18/06/2025
NILIYOYAONA KWENYE ZABURI 23:4
Zaburi 23:4
[4]Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
1. KUWA NA MUNGU HAIMAANISHI HUTAPITIA MAJARIBU, BALI MUNGU ATAKUVIKA NGUVU YA KUSHINDA.
Yohana 16:33 "Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu."
2. HATUISHI KWENYE MAJARIBU BALI TUNAPITA KWENYE MAJARIBU. Andiko linasema "... NIJAPOPITA KATIKA BONDE LA UVULI WA MAUTI....". Majaribu ni ya kitambo tuu.
2 Wakorintho 4:17 "Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana"
3. ILI MABAYA YAKUPATE NI LAZIMA UYAOGOPE KWANZA.
Moja kati ya mbinu anayotumia adui ili kuleta mabaya kwako ni kukujaza HOFU ya mambo ambayo anataka yakupate. Jiambie k**a Daudi kuwa SITAOGOPA MABAYA (kiri neno hili mara saba mfululizo)
4. BONDE LA UVULI WA MAUTI HALIKUOGOPI WEWE BALI LINAMUOGOPA ALIYE PAMOJA NAWE (MUNGU) NA KWASABABU HIYO HAURUHUSIWI KUFA KWA JINA LA YESU.
5. DAWA YA HOFU NI KUJUA SANA KUHUSU ULICHONACHO NA UWEZO ULIONAO. Hofu inakosa nguvu pale INAPOKUTANA NA MTU ASIYEJUA ALICHONACHO NA UWEZO ALIONAO. Pia, hofu inapata nguvu pale inapokutana na mtu asiyejua hayo.
Daudi anasema ".... SITAOGOPA MABAYA KWA MAANA WEWE UPO PAMOJA NAMI.." Azima huu ufahamu na utembee nao katika kila majira ya maisha yako. Isaya 5:13, Hosea 4:6
Ayubu 22:21 "MJUE SANA MUNGU, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia"
6. HATA MUNGU UNAYEMUAMINI HUWA ANAPITA KATIKA BONDE LA UVULI WA MAUTI, NA HUPITA WAKATI AMBAPO MTOTO WAKE ANAPITA. Hii inatakiwa ikutie moyo na iponye ufahamu wako unaokudanganya kwamba MUNGU amekuacha.
Andiko linasema "Nijapopita........, Maana WEWE (MUNGU) upo pamoja nami.
7. WAKATI WA MAJARIBU USIFANYE KOSA LA KUANGALIA UKUBWA WA JARIBU UNALOPITIA BALI ANGALIA UKUBWA WA MUNGU ULIYENAYE. Usiangalie mazingira yanayokuzunguka bali mwangalie MUNGU aliyekuzunguka.
8. USIFANYE KOSA LA KUFUMBA KINYWA CHAKO WAKATI WA MAJARIBU. Daudi alikuwa anakiri anachokijua na anachotaka kukiona kwenye mazingira anayopitia. Wakati wa majaribu ndio wakati mzuri wa KUKIRI NENO, KUTABIRI NENO, KUTAMKA NENO na KUOMBA KWA MUONGOZO WA NENO.
Andiko linasema ".... SITAOGOPA MABAYA KWA MAANA WEWE UPO PAMOJA NAMI.."
NOTE: KINYWA KILICHOFUMBWA NI HATIMA ILIYOFUNGWA
9. UFAHAMU ULIONAO KUHUSU MUNGU NA UWEPO WAKE UNA MCHANGO MKUBWA SANA KATIKA KUAMUA HATIMA YAKO WAKATI WA MAJARIBU. Jaza moyo wako Neno la Bwana, tafakari Neno na uombe kutoka kwenye Neno.
10. HATA KATIKA FIMBO YA MUNGU BADO KUNA FARAJA. Amesema "...Gongo lako na FIMBO YAKO VYANIFARIJI". Katika mzoga wa simba Samsoni alipata asali, ndivyo ilivyo katika kila jaribu Mungu anasema kuna Faraja. MATENDO 9:31
11. UVULI WA MAUTI MAANA YAKE NI MAUTI ISIYO HALISI AU ILIYOZUILIWA ILI ISIKUPATE K**A ILIVYOKUWA.
INATOSHA KWA LEO, JE UMEJIFUNZA KITU HAPA.!?
USISAHAU KUTENDEA KAZI ULICHOJIFUNZA
Pastor Joseph Makindi
SISI TUU ISHARA NA AJABU