29/10/2022
GOD'S LOVE SERIES
LIFAHAMU PENDO LA MUNGU.
PART 10.
10. PENDO LAKE HALINA UPENDELEO | ANAWEZA KUMTUMIA YEYOTE.
Matendo ya Mitume 10:34-35 "Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye."
Katika sehemu ya 9 iliyopita nilizungumzia zaidi upande wa namna Mungu anavyookoa, anavyohudumia, anavyowatendea wema wote kwa usawa bila kuwapendelea. Tukapata kuona kuwa kuwa Mungu amekusudia mazuri kwa watu wote na hakuna ambaye anapatwa na mabaya ambayo ni Mungu ameyapanga yatokee kwake.
Leo nataka tuangalie upande mwingine wa pendo la Mungu kutokea kwenye andiko letu la msingi hapo juu. Hasa kwenye msati wa 35 anaposema "Bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye".
Kuna mtu anaweza akausoma msari huu akaishia kujua kwamba huenda Mungu alimaanisha haki itokanayo na matendo ya sheria, na kwa hiyo ataishia kujiona hafai kutumiwa na Mungu kwa sababu hana matendo mazuri, kila akijiangalia anaona hajakamilika kutumiwa na Mungu, hafai na hana vigezo vya kutumiwa na Mungu.
Kila akifikiria kwa habari ya mtu ambaye Mungu anaweza kumtumia kwa kiwango kikubwa kwenye taifa na dunia kwa ujumla yeye hajioni, anafikiri huenda ni watu wa aina fulani wenye sifa na vigezo vya kutosha ndio Mungu anawatumia kufanya mambo makubwa. Haya ni mawazo mabaya kwa sababu kuhesabiwa kwetu kuwa wenye haki wa Mungu hakutokani na yale matendo mazuri tuliyonayo bali kunatoka na ile imani yetu kwa Yesu Kristo ambaye ametukamilisha.
Ulipomwamini Yesu Kristo siku hiyo hiyo ulipokea haki ya Mungu na kwa hiyo unepata kila kigezo cha Mungu kukutumia kufanya mambo makubwa kwenye ufalme wake. Acha kujiona kana kwamba huna vigezo, kigezo chetu kikubwa ni IMANI. Je unaamini?
Maandiko yanasema kwenye kitabu cha 2 Wakorintho 3:5, "Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu."
Paulo anasema sisi wewenye hatuwezi kufikiri neno lolote kwamba Mungu angeweza kuwatumia watu k**a sisi, wenye mapungufu kibao lakini ndio hao ambao Mungu amewatumia. Utoshelevu wetu, ukamilifu wetu haupo katika yale tuliyonayo au tunayoweza kufanya bali upo katika Kristo.
Kwenye 2 Wakorintho 3:6, akaendelea zaidi kusema "Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha."
Yesu Kristo amefanyika utoshelevu wetu (ametupa sifa na vigezo vyote vinavyohitajika). Ni makosa kwa mwamini kuona kwamba hastahili kutumiwa na Mungu, labda k**a huyu hajajua kikamilifu kile ambacho amekifanya Yesu msalabani. Yesu amekukamilisha, amekutosheleza na wala hujapungua kigezo chochote cha kutumiwa na Mungu.
Pale unapokuwa dhaifu ndipo nguvu zake zinakuwa halisi kwako. Usiangalie mapungufu yako ili Mungu akutumie, usiangalie ni nini ambacho huwezi kufanya uakaanza kujishusha na kujidharau. Neema ya Mungu inakutosha, neema ya Mungu ndio kibali chako, ndio leseni yako ya kufanya mambo makubwa duniani.
Kuna wakati Paulo alijiona hafai kwa sababu ya udhaifu wake, lakini Mungu akamwambia usiangalie udhaifu wako kwa sababu mimi nikitaka kumtumia Mtu naangalia neema yangu.
2 Wakorintho 12:9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Neema ya Mungu inayo uwezo wa kufunika udhaifu wako na ukatumiwa na Mungu kwa namna ambayo duniani itashangaa.
Wewe k**a wewe hujakamilika, ila ukiwa ndani ya Kristo kwa Imani unakuwa na ukamilifu wote.
Acha kujiona kwamba Mungu hawezi kukutumia wewe, huenda anao watu maalum aliowaandaa kiwatumia. K**a basi k**a wapo na wewe ni mmoja wapo kwa sababu umekuja duniani.
Ukitafuta kigezo chako binafsi kwanini Mungu akutumie huwezi kuwa nayo, ila ukitafuta kigezo cha Mungu utapata kwa sababu NEEMA YAKE IPO.
Ukisoma biblia utagundua kwamba watu waliotumiwa na Mungu kufanya mambo makubwa ni wale ambao hawakudhaniwa au wao wenyewe hawakudhani kuwa Mungu anaweza kuwatumia. Angalia watu k**a Daudi, aliua mtu akamchukulia mke wake (zinaa), angali Mtu k**a Paulo alikuwa muuaji ambaye amelitesa kanisa kwa muda mrefu (mpinga Kristo) lakini utagundua hao wao wana sehemu kubwa walioyofanya na kutumiwa na Mungu kwa sababu ya neema yake.
Orodha ya watu wa aina hii ni wengi sana, kwa hiyo na wewe ukijiona hufai na wala huna kigezo hiyo ndio sababu moja wapo kubwa kwanini Mungu atakutumia.
MUHIMU:
▪︎ Mungu hana watu maalum, kwenye kila taifa anaweza kumtumia mtu yeyote ambaye atachukua hatua ya kuamini kuwa Mungu anaweza kumtumia.
▪︎ K**a Mungu anao watu aliwachagua kuwatumia basi na wewe ni MIONGONI mwao ndio maana upo duniani.
▪︎ Usiangalie madhaifu yako, angalia neema ya Mungu. Kristo Yesu ndio utoshelevu wako.
▪︎ Wewe ni mwenye haki kwa sababu ulishamwamini Yesu. Haki yako binafsi haiwezi kukuokoa, haiwezi kujuoa kigezo cha kutumia na Mungu. Ikubali haki ya Mungu.
Asante kwa kufuatilia na kujifunza.
Somo litaendelea tena...
Devotion
GOD'S LOVE SERIES | MUNGU ANAMTUMIA YEYOTE.
Ap Pendael Long'ida
29 October 2022.