07/11/2025
K**A SI YESU, HABARI YETU INGEISHA ZAMANI SANA
Jina la Bwana na Mwokozi wetu, Mkuu wa Uzima na Mfalme wa Wafalme, Yesu Kristo, libarikiwe. Hakujawahi kutokea mtu wa muhimu, wa rehema, na wa uzima k**a Yesu. Leo, tutatafakari umuhimu wake mkuu katika maisha yetu.
Je, wajua kwa nini Maandiko yanasema kwamba Bwana Yesu alipigwa kwa ajili yetu?
> Isaya 53:5
“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”
Mungu hakumtuma Mwanawe kwa sababu alitaka kutuhukumu. Hapana! Hukumu tayari ilikuwa imetolewa juu ya wanadamu kwa sababu ya dhambi. Adhabu ilikuwa njiani kutufikia, lakini Yesu akaingilia kati na kuibeba juu yake.
Fikiria mtu ambaye amekwisharusha jiwe kumlenga mwingine. Wakati jiwe bado lipo angani, mtu mwenye huruma anaingia na kukubali kupigwa badala ya yule aliyelengwa. Hivyo ndivyo Yesu alivyofanya. Hakufuta hukumu—aliibeba. Ndiyo maana ilimpasa afe, kwa sababu adhabu hiyo ilikuwa yetu. Aibu, maumivu, na mateso yale yalipaswa kuwa yetu, lakini yeye aliyachukua yote.
K**a Yesu asingetokea, tungalipotea chini ya ghadhabu ya Mungu—k**a watu wa wakati wa Nuhu au Sodoma na Gomora. Tungalilia, tukaumia, tukateseka, na mwishowe kuangamia katika ziwa la moto.
> Isaya 53:4–6
“Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Sisi sote k**a kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.”
Maneno “Ameyachukua masikitiko yetu” yanamaanisha huzuni ambazo tulipaswa kupata baada ya kupigwa na Mungu. Yesu alibeba huzuni hizo kwa niaba yetu. Ndiyo maana alisema:
> Marko 14:34
“Nafsi yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa.”
Umeona umuhimu wa Yesu kwetu? Je, unamthamini kweli Bwana? Kumbuka, ghadhabu ya Mungu bado ipo kwa wale wanaoidharau kazi ya msalaba.
> Waebrania 10:29
“Mwaonaje? Haimpasi adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo k