Gospel Stewards Family - GSF

Gospel Stewards Family - GSF GOSPEL STEWARDS FAMILY

This is Christian born Again family, whose are willing to grow spiritual.

➡️FOLLOWING DIVINE GUIDANCE REQUIRES A HIGH LEVEL OF OBEDIENCE.I hope you’re doing well, my brethren. It is my pleasure ...
05/02/2026

➡️FOLLOWING DIVINE GUIDANCE REQUIRES A HIGH LEVEL OF OBEDIENCE.

I hope you’re doing well, my brethren. It is my pleasure to have you once again. Kindly follow this message to the end.

If you are committed to following divine instructions, you must ensure that your level of obedience is optimal. Just as people follow a doctor’s medical prescription, you also need the same capacity to obey divine guidance. When a person fails to follow a doctor’s prescription, medication can turn into drug abuse, which may even lead to loss of life.
The same discipline is required much more, in fact when it comes to following divine guidance.

Let us read together Exodus 40:36–37:
36. And when the cloud was taken up from over the tabernacle, the children of Israel went onward in all their journeys:
37. But if the cloud were not taken up, then they journeyed not till the day that it was taken up.

➡️This was the divine guidance given to the Israelites during their journey through the desert toward the Promised Land. They followed the sign of the cloud. When the pillar of cloud was taken up, they moved; when it was not taken up, they did not move. Even if it took many days, months, or years, they had to wait until the cloud was lifted.

Do you see the optimum level of obedience they demonstrated?
Their journey depended entirely on God’s guidance through the pillar of cloud. When the cloud did not move, they camped and waited. When it moved, they followed. Remember, all this happened in the wilderness.

Now let me ask you:
Are you ready to wait for God’s instructions?
Can you keep waiting even when there is silence concerning what you are praying and fasting for?

This message is for you, my brethren.
Are you ready to receive God’s guidance? And if yes, how ready are you to obey and wait when there are no visible signs to guide you? Can you continue believing in God according to what you read in the Bible? Or will you turn your face to another direction?

Following God’s instructions requires a very high level of obedience. Trace back the life of Abraham, and you will be enlightened on this truth. Where there is genuine faith in God, obedience will always accompany it.
Thank you so much for your time. I wish you all the best as you continue to follow God’s instructions.

Your loving brother,
Japhet Katana
You can follow me on social media:

Contact Details:
WhatsApp: +255 745 746 691
Ev. Katana Japhet

📌PEOPLE WITH A HAGAR-TYPE ATTITUDEGenesis 16:4 (KJV)“And he went in unto Hagar, and she conceived: and when she saw that...
16/01/2026

📌PEOPLE WITH A HAGAR-TYPE ATTITUDE

Genesis 16:4 (KJV)
“And he went in unto Hagar, and she conceived: and when she saw that she had conceived, her mistress was despised in her eyes.”

This is a very dangerous attitude to have. Hagar was a maidservant in Sarai’s household. She faithfully served her mistress and helped with various household responsibilities.
After many years of barrenness, Sarai persuaded her husband Abraham to take Hagar as a wife so that she might obtain children through her.

However, once Hagar conceived, her attitude changed. She began to despise her mistress. This negative attitude provoked Sarai to mistreat her, and the situation became so unbearable that Hagar decided to run away.
As she fled into the desert without knowing where she was going, the Angel of the Lord met her and instructed her, “Return to your mistress and submit yourself under her authority.”

This teaches us an important lesson. Some people, because of pride or a “Hagar-type attitude,” begin to despise others once they experience progress, promotion, or success. Sadly, they even look down on those who once helped them rise.
Today, brethren, I beseech you to remain humble. God resists the proud, but He lifts up the humble.

The Bible clearly states:
“Pride goeth before destruction, and an haughty spirit before a fall.”
— Proverbs 16:18 (KJV)

Examine your ways today. Do not act rudely or carelessly toward others. Choose humility, for humility brings favor before God and men. Cultivate an attitude of gratitude, because hidden within it is true greatness.

There is also a Chinese proverb that says:
“Be like the bamboo tree; the taller it grows, the lower it bends.”
Thank you for following these insights on the Hagar attitude.

Your friend, Ev. Japhet Katana.
For more biblical reflections and devotions, follow my page Japhet Katana.
Contacts:
WhatsApp: +255 745 746 691
🇹🇿 🇷🇼 🇲🇼 🇨🇩 🇿🇲 🇳🇦 🇲🇿 🇺🇸 🇰🇪 🇺🇬 🇧🇮 🇿🇦

🌍KATIKA KUSHEREKEA NA KUMSHANGILIA MUNGU KWAAJILI YA FAMILIA YA MAWAKILI WA INJILI(GOSPEL STEWARDS FAMILY - GSF) KUTIMIZ...
15/01/2026

🌍KATIKA KUSHEREKEA NA KUMSHANGILIA MUNGU KWAAJILI YA FAMILIA YA MAWAKILI WA INJILI(GOSPEL STEWARDS FAMILY - GSF) KUTIMIZA MIAKA MITANO

✍️ Mawakili wa injili (GSF) Hii ni familia ya watu walioamua kuwa watunza injili, inayounganishwa kwa kupitia WhatsApp group. Isiyojali madhehebu bali watu waliotayari kujifunza pamoja neno la Mungu na walioamua kumpa Yesu maisha yao kuwa Bwana na kiongozi wa maisha yao binafsi. Katika familia hii pamekuwa mahali salama pa kujifunza na kukua kiroho.

Tamtukuza Mungu kwaajili ya neema na rehema zake ametupa kutimiza mwaka wa tano tangu Familia hii kubwa ya Mawakili wa injili (GSF) ianze nitakuletea mambo kumi(10) yahusuyo familia hii usiyoyajua:

1. Familia hii ilianzishwa 15/1/2021 na EV. Japhet Katana. Ili kujifunza zaidi neno la Mungu na kulea watumishi mbalimbali wa Mungu, walio na kiu na shauku ya kujifunza neno la Mungu na wenye dhamira ya kumtumikia Mungu kwa ushuhuda mwema na viwango vikubwa kuufikia ulimwengu.

2. Familia hii ilianza ikiwa na idadi ya watu watano ukijumlisha na admin. Lakini ndani ya miaka hii mitano pamoja na kufuata ratiba zetu tumefikia watu 1000+ lengo letu kuwa na group zaidi za WhatsApp na kuwafikia watu wengi zaidi kwa injili ya upendo wa Yesu Kristo.

3. Familia hii inajiendesha kwa ratiba maalumu kila siku, ambayo inahusisha semina za watumishi wa ndani ya familia, kusoma neno la Mungu, maswali mbalimbali yanayotatiza watu kukua kiroho, maombi na maombezi, kufunga , kusoma vitabu, kuwasilisha tuliyojifunza makanisani kwetu n.k

4. Familia hii inaamini katika ubora na karama ambazo Mungu ameweka ndani ya watu hivyo huwa tunaandaa semina na kualika watumishi kutoa nje ya familia hii kufundisha mada mbalimbali k**a vile, uchumi wa Kiungu, ndoa, mahusiano, utakatifu, Roho mtakatifu, Imani, maombi, hekima, n.k

5. Familia hii inamchanganyiko wa watu wa rika zote na madhehebu mbalimbali ya watu wanaomuamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao binafsi na wameokoka, tunajifunza pamoja kwa upendo na kuheshimiana.

6. Familia hii inamuundo wa uongozi ambao kwa Sasa unaundwa na mwenyekiti, katibu mkuu, Mhazina, viongozi wa idara, Ndiyo viongozi wa familia hii.

7. Mwaka huu tunayo malengo ya kutanua huduma zetu kuendelea kuwaona yatima na walio katika Hali ngumu, kwenda hospitali kuhubiri na kuombea wagonjwa pia kuwapelekea matunda. Na malengo mengine mengi kuinua huduma zetu, na tunatazamia kukua hata kuwafikia magerezani wafungwa, na baadae kuanza kuwafikia hata wasiofikiwa na injili.
1/1/2025 tuliweza kwa msaada wa Mungu kufanya Charity 3 au matendo ya huruma. Katika mkoa wa Dar es salaam kituo BABU NA BIBI WATOTO (BABIWA) Huko madale
Geita kituo cha MOYO WA HURUMA
KIGOMA KASULU KATIKA GEREZA LA KASULU MJI.
1/1/2026 tuliweza kufanya tena charity katika maeneo matatu, Buloma foundation (Kibaha) Kituo cha kulea watoto Yatima Igogwe (Kiwira-Mbeya) naTulitembelea wagonjwa hospitali ya Wilaya Tunduru (Ruvuma)
Sehemu hizi tuliweza kufanya charity tukishirikiana na wadau wetu wanaopenda injili.

8. Tunayo channel yetu YouTube GOSPEL STEWARDS TV ambayo imeanza mwezi desemba 2021, tunatarajia kuwa na subscribers 10k kufikia mwisho wa mwaka huu. K**a hujasubscribe kwenye Television yetu tafadhali fanya hivyo kupitia link hapa chini ili kuendelea kujifunza zaidi na kutuwezesha kutimiza malengo yetu ya mwaka kwa utukufu wa Mungu. Hata Sasa tunao subscribers 1.05k
https://youtube.com/channel/UCCsdQYg1TSs1Z3Jlm6VEKvQ

9. Katika familia hii kweli ya Kristo yaani Neno la Mungu na maarifa kutoka kwa watumishi mbalimbali wanaoandika vitabu hata wanaotoa mafundisho kwa njia mbalimbali ili kuujenga mwili wa Kristo, tunahimizana kufuatilia na hata kuwaalika kufundisha semina katika familia yetu.

10. Tumeiita familia kwasababu malengo yetu ya kuwa pamoja na kuishi kwa upendo kujaliana, kuinua vipawa na kuwasaidia watu kujua na kutumikia kusudi la kuumbwa kwao, kuheshimiana pia kujaliana. Hii imefanya kuwa sehemu nzuri ya kukua na kustawi kiroho. Zaidi tumefanikiwa Kwa neema ya Mungu kufikia nchi zaidi ya 11 ambazo zinawanafamilia.

✍️Kipekee kabisa napenda kumshukuru Sana Mchungaji Imani Oscar Katana, mchungaji kiongozi wa kanisa la Moto Ulao Baptist Church lililopo Dege kigamboni na Moto Ulao online church, ndiye alikuwa mshauri wa kwanza kuona tunaweza kuwa na familia hii. Moja ya shuhuda mbalimbali zinapotajwa basi hakika siwezi kumsahau katika kudumu kwa familia hii.

🌺Ukiwiwa kutoa sadaka yako kwa haya tuyafanyayo au kujitolea bundle na zawadi kwa mtumishi wa Mungu basi unakaribishwa kuwasilisha kwa namba hizi;
+255745746691 M-pesa na +255693177947 Eartel money, jina Japhet Katana.

Endapo unaye mtu unatamani kuwa mmoja wa familia hii kwa moyo mkunjufu tunamkaribisha sana, mtumie malengo yetu na akiwa tayari tutaungana pamoja nawe. Ajitambulishe ni nani na anapatikana wapi ili kutunza kumbukumbu zetu.
Unaweza kubofya link hii kuja moja kwa moja WhatsApp. Https://wa.me/+255745746691/

HERI YA MIAKA MITANO KWETU SOTE MAWAKILI WA INJILI (GOSPEL STEWARDS FAMILY) TUNAWAPENDA WOTE.
🇹🇿🇲🇿🇲🇼🇿🇲🇰🇪🇨🇩🇧🇮🇳🇦🇺🇬🇷🇼❤️

WHEN YOU MAKE A COMMITMENT, PUT A SIGN FOR REMEMBRANCEGreetings, my lovely friend. Thank you for taking time to learn so...
15/01/2026

WHEN YOU MAKE A COMMITMENT, PUT A SIGN FOR REMEMBRANCE

Greetings, my lovely friend. Thank you for taking time to learn something from this post.

During my daily Bible study, I discovered something interesting about God’s covenant and the signs He gives for remembrance.
In the days of Noah, God flooded the earth. After that, God made a covenant and vowed that He would never again destroy all living things on the earth by water-that is, through floods. God did not end with words alone; He placed a rainbow in the sky as a sign of remembrance of this covenant.

God told Noah that whenever heavy clouds appeared in the sky, the bow would also be seen. This sign remains with us to this day as a symbol of God’s faithfulness to humankind.

The wisdom we learn from this is simple but powerful: when you make a commitment, ensure that you have a sign or reminder. This helps you remain faithful and fulfill what you have promised.
Use a diary or journal. Write down your plans and commitments. When you revisit them, even after forgetting, you will be reminded and realigned with your purpose.

Many people have lost great relationships and opportunities that God brought into their lives because of unfaithfulness. They make commitments or promises but fail to fulfill them. This lifestyle has caused mistrust among many. From now on, make sure you create signs or reminders that help you stay faithful to your commitments.

Scripture Reference: Genesis 9:14–15
“Whenever I bring clouds over the earth and the rainbow appears in the clouds, I will remember my covenant between me and you and all living creatures of every kind. Never again will the waters become a flood to destroy all life.”

I appreciate you for taking this devoted time to read this post. May God bless you abundantly.
I am your friend, Evangelist Japhet Katana.
Follow me for more spiritual thoughts and reflections from Bible study.

Contact:
📞 +255 745 746 691
🇹🇿 🇿🇦 🇧🇮 🇲🇼 🇨🇩 🇿🇲 🇳🇦🇲🇿🇺🇸🇰🇪🇺🇬🇷🇼❤️

07/01/2026

TUKUMBUSHE VERSE MOJA KUTOKA KWA BIBLIA, ITUFAE 2026
👇👇

HII NDIYO HESHIMA KWENYE UFALME WA MUNGU.Imekuwa shauku ya kila mtu kutaka kuheshimiwa au kuheshimika. Hili ni jambo jem...
07/01/2026

HII NDIYO HESHIMA KWENYE UFALME WA MUNGU.

Imekuwa shauku ya kila mtu kutaka kuheshimiwa au kuheshimika. Hili ni jambo jema ambalo kila mmoja wetu anapenda kuona thamani yake ikionekana kwa jamii yake au watu wanaomzunguka.

Katika kutafakari na kusoma neno la Mungu nikajifunza jambo moja muhimu sana kwetu watumishi wa Mungu. Wengi wanapopewa heshima na kuikumbatia sana kiburi huamka na k**a maandiko yasemavyo kabla ya anguko basi kiburi hutangulia.
Mithali 18:12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

📌Unajua kiburi kinainuka pale mtu anapoanza kijiona yeye ni Bora kuliko wengine. Hivyo huanza kuwadharau wengine na kuwachukulia kiwepesi yaani kana kwamba hakuna kitu mnaweza kuniambia. Jambo hili hugeuka kaburi la mtu huyo.

Sasa basi katika kusoma Ufunuo 4:9-11 nimejifunza moja ya tabia muhimu ya huko mbinguni, naomba tusome pamoja kwa makini ndipo tutaelewana.

9. Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,

10. ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,

11. Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.

Kwenye hii tabia ya Mbinguni kwanza najifunza huko maisha ni ya umilele yaani hayana mwisho wala mwanzo yanaendelea tuu. Sasa fikiria katika ulimwengu huo mtu anapata heshima ya kuwa mzee haina maana kuwa mzee huko una mvi au umechoka mwili au ngozi kukunjamana. Huko uzee unatokana na kuheshimiwa au neema ya Mungu k**a ilivyompendeza. Sasa wanachofanya hawa wazee 24 milele mbele za Mungu ndicho nimekitafakari sana.

Hawa wameheshimiwa na wamepewa mataji ambayo ni ishara ya kuheshimiwa mno wote wanavaa vichwani mwao. Sasa kazi yao ni kumtukuza Mungu daima na kumpa utukufu. Hawa hawaikumbatii heshima waliyopewa bali wao wenyewe wanaivua na kuiweka mbele za Mungu aliyewapa. Huku wakumtukuza kwa kusema mtakatifu mtakatifu mtakatifu umestahili kuupokea utukufu.

Hivyo tuu inawafanya wao pia wazidi kuheshimiwa na kuongezewa utukufu. K**a mtumishi wa Mungu umeruzukiwa au umepata neema ya kuheshimiwa na watu basi usikumbatie heshima hiyo mpe Mungu, mtukuze Mungu kwa neema hiyo. Kweli kabisa utazidi kutukuzwa maana unamfanya Mungu kutukuzwa. Utakapoanza kuangalia sababu za kustahili kuheshimiwa ndipo kiburi kitakapozaliwa kiburi kikija anguko lako linakuja.

Mtukuze Mungu heshima yako au taji lako unalitoa unaliweka mbele za Mungu. Huendi mbele za Mungu k**a mkurugenzi wa shirika fulani bali k**a mwana. Hapo hakika utazidi kuinuliwa zaidi sababu pasipo Mungu huwezi lolote na unapowezeshwa ni vema au ni busara kukiri kuwa si kwa nguvu wala uwezo wangu ila Bwana ameniwezesha.

Nakutakia tafakari njema. Ni Mimi ndugu yako Japhet Katana unaweza kuendelea kufuatilia masomo yaliyotangulia ili kujifunza.

Mawasiliano zaidi:
+255745746691
Ev. Katana Japhet

➡️ANAYEWASIKILIZA WATU NA KUTATUA MATAIZO YAO HUGEUKA KIONGOZI WAO.Mpendwa wangu katika jambo muhimu sana ambalo ningepe...
11/12/2025

➡️ANAYEWASIKILIZA WATU NA KUTATUA MATAIZO YAO HUGEUKA KIONGOZI WAO.

Mpendwa wangu katika jambo muhimu sana ambalo ningependa ufahamu ni kwamba, kuwasikiliza watu na kuwasaidia kutatua matatizo au kero zao ni kuwa kiongozi wao.

K**a akiwepo mtu anadhania kuwa kiongozi ni cheo amechelewa sana. Unaweza kuwa na madaraka na mamlaka lakini wewe si kiongozi. Uongozi ni ushawishi watu wasiposhawishika mioyo yao kukufuata huwezi kuwa kiongozi wao. Hatak**a utakaa katika cheo na ukawa na madaraka na ulinzi mkubwa. Nataka kukuonyesha jambo hili pia katika Neno la Mungu.

Alikuwepo mfalme Daudi mtu hodari, imara na zaidi ya hayo alikuwa amechaguliwa na Mungu kuwaongoza watu wake. Alikuwa na kijana wake aliyeitwa Absalomu huyu kijana alikuwa na kisasi na mwenzake aitwaye Amnoni ambaye walikuwa baba mmoja mama mbalimbali yaani kimahusiano Hawa walichangia baba. Ikatokea siku Huyu Amnoni akampenda Tamari mdogo wake na Absalomu ambaye ikafikia wakati akambaka.

Jambo hili lilimuumiza sana Absalomu kaka yake na Tamari, Baba yao mfalme aliposikia jambo hili hakulishughulikia kwa vyovyote. Kisasi kikakua ndani ya Absalomu kuna siku aliandaa karamu au sherehe watu wakaenda kusherekea na akamtaka Amnoni alewe sana Kisha akawaambia vijana wake mtoeni nje mkamwue.

Kweli Amnoni alipigwa na kitu kizito kichwani Pwaa..na akafa.

Baada ya jambo hilo Absalomu akakimbilia inchi ya mbali kumwepuka babaye mfalme Daudi. Baada ya muda mrefu kupita miaka mitatu kijana Absalom alikaa uhamishoni akataka kurudi kwa babaye. aliporudi babaye akawa hataki hata kuonana naye uso kwa uso.

Siku zikaenda kijana Absalomu alijua nguvu ya kusikiliza watu na kuwasaidia kutatua changanoto zao. Alinza kwenda langoni mwa mji kuingilia lango la kwenda kwa mfalme akawa akisikiliza matatizo ya watu hapo na kuwasaidia kutatua shida zao. Akawa akiwaambia kuwa wasingeweza kumuona mfalme heri shida zao awasaidie kuzitatua.

Hii ilipoendelea kwa muda wa miaka kadha Absalomu akawa na ushawishi mkubwa katika nchi yao. Akapanga njama za kumpindua mfalme Daudi babaye. Watu wengi wakamwamini na wakawa upande wake.

Kumbuka kilichompa ushawishi katika mioyo ya watu Absalomu ni kuwasikiliza watu na kuwapa au kuwasaidia kupata masuluhisho ya changamoto zao.

Soma kisa hiki na tafakari, kipo katika 2Samweli 10-15

2Samweli 15:2-
2. Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu ye yote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumwa wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli.

3. Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza.

4. Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake!

5. Tena ikawa hapo alipokaribia mtu ye yote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu.

Unaona namna huyu ndugu alipata ushawishi juu ya watu kwa kuwajali, kuwasikiliza na kujaribu kutatua changamoto zao kwa kuwaonyesha upendo mkubwa.

Kuwasikiliza watu matakwa Yao kwa upendo na kuwasaidia kutatua matatizo yao huo ndiyo uongozi. Hata ukikalia kitu

Nilikuwa nasoma nikitafakari..
Ni ndugu Yako Japhet Katana, unaweza kufollow ukurasa wangu kwa mafundisho mbalimbali ya kujenga roho yako.
+255745746691
Japhet Katana
🇹🇿🇲🇼🇷🇼🇺🇬🇰🇪🇿🇲🇿🇦🇧🇮🇳🇦🇲🇿🇨🇩🇺🇸🥰

02/12/2025

LEO SWALI MOJA TU..
"K**A KWELI UNAMPENDA MUNGU UNAFANYA NINI KUTHIBITISHA HILO?"

UNAUJUA MUUJIZA MKUBWA KULIKO YOTE?Rafiki yangu unaujua muujiza mkubwa kuliko yote? Unajua kuwa huu mujiza thamani yake ...
28/11/2025

UNAUJUA MUUJIZA MKUBWA KULIKO YOTE?

Rafiki yangu unaujua muujiza mkubwa kuliko yote?

Unajua kuwa huu mujiza thamani yake ni kubwa kuliko miujiza mingine yote ambayo ungeweza kuipokea?

Najua unatafakari najaribu kuona ukiwaza k**a rafiki yangu mmoja, ngoja nikupe kidogo tafakari yetu ilivyokuwa. Nilipozungumza naye kuhusu habari hii, kwanza aliguna na kukunja ndita usoni akiashiria mshtuko. Alaafu akajibu najua nikaanza kuhojiana naye..

Rafiki: muujiza huu mkubwa kuliko yote itakuwa ni kiwete kutembea au sio.

Mimi: Hapana labda fikiria tena..

Rafiki: Basi ni bubu kusema..

Mimi: Bado huu si muujiza mkubwa. Jaribu kufikiri zaidi..

Rafiki: oooh okay Kiziwi kusikia

Mimi: Hapana bado hautoshi kuwa muujiza mkubwa kuzidi yote. Fikiri zaidi..

Rafiki: basi aliyekufa kufufuliwa hapa nimekuweza waoooh kufufuliwa nasema..

Mimi: Bado huo sio muujiza mkubwa kuzidi yote?

Rafiki: Ninini basi? Naomba niambie...

Mimi: Ongeza kufikiri zaidi kidogo unakaribia kupata jibu...

Rafiki: Au ni ule Yesu kuwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili.

Mimi: Hapana huu si muujiza mkubwa kuzidi yote.

Rafiki: Ooh basi Yesu kutembea juu ya maji na na kutuliza dhoruba ...

Mimi: Hapana bado huu si muujiza mkubwa kuzidi yote.

Rafiki: Ooh sawa basi naomba niambie namimi niujue..

Mimi: Sawa..

✍️ SASA NISIKILIZE KWA MAKINI NIKUAMBIE NI MUUJIZA UPI MKUBWA KUZIDI YOTE.

Kwanza kabisa kwanini nimesema kufufuliwa kutoka kwa wafu sio muujiza mkubwa kuzidi yote kwa kuwa hata aliowafufua Bwana Yesu bado walikufa tena. Mfano Lazaro.

Aliowaponya bado baada ya miaka mingi walikufa tena. Mfano mwanamke aliyetokwa na damu.

Wenye njaa waliopewa chakula bado kesho yake walihisi njaa na kuendelea kumfuata awape tena mkate.

Yesu kutuliza dhoruba ilitulia lakini mpaka leo bado kuna dhoruba baharini.

✍️SASA MUUJIZA MKUBWA NI HUU HAPA...

Warumi 10:9-10
9. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
(That if thou shalt confess with thy mouth the Lord Jesus, and shalt believe in thine heart that God hath raised him from the dead, thou shalt be saved.)

10. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
(For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.)

✍️Muujiza huu unaitwa WOKOVU. yaani mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu aliyepotea katika dhambi(uasi) na kumpa tena mamlaka na kumrejesha katika hali yake ya mwanzo ya kuumbwa kwake yaani kumiliki na kutawala katika huu ulimwengu na zaidi ya hapo ni kumpa na uzima wa milele.

Kumbuka kwa kuamini moyoni mwako na kukiri kwa kinywa chako kuwa Yesu kristo ni Bwana, alikuja kukuokoa unaokolewa. Na jambo hili ni jambo la furaha mbinguni kuliko kiziwi akisikia, kiwete akitembea au kipofu kuona.

Tuone..
Luka 15:7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
(I say unto you, that likewise joy shall be in heaven over one sinner that repenteth, more than over ninety and nine just persons, which need no repentance.)

Kumbe aliyekuwa amepotelea dhambini akiamini akarejea kuamini mbinguni kuna furaha sana. K**a bado hujaamini nakukaribisha pokea muujiza huu mkubwa zifurahishe mbigu.

Kumbuka maneno ya Bwana Yesu kuwa yeyote atakayekunywa maji anayompa yeye hataona kiu tena.
Yohana 4:13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
(Jesus answered and said unto her, Whosoever drinketh of this water shall thirst again:) sehemunya mazungumzo ya Yesu na mwanamke msamalia..

Ukiamini ukampokea Yesu leo utumwa wa dhambi utaondoka, yaani KIU ya kufanya dhambi inayokutesa itaondoka utakuwa huru huru kweli kweli. Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
(And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.)

Mpendwa wangu dhambi huwezi kuishinda kwa kujitahidi pekee, unahitaji kuiamini injili Roho wa Mungu atakaa ndani yako na utaanza kuongozwa naye na itaanza kuwa rahisi sana kwako kushinda dhambi. Na kuishi vile Mungu atakavyo k**a alivyosema katika neno lake.

Ukiokolewa leo ndiyo bima au salama ya maisha yako hapa duniani na baada ya kuondoka duniani.

Rafiki yangu je, huu sio muujiza mkubwa kuliko yote?

Nakualika kumpokea Yesu Leo upokee muujiza huu mkubwa kuzidi yote. 👇

Fuatisha sala hii kwa sauti:
Sema,
BWANA YESU, NIMEKUJA KWAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI. NINATUBU LEO DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAFISHE KWA DAMU YAKO YA THAMANI. NIPOKEE KATIKA UFALME WAKO NA JINA LANGU LIANDIKWE KWENYE KITABU CHA UZIMA. BWANA YESU NINAOMBA UNIJAZE NA ROHO WAKO MTAKATIFU NA UNIONGOZE SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU. NIMEOKOKA LEO
AMEN.

Hongera sana sasa umeokoka na umepokea MUUJIZA MKUBWA HUU.👏👏👏
Karibu kwenye familia ya waamini.

K**a umefuatisha sala hii, tuwasiliane nitakupa msaada zaidi wa mafundisho na kitabu cha kukusaidia kukua kiroho.

TUWASILIANE KWA NAMBA HIZI, UKIWEZA WHATSAPP ITAPENDEZA ZAIDI +255745746691

Follow ukurasa wetu huu kwa mafundisho zaidi: Japhet Katana FOLLOW

EV. KATANA JAPHET
UBARIKIWE SANA
🇹🇿🇲🇿🇰🇪🇿🇲🇳🇦🇿🇦🇷🇼🇧🇮🇺🇲🇺🇬🇨🇩🇲🇼❤️

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gospel Stewards Family - GSF posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Gospel Stewards Family - GSF:

Share