Yesu ni Bwana na Mwokozi

Yesu ni Bwana na Mwokozi YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI WA ULIMWENGU, MTU HAENDI KWA BABA ISIPOKUA KWA NJIA YAKE.

WATU WANAULIZA SANA HILI SWALI JE MUNGU WA WAISLAMU NA MUNGU WA WAKRISTO NI MMOJA??  JIBU NI HAPANA, NARUDIA TENA HAPANA...
09/03/2026

WATU WANAULIZA SANA HILI SWALI JE MUNGU WA WAISLAMU NA MUNGU WA WAKRISTO NI MMOJA??

JIBU NI HAPANA, NARUDIA TENA HAPANA SIO MUNGU MMOJA NI MIUNGU WAWILI TOFAUTI KABISA.

HAKUNA MUNGU MMOJA HAPO SISI WAKRISTO TUNA MUNGU WETU NA WAO WANA MUNGU WAO

(1) MUNGU WETU ALITUUMBA WANADAMU TUMUABUDU NA AKATUPA NA AMRI KUHUSU KUWATOA PEPO NA MAJINI NA TAKATAKA ZAKE LUKA 10:19

-WAO MUNGU WAO ALIUMBA WANADAMU NA MAJINI YAMTUMIKIE, YAANI WAO NA MAJINI NI NDUGU NA YANAMUAMINI MUNGU WAO NA YANAMUOMBA HUYO MUNGU.

(2) SISI MUNGU WETU ANASEMA MKE MMOJA NA MUME MMOJA

-WAO MUNGU WAO ANASEMA WAOE WAKE WANNE

(3) SISI MUNGU WETU ANASEMA TUKIFA TUKIENDA MBINGUNI KAZI YETU NI KUMSIFU NA KUMUABUDU MUNGU WETU.

-WAO MUNGU WAO ANASEMA WAKIFA WAKIENDA PEPONI WATAPEWA MABIKIRA SABA KILA MTU NA WATAKUWA WANAKUNYWA POMBE HUKO KUTAKUWA NA MITO YA POMBE NA STAREHE MBALIMBALI.

ZAIDI YA YOTE SISI WAKRISTO TUNAMUAMINI YESU K**A BWANA NA MWOKOZI WA ULIMWENGU.

-WAO WANAKATAA KABISA

SISI WAKRISTO TUNAMUAMINI YESU KRISTO NI MUNGU WETU.

-WAO WANAKATAA KABISA

SISI WAKRISTO TUNAMUAMINI YESU NDIYE NJIA NA KWELI NA UZIMA, NA PIA TUNAAMINI ALIPO YESU NDIPO TUTAKAPOKUWAPO.

-WAO WANAKATAA KABISA

SISI WAKRISTO TUNAMUAMINI KATIKA NEEMA TULIYOIPATA KUPITIA YESU KRISTO KWA KUFA PALE MSALABANI

-WAO WANAKATAA KABISA

UKWELI NI KWAMBA MUNGU WA WAKRISTO, AMBAYE NI MUNGU WA ISRAEL SIO MUNGU MMOJA NA WAISLAM WALA DINI YOYOTE ILE.

WAISRAELI HATA K**A HAWAMUAMINI YESU KWA SABABU WALITARAJIA YESU ANGETOKEA KWENYE MAZINGIRA WALIYOYADHANI WAO LAKINI BADO HAO TUNAMUABUDU MUNGU MMOJA KABISA.

LAKINI HUYO MUNGU WA MAJINI, WANAWAKE NA POMBE HUYO HATUMJUI NA NI KOSA KUBWA KWA MKRISTO KWENDA KWENYE IBADA ZAO AU KUOMBA WAKUOMBEE, WANAKUOMBEA KWA MAJINI UJUE HILI NA WEKA AKILINI HII ISIKUTOKE KAMWE K**A MKRISTO.

YESU KRISTO WA NAZARETH, MUNGU WETU NA BABA YETU, BWANA NA MWOKOZI WETU, UTUKUZWE NA KUHIMIDIWA MILELE.

BWANA YESU ASIFIWE.MAISHA NI KUCHAGUA, AMUA VEMA LEO KWA FAIDA YAKO NA YA FAMILIA YAKO.Neno la Mungu lasema:“Nimeweka mb...
27/02/2026

BWANA YESU ASIFIWE.

MAISHA NI KUCHAGUA, AMUA VEMA LEO KWA FAIDA YAKO NA YA FAMILIA YAKO.

Neno la Mungu lasema:
“Nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai wewe na uzao wako.”
Kumbukumbu la Torati 30:19

“Chagueni leo mtakayemtumikia…”
Yoshua 24:15
“Tazama, sasa ndio wakati uliokubaliwa; tazama, sasa ndio siku ya wokovu.”
2 Wakorintho 6:2

MUAMINI YESU, MFANYE AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee…”
Yohana 3:16

“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.”
Yohana 1:12

“Amin, amin, nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka anao uzima wa milele.”
Yohana 5:24

MKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO NA UAMINI KWA MOYO WAKO.

“Ukimkiri kwa kinywa chako ya kwamba Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”
Warumi 10:9

“Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”
Warumi 10:10

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote isipokua Kwa YESU KRISTO PEKEE.
Matendo 4:12

YESU NDIYE NJIA, NA KWELI, NA UZIMA.

“Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.”
Yohana 14:6

“Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi ataokoka.”
Yohana 10:9

“Ndani yake ndimo uzima ulikuwamo, nao uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1:4

MPE ROHO MTAKATIFU UHALALI WA KUKUONGOZA.

“Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”
Warumi 8:14

“Lakini atakapokuja yeye, Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote.”
Yohana 16:13

“Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu?”
1 Wakorintho 6:19

HAKIKISHA JINA LAKO LIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA.

“Furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.”
Luka 10:20

“Na mtu ye yote ambaye hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika ziwa la moto.”
Ufunuo 20:15

“Yeye ashindaye… sitafuta jina lake kamwe katika kitabu cha uzima.”
Ufunuo 3:5

USISUBIRI HADI SIKU YA MWISHO NDIO UTUBU.
“Basi mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako…”
Mhubiri 12:1

“Msifanye migumu mioyo yenu.”
Waebrania 3:15

“Mtu atakayevumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka.”
Mathayo 24:13

MKATAE SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE.

“Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”
Yakobo 4:7

“Kesheni, simameni imara katika imani.”
1 Wakorintho 16:13

“Kwa sababu silaha za vita vyetu si za mwili…”
2 Wakorintho 10:4

NDUGU YANGU, AMUA VEMA LEO!
Usije ukaenda motoni huku ulitamani kwenda Mbinguni.
Mkiri Yesu hadharani, ishi kwa ajili Yake, mkatae kabisa Shetani na takataka zake zote kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, na kwa maisha yako yote

YESU MUNGU WETU NA BABA YETU BWANA NA MWOKOZI WETU UTUKUZWE NA KUHIMIDIWA MILELE.

SIKU YA 40:(DAY 40)MAOMBI YA KUMPA YESU SIFA NA UTUKUFU, KWA KUTUWEZESHA KUFUNGA NA KUOMBA, KWA SIKU 40.ZILIKUA NI SIKU ...
24/02/2026

SIKU YA 40:(DAY 40)

MAOMBI YA KUMPA YESU SIFA NA UTUKUFU, KWA KUTUWEZESHA KUFUNGA NA KUOMBA, KWA SIKU 40.

ZILIKUA NI SIKU 40 ZA MAOMBI YA MLIPUKO WA NEEMA.

Ee YESU KRISTO, Bwana na Mwokozi wetu,
leo tunainua sauti zetu kwa shukrani kuu.

Tunakuabudu, tunakutukuza, tunakupa heshima yote,
kwa sababu umetuwezesha kufunga na kuomba siku hizi 40
za MAOMBI YA MLIPUKO WA NEEMA.

Bwana, si kwa nguvu zetu wala si kwa uwezo wetu,
bali kwa Roho wako Mtakatifu.

Tunakushukuru Roho Mtakatifu, Msaidizi wetu mwaminifu,
kwa sababu umetusaidia katika udhaifu wetu.

K**a ilivyoandikwa katika Warumi 8:26,
kuwa hukutuacha peke yetu,
bali ulituombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

-Wakati hatukujua la kusema, ulisema kwa niaba yetu.
-Wakati tulipolia kimya kimya, uliwasilisha kilio chetu mbinguni.
-Wakati tulichoka, ulituinua kwa nguvu mpya.

YESU, tunakiri na kuamini
kuwa umetumwagia neema yako kuu
katika kila pembe ya maisha yetu.

-Mlipuko wa neema ya kukujua zaidi!

-Mlipuko wa neema ya kuishi k**a ulivyoagiza!

-Mlipuko wa neema kwenye kazi zetu!

-Mlipuko wa neema kwenye biashara zetu!

-Mlipuko wa neema kwenye malengo yetu!

-Mlipuko wa neema ya kibali kila tunapopita!

-Mlipuko wa neema ya afya na uzima!

-Mlipuko wa neema ya mafanikio kwetu na kwa uzao wetu hata milele!

Bwana, tunatangaza kwa imani
kuwa tutafanya mambo makuu
kwa neema yako YESU KRISTO.

-Tutakuwa ushuhuda hai wa wema wako.
-Tutatembea katika kibali kisicho cha kawaida.
-Tutang’aa kwa utukufu wako.

TUNAKUPA SIFA NA UTUKUFU WOOTE, POKEA SIFA ZOOTE, ENZI NA MAMLAKA VYOTE NI VYAKO YESU.

-Utukufu wote ni wako.
-Sifa zote ni zako.
-Nguvu zote ni zako.

YESU, endelea kutawala ndani yetu.

Roho Mtakatifu, endelea kuwasha moto usiozimika ndani yetu.

Tufanye vyombo vya heshima,
vya kuitangaza neema yako kila mahali.

Tunafunga siku hizi 40 kwa shukrani,
tunazifunga kwa ushindi,
na tunaingia katika msimu mpya
wa MLIPUKO WA NEEMA.

Katika Jina kuu la YESU KRISTO,
Bwana na Mwokozi wetu,
Amina na Amina .

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255689603780

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yesu ni Bwana na Mwokozi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share