24/08/2026
TAG LIGHTHOUSE
Mhbr.JEREMIAH OGWAN*
Somo. UMEBADILISHWA ILI KUBADILISHA WENGINE
Kitabu. WARUMI 12:1-2
Tarehe. 23/08/2026
💥*Kubadilishwa ni Nini?* Kubadilishwa ni kutoka sehemu/hali moja kwenda Hali nyingine mpya
*Imani Isiyo na Matendo Ni Mfu
Mabadiliko ya kweli hayaishii tu kwa mtu kusema "nimeokoka", bali lazima yaonekane wazi kupitia tabia, matendo, na jinsi unavyoishi na wengine. Mungu ameweka uwezo mkubwa ndani yako; hupaswi kubaki umekaa bure.
Njia 3 za Kudhihirisha Mabadiliko Katika Maisha Yako
1.Yatoe Maisha Yako Kikamilifu kwa Mungu_ (Surrender Your Life to God)
-Kujitoa kwa Mungu lazima kuwe kwa 100%(completely), sio nusu nusu(Partially).
-Kuchagua njia ya Mungu na kukataa njia/mashinikizo mengine ya kupelekea dhambi.
-Yatoe maisha yako, wazo lako, na njia zako zote mikononi mwa Mungu.
-Mtume Paulo anatukumbusha kutoa miili yetu kuwa dhabihu inayompendeza Mungu kwa sababu ya huruma zake kwetu.
2.Badilishwa Fikra/mawazo na Nia Yako (Be Transformed in Your Mind)_
-Ruhusu Mungu abadilishe namna unavyofikiri, kuishi na kuamini.
-Mabadiliko huanzia ndani (kile unachofikiri ndio kitazaa matarajio)
-Chukua Hatua: K**a hauna kazi au biashara au chanzo chochote Cha kipato, mtegemee Mungu huku ukiamka kwenda kutafuta fursa, kujifunza ujuzi mpya, na kufanya kazi kwa uaminifu.
-Acha mtazamo wa hofu na kujiona huna mtaji au uwezo. Mungu ameweka kitu ndani yako—kionyeshe nje.
3.Onyesha Upendo, Unyenyekevu na Msamaha_ _Ishi ukiwa na ushawishi Kwa wengine_
-Mabadiliko ya kweli huanzia ndani ya moyo na kutoka nje kupitia unyenyekevu, upendo, na msamaha kwa wengine.
-Tumia nguvu na mwili wako kutumika kanisani na kwenye jamii bila kusubiri kulipwa pesa au kuombwa. Utayari wako wa kutumika ndio unaowavuta wengine kwa Kristo.
-Mungu amekupa uwezo na huruma zake ili uwe mwanga. Amka, badili fikra zako, na ukawabadilishe wengine!