23/08/2021
💥 BTC-MORNING MESSAGE💥
Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.
Isaya 49:14-16
________________________
Hongera kwa kuiona siku hii tena!
Natamani kushiriki nawe ujumbe huu siku hii ya leo.
MUHIMU
✨Nimepata wasaa wakufikiri na kutafakari juu ya upendo alionao mama juu ya mtoto wake lakini niliposhangaa zaidi ni licha ya upendo huo bado mama anaweza akakimbia au akamtelekeza mwanae! Lakini upendo wa Mungu kwetu Ni mkuu Sana hawezi kukimbia katika Nyakati zote za maisha ,atakaa nasi, atatutia nguvu na kutupatia ujasili wa kuendelea mbele.
✨Amesema ametuchora katika vitanga vyake akiwa na maana kila wakati anapotazama anatuona Mimi na wewe, hawezi kutusahau kamwe na hatakaa atusahau kamwe.
✨Liko Jambo linautesa moyo wako, iko namna inayokunyima usingizi kiasi kuwa unafikiri Mungu hayuko nawe, hapana Mungu yu nawe na anajua kila unalolipitia anatamani uamini kuwa Yuko na wewe na anaweza kukupitisha katika hayo magumu! Simama tu ukauone mkono wa Bwana.
✨Mungu anakupenda Sana, Mungu anakupenda Sana, hatakuacha mguu wako usogezwe, hawezi kukuacha uwe mawindo ya mbwa mwitu, weka Imani kwake.
Kuzalauliwa na watu, kuonekana haufai na watu hakuondoi picha na sura yako katika vitanga vya Mungu, unapoonekana haufai yeye huuona uthamani na ubora ndani yako.
Endelea mbele utashinda.
ever give up upon God.
NI YETU
HADI TUIONE MBINGU.
Ubarikiwe sana.
Uwe na siku Njema.
Ev.William hezron.
Servant
0762599570.