The seer Shepherd Baitange

The seer Shepherd Baitange MUUNGANIKO WA KIDINI

Kuna wakati changamoto unazopitia zimebeba baraka zako za ajabu sana, upo  wakati unaweza pitia magumu na ukaona ni  bor...
26/07/2020

Kuna wakati changamoto unazopitia zimebeba baraka zako za ajabu sana, upo wakati unaweza pitia magumu na ukaona ni bora ufe au ukimbie changamoto , kumbuka tatizo halitatuliwi kwa kulikimbia Bali tatizo utatuliwa kwa kulikabli, ukiona majaribu yamekuzongaaa na ukahisi kuona Giza hakika ujue NURU inazuka na njia utaiona. Usipende sana kulaumu upitiapo shida nyingi , usipende kukimbia tatizo ukidhani umelitatua maana hata kule ukimbiliako unaweza kuta mengine 100 zaidi ya kule ulikotoka, jifunze kukaa chini, kuweka amani , kutafuta namna ya kusawazisha mahali ambapo hapajakaa sawa kwa kutumia hekima na nakwambia utaishi kwa amani na furaha sana. Kumbuka nimekwambia wewe ni ile NYOTA YA ASUBUHI na nimekwambia haya nkiwa na roho wa mungu na shetani akijaribu kunizuia ila hakuweza. Inuka na uangaze usipende kuyakimbia matatizo maana huo ni utoto wa kiakili na mpango wa shetani au adui kukuzuilia baraka zako.

The Great 01

WEWE NI NANI ?Kuna wakati katika  maisha ambapo mtu  upitia magumu sana na kuliona Giza mbele zake hadi  kuhisi hakika h...
26/07/2020

WEWE NI NANI ?

Kuna wakati katika maisha ambapo mtu upitia magumu sana na kuliona Giza mbele zake hadi kuhisi hakika hamna matumaini katika maisha, shida tunazopitia zinatofautiana kila mtu anao mzigo wake , lakini shida unayoipitia au magumu na yakuumiza moyo ulowahi kupitia usikate tamaa, yesu alisema duniani mnayo dhiki nyingi lakini bwana atawaponya nayo yote, usiogope hata k**a utaanguka lakini utasimama Mara saba , usikubali katu kukata tamaa kwasababu ya magumu ulopitia maana unayo nguvu ndani yako hakika ukiamua inawezekana , binadamu wapo Wa aina mbili , kuna mtu anaonekanaye Kwa umbo LA nje mpaka unaitwa Fulani nisababu tunavokuona, pia kuna binadamu Wa ndani hasiyeonekana na huyu ndo binadamu hatari zaid hapa duniani , binadamu Wa aina hii upatikana ndani ya mfumo Wa akili wa mtu na amebeba nguvu za ajabu sana , pale unapo fukuzwa kazini kwamfano, biashara zinapoharibika, mke akaukimbia , hauna uhakika Wa kula, ndo wakati ambapo aina yako ya pili isiyoonekana udhihirika na kupambana na changamoto, wewe ni nani ? wewe ni nuru ya ulimwengu unayaweza mambo yote kwake yeye akutiaye nguvu , usikubali kukata tamaa maana wewe ni chumvi ya ulimwengu, mungu amekuahahidi kuwa hatokuacha wala hatokutupa kamweeee, yuko nawe hadi ukamilifu Wa nyakati, ni nani huyo anayesema hauwezi ? Hata ukikutana na vikwazo vingi mbele zako usife moyo amini na inuka tena maana maandiko yanasema nitakwenda mbele yako , na kupasawazisha mahali palipo paruza, nitavunja vipande vipande milango ya shaba na kukatakata mapingo ya Chuma, nami nitakupa hazina za gizani , na Mali zilizofichwa mahala pa siri ijapokuwa haukumjua ( ISAYA 45:2-6) wewe ni mfalme, wewe ni mmiliki wewe ni mtawala katika hii dunia, usiogope hata ukatishwe tamaa na maelfu simama maana bwana ni nuru yako na wakovu wako , usimwogope mtu , yeye ni ngome ya uzima wako husimhofu mtu hakika atakupigania (zaburi 27) , inuka pambana usife moyo wewe ni ile NYOTA YA ASUBUHI

The Great 01

Bwana ametoa bwana ametwaa , hakika nilikuwa nkisikia kumuhusu huyu mtu  nkiwa mdogo kiakili juu ya uongozi wake naamini...
24/07/2020

Bwana ametoa bwana ametwaa , hakika nilikuwa nkisikia kumuhusu huyu mtu nkiwa mdogo kiakili juu ya uongozi wake naamini amelipigania taifa Kwa nafasi nzuri sana mpaka hapa lilikofikia mchango wake mkubwa ameutoa wakutosha. Mungu anatufundisha kitu kikubwa kiitwacho upendo maana Leo tupo kesho hatupo kwake twarejea ni vema kuishi Kwa upendo na amani na kila MTU maana hatuijui saa wala dakika mwana Wa adamu atakapo tuitaji.

Mungu baba akuweke mahala unapostahili@benjamin William mkapa: RAIS Wa awamu ya tatu ya jamhuri ya muungano Wa Tanzania.

The Great 01

Nayaweza mambo yote kwake yeye (yesu) anitiaye nguvu !!  Nani anaweza kuwa kinyume changu akanishinda ? The Great 01
21/07/2020

Nayaweza mambo yote kwake yeye (yesu) anitiaye nguvu !! Nani anaweza kuwa kinyume changu akanishinda ?

The Great 01

Mpakwa m...a...f....u...t...a !!!The Great 01 ( jina langu  la  kiroho )
20/07/2020

Mpakwa m...a...f....u...t...a !!!

The Great 01 ( jina langu la kiroho )

Hii couple bila shaka ni  moja kati ya couples bora duniani na zenye mvuto Wa hali ya juu sana. Nadhani umenielewa alafu...
20/07/2020

Hii couple bila shaka ni moja kati ya couples bora duniani na zenye mvuto Wa hali ya juu sana. Nadhani umenielewa alafu mi sinaga wivu, hasira , vinyongo maana hizo ni tabia za shetani .....

Kasi ileile ninayotembea nayo katika kristo yesu Kwa kila jambo na mfumo mzima Wa maisha yangu haitopungua hata kidogo n...
16/07/2020

Kasi ileile ninayotembea nayo katika kristo yesu Kwa kila jambo na mfumo mzima Wa maisha yangu haitopungua hata kidogo na itazidishwa Mara saba hivi punde baada ya kuhitimu shahada ya kidunia ya falsafa na maadili mwezi Wa nane mwaka huu , nguvu , jitihada, hekima na maarifa yote yatahamia katika kile tumeitiwa tangu Asili. Hakuna kurudi nyuma iwe ni kiroho, kiafya au kiuchumi hakuna kurudi nyuma ni kwenda mbele na kubaki kuwa juu. Mi ni mfanya kazi hapa duniani napaswa kuyakamilisha majukumu niliyotumwa Kwa wakati niliohitiwa , Mungu atayashangaza mataifa na ninakuombea nawe unayeonekana hauwezi mi naona we unaweza inuka na ukaangaze Kwa maana nuru ya bwana wangu imekuzukia amka hapo ulipo kajaribu, k**a ni biashara nenda kajaribu, usiogope, ndiyo najua mwanzo utakutana na changamoto lakini ipo nguvu itayokupatia hekima ya namna ya kukabiliana nazo na kuzishinda hizo changamoto, sema huu ni wakati wangu na inuka ukadhihirishe mwana Wa mungu na hakika utafanikiwa sana . kazi yangu kubwa kwako ni kukuombea na kuzuia hila za shetani juu ya maisha yako. Imekuwa !!

The Great 01

Ninakuombea NEEMA ya mungu baba iendelee kukulinda, KIBALI chake kikakufanikishe na UPENDO ukawe sehemu ya maisha yako, ...
16/07/2020

Ninakuombea NEEMA ya mungu baba iendelee kukulinda, KIBALI chake kikakufanikishe na UPENDO ukawe sehemu ya maisha yako, Zaidi ya yote nakuombea mafanikio ya kiroho na kimwili katika jina LA yesu aliye hai.

The Great 01

Mda mfupi kutokea hivi sasa ntakuwa kwenye mlima Wa maombi kukuombea mbele za bwana na ushindi wako umehakikishwa Kwa ji...
15/07/2020

Mda mfupi kutokea hivi sasa ntakuwa kwenye mlima Wa maombi kukuombea mbele za bwana na ushindi wako umehakikishwa Kwa jina la yesu aliye hai. Unaweza kuhoji 1+1 lakini hauwezi kuhoji kuhusu 2 maana ndo jibu la 1+1. Bwana atafanya tena na tena k**a ambavyo amekuwa akifanya.

The Great 01

KITU KILICHOFICHWA NDANI YA UTUKUFU.Nafikiri, Kwa fikira za kimantiki , bado watu wengi hawajaelewa udhihirisho au ushai...
15/07/2020

KITU KILICHOFICHWA NDANI YA UTUKUFU.

Nafikiri, Kwa fikira za kimantiki , bado watu wengi hawajaelewa udhihirisho au ushaidi Wa utukufu.

Kulingana na biblia, Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo au mambo yajayo yasiyoonekana. Kuna mda ambapo mtu hapaswi kusema kwamba anayo imani, Bali uanza kuona udhihirisho au ushaidi Wa vile vitu vitarajiwavyo. Ninaamini unaweza kuhitimu kutoka kwenye hatua au viwango vya kusema au kutamka vitu hadi kuingia kwenye hatua ya kuona vile unavyoviamini vikijidhihirisha waziwazi.

Mahak**ani kwamfano, pale ambapo hakimu anakaribia kutoa hukumu au kuipitisha hukumu juu ya mtu na Mara ghafla ushaidi mpya ukaibuka , anaweza kujikuta ghafla anaacha kuipitisha ile hukumu alokuwa akiisoma juu ya mtu fulani kwasababu ya ule ushaidi uloibuka ghafla..

Hakika nakwambia , Mungu atakupatia ushaidi mpya na Wa ajabu utakao wanyamazisha maadui zako k**a unaamini .

The Great 01

Wale aliowajua tangu  asili , aliwachagua tangu  asili  wafananishwe na mfano Wa mwana wake , ili yeye awe mzaliwa Wa kw...
14/07/2020

Wale aliowajua tangu asili , aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano Wa mwana wake , ili yeye awe mzaliwa Wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili , hao akawaita , hao akawahesabia haki , na wale aliowahesabia haki , hao akawatukuza. ( warumi 8:29:30 )

The Great 01

Maandiko usema vile ajionavyo mtu  nafsini mwake hakika ndivyo alivyo. Wewe je unajionaje ndani yako ? ByThe Great 01
14/07/2020

Maandiko usema vile ajionavyo mtu nafsini mwake hakika ndivyo alivyo. Wewe je unajionaje ndani yako ?

By

The Great 01

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Opening Hours

Wednesday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255683935805

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The seer Shepherd Baitange posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share