Efatha Nazareth - Kiyombo Church

Efatha Nazareth - Kiyombo Church We Bring The World To Jesus. Instagram: EfathaChurchKiyombo

Telegram: https://t.me/EfathaNazarethChurch

Heri ya siku ya kumbukizi ya Kuzaliwa Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.Tunamshukuru Mungu kwa ajili Yako...
01/01/2024

Heri ya siku ya kumbukizi ya Kuzaliwa Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Tunamshukuru Mungu kwa ajili Yako. Tunathamini uwepo wa Mungu katika maisha yako na uaminifu na haki yako. Katika siku yako maalum ya kumbukizi ya kuzaliwa, hakuna kitu bora zaidi kuliko kumshukuru Mungu kwa rehema zake juu ya maisha yako.

Umeathiri maisha ya watu wengi kwa njia chanya kupitia maneno yako ya hekima. Wema na rehema za Mungu ziendelee kuwa na wewe leo na daima. Tunakuombea upako mpya, nguvu mpya, hekima mpya na maisha marefu kwa jina la Yesu.

Asante Baba kwa kusema ndiyo kwa mwito huu mkuu wa Mungu, sisi kwa mamlaka ya mbinguni tunakupenda na tunathamini mchango wako katika kuujenga mwili wa Kristo. Furaha, Kicheko na Baraka za Mungu zisipungue kwako. Mungu Akubariki uingiapo na utokapo siku zote za maisha yako. Amen

HERI YA MWAKA MPYA 2024HAPPY NEW YEAR 2024
31/12/2023

HERI YA MWAKA MPYA 2024

HAPPY NEW YEAR 2024


SUNDAY SERVICE, 17.09.2023, EFATHA CHURCH MWENGE DAR ES SALAAM, TANZANIA.APOSTLE BARIKI URASSAPsalms 103:1-5 “Bless the ...
17/09/2023

SUNDAY SERVICE, 17.09.2023, EFATHA CHURCH MWENGE DAR ES SALAAM, TANZANIA.

APOSTLE BARIKI URASSA

Psalms 103:1-5 “Bless the LORD, O my soul: and all that is within me, bless his holy name. Bless the LORD, O my soul, and forget not all his benefits: Who forgiveth all thine iniquities; who healeth all thy diseases; Who redeemeth thy life from destruction; who crowneth thee with lovingkindness and tender mercies; Who satisfieth thy mouth with good things; so that thy youth is renewed like the eagle's.”

David figured out how to have a heart of praise and thanksgiving for the Creator; similarly, we need to have an attitude of praise and thanksgiving for our God, who is able to provide all of our needs. Yes, you face a number of difficulties that trouble you and torment your heart and soul, but the solution to all of that is to have a grateful heart and give thanks to your God. Don't just be grateful to God because he has done something for you, but have a life of praise and thanks to your God whether you have earned it or not. That is why David said "O my soul, praise the Lord." Yes, all that is in me Praised his holy name." Make sure your thoughts, words, actions and behavior praise the Lord's name.

The way for you to get out of challenges, troubles, problems, need and poverty that bother you is not to talk about the things that bother you, no! But you put them aside and you send a heart of praise and gratitude to the one who can fight with what bothers you.

If you want heaven to deal with your problem, have a heart of gratitude to your God for what you want him to do for you and not explain the problems and problems that bother you.

CONFESSION: Oh my Lord, many things torment me, but I will accompany you who can do more than what torments and bothers me; I and all that is within me will praise your name, you who can do more than what I think.

30/08/2023
IBADA YA JUMAPILI YA  TAREHE 16/07/2023  KATIKA KANISA LA EFATHA KIYOMBO. DAR ES SALAAM - TANZANIA.MCHUNGAJI VAILETH DAV...
16/07/2023

IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 16/07/2023 KATIKA KANISA LA EFATHA KIYOMBO. DAR ES SALAAM - TANZANIA.

MCHUNGAJI VAILETH DAVID.

Sasa ili upate uzima wa milele Nia Yako ya Rohoni lazima iwe na nguvu kuishinda Nia ya mwili na ukifikia hapo; Lolote utakaloomba Kwa Mungu atakusikia na kukujibu.

Unasikia kijana anasema Mchungaji unajua nikimwona Binti tu k**a na changanyikiwa ujue tu Nia ya mwili inamtawala, imechukuwa nafasi, inanguvu kuliko Nia ya roho. Lakini k**a Nia zenu za rohoni nyie zikiwa na nguvu kuliko Nia ya mwili ukiwaoona wadada hutababaika utawaona Ni dada zako tu.

Ukiwa na Nia ya roho yenye nguvu kuliko Nia ya mwili hata ukitokea ugomvi kwenye familia au kwenye ndoa ni rahisi sana kuumaliza Kwa maneno machache ya unyenyekevu.

Changamoto inakuja tunapokuwa tumezaliwa katika roho lakini tunaishi katika mwili huu ulimwengu wa mwili; Ndipo Biblia inasema hizi zimepingana hata hamwezi Kufanya mnayoyataka

Unawezaje kuishinda Nia ya mwili Kwa kufanya mapenzi ya Mungu ambalo ni tunda la roho kwa mfano kuwa na tabia ya kusamehe unyenyekevu utii na kujitoa hizi tabia zikiumbika Kwako utaishinda Nia ya mwili na haitakuwa na nguvu Kwako.

Nia ya roho itakufanya uwe na Upendo Kwa yeyote pasipo sababu pendo la Kristo na Kwa pendo Hilo Yesu anataka tuwafikie ulimwengu Kwa neno lake ili waokolewe.

Ukiwa na Nia ya roho yeyote utakae mwona katika nyumba ya Mungu huyu ni Ndugu yako katika Bwana na Hali hiyo ikiisha tawala ni rahisi sana Mungu Kufanya maajabu yake katikati yenu kwasababu Nia ya roho inatawala ndani yenu

Nia ya roho ikitawala kuna kuwa na amani Upendo maelewano na ustawi.

Tukija kwenye Nia ya mwili Huwa inakawaida ya kumsemesha mtu kumwaminisha mtu kwamba unaweza hakuna k**a wewe lakini mwisho wake ni mauti.

ZABURI 46:1-2

"Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari."

Sisi Efatha Kiyombo hatuogopeshwi na Lolote kwasababu tunae Mungu ambae ni kimbilio letu sisi, Unajua sisi hatukijileta hapa ni Mungu mwenyewe amekuweka hapa kwahiyo anapotokea adui kupambana na wewe. Wewe Kaa pembeni umwache apambane na Mungu aliekuweka hapa.

Hatuogopi kwasababu tunauhakika nae Yeye ni Mungu sio mwanadamu Yeye ni Mungu wa wote wenye mwili.

Walio na Nia ya Roho wamehamishwa; wamehamishwa toka nguvu za Giza na kuingizwa katika ufalme wa mwana wa pendo lake.

WAKOLOSAI 1:13-14
"Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi."

Kwahiyo k**a umehamishwa usifanye Tena matendo maovu ya kule ulikotoka màana upo katika ufalme wa mwana wa pendo lake hutakiwi kabisaa kufanya mambo ya Giza ya matendo ya mwili wakati upo Nuruni umeshamishwa Tayari.

Fikria katika ukoo wenu wewe pekee Yako ndio umeokoka hujiuuliza ni Kwa namna gani Mungu anavyokupenda, Alikupenda Wewe ndio màana katikati ya wengi katika ukoo wenu wewe pekee yako umehamishwa na kuingizwa katika ufalme wa Nuru kwenye Nia ya Roho kwenye mapenzi ya Mungu.

Kwahiyo ukiwa huku tembea katika Nia ya roho; ya mapenzi yake na makusudi yake Hivyo sisi tu mali yake tu wakwake kwasababu Kuna mahali ametutoa na kutuweka hapa. Kwahiyo nachokijua Mimi ni mali ya Mungu chini ya Efatha na Mtumishi wake Josephat Elias Mwingira.

Tutulie Wana Efatha Kiyombo tusiyumbishwe na mwanadamu màana tunamjua anaetumiliki ili tuweze kumwona Mungu Katika maisha yetu.

Address

Kitunda, Kiyombo
Dar Es Salaam
12111

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Nazareth - Kiyombo Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share