tz_worships

tz_worships Hii ni page maalumu kwa ajiri ya vijana wakristo waamini. Tupo hapa ili kupeana habari za ufalme wa Mungu.

Ipo wazi kabisa. Vita sio vya kwetu Bali vita ni vya Bwana. Ukijifanya kuiruka hii formula basi kazi unayo😀😀
31/01/2021

Ipo wazi kabisa. Vita sio vya kwetu Bali vita ni vya Bwana. Ukijifanya kuiruka hii formula basi kazi unayo😀😀

Hesabu 31:49
30/01/2021

Hesabu 31:49

Ili ufanikiwe ni lazima kwanza uache kuangalia hali na kanuni za kibinadamu. 🦅Yamkini kweli hali ya uchumi hairuhusu wew...
29/01/2021

Ili ufanikiwe ni lazima kwanza uache kuangalia hali na kanuni za kibinadamu.

🦅Yamkini kweli hali ya uchumi hairuhusu wewe kufanya jambo fulani, au ugonjwa ulionao ki kanuni za kibinadamu hauwezi kupona...

🦅Mungu anasema neno leo ya kwamba yeye hatazami Kanuni za dunia hii ili atende jambo, yeye aliyetoa mito jangwani,aliyenyesha mvua kwenye ukame mzito wa israel, yeye aliyesimamisha dunia Joshua akashinda vita ,asema hivii

"Yote yanawezekana kwake aaminiye"


🦅Ili ufanikiwe ni lazima kwanza uache kuangalia hali na kanuni za kibinadamu. 🦅Yamkini kweli hali ya uchumi hairuhusu we...
29/01/2021

🦅Ili ufanikiwe ni lazima kwanza uache kuangalia hali na kanuni za kibinadamu.

🦅Yamkini kweli hali ya uchumi hairuhusu wewe kufanya jambo fulani, au ugonjwa ulionao ki kanuni za kibinadamu hauwezi kupona...

🦅Mungu anasema neno leo ya kwamba yeye hatazami Kanuni za dunia hii ili atende jambo, yeye aliyetoa mito jangwani,aliyenyesha mvua kwenye ukame mzito wa israel, yeye aliyesimamisha dunia Joshua akashinda vita ,asema hivii

"Yote yanawezekana kwake aaminiye"


29/01/2021

Pastor Mungu azidi kukuinua.

24/03/2020

KESHO KESHO KESHO
(Siku ya maombi)
📌Tzworships

K**a tulivyoongea kuwa kesho tutaanza maombi k**a kawaida (Jumatano).

Maombi yatakuwa ya masaa 12 k**a kawaida. Ombi kubwa la kesho ni kuhusu dunia nzima juu ya ugonjwa huu (corona).

Sisi k**a waamini tumuombe Mungu atupe roho ya ujasiri ya kuweza kukabiliana na kila changamoto zitakazoinuka

👉🏽Hatukupewa Roho ya woga iletayo hofu. Kila hofu ambazo zimepandwa mioyoni mwetu zituachie.
👉🏽Maneno ambayo tumejitamkia sisi wenyewe kipindi hiki cha ugonjwa tuyafute... Kwa kinywa chako utahukumiwa.

Nb: umek**atwa na umetegwa kwa maneno ya kinywa chako.

👉🏽Tuombe afya kwa dunia nzima. Kila kilichokufa/kidhaifu Mungu akakirudishie afya maana yeye ndiye huo ufufuo na uzima.

ANDIKO LA KUSIMAMIA

📌2 NYAKATI 7:15📌

(Group litafungwa kesho asubuhi kupisha maombi)

Amen
10/03/2020

Amen

10/03/2020

Bwana Yesu asifiwe

THE PRINCIPLES OF CREATION(KANUNI ZA UUMBAJI) - 3Bwana Yesu asifiwe sana sana. Leo tunaendelea tena na mada hii ya uumba...
16/02/2020

THE PRINCIPLES OF CREATION
(KANUNI ZA UUMBAJI) - 3

Bwana Yesu asifiwe sana sana. Leo tunaendelea tena na mada hii ya uumbaji hasa kutoka kwenye kitabu cha MWANZO katika kuichambua biblia.

Leo tutaangazia jambo la msingi sana kwenye maisha ya mwanadamu. Hili si lingine bali ni Asili ya mwanadamu na chimbuko lake.

Hivyo mistari yetu ya kusimamia leo itakuwa hii hapa
(MWANZO 1:26-27)

Nanukuu
"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
MWA. 1:26‭-‬27 "

Mambo mazito sana yamezungumzwa hapa. Ngoja tuanze kuangazia moja badala ya lingine.

1.Mwanadamu aliumbwa,hakutokea tu. Yesu anathibitisha hili kwenye MARKO 10:6.
- Kuna mambo mengi sana sasa hivi ulimwenguni yanajaribu kukenguesha uumbaji wa Mungu. Kumekuwa na wachunguzi wengi wa mambo pamoja na wanasayansi mbali mbali hasa ma atheist (wapagani) ambao wanaamini kuwa mwanadamu aliibuka tu yaani alitokea tu na hakuumbwa. Biblia ni neno la Mungu na limethibitishwa mara 7 na kupimwa kwa moto kuwa linafaa kwa matumizi yetu,na neno hili ambalo linatoka kwa Mungu na ni Mungu mwenyewe leo linatupa historia nyingine kabisa kuwa mwanadamu aliumbwa tofauti na wanasayansi na wapagani wanavyodai. (Ipo siku nitakuja kuelezea kwa undani juu ya swala hili zito).

2.Jambo la pili na lamuhimu sana ni hili.
MWANADAMU AMEUMBWA KWA MFANANO SAWA NA MUNGU ,aneumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mwenyewe.

Mungu ni Roho na mtu ni Roho. Usichanganye hapa.

Mungu alianza kumuumba MTU na sio MWANADAMU.
yule mtu aliyemuumba ndiye biblia inaemsema kuwa anafana na Mungu na yupo k**a Mungu (kiroho). Ila baadae Mungu akamfanyie yule mtu nyumba ya nje inayoitwa mwili,yule mtu akaanza kuitwa mwanadamu.

Kwa hiyo mwanadamu ni Muunganiko wa vitu vitatu.
MWILI,NAFSI NA ROHO. Kati ya hivi vitatu,iyo roho ndiyo inayofanana na Mungu wetu.

Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
1 THE. 5:23

Andiko hili linathibitisha utatu wa mwanadamu.

a) Roho ni sehemu ya mwanadamu yenye kujua na yenye ufahamu juu ya Mungu. The part of man that KNOWS. 1 kolosai 2:11

b) NAFSI ni sehemu ya mwanadamu yenye ufahamu na akili. Hisia zote ,akili,maamuzi hayakai rohoni bali kwenye nafsi. Kuna muda biblia inachanganya kati ya nafsi na moyo.

C)MWILI ndiyo sehemu pekee iliyotofauti na roho na nafsi. Mwili ndio unaokufa. Nafsi na Roho hazifi.

Katika somo UTAMBUE UFALME WA MUNGU nimeongelea sana juu ya mwili na thamani ya mwili wako.

Huu ndio muunganiko wa mwanadamu.

Pia ni lazima ujue kuwa,mwanadamu pekee ndiye aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mimea na wanyama hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu. Ukisoma sehemu ya pili ya somo hili utaona jinsi mimea ilivyotokea.. "MUNGU akasema nchi itoe mimea kwa aina yake" lakini ilipokuja kwenye swala la kukuumba wewe,Mungu alijifananisha na wewe..

Kwahiyo usije ukajidharau hata kidogo wala usimuache mtu audharau uwanadamu wako,wewe ni final master piece of God. Katika vitu alivyoviumba Mungu ,basi wewe umevizidi vyote.

👉🏽pia kuna aina mbili za uumbaji zinazoonekana kwenye kitabu cha mwanzo (tutazungumzia mbeleni)

Ila kwenye mstari wa 27..Mungu anasema alimuumba mwanamke na mwanaume, hao wote aliwaumba.

Mwanaume ni Adamu,je mwanamke ni nani???

Bila shaka utasema EVA na kweli ni EVA. ila kuna nadharia nyingi hapa ambazo mimi naona sio za kimungu kabisa kuhusu swala hili.

Yote haya na mengine tutayaangalia kwenye sehemu ya nne.
Mungu akubariki sana snaa

Tzworships.blogspot.com
By Maestrorabbon

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when tz_worships posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to tz_worships:

Share