamini Yesu Kristo k**a Bwana na mwokozi wa maisha yako yaani kumpokea Kristo. Mema ya nchi yamefichwa kwenye kuamini mauti na kufufuka kwake Yesu Kristo.

Ukimuamini Yesu Kristo atakupa nguvu ya kumtii Mungu kwa kulishika na kulitenda Neno lake na kuyapata mema yaliyoandaliwa kwa ajili yako.

Mema ya nchi yanapatikana kwa kumwamini Yesu Kristo ambaye ndani yake imo ahadi ya kuyapokea Mema yote ambayo umeandaliwa kuyapata hapa duniani kwani kwa kila aliyeviacha vyote na kumfuata Yesu ameahidiwa kuvipata.

YESU ANASEMA.

Mathayo 19:27-29
[27]Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
[28]Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
[29]Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa k**e, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.

Hakuna ambaye ataviacha vyote kwa ajili ya Yesu Kristo halafu akayapata mabaya ya nchi kwani ndani yake umo ulinzi na tiba za urogaji wote, anaondoa laana na mikosi yote kwa jina lake na huo ndio upako uliopo ndani yake Kristo.

Ndugu Yangu Mkristo kabla hujaanza kufanya bidii kuyatafuta mema ya nchi anza kwanza kutafuta kumtii Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo kwa kuukubali wokovu na kumpatia maisha yako ayaendeshe.

Tengeneza mambo yako kwanza ndipo uyapate mema ya nchi. Unajua wapi ulipoanguka au nini kinachokuzuia usimuone Yesu anza kwanza kukiondoa na Yesu atakuandalia Fungu lako.

Usishindie maombi na kujiliza mbele za Mungu ukitaka mafanikio wakati unatambua moyoni mwako wapi umekosea na hujatengeneza bado, usikimbilie kumtwisha mzigo mchungaji wako kumuona hana upako kumbe wewe mwenyewe umebeba hatia na madhambi yanayokuzuia usisonge mbele, acha kubadili makanisa ukiamini utayapata mema anza kwanza kuubadili moyo wako ili hayo Mema yatakujia.

Sheria ni moja tu Anza kumtii Mungu kwanza ndipo upate mema yako na hakuna mema nje ya kumtii Mungu haijalishi umesoma sana, mzuri sana, una bidii sana, unajiweza kifedha au uwepo wa msaada mkubwa kwako.

Pasipo kumtii Mungu hata uoge kwenye p**a la mafuta ya upako utabaki kapuku vile vile mpendwa wewe, utazunguka makanisa yote na shida zitakuwa nawe.

HAKUNA MEMA PASIPO KUMJUA MUNGU.

Ayubu 22:21
[21]Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.

HAKUNA MAFANIKIO PASIPO MUNGU.

Zaburi 127:1
[1]BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.

Usikeshe baharini usiku mzima k**a petro kwa bidii na ujuzi wako ila nenda kwa jina la Yesu pekee utafanikiwa na kupata zaidi.

Unaitaka familia bora, ndoa bora, mke bora, mume bora, maisha bora, afya njema, maisha marefu, mali na mafanikio kubali kumtii Yesu Kristo akupe yaliyo mema kwa ajili yako.

Pasipo kumtii Mungu tambua kuwa ulivyopaswa kuvitawala vitakutawala wewe na kukuendesha.

YESU ANAPIGA HODI KWAKO MFUNGULIE MLANGO KWANI ANASEMA.

Mathayo 11:28-30
[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

MWAMINI YESU KRISTO AKUTUE CHINI DHAMBI ZAKO ULE MEMA YA NCHI.

NIKUTAKIE WAKATI MWEMA.

Mwandishi ni: Msemaji Wa Injili
Mwenye whatsapp

WhatsApp Group Invite

USIISHI NA  UDHAIFU.BWANA YESU ASIFIWE MPENDWA KATIKA BWANA.Ni siku nyingine tena Mungu ametupatia neema na kibali cha k...
12/04/2024

USIISHI NA UDHAIFU.

BWANA YESU ASIFIWE MPENDWA KATIKA BWANA.

Ni siku nyingine tena Mungu ametupatia neema na kibali cha kuifikia, hivyo kwa neema ya Yesu Kristo nimepata kibali cha kuandaa somo la kukuvusha siku hii ya leo.

NAJUA
Umewahi kusikia au kuwa msemaji wa kauli hii " HUU NDIO UDHAIFU WANGU KWAKWELI" watu wengi hutumia maneno haya pasipo kuelewa maana yake, hivyo leo hii tutaenda pamoja tuone madhara na matokeo ya kitu kinachoitwa udhaifu.

Udhaifu ni msamiati wenye maana mbaya ila kibinadamu hutumika kwenye kitu au jambo ambalo mwanadamu analipenda sana na kulitenda mno yaani udhaifu unatumika kuficha neno Upendo usiosahihi.

NINI MAANA YA UDHAIFU?

NI ukosefu wa nguvu, uimara, nguvu, au kadhalika; unyonge pia inaweza kueleweka k**a ubora duni au kasoro, k**a katika tabia ya mtu, kidogo kosa au kasoro.

Hivyo udhaifu ni kasoro au ukosefu wa nguvu. Na kwa Mkristo udhaifu unaweza kuwa ni jambo ambalo unalichukia na hupendi kulifanya wakati lina usahihi ndani yake au lile ambalo unalifanya na kulishikilia lakini unalifahamu kuwa sio sahihi na ni kosa kulifanya.

Udhaifu unasimama k**a kosa yaani kutofanya jambo unalopaswa kufanya na ambalo ni sahihi kulifanya au kufanya jambo usilopaswa kulifanya kwani sio sahihi kulifanya.

UDHAIFU WA MKRISTO UNAWEZA KUWA NI:

Dhambi ambayo ameishikilia na kuiona ni vigumu mno kuiacha mfano ulevi wa pombe ambao umekuwa jambo la kawaida ndani yake, zinaa yaani uzinzi na usherati, matusi na maneno mabaya, tamaa, na mambo mengine madogo madogo.

Hasira, visasi na kushindwa kusamehe yaani umekuwa mtu unayebeba watu moyoni mwako na umejaa uchungu.

Uvivu au kupuuza misingi ya wokovu mfano kutofika ibadani kwa wakati, kusoma Neno la Mungu na kupuuzia maombi yaani utashangaa wakati wa kusoma au wakati wa maombi ndio usingizi unaingia na kukudhoofisha usiombe tena.

Kupenda kupitiliza yaani kuweka tumaini kwa mwanadamu na kumsahahu Mungu. Udhaifu wako anaweza kuwa mume wako, mke wako , watoto wako, wazazi wako au mtu wako yeyote wa karibu.

MADHARA YA UDHAIFU.

Kitu kinachoitwa udhaifu ni sawa na ufa kwenye ukuta uliojengwa yaani mbomoaji huanzia kwenye ufa ambapo anatambua kuwa ni mahali dhaifu ambapo anaweza kuuangusha ukuta na nyumba nzima.

Hivyo udhaifu ndio mwanzo wa anguko la mwanadamu yaani mbomoaji ambaye ndiye Shetani hawezi kupambana kukuangusha kwa kutumia nguvu zako ila anatumia udhaifu wako k**a ndio eneo la kukuangusha.

Yaani shetani anautumia udhaifu wako unaoushikilia kukuvuta dhambini yaani anatafuta kosa kwako au kasoro yako moja unayoifanya ili akuangushe kwenye himaya yake.

JIFUNZE KWENYE ANGUKO LA ADAMU PALE EDENI

Mungu alimuumba Adamu na kumpatia Jukumu la kuitunza bustani ya Adamu na kumpatia utaratibu wa kuisimamia bustani pamoja na matunda ambayo anayoweza kuyatumia.

Mwanzo 2:16-17
[16]BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Adamu alilisikiliza na kulitenda jambo hili kwa usahihi na akafanyiwa msaidizi wa kumsaidia kwenye utunzaji wa Bustani lakini shetani anakuja kutafuta namna ya kumuangusha Mwanadamu pale bustanini naye hakumtafuta Adamu ambaye anatambua anafahamu anazo nguvu za kumpinga ila anaenda kutumia udhaifu wake ambao ni mke wake ambaye anampenda na anamsikiliza sana.

Mwanzo 3:4-6
[4]Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
[5]kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa k**a Mungu, mkijua mema na mabaya.
[6]Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
[7]Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

Udhaifu wa Eva ulitosha kumwangusha Adamu ambaye alikuwa mwenye nguvu yaani kosa la Adamu la kushindwa kusimama kwenye nafasi yake k**a Mume na mlishaji wa nyumba liliweza kumuangusha na kumkosea Mungu kwani makosa mawili au madhaifu mawili ya Adamu ni haya

1. Adamu hakusimama kwenye nafasi yake.
Adamu ndiye aliyepaswa kumlisha matunda eva kwani yeye ndiye aliyepokea amri na maelekezo ya kuitunza bustani lakini matokeo yake akamuachia kazi hiyo mkewe.

2. Adamu hakuambatana na mkewe.
Adamu alipewa msaidizi wa kuambatana naye lakini matokeo yake alimuacha peke yake na mwisho akaambatana na shetani. Adamu angeambatana na mkewe shetani asingepata nafasi ya kuongea na eva.

NINI MAANA YAKE?

Ndugu Yangu Mkristo udhaifu wako unaoushikilia na kuona ni jambo unalolipenda tambua kuwa shetani anakuja kuutumia huo huo kukuteka na kukuangusha kwenye wokovu na kukurudisha nyuma.

Huo udhaifu wako wa uvivu wa kusoma na Kutafakari Neno la Mungu shetani atautumia kukuletea tafsiri za uongo ambazo anatambua atakupoteza kwenye wokovu.

Udhaifu wako wa kutopenda maombi au kuomba wewe mwenyewe binafsi shetani anaweza kuutumia mlango huo kukuua kabisa kiroho na hutoinuka tena.

Udhaifu wako wa kutosamehe na kubeba hasira shetani anaweza kukuangushia hapo kwa kukuzalishia chuki ambayo itaua nguvu yako yote ya rohoni.

Udhaifu wako wa dhambi ndogo ndogo za sirini unaweza kutumika kukuangusha na kukutoa kwenye wokovu. Hayo mambo unayoyafanya pasipo watu kukuona yanaweza kuzaa mengine makubwa na baadaye utaanza kuyafanya yanayoonekana hadharani.

Usiendelee kuufurahia udhaifu na kuona ni jambo jema kwako ila chukua hatua ya kuuondoa kabisa moyoni kwako ili shetani asipate nafasi ya kukupiga eneo lako dhaifu.

Kila unaloliona linakukosesha nafasi ya kuisikia sauti ya Mungu liondoe kabla halijakua na na kukuondolea usikivu wa milele. USIPOSIMAMA KWENYE NAFASI YAKO shetani ATASIMAMA YEYE NA KUIFANYA KAZI YAKE MBAYA.

USIPOZIBA UFA LEO HII TAMBUA IPO GHARAMA KUBWA YA KUJENGA UKUTA HAPO KESHO KWA KOSA MOJA LA KUUANGALIA UFA UKIKUA.

NINI UFANYE?
Je unasumbuliwa na udhaifu unaokuzuia usiendelee mbele? Au una jambo ambalo umejaribu kuliacha na kulichukia ila bado moyo unalipenda na umejikuta unalirudia yaani umefanya bidii kubwa ya kimwili lakini hujafanikiwa? Leo hii naomba nikusaidie njia moja ya kulishinda.

Njia pekee ya kulishinda ni KULITUA MSALABANI kwani msalaba ndio sehemu pekee ya kuitua mizigo yako yote uliyoibeba na kusumbuka nayo. Huna sababu ya kuteseka tena na kuendelea kuwa mtumwa wa dhambi tambua kuwa KUFUFUKA KWA YESU ni ushindi wako dhidi ya madhaifu yako yote.

Hata mimi nimeteseka na udhaifu kwa muda mrefu ila Damu ya Yesu iliyomwagika msalabani imenipa nguvu ya kuishinda zinaa , matusi, ibada za miungu na sanamu, msukumo rika na hatimaye ninayo nguvu nyingine mpya ndani ya Yesu Kristo.

USIONE HAYA KWA BWANA , NENDA MSALABANI YESU AKUTUE MZIGO WAKO UNAOTAKA KUKUANGAMIZA kwani maandiko yanasema.

1 Petro 5:6-7
[6]Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
[7]huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

MTWIKE UDHAIFU WAKO NAYE ATAKUTUA NA KUKUPATIA NGUVU MPYA.

USIKUBALI KUTESEKA NA KUANGAMIA.

Nikutakie wakati mwema mpendwa.

Karibu facebook Msemaji Wa Injili

Karibu watsapp.

WhatsApp Group Invite

28/03/2024

Mwambie Mungu ahsante kwa kukupa uzima mpaka leo. Kuna wengine wamekufa na wengine ni wagonjwa lakini wewe ni mzima. Mshukuru Mungu

27/03/2024

Hakuna aliye k**a Bwana YESU

16/03/2024

Ainuliwe Bwana wa Mabwana, ainuliwe ametenda mema.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Injili Na Utakatifu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Injili Na Utakatifu:

Share