Kinyerezi SDA Church

Kinyerezi SDA Church Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo, Shahidi mwaminifu na wa kweli, Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Huu ni ukurasa rasmi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Kinyerezi. Karibu ujiunge kwenye ukurasa huu.

06/09/2026

Tunawakaribisha Nyote katika , Makambi ya Mtaa wa Kinyerezi , yanayoanza siku ya Jumamosi tarehe 12 - 19 / 9 / 2026

Na hizi ni Salamu kutoka kwa mmoja ya wazee wa Kanisa akiwakaribisha watu wote kushirili katika Makambi


04/09/2026
Tunawakaribisha wote katika sikukuu za    ya Mtaa wa Kinyerezi yatakayoanza Tarehe 12 - 19 September 2026 , Njoo tuchote...
28/08/2026

Tunawakaribisha wote katika sikukuu za ya Mtaa wa Kinyerezi yatakayoanza Tarehe 12 - 19 September 2026 , Njoo tuchote baraka za Bwana , Njoo Turudishe sifa na Shukrani kwa Mungu kwa Makuu aliyotutendea kwa mwaka mzima ,

Neno la Mungu litahubiriwa , Nyimbo zitaimbwa za kumtukuza Mungu ,
Njoo wewe na Familia Yako , alika ndugu , jamaa na Rafiki




**UJUMBE WA SHUKRANI****“Bwana ndiye aliyekuwa upande wetu; mioyo yetu inasema: Asante.”**Ndugu, jamaa, marafiki, waumin...
10/08/2026

**UJUMBE WA SHUKRANI**

**“Bwana ndiye aliyekuwa upande wetu; mioyo yetu inasema: Asante.”**

Ndugu, jamaa, marafiki, waumini na wadau mbalimbali,

Kwa unyenyekevu mkubwa, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja wenu aliyesimama nasi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kufuatia ajali iliyosababisha kuondokewa na ndugu zetu na kuwaacha wengine wakiwa majeruhi.

Tunatambua kwamba maneno hayawezi kutosha kueleza namna tunavyothamini upendo, faraja, mshikamano na msaada mlioendelea kutupatia. Katika wakati ambao mioyo yetu ilikuwa imejaa huzuni na maswali mengi, uwepo wenu, sala zenu, salamu za pole, michango yenu na msaada wenu wa aina mbalimbali vimetupa nguvu na kutukumbusha kwamba hatuko peke yetu.

Kwa namna ya pekee, tunatoa shukrani kwa Taasisi mbalimbali za Serikali kwa ushirikiano, uratibu na huduma mlizotoa katika kipindi hiki cha majonzi na katika kushughulikia madhara yaliyotokana na ajali hiyo.

*ASANTENI SANA KWA UPENDO WENU, FARAJA YENU, MAOMBI YENU NA MSHIKAMANO WENU.*

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.Tunawakaribisheni sana kushiriki baraka za juma la Kaya na Familia ambalo masomo yake y...
08/08/2026

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.

Tunawakaribisheni sana kushiriki baraka za juma la Kaya na Familia ambalo masomo yake yataanza tarehe 09/08/2026 saa 11:30 jioni mpaka saa 1:00 usiku.

Mungu atubariki sote na atuwezeshe kuhudhuria na kushiriki baraka hizi kanisani Kinyerezi.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kinyerezi SDA Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share