MKATE WA KILA SIKU

MKATE WA KILA SIKU “kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;"

27/03/2026

*MAKAVAZI YA USHUHUDA NA SHUHUDA ZA BWANA NI URITHI WETU NA VIZAZI VYETU. [ZAB 119:111]*

*"UJUMBE WETU, UHURU WETU NA VIZAZI VYETU."*

_"...tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru..."[Yn 8:32 SUV]_

Shalom Taifa la Kweli ya Kristo Yesu iliyofunuliwa kwetu na Roho Mtakatifu katika Ujumbe wa Uana na Ufalme wa Mungu tulionao. Hongereni nyote kwa kuendelea kudumu katika Kweli hii huku mkiendelea kutafiti ndani yake kila siku.

Ninapenda kumshuhudia Mungu Baba kwenu kwa ajili ya Ujumbe wa Uana na Ufalme wa Mungu wa Taifa la Bwana Pete ya Muhuri jinsi ambavyo kupitia Ufahamu wa Ujumbe huu umekuwa hifadhi yangu na uzao wangu na vizazi vyangu dhidi ya kila hila, uongo na uharibifu wowote. Ujumbe huu umekuwa ulinzi na usalama kwangu na vizazi vyangu vyote. Ujumbe huu umekuwa Wokovu hata katika nyumba ya Baba na mama yangu wa kimwili. Ujumbe huu umekuwa uhuru wetu ndani ya Kristo hata kutufanya kuwa wanufaika wa Baraka zote zilizo katika Ujumbe huu. Ujumbe huu ambao ni mafanikio na ustawi wetu kwa vizazi hata vizazi.

Ninakumbuka katika Ibada ya tarehe 8/3/2026 Bwana Mwenyewe alimtumia Mwana na Urithi wake kutuongoza ombi hili;
*"kumshukuru Yeye (Mungu Baba) kwa ajili ya Kweli yake (Ujumbe wa Uana na Ufalme wa Mungu) ambayo ni ulinzi na usalama na hifadhi yetu dhidi ya kila uongo, hila na uharibifu, udanganyifu. Kweli ambayo imetufanikisha, imetustawisha, imetuinua."*

Hakika baada ya ombi hili siku tano mbele yaani 13/3/2026, Bwana alinifunulia jinsi ambavyo kupitia Kweli hii (Ujumbe wa Uana na Ufalme wa Mungu) amekomesha uzao wote wa hila, uongo na uharibifu vilivyokuwapo kabla yangu katika familia ya kimwili na sasa ameanza rasmi kizazi chake kipya na mimi. Kizazi cha Wana wa Mkono wa Kuume wa BABA ambao ni waendelezaji wa Maono ya Ufalme wa Mungu Baba hapa duniani.

Ama kwa hakika, mimi na uzao wangu wote na vizazi vyangu vyote tunaungana na Watakatifu wote Mbinguni na duniani kusema ya kwamba tumekombolewa na kuwekwa huru na Kristo milele!
Shalom!

Na,
Mwana wa Mungu,
Taifa la Bwana Pete ya Muhuri (Hag 2:23),
Dar es salaam, Tanzania.
@2026.

26/03/2026

*MAKAVAZI YA USHUHUDA NA SHUHUDA ZA BWANA NI URITHI WETU NA VIZAZI VYETU. ZAB [119:111]*

_MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA TAIFA LA BWANA PTM!_

*NIMEMUONA BWANA, NIMEMUONA BWANA ANAPENDEZA!*

Taifa la Bwana, wana wa Mungu, wana wa upendo na nguvu yake, mlio na Roho wa Kristu anayewaongoza na kuwaimarisha daima. Taifa la ishara, maajabu, miujiza na matendo makuu ya Mfalme Elohim, Shalom Shalom.

K**a vile nuru ifukuzavyo giza wala giza lisiweze kukinzana nayo, wala lisiweze kutanusha misuli yake na kuifungia nuru nje, ndivyo ambavyo nuru ya kweli ya Kristu Mfalme hufukuza na kuondoa kila giza katika fahamu na fikra zetu k**a ilivyofanya katika roho zetu.

Katika miaka hii sita katika Taifa la Bwana Pete ya Muhuri, napenda kumtukuza Mungu Baba kwa kujibu hamu ya moyo wangu na ombi langu.

Katika miaka ya mwanzo ya Taifa la Bwana, nikiwa nasoma kitabu cha mtumishi wa Mungu Heidi Baker akifunua jinsi kukutana na Mungu Baba na upendo wake katika ibada mojawapo kulivyombadilisha kabisa nami nilitamani sana kukutana na kumjua Mungu Baba katika namna ambayo itabadilisha kabisa mtazamo na vipaumbele vyangu.

Nikatafakari juu ya Musa aliyeziacha raha na vyeo Misri kwaajili ya Kristu, Daudi aliyesema kwamba siku moja nyumbani mwa Bwana ni zaidi ya siku elfu mahali pengine popote, alifurahia kuwa mngoja mlango nyumbani mwa Mumgu kuliko kuwa sehemu nyingine, nikamtazama Paulo na wengine wengi katika Biblia, hata mwishoni nikamtazama Baba yangu Mtume Wilbert Maridadi nikitaka nami kufunuliwa hilo ambalo liliwafanya kuacha vyote kwaajili ya Mungu, kuishi maisha yaliyotolewa kikamilifu kwaajili ya Bwana na wazo lake duniani.

Habari hizo nilizozisikia nami nilitaka nizione na nizishike, niziishi, ziwe uhalisia unaoshikika maishani mwangu.
Namtukuza Mungu Baba kwakuwa sasa nami naweza ungana na Ayubu kusema:

*“Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.”*
‭‭*Ayu‬ ‭42‬:‭5‬ ‭SUV‬‬*

Namshukuru Mungu Baba kwasababu sasa nimeijua sababu, sababu haikuwa kitu bali alikuwa Mungu Baba Mwenyewe, Kristu Mwenyewe ambaye amejifunua wazi wazi na kuwa halisi katika upendo wake.
Sasa kutafuta tafuta kumekoma, sasa nimepata hakikisho ndani yake Kristu Yesu, sasa nimemuona na kumgusa, sasa Kristu Yesu amekua kikamilifu sababu yangu ya kuishi.

Neno aliloniambia kuwa siku nitapouelewa vyema Ubwana wake juu ya maisha yangu basi hakuna tena changamoto binafsi itakayoweza kusimama sasa nimeanza kuliishi.

Nimekuona Bwana Yesu, nimekuona nimekushika na sasa ninaishi. Nimekuona Bwana unapendeza.

Na:
Mwana wa Mungu,
Taifa la Bwana PTM,
Hagai 2:23
Dar es Salaam - Tanzania.
@2026

Pete Ya Muhuri Int'l Ministries
21/03/2026

Pete Ya Muhuri Int'l Ministries

21/03/2026

*MAKAVAZI YA USHUHUDA NA SHUHUDA ZA BWANA NI URITHI WETU NA VIZAZI VYETU KATIKA KRISTO YESU.* *[ZAB 119:111]*

_MAADHIMISHO YA MIAKA 6 YA TAIFA LA BWANA PTM_

*KUMSIKIA NA KUMUELEWA ROHO MTAKATIFU NI MAISHA!*

Shalom! Wana wa Mungu.
Namtukuza BWANA wa Majeshi na Amani kwa namna ambavyo ameendelea kunijenga na kuniimarisha kila siku nyakati zote. Nakumbuka mwezi wa sita mwaka 2019 aliposema nami kuwa *“Never be afraid of anything unless you begin to lose your faith in Jesus Christ”* Neno na sentensi ambayo naweza kusema imekuwa muhimili mkubwa na nguzo katika maisha yangu na hata leo ninakiri sina ninacho kihofia katika maisha yangu isipokuwa kupoteza au kuacha kumwamini Kristo Bwana wangu.

*”….Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu…”*

[Waroma 8:37-39 SUV

Namtukuza BWANA kwa ajili ya miaka 6 ya kushindiliwa kicheko, tabasamu na ufahamu wa ajabu lakini zaidi ya kupewa jina jipya.

Hapa huwa ninapenda kusikiliza wimbo wa mpakwa mafuta N
Baba ninakushukuru, umefanya hili umefanya lile umenipa jina! Sijapewa tu jina bali kielezo cha maisha yangu, utu wangu, ufahamu na hatima yangu na vizazi vyangu.
IAM VICTOR!

Nakumbuka tarehe 19 mwezi Novemba 2025 Roho Mtakatifu alisema nami katika maono ya wazi baada ya picha nyingi sentensi hii , *"…Winning again is not hard, but you have to live first…"* Yaani ISHI!
Baada ya hayo maono katika kutafakari nikapata maana yake kwamba To Live is to be active, blessed, full of vigour, to be fresh, strong and efficient. To live is to see, hear, meditate, act on the Word of God for its life, anointed and incorruptible seed.

Baada ya hapo nikafahamu kuwa huwezi kushinda au kuishi maisha ya ushindi endelevu k**a hauishi, na kuishi ni kusikia, kuona, kutafakari na kufanyia kazi Neno la BWANA na MFALME wetu ELOHIM.

Nakumbuka tukuwa katika kusanyiko la BWANA BENDERA YA USHINDI WETU, Roho Mtakatifu akanikumbusha hili Neno na kunipa muendelezo kuniambia _"….Hakuna mshindi aliye mfu, washindi wote ni hai, wana maisha, wanaishi hata sasa na ujio wa mara ya pili wa BWANA wetu Kristo. Kwakuwa hakuna mshindi aliye mfu, ndio maana Bwana wetu Yesu Kristo aliishinda mauti ya msalaba, akafufuka anaitwa mzaliwa wa kwanza katika wafu na walio hai!_

*”…Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae…”*
[Wakolosai 1:16-19 SUV]

*”…Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo…”*
[1 Wakorintho 15:55-57 SUV]

Changamoto na fujo za mazingira zinaweza kuathiri namna utakavyo msikia Roho Mtakatifu katika mazingira hayo hayo, lakini jambo la kufahamu ni kuwa kamwe haachi kusema nawe kwa lugha rahisi ambayo utaelewa na kuchukua hatua, kwani moja wapo ya jukumu lake kwetu ni kutufunulia uhalisi wetu katika Kristo, kuturejesha katika Neno la BABA.

*”…Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia…”*
Yohane 14:26 SUV

Ukiniuliuza najivunia nini miaka 6, nitakueleza najivunia kumsikia Roho Mtakatifu, Kuzungumza naye, kutembea naye, kufanya kazi pamoja naye na kufundishwa naye siku zote, nyakati zote miaka 120 niliyojichagulia hata Kristo atakaporudi mara ya pili.

Na,
Mwana wa Mungu,
Taifa la Bwana PTM,
Dar es salaam, Tanzania.
@2026.

20/03/2026

*MAKAVAZI YA USHUHUDA NA SHUHUDA ZA BWANA NI URITHI WETU NA VIZAZI VYETU [ZAB 119:111]*

_MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA TAIFA LA BWANA PTM!_

*"NYUMBANI MWA BABA KILA KITU KINAPATIKANA!"*

Shalom familia ya Mungu Baba katika Kristo Yesu, namshukuru BWANA kwa ajili ya familia hii ya wakuu, ya thamani na weledi wa ajabu.

Namshukuru BWANA kwa kunipa nafasi ya usimamizi katika taasisi ya Yaliyojiri Habari Mseto lakini pia Mkurugenzi Mtendaji kwa kurusu hilo hata sasa ninapo karibia kutimiza mwaka ikiwa imebaki miezi 2 tangu nilipoanza utendaji kazi katika taasisi hii. Hakika hili nalo ni la kusherehekea ndani ya miaka sita. Bwana ameniponya na mahangaiko ya kutafuta kazi nje ya Mwili wake.

Wafilipi 1:2-6
*”…Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo,sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi.Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu…”*

Mosi, napenda kumshukuru BWANA kwa kuniamini na kuaminiwa katika taasisi kupitia Roho wa Neema, Uana, Ubunifu Usimamiz na Ukalimani. Hakika imekuwa Fahari kwangu na neema ya kuongeza palipopunguka katika eneo la Uchumi na Fedha.

Pili, namshukuru BWANA kwani kupitia Yaliyojiri Habari Mseto nimepata kuona kile ambacho ilikuwa ni shauku yangu kwa muda mrefu, kwamba kupata chombo cha habari ambacho kitakuwa kinatoa habari zenye kunijenga, kuniimarisha, kunitia nguvu, kunirejesha na kunistahimilisha sawasawa na asili yangu ndani ya Ufalme wa Mungu na eneo hilo ni Yaliyojiri Habari Mseto.

Tatu, nimeendelea kufaidika kwa kuweza kujengwa katika maeneo mbalimbali ambayo ni muhimu na afya kwangu hasa nikiwa msimamizi nyumbani mwa Baba ni muhimu kuwa na ufahamu katika mambo yote, nimejengwa katika eneo la uongozi kwa kuona namna ambavyo usimamizi katika mgawanyo wa majukumu unafanya kazi, kufanya kazi kwa pamoja, eneo moja, wakati mmoja na watu wamoja ni moja ya nguzo muhimu sana ya ustawi na maendeleo ya taasisi na watu wake kwa jumla.

Waefeso 4:4-7
*”…Mwili mmoja, na Roho mmoja, k**a na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo…”*

Nne, kupitia taasisi hii nimeweza kushuhudia maendeleo binafsi hasa katika eneo la uweledi wa kila ninachokifanya ambapo nimejifunza na kuendelea kuona kuwa si kila habari ni habari au kila taarifa ina faida na manufaa kwa walaji bali kile ambacho sisi tumekisikia, tumekiona, tumekishuhudia hiko ndiko habari (giving who and what we are) na si vinginevyo kuwalisha wana wa Mungu vitu ambavyo hata sisi hatuna vielelezo navyo. Hii imenisaidia katika utendaji wa kazi zangu mbalimbali na taasisi yangu katika maeneo ambayo nimeaminiwa kufanya. Kila kitu kutoka katika ujumbe wetu wa Uana na Ufalme wa Mungu ni habari!

Tano, nimeendelea kuthibitika katika eneo la maombi kwa kufahamu kuwa hakuna taasisi imara inayojengwa katika Idara mbalimbali pasipo kuwa na maombi (eneo la sirini) na hii inapelekea kuweza kuwa na utofauti siku hata siku, ubora siku hata siku na kamwe kutokaukiwa chakula cha kula mimi mwenyewe pamoja na walaji kwani ninayo chemichemi iliyo hai.

Sita, nimekuwa shahidi wa namna ambayo nimeendelea kufanywa upya na kuona matokeo yake siku hata siku, ambapo katika eneo la Uchumi na fedha nimeshuhudia mabadiliko na maendeleo katika eneo langu la Uchumi na taasisi yangu pia. Hivyo, Yaliyojiri Habari Mseto imekuwa mahali si tu ambapo nimefaidika k**a mtenda kazi bali nimefaidika k**a mlaji, na kiongozi mwenye maono ambaye pia ninasimamia maono ya taasisi yangu.

*“Zaidi napenda kusema nina furaha, ninapenda na kufurahia ninachokifanya na hii imenifungulia milango ya sehemu mbalimbali watu wakihitaji kujifunza kwa habari ya Uchumi na Fedha.”*

Na,
Mwana wa Mungu,
Taifa la Bwana PTM,
Dar es salaam,Tanzania.
@2026.

09/03/2026
09/03/2026

Address

Daresalaam
Dar Es Salaam
141101

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MKATE WA KILA SIKU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to MKATE WA KILA SIKU:

Share