Viwawa Mt.Theresia_Mbezi mwisho

Viwawa Mt.Theresia_Mbezi mwisho Kumtumikia Mungu Kuna Faida

🕯️TANZIA🕯️Uongozi wa VIWAWa Parokia ya Mt Theresia wa Mtoto Yesu - Mbezi mwisho, Unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuw...
25/06/2024

🕯️TANZIA🕯️
Uongozi wa VIWAWa Parokia ya Mt Theresia wa Mtoto Yesu - Mbezi mwisho, Unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa kiongozi wao mpendwa, Ndugu Deogratius Mausa kilichotokea siku ya jumamosi tarehe 22-06-2024 usiku.
Marehemu alikuwa ni Mwenyekiti Msaidizi wa Vijana Parokia, na Mwenyekiti wa Vijana Dekania ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Mavurunza, Jimbo kuu la Dar es Salaam.

🕯️BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.🕯️

Furaha yetu k**a vijana wakatoliki baada ya kushiriki bonanza ndani ya dekaninia pamoja na vijana wa parokia nyinginezo....
25/07/2023

Furaha yetu k**a vijana wakatoliki baada ya kushiriki bonanza ndani ya dekaninia pamoja na vijana wa parokia nyinginezo. Hakika ilipendeza sana....

Je umemtambua nani hapo?!

🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼



🌼JUMUIYA YA VIJANA🌼Picha mbalimbali zikionyesha kusanyiko la vijana wakisali Pamoja Sala za asubuhi.MAHALI: Parokiani, M...
22/07/2023

🌼JUMUIYA YA VIJANA🌼

Picha mbalimbali zikionyesha kusanyiko la vijana wakisali Pamoja Sala za asubuhi.

MAHALI: Parokiani, Mt. Theresia wa mtoto Yesu.

Historia ya Mt. Kamili wa Lelis , Padre na Mwanzilishi wa ShirikaKamili alizaliwa karibu na Chieti katika mkoa wa Abruzi...
14/07/2023

Historia ya Mt. Kamili wa Lelis , Padre na Mwanzilishi wa Shirika

Kamili alizaliwa karibu na Chieti katika mkoa wa Abruzi (Italia) mwaka 1550. Mama yake alifariki mapema, yeye alipokuwa na umri wa miaka kumi na mitatu. Kwa sababu ya kufiwa mapema na mamaye, alipotoka tabia akawa mvivu na mwasherati. Mwaka 1569, alipopata umri wa miaka kumi na tisa, aliingia uaskari pamoja na baba yake huve Venisi (Italia) wakati wa vita na Waturuki. Huko vitani yeye na baba yake walipatwa na ugonjwa. Babaye alikufa, yeye alipatwa na donda-ndugu mguuni, nalo liliendelea kumsumbua maisha yake yote.

Kamili alipenda sana kucheza k**ari. Lakini katika kucheza k**ari, alifilisiwa mali yake yote. Kwa sababu hiyo, ilimpasa kufanya kazi kwa Wakapuchini akisomba matofali ya kujenga nyumba. Alipoona kutokana na mwenendo safi wa mapadre Wakapuchini, alioushuhudia, naye akaongoka. Alizitupilia mbali furaha zake mbaya, akaziungama dhambi zake, kisha akawaomba mapadre hao Wakapuchini wampokee katika monasteri yao. Kwa sababu alikuwa na donda-ndugu mguuni, hakupata ruhusa ya kukaa humo. Alijaribu mara nne lakini alikataliwa tu.

Baada ya hapo alikwenda Roma, akaanza kuwahudumia wagonjwa katika hospital ya Mt. Yakobo. Siku zile huduma kwa wagonjwa katika hospital ziikuwa mbaya sana. Basi, Kamili alipoona watumishi wa hospitali hiyo wakiwatunza wagonjwa kwa uzembe bila kuwajali, alifanya shauri la kukusanya vijana ambao wangewatunza wagonjwa vizuri zaidi si kwaajili ya Yesu Kristu. Ilikuwa mwaka 1582 hivi, Kamili alipoanzisha shirika la kitawa la kuwahudumia wagonjwa hospitalini. Mwanzoni alipata migogoro mingi.

Kwa maongozi ya Mt. Filipo Neri; Kamili alipewa upadre mwaka 1584. Miaka miwili baadaye, Papa alilikubari shirika lake la wahudumu hospitalini, likaenea upesi nchini Italia. Wanashirika wanaitwa Wakamiliani. Ingawa Kamili alipata mateso mengi kwa kuugua, hakuchoka kuwatunza wagonjwa kwa upendo. Siku zake za mwisho, alipokuwa huko Genoa, ugonjwa wake ulimzidi sana. Alipokea mpako wa wagonjwa, akaaga dunia tarehe 14 Julai 1614. Alitangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1746. Yeye pamoja na Mt. Yohani wa Mungu na wasimamizi wa wagonjwa, na pia wasimamizi wa wauguzi na mashirika ya wauguzi.

Historia ya Mt. Henriko, Kaisari wa UjerumaniHenriko alizaliwa Regensburg mkoani Bavaria (Ujerumani) mwaka 973. Mtakatif...
13/07/2023

Historia ya Mt. Henriko, Kaisari wa Ujerumani

Henriko alizaliwa Regensburg mkoani Bavaria (Ujerumani) mwaka 973. Mtakatifu Wolfgang, askofu wa Regensburg, alimlea katika ibada na uchaji wa Mungu. Baba yake alipokufa aliirithi nchi ya Bavaria, akamwoa mke, jina lake Kunegunda.

Miaka kadhaa baada ya hayo, Henriko alichaguliwa kuwa Mfalme wa Ujerumani. Tangu siku ile, alifanya bidii kuistawisha dini katoliki katika nchi zake. Aliyajengesha upya makanisa mengi yaliyoharibiwa na maadui wa dini, akamrudisha Roma Papa Benedikto wa Nane, aliyefukuzwa na papa wa uwongo. Baba Mtakatifu naye alimwita aje Roma, akamvika kichwani taji la Ukaisari, k**a tuzo kwa kazi zake njema za kumkinga Papa.

Kaisari Henriko, siku zote, aling'amua hatari zinazowanyemelea watu wanaokuwa katika madaraka makubwa. Kwa kusali aliweza kushika moyoni mwake fadhila za unyenyekevu na uchaji wa Mungu alizohitaji maishani mwake. Alifanya bidii kubwa kuleta amani na furaha katika milki yake, akasaidia kuwaongoa watu wa Hungaria wawe wakristu.

Alijenga kanisa kuu na monasteri mjini Bamberg. Kisha akaweka akiba fedha nyingi sana kwa ajili ya makanisa na maskini, kusudi ibada takatifu na huduma ya maskini viweze kuendelea mpaka mwisho wa nyakati. Alikufa mwaka 1024 akatangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1146.



Historia ya Mt. Yohani GualbertMtakatifu Yohani Gualbert alizaliwa mwaka 985 huko Florence nchini Italia na alisoma mape...
12/07/2023

Historia ya Mt. Yohani Gualbert

Mtakatifu Yohani Gualbert alizaliwa mwaka 985 huko Florence nchini Italia na alisoma mapema.

Kaka yake wa pekee aliyeitwa Hugo aliuawa.

Mtakatifu Yohani aliamua kuacha vyote ili alipize kisasi kwa kumuua mtu aliyemuua nduguye.

Ikatokea siku ya Ijumaa kuu Yohani aliingia Mjini Florence akifuatana na wenzake,wakiwa na silaha.

Katika njia nyembamba alikutana na muuaji wa kaka yake na akaamua kumuua ili kutimiza kisasi chake.Wenzake wote wakapiga magoti mbele silaha zao wakaziweka k**a msalaba wakimuomba Yohani asimuue mtu yule kwa kuwa ilikuwa siku ambayo Wakristu hukumbuka kifo cha Bwana YESU.

Mtakatifu Yohani akamsamehe na akaingia katika Kanisa la Wabenedictine huko San Miniato.

Alipoangalia msalaba uliokuwa mbele yake alitambua kuwa alipaswa kusamehe kwa nia moja na Mtakatifu Yohani Albania akajiunga na Watawa Wabenedictine.

Kwa misimamo ya ukweli wake Mtakatifu Yohani alikosana na mkuu wake na Askofu wa Florence . Aliondoka hapo akaenda Camaldoli na baadaye akaweka makazi yake Vallombrosa.

Huko Mtakatifu Yohani akaanzisha makao mapya ya watawa. Eneo kuzunguka hapo lilikuwa pweke na tupu. Akaanza kupanda miti kulizunguka eneo hilo akishirikiana na watawa wenzie wakatengeneza sehemu nzuri za kusali na mazingira mazuri.

Akawezesha kuanzisha sehemu monasteri zingine akihudumia maskini na wasiojiweza.

Mtakatifu Yohani alikufa mwaka 1073, huko Badia Passignano, Florence katika ardhi ya Taifa la Italia na Baba Mtakatifu Celestine III akamtangaza kuwa Mtakatifu mwaka 1193.



Historia ya Mt. Benedicto , AbateMama Kanisa anatuomba tuungane naye katika sherehe kwa heshima ya Mtakatifu Benedict al...
11/07/2023

Historia ya Mt. Benedicto , Abate

Mama Kanisa anatuomba tuungane naye katika sherehe kwa heshima ya Mtakatifu Benedict aliyezaliwa March 2, 480 huko Nursia, Umbria katika ardhi ya Taifa la Italia. Alipelekwa Roma kusoma lakini hakuridhishwa na mazingira ya pale.

Mwaka 500 Mtakatifu Benedict aliamua kuacha masomo yake na akaamua kwenda Subiaco, akakaa huko peke yake pangoni akisali.

Baadaye akaombwa na Jumuia ya Watawa waliokuwa wakiishi katika Monasteri ya Vicovaro kuwa Abate wao.

Mtakatifu Benedict aliweka sheria ngumu na kufuata kikamilifu maisha ya kitawa na baada ya muda yakafanyika majaribio kadhaa ya kumuua.

Mtakatifu Benedict akaondoka hapo na kwenda kuishi tena pangoni peke yake na huko napo akakutana na watu waliotaka kumletea matatizo na hivyo akaondoka tena mwaka 530.

Kutokea hapo Mtakatifu Benedict alizunguka sehemu mbalimbali na kuanzisha monasteri 12 na mwisho akaanzisha Monasteri ya Monte Cassino iliyokuwepo kati ya Roma na Naples.

Mtakatifu Benedict alikufa mwaka 547 huko Monte Cassino na Baba Mtakatifu Humorous III akamtangaza Mtakatifu mnamo mwaka 1220 .



Historia ya Mt. Mwenyeheri Emmanuel Ruiz na Wenzake, MashahidiMwenyeheri Emmanuel Ruiz alizaliwa Mei 5, 1804 huko Santan...
10/07/2023

Historia ya Mt. Mwenyeheri Emmanuel Ruiz na Wenzake, Mashahidi

Mwenyeheri Emmanuel Ruiz alizaliwa Mei 5, 1804 huko Santander katika Taifa la Hispania.

Baada ya masomo yake Mtakatifu Emmanuel alijiunga na Shirika la wa Francisan na akapata Daraja Takatifu la Upadri.

Mwenyeheri Emmanuel Ruiz alienda kufanya kazi huko Damascus nchini Syria akiwa Padri na Mkuu wa Nyumba ya Watawa wa Francisan.

Nyakati hizo kulikuwa na vurugu kubwa iliyosababishwa na waislamu ambao waliwak**ata na kuwatesa na kisha kuwaua Wakristo, ambao walishikilia imani yao.

Wauaji walipofika katika Convent ya Wafrancisan Mwenyeheri Emmanuel Ruiz na wenzake 7 pamoja na Walei 3 walikataa kukana imani yao jambo lililopelekea mateso makali na mwisho kuuwawa na Ilikuwa mwaka 1860 Mjini Damascus.

Walitangazwa Wenyeheri Oktoba 10, 1926 na Baba Mtakatifu Pius XI

Leo Julai 18 Kanisa linamkumbuka  Mtakatifu Frederiko, Askofu na Mfiadini Haijulikani kwa hakika kabisa Frederiko alizal...
18/07/2022

Leo Julai 18 Kanisa linamkumbuka  Mtakatifu Frederiko, Askofu na Mfiadini 

Haijulikani kwa hakika kabisa Frederiko alizaliwa wapi, lakini ionekanavyo asili yake ni katika mkoa wa frisia, upande wa Kaskazini wa Uholanzi na Ujerumani. Baada ya kupewa Upadre, Askofu wake alimpa kazi ya kuwafundisha waongofu wa dini. Baadaye mnamo mwaka 825 alichaguliwa kuwa Askofu wa Utrekt (Uholanzi).

Askofu Frederiko alituma Mapadre wenye bidii katika mkoa wa Frisia ambako kulikuwa bado na wapagani wengi mwenyewe alichukulia kisiwa cha Walkeren, upande wa Kusini – Magharibi wa nchi hiyo. Kazi yake ilikuwa ngumu, kwakuwa wakazi wengi wa Kisiwa hiki walikuwa wamefunga ndoa zisizo halali kwa mujibu wa udugu wao, na kuwatenganisha ilikuwa taabu kabisa na hata kazi yenye hatari.

Yawezekana kusema kwamba wakati ule uhusiano kati ya Kaisari wa siku zile aliyeitwa jina lake Lui Mchaji, na Maaskofu wa nchi yake, ulikuwa si mzuri, hasa kwa kuwa Kaisari aliyaangalia majimbo ya Kanisa k**a mali yake na k**a chemichemi ya mapato kwa faida yake binafsi. Lakini Askofu Frederiko hakuogopa. Alimkabili Kaisari kwa uhodari, na hata aliweza kumwambia kwamba desturi yake ilikuwa siyo nzuri.

Lakini Frederiko alipothubutu kumpinga Kaisari asimwoe yule aliyekuwa amemchagua kuwa mke wake kwa sababu alikuwa mwanamke mpotovu, Kaisari na Askofu waligombana sana. Mnamo tarehe 18 Julai, mwaka 838, Askofu, mara alipomaliza kuadhimisha Ekaristi katika Kanisa lake kuu, alivamiwa na majambazi wawili waliompiga visu. Inasimuliwa kwamba majambazi hao walikuwa watu wa Walkereni waliotaka kujilipiza kisasi, na yasemekana pia kwamba wauaji hao walikuwa wameajiriwa na Kaisari. Askofu Frederiko alikufa dakika chache tu baada ya kupigwa visu, huku akisema maneno ya zaburi 116:”Nitaenenda mbele ya Bwana katika nchi ya walio hai”

Mtakatifu  Frederiko, Askofu na Mfiadini - UTUOMBEE

Watakatifu wote - MTUOMBEE

Leo Julai 16 Kanisa linaadhimisha Sherehe ya  Bikira Maria Wa Mlima KarmeliKarmeli ni jina la Mlima wa Palestina unaosif...
16/07/2022

Leo Julai 16 Kanisa linaadhimisha Sherehe ya  Bikira Maria Wa Mlima Karmeli

Karmeli ni jina la Mlima wa Palestina unaosifiwa katika Maandiko Matakatifu kwa uzuri na usitawi wake. Nabii Eliya aliitetea imani ya Taifa la Israeli kwa Mungu aliye hai.

Karne ya 12 kikundi cha Watawa wakaa pweke kilifanya maskani yake huko Mlimami, na baadaye kukaanzisha Utawa wa Wakarmeli. Lengo la Watawa hao ni kuishi maisha ya fikara chini ya ulinzi na  Malezi ya Mama wa Mungu.

Katika karne ya 13, Bikira Maria alimtokea Mkuu wa Wakarmeli katika bara ya Uingereza, jina lake Simoni Stock. Inasemekana kwamba Mama Maria alimwonyesha Skapulari akamwambia:’’Mwanagu mpenzi, pokea Skapulari hii k**a alama ya mapendo yangu kwa Wakarmeli wote. Skapulari hii itakuwa alama ya wokovu, itawakinga katika hatari zote wale wanaoivaa.’’

Neema hiyo haikuwahusu Wakarmeli tu, bali imewaneemesha hata watu walioshirikiana nao. Matumizi na ibada ya Skapulari imeenea sana, na Mama yetu akaithibitisha uwezo wake kwa msaada wake.

Bikira Maria wa mlima karmeli - Utuombee



Karibuni Carmelite Secondary Kwa Elimu na Malezi Bora.Kwa Mawasiliano; +255733145050
15/07/2022

Karibuni Carmelite Secondary Kwa Elimu na Malezi Bora.
Kwa Mawasiliano; +255733145050

Historia ya Mt. Landri, Askofu wa ParisMtakatifu Landri alikuwa askofu wa mji wa Paris (Ufaransa) zamani za Mfalme Klovi...
10/06/2022

Historia ya Mt. Landri, Askofu wa Paris

Mtakatifu Landri alikuwa askofu wa mji wa Paris (Ufaransa) zamani za Mfalme Klovis. Hatuna habari zake nyingi, ila alikuwa na huruma sana kwa wagonjwa na maskini. Yeye ndiye aliyeijenga ile hospital moja kubwa iliyoko Paris mpaka hivi leo, iitwayo Hotel-Dieu. Jina hili maana yake "Hospitali ya Mungu".

Mwaka mmoja ilitokea njaa kuu, Landri aliuza mali zake, akauza na vyombo vya nyumbani mwake apate kununua vyakula kuwapa watu wa mji. Njaa ilipozidi, kusudi watu wasife maana fedha zilikuwa zimemwishia, aliuza hata baadhi ya vyombo vitakatifu vya kanisa.

Ukarimu wake haukufa naye, kwa maana miujiza mingi ilitendeka kaburini pake. Wagonjwa walipokuwa pale kuomba, waliponywa. Siku moja ulizuka moto mkubwa katika mji wa Paris, nyumba nyingi zilianza kuwaka. Na watu walimkumbuka askofu marehemu baba yao, walikwenda wakatwaa sanda yake, iliyotunzwa tangu zamani katika kanisa ya Mtakatifu Jermano; wakaitia katika ncha ya ufito mrefu, wakaitandaza mbele ya moto. Mara ndimi za moto zilififia, na moto ukazimika.

Mt. Landri Askofu, - Utuombee

Address

Mbezi Mwisho, Goba Road
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Viwawa Mt.Theresia_Mbezi mwisho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Viwawa Mt.Theresia_Mbezi mwisho:

Share