17/09/2020
_18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa_ Roho Mtakatifu.
*19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.*
*Mathayo 1:19*
Naye Yusuph mumewe kwa vile alivyokuwa mtu wa *haki*
_Asitake kumuabisha_
Mtu yeyote wa *Haki* hawezi muabisha mtu mwingine
Sifa kuu ya mwenye Haki ni kuto aibisha mwengine kwa vitu usivyokuwa na uhakika navyo
Japo Daudi alijua fika kuwa mfalme Sauli Roho wa Mungu amemuacha hakutaka kumuaibisha kwa neno wala Tendo, kwakuwa alikuwa ni mtu wa haki
```Kuwa na haki na kuwa mtu wa haki ni vitu viwili tofauti```
Yusuph alijua mkewe kapewa mimba na mtu mwingi kwa akili zake hakupiga kelele yoyote mtaani aliazimu kumuacha kwa siri .
Ukiona una ndugu hakuelewi au hamuelewani usipange kumuabisha
Azimia kumuacha kwa siri bila kuongea chochote .
Kwani kati ya vitu muhimu ambavyo Mungu amemkirimia mwanadamu ni *Heshima .*
_Mwanadamu nini hata umuangalie au mwana wa binadanimu nini hata umkumbuke ? Umemfanya mdogo punde kuliko malaika lakini._
*umemvika taji ya Heshima*
Mwanadamu ni kiumbe dhaifu sana kisicho na thamani yoyote kimechukuliwa toka kwenye udongo
Lakini kitu pekee alichopewa kinacho mfanya hata malaika wamlinde ni *Heshima*
Ukikuta wewe ni mtaalam wa kuharibu heshima za watu ujue unamsaidia shetani kazi
Neno *uchawi* lina maana zifuatazo
1.kubaribu
2.kushusha thamani
3.kuiba
4.kuchinja
Hizi ni ndizo kazi kuu za neno uchawi
Yesu aliwaonya wanafunzi pale aliposema jihadharini na *wanadamu*
Kazi kuu ya watu hasa wanaotumiwa na shetani ni kuharibu kile ambacho Mungu alikitengeneza kwa gharama kubwa
Nyakati zilizo baki za ujio wa kristo
Tujihadhari na watu .